4 Apr 2011


Magufuli atamba mbele ya Rais
• Atoa onyo la bomoabomoa kwa wakazi Dar

na Bakari Kimwanga

SIKU chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kumtaka Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, aache ubabe katika kutekeleza zoezi la bomoabomoa, jana waziri huyo alitoa onyo mbele yake akiwataka wakazi wa Tegeta jijini Dar es Salaam hasa waliokuwa katika hifadhi ya barabara ya Mwenge hadi Tegeta, wahame wenyewe kabla hajachukua hatua za kuwaondoa kwa nguvu.

Magufuli aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana huku Rais Kikwete mwenyewe akiwa pembeni yake, wakati wa sherehe za uzinduzi wa mradi wa upanuzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 12.9 inayojengwa kwa msaada wa serikali ya Japan kupitia shirika lake la maendeo (JICA).

Waziri huyo makeke alisema katu hataacha kusimamia sheria namba 18 ya mwaka 2007 ambayo ilisainiwa na Rais mwenyewe ambayo inakataza watu kuingilia eneo la hifadhi ya barabara kwa kujenga makazi au kufanya biashara.

“Mheshiwa Rais, hata wakileta malalamiko kwako usiwasikilize, kwani sheria namba 18 uliyoisaini inakataza….naahidi kuisimamia na kuwepo kwa Makatapila katika eneo la Tegeta sasa ni ishara tosha kwa wakazi waliovamia hifadhi ya barabara kuondoka wenyewe kabla sijaanza kuwaondoa kwa nguvu!”

“Mradi huu utachukua miezi 27 kuanzia mwezi Februari na unatarajiwa kukamilika Mei, 2013 na utagharimu shilingi bilioni 88 na fedha zote ni msaada toka serikali ya Japan,” alisema Magufuli.

Barabara hiyo inapanuliwa kwa kiwango cha lami na itakuwa na njia nne na vituo rasmi vya mabasi 22.

Aidha, alieleza kuwa hatua ya Rais Kikwete kumteua kushika wadhifa huo ni msukumo tosha kwa yeye na wasaidizi wake kuhakikisha wanasimamia sheria na ikiwa kutatokea utata Naibu Waziri wake, Harrison Mwakyembe, kwa kushirikiana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Hebert Mrango, wanaweza kuutatua kwani wao ni wanasheria kitaaluma.

Awali akizindua mradi huo, Rais Kikwete aliiagiza wizara hiyo kukishughulikia mara moja kile alichokiita “genge la watu waliojipanga kuidhulumu serikali na wananchi” kwa kuwalipa mabilioni ya fedha makandarasi ambao ujenzi wao wa barabara ni wa kiwango hafifu na cha chini.

Pia aliiagiza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuacha mara moja kugawa maeneo ya wazi na badala yake iyasimamie ipasavyo maeneo hayo yakiwamo yale ya watoto kuchezea kwa kuzuia kabisa ujenzi katika maeneo hayo.

Hata hivyo agizo hilo la Rais Kikwete linaonekana limechelewa sana kwani tayari kuna tuhuma na malalamiko mengi yanayoonyesha kuwa tayari maeneo mengi ya wazi yamekwishagawiwa kwa watu binafsi wenye uwezo kinyume cha taratibu, huku ikielezwa kuwa wahusika bado hawajachukuliwa hatua.

“Tumejitahidi kupandisha bajeti ya barabara mwaka 2006; ilikuwa bilioni 470 na hivi sasa tumepanda hadi trilioni 1.3 ili kuimarisha miundombinu ya barabara za ndani.”

“Wizara na Tanroads sasa msifanye malipo kwa watu ambao ujenzi wao ni wa kiwango cha chini na msipokee barabara ambayo iko chini ya kiwango ili kuongeza ufanisi wa barabara zetu jamani,” alisema Rais Kikwete.

Alisema kukamilika kwa upanuzi wa barabara ya Mwenge hadi Tegeta kutapunguza msongamano jiji la Dar es Salaam ambao kila mara umekuwa ukisumbua wakazi wa jiji.




Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Teresya Huvisa akipata kikombe cha Babu Loliondo.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Abbas Kandoro na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dk Yohana Balelel wakipata tiba ya mchungaji Ambilikile Mwasapile wa kijiji cha Samunge, Loliondo.

Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Steven Wassira (aka Tyson) na Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), Nimrod Mkono

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, akipata kikombe cha tiba ya babu, katika Kijiji cha Samunge, Loliondo wilayani Ngorongoro

Waziri wa Mwasiliano na Ujenzi DOKTA John Pombe Magufuli.International insult to the Doctorate of Philosophy (PhD)?


At least ishu ya "Babu" imetusaidia wengine kufahamu kuwa wengi wa viongozi wetu wana afya zenye mgogoro.Na haihitaji rocket science kuhisi kilichowapeleka kwa "Babu" ni tiba ya maradhi gani...

KWA VIONGOZI WA NAMNA HII TUANDIKE TUMELIWA

3 Apr 2011


Japo mechi ni ngumu sana,na maandalizi yalikuwa duni, historia ya Wana-Msimbazi Simba Sports Club kwenye michuano ya kimataifa ni ya kupigiwa mstari.Na hilo linatupa matumaini ya kuweka historia nyingine kwa kuwafunga hao Wakongomani TP Mazembe na hatimaye kuwavua ubingwa.

Laiti Mazembe wangekuwa na uhakika wa ushindi dhidi ya Simba katika mechi ya awali basi wasingehangaika kutaka kutoa rushwa kwa waamuzi na hatimaye kuwatishia vifo laiti wangemwaga siri hiyo baada ya waamuzi hao kukataa.Habari hiyo nimeisoma HAPA

Kila la heri wana Msimbazi

2 Apr 2011


Baadhi ya magazeti ya Tanzania yanaelekea kutothamini kabisa uwepo wake mtandaoni.Hivi inaingia akilini kweli kwa msomaji kutembelea tovuti ya gazeti na kukutana na "habari mpya" za Februari 3,2011?Hiyo ndio hali niliyokutana nayo kwenye tovuti ya gazeti la Tanzania Daima.

Awali,gazeti hili lilikuwa makini sana katika kuweka habari mpya kwenye tovuti yake lakini sijui "kirusi" gani kimewakumba.Tovuti yao imeendelea kuwakaribisha wasomaji na ujumbe kuwa ipo "off-line kwa matengenezo".Matengenezo gani hayo ya zaidi ya mwezi mzima?

Tatizo la msingi kwa magazeti yetu mengi ni dhana potofu kuwa toleo la mtandaoni ni kama fadhila kwa wasomaji.Pengine dhana hiyo inajengwa na ukweli kwamba matoleo ya mtandaoni husomwa bure,na hivyo kuwafanya wahusika kujiona kama "wanafanya kazi ya Kanisa" (yaani isiyo na ujira).

Sasa,kama wanataka habari zao zisomwe mtandaoni kwa malipo wanaweza kuanzisha huduma ya kulipia (paywall).Lakini kama wameamua kwa hiari yao kuanzisha tovuti na kuweka habari zisomwe bure basi wanapaswa kuwajibika kwa kutuwekea habari mpya kama inavyostahili.


Bwana Alitoa,Bwana Ametwaa.Jina lake lihimidiwe milele.
Sie tulimpenda Adam-hasa kwa makala zake zilizosheheni ufundi mkubwa "wa kuchezea lugha ya Kiingereza" huku akifikisha ujumbe mzito.Lakini sie ni nani zaidi ya Muumba?Yeye Alimpenda Adamu zaidi yetu,na sasa ameamua kumrejesha katika makazi yake ya milele.Adamu ametangulia,na sisi sote tupo njiani.

Pumziko la Milele umpe Ee Bwana na mwanga wa milele umwangazie,astarehe kwa amani,Amina

1 Apr 2011



Hivi msomaji mpendwa umeshwahi kujiuliza ungekuwa unafanya shughuli gani kama sio hiyo unayofanya sasa?Binafsi,ukiweka kando ndoto zangu za kitaaluma,nilikuwa na ndoto nyingine mbili.Moja ni kuwa daktari,ndoto iliyoyeyuka baada ya kupata F kwenye Fizikia na D kwenye Hisabati,japo nilikuwa na A ya Kemia na C ya Bailojia.Nilipofaulu kujiunga na Kidato cha Tano nikaamua kuchukua mchepuo wa Historia,Jiografia na Kiingereza (HGL).

Ndoto ya pili ilikuwa kuwa mtengeneza muziki au prodyuza.Msanii aliyenivutia sana (na anayeendelea kunivutia hadi leo) ni Dr Dre.Bahati mbaya,masuala ya shule yakanielemea zaidi na ndoto hiyo pia ikaenda na maji.Hata hivyo,tangu wakati huo nimekuwa nikiwathamini sana watu wanaofanya kazi kubwa japo haionekani waziwazi na pengine hawafahamiki zaidi ya wanaoonekana.

Chukulia mfano wa prodyuza wa muziki.Wakati takriban dunia nzima inawajua akina Lady Gaga,Beyonce na wengineo,ni watu wangapi wanaowafahamu wanaotunga nyimbo za wasanii hao?Au wataalamu wanao-prodyuzi miziki yao?

Mfano mwingine ni kwenye filamu.Wakati majina yanayovuma ni ya actors na actresses,watengeneza filamu-kwa maana ya waandishi wa script,waongozaji,nk wanabaki kuonekana kwenye shukrani za mwisho wa filamu tu japo wao ndio hasa wanaowawezesha actors na actresses kupata majina na kufanya movies zivunje rekodi za mauzo.

Na unapoangalia runinga,unapata wasaa wa kujiuliza kuhusu watu walio nyuma ya kamera,waandaaji wa kipindi,na wengineo wanaofanya mtangazaji unayemowna kwenye runinga afanye kile unachotarajia kama mtizamaji?

Hizi ndizo sababu zilizopelekea tovuti hii kumsaka Sophia Mwanauta,binti wa Kitanzania anayeishia hapa Uingereza,ambaye ni "moyo" wa utengenezaji wa kipindi maarufu cha Sporah Show,kinachoandaliwa hapa na kurushwa hewani na vituo vya BEN TV ya Uingereza na Star TV ya huko nyumbani.

Historia ya maisha ya Sophia,na namna alivyoingia kwenye fani ya kutengeneza vipindi vya televisheni kwa kamera,na hadi kuimudu fani hiyo,sio tu ya kuvutia bali inatia moyo na kutoa changamoto kubwa kwa Watanzania wengine,hususan akina dada.

Basi nisiongee kwa niaba yake bali nikuachie msomaji mpendwa usome mwenyewe historia ya maisha ya mwanadada huyu kwa maelezo yake mwenyewe.

Kwa jina naitwa Sophia Mwanauta ni mtoto wa kwanza katika familia ya watoto watatu ya Mr & Mrs Mwanauta. Nilizaliwa Arusha, Nimesoma Primary Arusha international school liliyopo Arusha, Secondary nimesoma Arusha Day Secondary school mpaka form four na A-level nilitoka nje ya nyumbani kidogo na kwenda Kampala Uganda katika shule ya St.Marys Kitende. Safari haikuishia hapo nilipomaliza A-level nilirudi nyumbani na kujiunga na Chuo cha Uhasibu Arusha (Arusha School of Accountant) ambapo nilitunikiwa cheti cha Certificate ya Accounting and Finance na baada ya hapo ndio nilikuja London na kufanya Joint Degree ya Accounting and Business of which I finished last year June.


Nini kilimvutia Sophia hadi akaingia kwenye fani yake anayoimudu vilivyo?
Ni swali ambalo nalipata kilaniendapo kufanya kazi. Being behind the camera nikazi amboyo niliipenda sana tangu mdogo i really enjoy it. Nakumbuka wakati na maliza darasa la saba mama yangu aliniandalia mtu wa kuchukaa video katika graduation yangu! Alie kuja kufanya hiyo video alikuwa ni mwanamke alinivutia sana, since nilijiambia ningependa kufanya kazi hiyo nikiwa mkubwa japo wakati huo kazi za camera, haikua kazi ambazo wanawake wengi waliifanya hivyo sikuweza kujitoa directly kwamba hii ndio kazi nataka kuifanya in future ndio maana nilienda kusoma course tofauti kabisa.
Wakati nilipofika London kufanya Degree yangu, sikumoja tulikaa na ndugu yangu Sporah na katika maongezi yetu tulikutana na interest zinazofanana yeye alipenda kuwa Talk Show Host na mimi nilipenda kufanya kazi ya Camera hivyo tukaungana na kuamua kufanya tunachofanya sasa ( THE SPORAH TV SHOW) Kusema kweli at that point sikuwa na any knowledge ya camera so nilichokuwa nafanya nikuwa nyuma ya Ma camera men walipokuja kufanya filming kwenye SPORAH SHOW. Niliendelea hivyo hivyo bila kuchoka mpaka nikajua atleast the basic things to do on a camera, believe me nilikuwa so determines baada ya muda mfupi tu nilijua kipi kinafanya nini kwenye camera. Mwisho nikaamua kwenda kufanya training ndogondogo ilikuelewa kazi vizuri zaidi.
Kwakweli mwanzo ilikua ni ngumu sana maana wote mimi na SPORAH tulikuwa bado tupo University na tulikuwa tunasoma course tofauti kabisa na kazi tunazozifanya lakini kwasababu tulikuwa determided tuliweza.


Sote tunafahamu kuwa kila safari ya maisha ya mwanadamu ni mchanganyiko wa milima na mabonde,vihunzi na tambarare.Je safari ya mwanadada Sophia ilikuwaje?
It was not an easy journey, kwani ilibidi tuachane na mambo yoote ili kufanya kazi, tulipoteza marafiki zetu wakaribu wakati mwingine hata familia zilikua hazituelewi maana hata kupiga simu nyumbani haikua sana kama mwanzo, na hii ilikua napale tulipokua tunakimbizana na shule na hapo hapo kurun a TV SHOW Every Week.
NO, IT WAS NOT EASY AT ALL!! , lakini namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwani tumefika tulipo leo inaonyesha matumaini.


Maisha ni changamoto.Ukipiga hatua moja unapata changamoto ya kupiga hatua zaidi.Lakini kuna changamoto nyingine zinatokana na jinsia,hususan mfumo dume unaopendelea kuangalia fani flani kama ni za kiume pekee.Je ni changamoto zipi anazokabiliana nazo Sophia?

Kwa mimi binafsi kwanza kabisa ni kuwa Mwanamke katika field hii, watu wengi wakikuona umevaa umependeza basi wanaona huwezi kushika Camera. Wakati mwingine nakutana na wanaume ambao wana just basic knowledge kuhusu Filming, lakini mara tu wakikuona we ni mwanamke then wanaona kama huwezi kazi, "Wakati mwingine inauzi sana"
So am always on computer and reading alot of books ili tu kujua mengi kuhusu Filming. Naipenda sana kazi yangu.


Maisha ni malengo.Mtu asiye na malengo ni sawa na mtu asiyejua kwanini yupo duniani.Je Sophia ana malengo gani ya baadaye?

My future plan is to have my own production company one day and be successful in what am doing ,i would love to be recognise internationally.

Je ana ushauri gani kwa akina dada wenzake-hususan wanaokubali dhana potofu kuwa fani flani ni kwa wanaume tu?
Kwanza kabisa ningependa kuwaambia wakinadada waondoe wazo la kuona wanamke ana tofauti na wanaume kwenye kazi kwani binadamu wote nisawa anachoweza kufanya mwanaume ,mwanamke pia anaweza kukifanya. Pia kama ukiweka nia, dhamira na juhudi katika kitu hicho utafanikiwa. (“Think like a queen. A queen is not afraid to fail. Failure is another stepping stone to greatness
The big secret in life is, Whatever your goal, you can get there if you're willing to work.

Tovuti hii inampongeza sana mwanadada Sophia Mwanauta kwa bidii na jitihada zake zinazostahili kuwa mfano wa kuigwa.Pia inamshakuru kwa mahojiano haya.Lakini kabla ya kumaliza,aliulizwa kama ana ujumbe wowote kwa jamii,hususan wapenzi wa Sporah Show,na alikuwa na haya kusema


Asante sana na Msikose kuangalia THE SPORAH SHOW, kila IJUMAA SAA KUMI NA MBILI Jioni na JUMAMOSI SAA SABA Mchana STAR TV IN TANZANIA.
And in EUROPE EVERY MONDAY 9:30PM BEN TV SKY 184.
Pia tembelea tovuti yetu inayopatikana www.sporah.com na www.sporahshow.com.Pia karibuni sana kutembelea blogu yetu inayopatikana www.thesporahshow.blogspot.com.

Join Us On Face Book at:

Check Our Video's on Youtube http://www.youtube.com/user/sporahshow
Asanteni





Moto ulioikumba Tanzania na nchi jirani baada ya kupatikana habari kwamba Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kiluteri Tanzania (KKKT),Ambilikile Mwasapile,anatoa matibabu ya magonjwa sugu ukiwemo Ukimwi,sasa unatarajiwa kuhamia Bara la Ulaya na Marekani.

Kwa mujibu wa Mchungaji Conrad Munro wa Jumuiya ya Makanisa la Kiluteri Duniani,Mchungaji Ambikile,almaarufu kama "Babu",atazuru nchi kadhaa za Ulaya kabla ya kuelekea Marekani kwa huduma za uponyaji.

Akieleza ratiba ya "Babu",Mchungaji Munro alibainisha kuwa ziara hizo za uponyaji zilizopewa jina Jesus Heals,yaani Yesu Huponya,zitaanzia jijini Edinburgh Scotland mnamo April 15,kabla ya kuendelea katika majiji ya London,Manchester na Birmingham.Baada ya hapo,Mchungaji Ambilikile ataelekea Sweden,Ujerumani,Poland na hatimaye Ufaransa,kabla ya kuhitimisha ziara hiyo yake ya kwanza nje ya Tanzania kwa kutembelea Marekani.Mchungaji Munro alitaja baadhi ya majimbo yatakayobahatika kupata huduma ya "Babu" ni pamoja na Texas (ambapo atazuru Houston na Dallas).

Tovuti hii ilipowasiliana na Mchungaji Munro kwa barua-pepe  ili kufahamu utaratibu wa jinsi ya kuhudhuria huduma hiyo ya maombezi,alieleza kuwa wanaohitaji kuhudhuria wanaweza kuwasiliana naye kupitia tovuti hii kuanzia leo April Mosi hadi hapo utapoandaliwa utaratibu maalum wa mawasiliano.Alisisitiza kuwa ni muhimu kwa kila anayetaka kuhudhuria kujiandikisha mapema ili kuwezesha upatikanaji wa ukumbi utakaomudu idadi ya wahudhuriaji.

31 Mar 2011


Makala yangu katika toleo la wiki hii la jarida mahiri la Raia Mwema inazungumzia changamoto zinazoikabili Idara yetu ya Usalama wa Taifa (TISS).BONYEZA HAPA kuisoma pamoja na habari na makala nyingine moto moto ndani ya jarida hili makini kwa habari na uchambuzi.

26 Mar 2011

Habari na picha hii zimetumwa na mdau wa Mbeya yetu,nami naiwasilisha kama ilivyo...with no comment!



Mganga mwingine wa tiba za magonjwa Sugu aliyefahamika kwa jina la Jafar Welino(17) mkazi wa mtaa wa Mianzini Kitongoji cha Mabatini jijini Mbeya ameibuka na kutoa tiba kwa mamia ya wakazi wa jiji la Mbeya na viotongoji vyake.



Umati wa watu ulionekana katika nyumba anayoishi kijana huyo wakisubiri kupatiwa tiba hiyo huku wakiwa na vikombe vyao mikononi. Baadhi ya wananchi waliofika eneo hilo walidai kuwa wamefika hapo kutokana na taarifa za kuwa kijana huyo anatibu magonjwa Sugu bure kama vile ambavyo anatibu Mchungaji mstaafu wa Loliondo Mzee Ambilikile Mwasapila.



Akizungumza kwa niaba ya kijana huyo mama mkubwa wa mganga huyo aliyejitambulisha kwa jina la Edina Sanga alisema kuwa kijana huyo alianza tiba hiyo wiki mbili zilizopita ambapo kabla ya kuanza kutibu alimueleza mama yake huyo kuwa alitokewa na mama yake mzazi a,mbaye kwa sasa ni marehemu akimuelekeza kurithi mikoba yake.



Bi.Sanga alisema kuwa mama yake kijana huyo ambaye kwa sasa ni marehemu alikuwa ni mtu mwenye maruhani ambapo kwa kutumia maruhani hayo alikuwa akitoa tiba kwa wakazi mbalimbali mjini Mbeya.Alisema kijana huyo ambaye wamezaliwa mapacha na dada yake aliyemtambulisha kwa jina la Hadija Welino kwamba yeye anasoma kidato cha Nne katika shule ya sekondari Itende.

Hata hivyo Bi.Sanga alisema kuwa kijana huyo aliitwa katika ofisi ya Ofisa Mtendaji ili kutoa maelezo ya namna ambavyo anaendesha tiba hiyo na kuwa hata hivyo anaendelea kutoa tiba kwa watu kwa kunywa vikombe viwili kwa muda wa siku mbili. Alisema kuwa dawa hiyo aliifuata katika kijiji cha Iyula kilichopo wilayani Mbozi na kuwa mara alipofika alianza kuichemsha na kuwagawia wananchi wanaosumbuliwa na maradhi sugu. Aidha umati wa watu walikuwa wamejipanga katika mistari kusubiri tiba hiyo ambapo


Mwenyekiti wa mtaa wa Mianzini Bi.Elizabethy Mwakabungu aliweka utaratibu wa wananchi kupata tiba ikiwa ni pamoja na kuchangia fedha kidogo kwa ajili ya kununulia kuni za kuchemshia dawa hiyo.Akizungumza na umati wa watu waliokuja kujipatia tiba hiyo Mwenyekiti huyo wa mtaa alisema kuwa kila ambaye atapata kikombe kimoja cha dawa anatakiwa kupata kikombe cha pili siku inayofuata.



‘’Mganga katuagiza kuwa kila anayekunywa kikombe kimoja anatakiwa kunywa kikombe cha pili siku inayofuata…yeyote atakayekunywa hatakiwi kunywa pombe kwa muda wa siku saba,’’alisema Bi. Mwakabungu


Wakipata kikombe

maelekezo ya kufika eneo hilo

Pamoja tunaendeleza kupashana Habari


HABARI NA PICHA: Mbeya Yetu


Kwa kumbukumbu tu,kwa hapa Uingereza msimu wa majira ya joto (summer) unaanza hapo saa 7 usiku.Kama ilivyo ada,inalazimu kusogeza muda kwa saa moja.

Tovuti hii inawatakia nyote Summer Time njema

Jasusi ChatBot

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.