2 Nov 2011

30 Oct 2011




BLOGU HII INAPENDA KUTOA SALAMU ZA HERI YA SIKU YA KUZALIWA KWA JARIDA MWANANA LA RAIA MWEMA AMBALO LILIZALIWA SIKU KAMA YA LEO MIAKA MINNE ILIYOPITA.

BINAFSI,JARIDA HILI NI KAMA SEHEMU YA MAISHA YANGU.TANGU WAHUSIKA WANIPATIE NAFASI YA KUANDIKA KATIKA JARIDA HILO KWWENYE SAFU YA TAIA MWEMA UGHAIBUNI NIMEKUWA NIKISHIRIKIANA NAO HATA NJE YA FANI YA UANDISHI.NILIPOUGULIWA NA MAREHEMU MAMA MWAKA 2008 NA HATIMAYE ALIPOFARIKI,WAHUSIKA WA JARIDA HILI WALIKUWA NAMI BEGA KWA BEGA.

NAKUMBUKA VIZURI SIKU NILIPOZURU OFISI ZAO KWA MARA YA KWANZA NA JINSI NILIVYOPOKELEWA KANA KWAMBA SOTE TULIKUWA TUKITANA HAPO OFINI KILA SIKU YA WIKI.

LAKINI KUBWA ZAIDI NI MCHANGO WA JARIDA HILI KWA JAMII.LICHA YA HABARI ZAKE MAKINI JARIDA LA RAIA MWEMA LIMEJIJENGEA SIFA KUBWA KWA KUWA NA MAKALA ZINAZOANDIKWA KWA UMAKINI WA HALI YA JUU NA LIMEFANIKIWA KWA ASILIMIA 100 KUTOELEMEA UPANDE WOWOTE ZAIDI YA KUSEMA UKWELI NA KUWA SAUTI YA WASIO NA SAUTI.

NAJISIKIA FAHARI KUBWA KUWA MIONGONI MWA WANA-TIMU WA JARADA HILI,NA NI FURAHA KUBWA KUONA RAIA MWEMA LIKITIMIZA MIAKA MINNE HUKO LIKIZIDI KUPAA KWA KUAMINIKA KATIKA JAMII NA KUENDELEA KUUTUMIKIA UMMA KWA UADILIFU.

KWA MARA NYINGINE TENA,NA KWA NIABA YA WASOMAJI WA BLOGU HII,NAOMBA KUSEMA TENA HAPPY BIRTHDAY RAIA MWEMA



Angalizo hili linawahusu wakazi wa Uingereza,kuwakumbusha kurekebisha muda katika saa zao itakapotimu saa nane alfajiri (kurejesha saa moja nyuma).

25 Oct 2011










24 Oct 2011

 Frank Eyembe kutoka Urban Pulse, Lynn Kapinga, Jestina George, Mashel & Musa Sissasi Sarr

 Jestina akienda kupokea Tuzo Baada ya Blog of the year 

 Jestina Akila Pozi na wadau waliokuja kushoo Love

 Jestina Akimwaga speech ya kuwashukuru wote walioweza kumpigia kura

 Jestina akiwa katika pose na Tuzo yake

 Jestina akiwa na mdogo wake Luiza baada ya kupokea tuzo

 Jestina_akiwa_na_marafiki_zake_walikkwenda_kumsupport_kutoka_kushoto_Jacque_Maina,_Jestina_George,_See_Li,_Amina_Mussa_&_Zulfa_Mussa

Zulfa, jestina, Lynn & Frank kutoka Urban Pulse wakifurahia ushindi

Urban Pulse Creative inapenda Kumpongeza dada yetu Jestina George kwa kushinda tuzo muhimu ya Blog ya Mwaka  katika  tuzo za BEFFTA zilizizofanyika Jumamosi tarehe 22 Octoba 2011 ndani ya ukumbi wa Lighthouse, Camberwell jijini London.

Wakati akitoa Hotuba yake Jestina alianza kwa kumshuru Mungu ambae amemwezesha kumpatia uzima, afya njema pamoja na mafanikio  makubwa aliyopata mwaka huu.  Aliendelea kwa kuwashukuru Wazazi wake na mwisho wadau wote ambao walimpigia kura Pia Mabloggers na Tovuti mbalimbali ambazo zimemsaidia kumpigia debe na kuibuka mshindi wa BLOG OF THE YEAR 2011 kutoka kwenye kundi lenye Blog 15 za kimataifa. Hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa Mtanzania kuingia, kushinda na kumfanya kuwa Mtanzania wa Kwanza kupokea tuzo za BEFFTA  kwa upande wa Blogs

Jestina George ameitoa wakfu Tuzo yake kwa dada yake mpendwa Kissa George ambaye hatunaye tena hapa Duniani.

Vazi lake lilibuniwa na KIKI wa Kiki's Fashion Tanzania. Kwa maelezo zaidi na taswira mbalimbali za tukio hili Tembelea http://missjestinageorge.blogspot.com/

Asanteni,

Urban Pulse Creative

--
Jestina George
CEO & Founder - MISS JESTINA GEORGE BLOG
Telephone: +447404332910
Facebook: JestinaGeorge


MIMI BINAFSI NA KWA NIABA YA WASOMAJI WA TOVUTI HII YA KULIKONI UGHAIBUNI TUNAKUPONGEZA SANA MISS JESTINA KWA MAFANIKO YAKO MAKUBWA.HONGERA SANA.
I AM EXCEEDINGLY PROUD OF YOU MY SISTA

Lighting the fuse: Mario Balotelli strikes the ball towards the bottom corner of United's goal
Mario Balotelli akifungua ukurasa wa mabao
No stopping that: United goalkeeper David De Gea attempts to get across but can't prevent the shot going in
Mpende au mchukie lakini Mtaliano huyu mweusi ni moto wa kuotea mbali
Read all about it: Balotelli (left) celebrates by revealing a t-shirt that read 'why always me?'
Kama kawaida yake,Balotelli haishiwi vituko.Hapa akionyesha maandishi "Kwanini Mimi?" 
Super Mario: Balotelli (right) pops up at the far post to score City's second goal
Balotelli akitundika bao la pili

Three is the magic number: Sergio Aguero (left) followed Balotelli onto the scoresheet for the third goal
Aguero akiandika bao la tatu

Kneesy does it: Edin Dzeko (left) bundles in his side's fourth goal from close range
Dzeko akifunga bao la nne
Still scoring: Spanish midfielder Silva slots his finish under De Gea (not seen) in injury time
Silva akitundika bao la tano
That does it: Dzeko rounds off the scoring with a cool finish for City's sixth goal
Dzeko akifunga bao la sita
Let's all do the Poznan: City fans celebrate their stunning win at the home of their rivals
Mashabiki wa Manchester City wakishangilia kipigo ha haja kwa majirani zao wa Manchester United
Plenty to ponder: Sir Alex Ferguson was left to reflect on a devastating defeat
Kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson akiwa hoi
Game for a laugh: City manager Roberto Mancini enjoys his side's thrilling performance
Kocha wa Manchester City Roberto Mancini akifurahia kazi ya vijana wake

CHANZO: DailyMail

23 Oct 2011


Makala hii ilitarajiwa kuchapishwa katika tole la wiki hii la jarida la Raia Mwema.Sina hakika kama ilichapishwa au la kwa viletovuti ya gazeti hilo haipatikani mtandaoni hadi muda huu


Kuna msemo miongoni mwa Wamarekani Weusi kwamba unaweza kumtoa Mtu (Mmarekani) Mweusi kutoka ghetto lakini huwezi kutoa ghetto ndani ya Mtu Mweusi. Kwa kifupi kabisa, ghetto ni makazi ambayo kwa tafsiri isiyo rasmi ni kama ‘uswahilini.’

Kadhalika, katika mazingira yetu tunaweza kabisa kusema unaweza kumtoa mshamba kutoka kijijini lakini huwezi kuondoa ukijijini ndani ya mshamba. Hapa neno mshamba halina maana ya kudharau watu ambao hawakuzaliwa mijini, mie nikiwa mmoja wao.

Wakati nikiwa kijana mdogo kulikuwa na mtizamo kuwa ushamba (kwa maana ya kutozaliwa mjini) ni kama ugonjwa flani hususan kwenye mikusanyiko kama mashuleni au hata vijiweni (mijini).Ninakumbuka wakati ninasoma Tabora Boys’ High School, rafiki yangu mmoja aliomba nimpatie albamu yenye picha zangu.

Nyingi ya picha hizo, kama si zote, nilipiga katika mjini mdogo wa Ifakara, ambapo katika suala la mjini na kijijini, inaangukia kundi la pili. Si kwamba Ifakara ni kijiji au sehemu iliyojaa mashamba lakini pia Ifakara si mjini kama Dar es Salaam. Kwahiyo kwa minajili ya makala hii, tuafikiane kuiita Ifakara kijijini.

Basi picha hizo kwa rafiki yangu huyo ambaye sio tu alikulia mjini bali pia alizaliwa “hospitali ambayo kila mtoto wa mjini kazaliwa,” (nikimaanisha hospitali ya Ocean Road) zilizua vicheko miongoni mwa wanafunzi wengine ambao walikuwa wanatokea Dar. Sikujilaumu kwa uamuzi huo wala sikuona aibu. Kwako ni kwako hata kukiwa porini.

Nilifika Dar kwa mara ya kwanza nilipokuwa kidato cha pili (katikati ya miaka ya 80).Nakumbuka jinsi lafidhi yangu ya Ifakara ilivyogeuzwa chanzo cha vichekesho kila nilipokwenda kwenye magenge ya maongezi (vijiweni).Lakini sikuona aibu kwa sababu lafidhi ya ‘kishamba’ si ugonjwa.

Nilipokuja Uingereza mara ya kwanza nikakumbana na tatizo kama hilo, ambapo lafidhi ya Kiingereza change ilikuwa imetawaliwa sana na Kiswahili, kiasi kwamba mara nyingi nilipoongea na wenyeji wa hapa waliuliza mara mbili mbili nilichokuwa nakiongea. Miaka 10 baadaye, lafidhi yangu haijabadilika sana.

Ahueni niliyopata kwa huku Scotland ni ukweli kwamba lafidhi ya Kiingereza cha Waskochi inawasumbua hata Waingereza wenzao wa sehemu nyingine (kwa mfano England).Lakini kikubwa zaidi kwa hapa ni ukweli kwamba lafidhi yako ni kitu cha kujivunia, ni sawa na utambulisho wako.

Msimamizi  (Supervisor) wangu wa kwanza wa kozi yangu ambaye alikuwa mzaliwa wa Wales (na hivyo kujikuta anahangaika na lafidhi za Waskochi) alinitia hamasa kwa maelezo haya, “ukiongea huku una lafidhi flani basi inamaanisha una lugha au utamaduni zaidi ya mmoja, na hiyo ni faida kwako.”

Lengo la makala hii si kuchambua lafidhi au lugha bali kuzungumzia nafasi ya tabaka la kati ambalo kwa kiasi kikubwa linapatikana mijini, hususan jijini Dar. Katika jamii ya kinadharia, tunaweza kuwa na matabaka makuu matatu: tabaka la juu (Upper Class),tabaka la kati (Middle Class) na tabaka la chini (Lower Class).Kwa kifupi, kinachotenganisha matabaka hayo ni nguvu yao katika jamii (au power kwa kimombo).Kwa mantiki hiyo, tunaweza kuigawa jamii katika makundi ya ‘wenye nguvu’ (the powerful) na ‘wasio na nguvu’ (the powerless).  

Ugumu uliopo katika kuielezea dhana ya matabaka katika jamii inatokana na ukweli kwamba takriban kila fani inayaangalia matabaka kwa mtizamo wake. Japo kuna mwingiliano, lakini dhana ya matabaka inaweza kueleweka tofauti kati ya fani ya siasa, uchumi, elimu jamii (Sociology), nk. Hapa nitaizungumzia dhana hiyo kwa mtizamo wa jumla pasipo kuelemea fani moja.

Ukiingia kwa undani sana utakuta kati ya matabaka hayo matatu kuna matabaka madogo madogo kwa namna hii: tabaka la kati la juu (Upper Middle Class), tabaka la kati la chini (Lower Middle Class), na tabaka la wafanyakazi (Working Class).Labda nitumie mchoro kama hivi: Tabaka la JuuTabaka la Kati la JuuTabaka la Kati la ChiniTabaka la WafanyakaziTabaka la Chini. Hii ni kwa mujibu wa mchanganuo wa kitaaluma wa matabaka wa karibuni zaidi (mwaka 2005) na ni kwa mujibu wa mtizamo mmoja wa kitaaluma wa Marekani.

Ili tuelewane, ni muhimu kuzingatia tahadhari niliyoitoa awali kuwa mgawanyiko huu ni wa jumla-jumla kwani kuna tofauti za kimtizamo miongoni mwa wachambuzi, fani na kanuni (theories) zinazohusu mada ya matabaka.

Pengine katika kurahisisha maelezo, mfano mwepesi ni wa kijana kama mie niliyekulia kijijini, mtoto wa mkulima, kisha nikaja mjini kupata elimu ya juu, na hatimaye kupata kazi. Ukiangalia mlolongo huo unaweza kubaini kuwa, kwa namna flani, nimetoka tabaka la chini na kuingia tabaka la kati. Pengine nikagombea ubunge (hapana, sina wazo hilo) nikamudu kuingia tabaka la juu.

Kwanini tabaka la kati lina umuhimu mkubwa katika mabadiliko ya jamii? Jibu jepesi ni kwamba tabaka hilo linatarajiwa kuelewa zaidi masahibu yanayolikabili tabaka la chini. Yaani kwa kutumia mfano wetu wa mie niliyetoka kijijini, sio tu ile lafidhi yangu iliyonifanya nichekwe mjini bali pia uzoefu wangu wa kijijini kuulinganisha na wa mjini unaweza kuniweka katika nafasi nzuri zaidi ya kuwa na msaada wa namna flani kwa ‘tabaka la kijijini’ (la chini).

Lakini tatizo lililopo katika jamii yetu (na hii ni kwa jumla-jumla) ni tabaka hilo la kati kutamani kuwa tabaka la juu, na hapo hapo kulipuuza tabaka la chini. Kwa kutumia mfano, kijana aliyetoka kijijini na kuwaacha wazazi wake wakihangaika na ufukara uliozoeleka kwenye tabaka la chini, anapata ajira baada ya kuhitimu masomo, na anajaribu kuishi maisha kama yale ya vigogo au watoto wao.

Ofkoz, Wanasema ukienda Roma inabidi uishi kama Warumi. Lakini hiyo haimaanishi usahau ulipotoka. Hapa ninamaanisha kuwa hakuna ubaya kwa kijana kutoka kijijini kujaribu kuendana na maisha ya ‘kimjini’ bali tatizo ni pale anaposahau ‘wajibu’ wake (ambao si wa lazima) wa kutumia nafasi aliyonayo kuhamasisha au kuchangia kuboresha tabaka wanaloishi wazazi, ndugu, nk huko kijijini.

Naomba pia tuelewane kuwa hapa ninatumia ‘umjini’ kama aina ya maisha ya jumla (kinadharia na wakati mwingine kiuhalisia) ya wakazi wa mjini. Yaani katika dhana ya kufikirika, chaguo la makazi kwa tabaka la juu ni mjini (japo haimaanishi kila anayeishi mjini yupo kwenye tabaka hilo).

Kuna wenzetu ambao hawajawahi kufika kijijini, na kwao Tanzania ni ile wanayoishi na kuiona mijini. Lakini kama ilivyo kwa nchi nyingi masikini, idadi kubwa ya wananchi wake wanaishia vijijini. Ukiwa umezaliwa na kukulia Masaki, Upanga, Mbezi Beach, nk na sehemu yako ya kazi ikawa Mjini Kati na maeneo kama hayo (na ikatokea hajawahi kufika kijijini) basi inaweza kuwa vigumu kwako kuielewa ‘Tanzania nyingine’ huko vijijini.

Wakati nipo huko nyumbani, kila mara niliposafiri kati ya Dar na Ifakara nilikuwa ninajaribu kuangalia namna mandhari na pengine hali ya mjini ‘inavyoyeyuka’ kadri safari ya kuelekea ‘kijijini’ ilivyokuwa inashika kasi. Na Nilipofika kijijini tofauti zilikuwa ni za wazi. Kwa mfano, wakati vitu kama magari na runinga vilionekana vya ‘kawaida’ kwa kijijini viliangaliwa kwa mtizamo ‘zaidi ya wa kawaida.’

Lakini pia hata katika suala la tabia za kibinadamu kulikuwa na tofauti. Kwa mfano, wakati mwanamke kuvaa suruali mjini halikuwa jambo ‘kubwa, kwa kijijini lingeweza kuzua picha tofauti. Ninasisitiza, huu ni mtizamo wa jumla na haimaanishi hali iko hivyo kila kijiji.

Wakati Tanzania yetu inahitaji mno maendeleo na kuondokana na umasikini (hususan huko vijijini), tabaka la kati lingeweza kuwa kiungo na nyenzo muhimu kwa, aidha kushiriki au kuunga mkono harakati za tabaka la chini, au kwa vile lina ukaribu na tabaka la juu, kujaribu kushawishi-au hata kuilazimisha- tabaka la juu liangalie na/au kushughulikia matatizo ya tabaka la chini.

Mabadiliko tunayoshuhudia yakiendelea kutokea sehemu mbalimbali duniani (kwa mfano nchini Tunisia, Misri, Libya, nk) yamechangiwa zaidi na muungano wa nguvu za matabaka haya mawili-la kati na la chini. Kwa bahati mbaya (au makusudi) kwa kiasi kikubwa tabaka la kati kwetu limekuwa likitamani zaidi kuwa tabaka la juu (kitu ambacho si kibaya endapo kitasaidia kulikwamua tabaka la chini) na kulisahau tabaka la walalahoi.

Nimalizie kwa kukiri kuwa ninafahamu mada hii inaweza kuleta mkanganyiko wa aina fulani lakini lengo ni kuhamasisha tabaka la kati kuunganisha nguvu na tabaka la chini katika kuikwamua Tanzania yetu kutoka kwenye lindi la umasikini (na ufisadi) na hatimaye kila Mtanzania aone fahari ya kuwa mwananchi wa Tanzania.

Inawezekana, timiza wajibu wako

Barua-pepe: [email protected]
Blogu: www.chahali.com  


Kwa mnaojifanya kusahau: pichani juu ni Nduli Idi Amin akimtambuliha swahiba wake Gaddafi ka makamanda wa jeshi la Uganda,Machi mwaka 1974.Gaddafi alikuwa nchini humo kumkabidhi Amin ndege za kivita ambazo miaka minne baadaye zilitumika kwenye uvamizi wa Amin nchini mwetu (akisaidiwa zaidi na Gaddafi).Halafu Gaddafi huyuhuyu anastahili kufanyiwa maombolezo!!!!????

Ukiishi kwa upanga utakufa kwa upanga,na picha na video zifuatazo zinaonyesha dakika za mwisho za dikteta huyo  kabla ya kupelekwa mbele ya haki


















Kwa Freestyles za wiki zilizopita bonyeza hapo kulia kwenye nembo ya Cheusi Dawa TV (FID-Q)

Jasusi ChatBot

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.