Sababu
Tisa kwanini CCM itashinda katika Uchaguzi Mkuu Jumapili hii, Oktoba 25
Na
January Makamba
Tarehe 25 mwezi huu Oktoba, Watanzania
watapiga kura kumchagua rais wao wa tano, wabunge na madiwani. Uchaguzi Mkuu wa
mwaka huu umekuwa na msisimko mkubwa zaidi tangu kuanzishwa kwa mfumo wa siasa
za vyama vingi mwaka 1995. Mengi yamendikwa kuhusu uchaguzi huu, hususan
kutokana na hisia kwamba safari hii Upinzani una nafasi ya kukiondoa madarakani
moja ya vyama vikubwa na vyenye muundo bora barani Afrika, chama tawala, Chama
Cha Mapinduzi (CCM). Matukio mbalimbali kuelekea uchaguzi huo yameleta shauku
inayoweza kutengeneza hadithi ya kusisimua.
Nikiwa sehemu ya Timu ya Kampeni ya CCM,na
kwa manufaa ya wote ambao wangependa kuwa na mtizamo tofauti, ninatoa sababu 9
kwanini tunaamini kuwa CCM itaibuka mshindi na kwanini Dkt John Pombe Magufuli
atakuwa Rais ajaye wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
1.
Ugombea ‘fyongo’ (flawed) wa Edward Lowassa
Ilishabainika kuwa uchaguzi huu ungekuwa mgumu kwa CCM
bila kujali nani angekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Upinzani. Lakini matokeo
ya uchaguzi huu yalielemea upande wa CCM pale Upinzani ulipomchagua Lowassa
kuwa mgombea wao. Ni rahisi kwa CCM kuchuana na Lowassa kuliko laiti mgombea wa
Upinzani angekuwa Dkt Wilbrod Slaa, ambaye ndiye aliandaliwa kuwa mgombea kabla
ya ‘ukusukumwa kando’ na nafasi hiyo kupewa Lowassa. Slaa alikuwa na uadilifu
katika maeneo mengi, na aliaminika. Kwa Lowassa, ni vigumu na inanyima raha
kuchuana na mfumo aliyoshiriki kujenga na ambao ulikuwa sehemu ya maisha yake
hadi Agosti mwaka huu alipohamia Upinzani. CCM ilikuwa na nafasi ya kumpitisha
Lowassa kuwa mgombea wake wa nafasi ya urais. Hatukufanya hivyo kwa sababu
rahisi tu kwamba ingekuwa vigumu mno kumkabidhi kwa wananchi mgombea wa
matarajio ya baadaye ambaye ni kiashirio cha yale yasiyowaridhisha wananchi
kuhusu CCM. Kuna wanaoamini kuwa uchaguzi huu ni mgumu kwa vile Lowassa ndiye
mgombea wa Upinzani. Sisi twaamini kwamba uchaguzi huu ungekuwa mgumu mara kumi
zaidi laiti Lowassa angekuwa ndiye mgombea wetu.
2.
Upinzani umesalimisha ajenda yake ya
kupinga ufisadi
Kipindi cha miaka 10 iliyopita kimetawaliwa na matukio
mbalimbali ya kuwabainisha mafisadi na kuwachukulia hatua. Vyombo vya habari,
taasisi za kiraia na Bunge vimefanya kazi nzuri kushughulikia suala hilo. Rais
Jakaya Kikwete ameweka historia kwa kuamuru ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu
wa Hesabu za Serikali kupatikana kwa wananchi na kujadiliwa kwa uwazi Bungeni.
Waziri Mkuu aliyekuwa madarakani, si mwingine bali Lowassa, alijiuzulu kwa
sababu ya kashfa ya rushwa. Mawaziri kadhaa walitimuliwa kazi na manaibu waziri
wawili wanatumikia vifungo jela. Huu ni uwajibikaji wa hali ya juu japokuwa
kuna wanaoweza kudhani ni hatua ndogo. Umma umeamka.
Upinzani ulijenga hadhi yake kwa kuongelewa sana
kuhusu ufisadi. Kilele cha Upinzani kilijiri mwaka 2007 katika mikutano mkubwa
wa hadhara ambapo walitangaza majina 10 ya watu waliowaita mafisadi wakubwa
zaidi, katika kilichokuja kufahamika kama Orodha ya Aibu (List of Shame).
Lowassa alikuwa kinara kwenye orodha hiyo.
Ilitarajiwa kuwa Uchaguzi Mkuu huu uwe ‘hukumu’ kwa
CCM kuhusu ufisadi. Upinzani ulitarajiwa kuitumia ajenda ya ufisadi ambayo
inawagusa watu wengi. Lakini ghafla, kwa kumteua mwanasiasa, ambaye kwa jitihada
zao wenyewe Wapinzani, amefahamika zaidi
kwa ufisadi, iliwalazimu kuzika ajenda hiyo. Kilichofuata baada ya hapo ni
kituko na kichekesho. Wale mashujaa wa mapambano dhidin ya ufisadi walijikuta
wakilazimika ‘kulamba matapishi yao.’ Wengi wao waliokuwa mahiri katika
mitandao ya kijamii walilazimika kufuta historia ya baadhi ya waliyoyaandika
mtandaoni walipokuwa wakikemea ufisadi, lakini si kabla ya maandiko yao kunaswa
kwa ‘screenshots.’ Ulikuwa ni ukweli wa kushangaza. Ni Dkt Slaa na Professa
Ibrahmi Lipumba, viongozi muhimu wa Upinzani tangu miaka ya Tisini, walioamua
kujiuzulu nyadhifa zao kwa kukerwa na uamuzi wa Upinzani kumpokea Lowassa.Matokeo
yake, Upinzani walijikuta wakichana kadi yao turufu- ajenda dhidi ya ufisadi.
Ni nadra kwao kuongelewa suala hilo, na wanapojaribu kufanya hivyo, ni kwa
kujitetea tu.
Jioni moja mwezi Agosti, nilimwona Mbunge wa Upinzani,
Peter Msigwa, katika mdahalo kwenye runinga. Aliongelea kitu ambacho
kilijumuisha mtizamo wa Upinzani kwa muda huo, na kiliniacha hoi. Alisema,
kabla hawajampokea Lowassa, walifanya utafiti wao, na “ufisadi sio ajenda
muhimu kwa taifa letu.” Alidai kwamba wenye ushahidi kuhusu ufisadi wa Lowassa
wajitokeze hadharani.Alionekana kusahau kuwa walipomtaja Lowassa katika List of
Shame, walitangaza hadharani kuwa wana ushahidi. Muda si mrefu uliopita, CCM
ilikuwa ikiwaomba Wapinzani kuleta ushahidi kila yalipojitokeza madai ya
ufisadi dhidi ya viongozi wa chama na serikali allegations were leveled against
the party and its leaders. Haikupendeza kuingiza hoja za kisheria katika
masuala ya kimaadili. Upinzani sasa umeamua kwa hiari yao kuchukua ‘chembemoyo’
wakati ambapo viongozi wa CCM wanaongelea ufisadi kwa ujasiri na msisitizo.
Uchaguzi huu Mkuu ni muhimu sana kwa Upinzani.
Kimsingi, unaweza kuwa na madhara makubwa. Endapo watashindwa hapo Jumapili, ‘watapotea’
kwa muongo mzima ujao. Ndio maana inashangaza kuona wamechukua uamuzi wa
kukimbia ajenda yao kuu ya kupambana na ufisadi
ambayo iliwatambulisha na kuwaimarisha. Na kuwapa nguvu kukubalika kwa
wapigakura. Kuona wanatarajia kushinda ni miujiza mkubwa.
3.
Mabadiliko ambayo kamwe huwezi kuyaamini
Ukizinguka jijini Dar es Salaam utakutana na mabango
ya Upinzani yanayodaia “Ni Muda wa Mabadiliko.” Lakini ukisikiliza mikutano yao
ya kampeni, ni porojo na hasira tu. Wasemaji wakuu katika mikutano hiyo ni Waziri
Mkuu wa zamani na kada wa muda mrefu wa CCM, Frederick Sumaye na Lowassa
mwenyewe. Kwa pamoja, wamekuwa wana-CCM na katika nyadhifa za juu serikalini kwa zaidi ya miaka 50. Kwa
hiyo inasikitisha kusikiliza kauli zao – zinazokosa imani na kupalizwa na aibu
– wakipambana na mfumo walioshiriki kujenga, uliojenga tabia zao za kisiasa, na
ambao walikuwa wakiusifu miezi mwili tu iliyopita.
Kutokuwa wakweli na kuweka mbele maslahi binafsi
kwawatuma kudai kuwa CCM haijafanya chochote katika miaka miaka 50 iliyopita.
Inapotokea viongozi wawili waandamizi wa chama na serikali kwa zaidi ya miaka 30, wote wakiwa walioshika
Uwaziri Mkuu, kudai kuwa hakuna chochote kilichofanyika katika miaka 50
iliyopita, wajihukumu wenyewe. Si kwa muundo, mwonekano au ukweli, wanasiasa
hao wanasimamia mabadiliko. Yayumkinika kuhitimisha kuwa mabadiliko wanayoongelea
ni kuhusu kubadili chombo kilichowaingiza madarakani, mabadiliko ya sare tu za
chama. Hawana habari na mabadiliko ya maisha ya wananchi wa kawaida. Wapigakura
wameanza kushtukia ukweli huo.
4.
Migogoro na mkanganyiko ndani ya UKAWA
Huko nyuma, kila ulipojiri uchaguzi, Upinzani
ulijaribu kuunganisha nguvu ili kuing’oa CCM madarakani.Na kila mara jitihada
za ushirikiano zilishindikana. Mwaka 2014, mjadala kuhusu Katiba Mpya kuataka
serikali tatu uliwapatia ajenda ya kuwaunganisha pamoja. Kisha wakaamua
kutafsiri ushirikiano huo kuwa wa kisiasa, wakaafikiana kusimamisha mgombea
mmoja katika nafasi ya urais na kugawana majimbo.
Baada ya hapo kukajitokeza unafiki wa wazi. Kuonyesha
kuwa matamanio yaliwekwa mbele ya kanuni zilizopatikana kwa jitihada ngumu,
chama ambacho jina lake linajumuisha maneno ‘demokrasia’ na ‘maendeleo’ kilitemea
mate mchakato wake chenyewe wa kidemokrasia na mshikamano kupata mgombea wake
wa urais, na kukurupuka kumpitisha kada wa muda mrefu wa CCM ambaye jitihada
zake kuwania urais kwa tiketi ya chama hicho tawala ziligonhga mwamba.
Waliamini kwamba uamuzi wa Lowassa kuhama CCM
ungekiathiri chama hicho tawala, wakitarajia vigogo kadhaa wangemfuata huo
Upinzani. Badala yake, ujio wake huko ukapelekea kuondoka kwa wanasiasa wawili
waliokuwa nguzo muhimu kwa Upinzani, Dkt Slaa na Prof Lipumba.Kadhalika,
wanachama wengine muhimu waliohama na kujiunga na chama cha ACT- Wazalendo,
ambacho hakikujiunga na UKAWA.
Kana kwamba hiyo haitoshi, makubaliano ya UKAWA
kusimamisha mgombea mmoja kila jimbo
yalikumbwa na mushkeli katika majimbo kadhaa na kupelekea malalamiko
yaliyosababisha ugumu katika kampeni za Lowassa.
Huko Masasi, mgombea mwenza wa Lowassa, Juma Duni,
alilazimika kuokolewa jukwaani baada ya waliohudhuria mikutano wake wa kampeni
kupiga kelele kuwa wataipigia kura CCM. Katika jimbo la Nzega, Lowassa
alilazimika kuendesha ‘kura ya sauti’ kuwauliza waliohudhuria mikutano wake wa
kampeni wanamhitaji mgombea gani kati ya wawili wa UKAWA waliokuwa wanachuana.
Mpango mzima wa ushirikiano miongoni mwa vyama vinavyounda UKAWA umekwenda
mrama.CCM sasa ipo katika nafasi nzuri ya kujinyakulia majimbo ambayo
vinginevyo yangekwenda kwa wagombea wa Upinzani.
Lakini kilele cha unafiki wa UKAWA ni hiki. Umoja huo
uliundwa ili kutetea Katiba Pendekezwa iliyoshauri muundo wa Muungano wa serikali
tatu. Kanuni hiyo ya msingi iliwekwa kando pale UKAWA walipomchagua mgombea wao
wa tiketi ya urais, Lowassa, ambaye alikuwa mtetezi mkubwa wa muundo wa
Muungano wa serikali mbili. Kwa wengi wasioendeshwa na propaganda, uamuzi wa
kutelekeza suala la msingi lililopelekea umoja wa vyama hivyo, kwa ajili tu ya
imani ya kufikirika ya kushinda urais, yaashiria uchu wa madaraka na sio
mabadiliko yanayohubiriwa kwa wananchi.
5.
Lowassa kushindwa kufanya kampeni nchi
nzima
Lowassa anaonekana kutokuwa na uwezo wa kusafiri kwa
urefu na upana wa Tanzania kufanya kampeni. Mara nyingi amekuwa akitumia
usafiri wa anga kwenda mikoani ambako hufanya mikutano mikubwa kwenye makao
makuu ya mikoa, kutembelea majimbo mawili au matatu ya jirani kwa helikopta, na
kurejea jijini Dar es Salaam. Huko Tanga, kwa mfano, alifanya kampeni katika
majimbo matatu tu kati ya tisa mkoani humo. Mkoani Ruvuma, alifanya kampeni katika
majimbo matatu kati ya tisa, Kigoma majimbo mawili kati ya manane, na Kagera
majimbo matatu tu.
Kinyume chake, mgombea wa CCM, Magufuli amekuwa
barabarani tangu Agosti 23, huku akipumzika kwa siku tatu. Anatumia usafiri wa
gari, akitembelea kijiji baada ya kijiji, na kufanya mikutano kati ya minane
hadi 12 kwa siku. Aina hii ya kufanya kampeni ‘kwa rejareja’ inabaki kuwa nguzo
pekee ya kujihakikishia ushindi kwenye uchaguzi mkuu nchini Tanzania, hususan
katika maeneo ya vijijini ambayo usikivu na kuonekana kwa vyombo vya habari ni
mdogo. Wakati Lowassa anavutia wahudhuriaji wengi katika mikutano yake katika
miji mikubwa, Magufuli anajipatia wahudhuriaji wengi katika kila kona ya
Tanzania. Kama idadi ya wahudhuriaji katika mikutano hiyo ya kampeni
inamaanisha wingi wa kura, basi kwa hakika CCM itashinda. Lakini tofauti na
Upinzani, CCM haidanganyiki na wingi huo wa wahudhuriaji katika mikutano ya
kampeni. Rekodi ya mahudhurio makubwa ilikuwa ikishikiliwa na Agustino Lyatonga
Mrema, mgombea maarufu wa kiti cha urais kwa tiketi ya Upinzani mwaka 1995 (ambaye
pia alijiunga na Upinzani akitokea CCM). Hata hivyo alishindwa kwenye uchaguzi
huo. Sie twategemea kitu kingine.
6.
Mfumo imara wa CCM katika uhamasishaji
kuanzia ngazi ya chini kabisa.
Katika Tanzania, vyama vichache mno vinavyoweza
kuchuana na uwezo wa CCM kuhamasisha wananchi. Wakati Wapinzani huhadaiwa na
‘mahaba’ wakati wa kampeni za uchaguzi, mahudhurio makubwa kwenye mikutano yao
ya kampeni na vichwa vya habari magazetini, CCM hutumika nguvu yake ya kimuundo
na kuwasha ‘mashine zake za kisiasa,’ kuanzia ngazi ya mtaa (ujumbe wa nyumba
kumi) kwa nchi nzima. Kimuundo, jumiya ya wanawake wa CCM (UWT) pekee ni kubwa
kuliko Chadema, chama kikuu cha upinzani. CCM Haihitaji kusafiri ili kufanya
kampeni. CCM ipo kila mahala, ikifanya kampeni katika makundi madogo, vijijini
na mitaani, kila siku na mbali ya upeo wa vyombo vya habari. Kwa wanaofahamu
muundo wa chama hicho, ushindi kwake si jambo la kushangaza.
Kwenye miaka ya 1950s, wakati wa harakati za kusaka
uhuru kutoka kwa mkoloni, uwezo wa TANU kuhamasisha ulikuwa nguzo muhimu kwa
Tanganyika kupata uhuru wake.CCM imerithi vinasaba vya TANU. Mwalimu Nyerere
aliijenga CCM kuwa imara kwa nyakati kama hizi. Mwaka jana, huku umaarufu wake
ukiwa umepungua, CCM ilimudu kushinda uchaguzi wa serikali za mitaa kwa
asilimia 80 dhidi ya umoja Huohuo wa Upinzani inaokabilina nao katika uchaguzi
huu Mkuu.Tofauti haipo kwenye nini kinachoonekana kwenye vyombo vya habari au
mitandao ya kijamii bali jinsi gani makada wa chama hicho tawala walivyofanya
uhamasishaji katika kila mtaa na kijiji. Uchaguzi huo wa serikali za mitaa,
ambao hufanyika mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mkuu, hutoa dalili nzuri kuhusu
matokeo ya uchaguzi mkuu.
7.
Umahiri wa Dkt Magufuli
Mwaka jana, baadhi ya waandishi wa habari walikiri
kwamba ni vigumu mno kumshambulia na kumshinda Dkt Magufuli. Ana rekodi imara
ya usafi, uchapakazi na anayetaka kuona matokeo sahihi. Hajawahi kuvutiwa na
harakati za kisiasa, na ilikuwa mshangao alipotangaza kuwania urais. Na
alipotangaza, hakufanya mbwembwe wala kijitangaza kwenye vyombo vya habari.
Alizingatia kanuni za chama kwa ukamilifu. Dkt Magufuli analeta kumbukumbu za
mgombea mwingine aliyekuwa hajulikani mwaka 1995 - Benjamin Mkapa. Wakati umaarufu wa CCM ukiwa
chini, huku ikikabiliwa na upinzani kutoka kwa Naibu Waziri Mkuu aliyehama
kutoka chama hicho tawala, CCM ilimchagua turufu yake ambayo ilikuwa ngumu
kuikabili.Miaka 20 baadaye, ikikabiliwa na upinzani wa Waziri Mkuu maarufu wa
zamani aliyehama chama hicho na kujiunga na Upinzani, CCM imefanya tena ‘vitu
vyake.’ Siku zote, CCM hujua ‘kufanya pigo la haja.’
8.
Ufanisi wa CCM katika maeneo ya vijijini
Mimi ni Mbunge wa jimbo lisilo mjini, lenye idadi ya
wastani ya wapigakura. Mwaka 2010, katika uchaguzi ulionekana kuwa mgumu, CCM
ilishinda jimbo langu kwa asilimia 80., na kitaifa kwa asilimia 61. Hivi sasa,
tunatarajia ushindi wa CCM kuwa wa asilimia 90 hivi. Tanzania ina majimbo kadhaa yaliyo kama jimbo langu.
Upinzani hupenda kuwapuuza wananchi katika majimbo yasiyo ya mijini, kama jimbo
langu, kwa kudai kuwa wanaichagua CCM kutokana na ujinga wao. Wasingeweza
kukosea zaidi ya hivyo.
Popote walipo, watu hupiga kura kulingana na mahitaji
yao. Mwaka 2000, vijiji vinne tu katika jimbo langu ndivyo vilikuwa na umeme.
Leo, vijiji 44 vina umeme. Japo hatujaweza kutoa huduma zote kwa kiwango cha
kumfurahisha kila mtu, lakini hali halisi yaonyesha wingi wa wanafunzi mashuleni,
walimu zaidi, madaktari na manesi zaidi, zahanati nyingi zaidi zimejengwa,
huduma za mawasiliano ya simu zinapatikana kwa wingi, barabara nyingi za lami,
nk. Porojo kuwa hakuna kilichofanyika Kwahiyo wapigakura wasiichague CCM
haieleweki katika maoneo hayo ambay kimsingi ndiyo yenye wapigakura wengi. Na
wagombea wa CCM wanaposema watafanya zaidi ya waliyokwishafanya, kwa kuzingatia
mafanikio yaliyokwishapatikana, wananchi wanawaamini. Hotuba za kampeni ni
mwonekano na mantiki.
Chaguzi sio kuhusu ahadi tu bali jinsi gani ahadi hizo
zitaandaliwa na kutekelezwa. Jukwaa ambalo kila chama kitanadi ajenda zake za
uchaguzi hujengwa wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama husika. Yahitaji mtu
kuangalia tu uzinduzi wa kampeni za za Lowassa na Magufuli. Lowassa aliongea
kwa dakika 9 tu - akiahidi, pamoja na
mambo mengine, kuwaachia huru wabakaji (sio kama ninazusha hili) wanaotumikia
vifungo vyao na watuhumiwa ugaidi wanaosubiri kesi zao. Bila kujali alikuwa na
malengo gani wakati anatoa ahadi hizo, makosa hayo hayastahili msamaha wa
rais. Kwa upande wake, Magufuli aliongea
kwa dakika 58, akielezea kwa undani ajenda za maendeleo katika nyanja za elimu,
ajira, afya, ufisadi, huduma za maji, na miundombinu. Kuanzia hapo, kwa muda
wote wa kampeni, mwenendo umekuwa hivyo, kwa uzito wa ujumbe kwenye hotuba zake
na muda wa kuhutubia
Wanaohudhuria mikutano ya Dkt Magufuli huondoka katika
mikutano hiyo wakiwa na matumaini na wenye nguvu. Kwa upande mwingine,
wahudhuriaji katika mikutano ya Lowassa huondoka wakiwa wamekanganywa. Siku ya
kupiga kura, wapigakura wanamkumbuka jinsi mgombea alivyoonekana na
alivyoongea, na jinsi walivyojisikia walipomwona jukwaani. Kwa kigezo hiki, ni
bora ningekuwa upande wa Magufuli.
9.
Uongo, uongo na takwimu
Tanzania haina utamaduni wa kura za maoni kupima
nafasi za wagombea katika uchaguzi. Tuna utaratibu wa muda mrefu wa kupata
maoni ya wananchi katika maamuzi makubwa ya kisera – kuingia mfumo wa vyama
vingi vya siasa, marekebisho ya Katiba, na kadhalika. Mwaka 2005, kulifanyika
kura ya maoni, iliyobashiri ushindi mkubwa kwa CCM. Na kwa hakika, CCM
ilishinda kwa asilimia 80. Mwaka 2010, kura ya maoni iliyoendeshwa na kampuni
ya Ipsos-Synovate iliashiria kuwa idadi ya kura za CCM ingepungua hadi kufikia
asilimia 61. CCM ilipinga matokeo ya kura hiyo ya maoni ikidani kuwa yalikuwa
kiasi kidogo sana. Matokeo ya uchaguzi huo yalikuwa kama yalivyotabiriwa katika
kura hiyo ya maoni. CCM ilipata asilimia 61 ya kura zote.
Hivi karibuni, kura mbili za maoni zilichapishwa. Zote
zilifanywa na taasisi huru zinazoheshimika. – Twaweza and Synovate-Ipsos tena- zote
zikijihusisha na utafiti wa kusaka maoni. Taasisi mbili tofauti, zilizotumia
mbinu tofauti za kufanya utafiti, katika nyakati tofauti, matokeo yaleyale. CCM
itashinda kwa asilimia 62 ya kura zote.
Inaruhusiwa, na kwa
yumkini ni jambo zuri, kupingana na sababu hizi tisa za kwanini CCM itashinda.
Lakini namba zina tabia ya ukandamizaji. Ndio mwelekeo wa kura huwezi
kubadilika. Lakini kwa kuzingatia yote yaliyokwishaongelewa kuhusu kinachodaiwa
kuwa ufuasi mkubwa kwa Upinzani, basi muda huu ingetarajiwa tuwa tunajadiliana
kuhusu ufuasi wa wengi kutoka Upinzani kuelekea CCM– na sio kutarajiwa ufuasi
wa wengi kutoka CCM kuelekea Upinzani. Na ndiyo, kura za maoni zaweza kukosea,
na tusiwekee mkazo sana.Lakini hoja hii sasa ndiyo hupendelewa zaidi na upande unaelekea
kushindwa kwenye uchaguzi.
January Makamba ni Mbunge wa Bumbuli (CCM), Mjumbe wa Halmashauri
Kuu ya CCM, na msomaji wa Kampeni za CCM