Nimefarijika sana kuona mahojiano niliyofanya na msanii mahiri wa Bongoflava,Hamis Mwinjuma a.k.a Mwana FA,yamechapishwa katika tovuti ya kimataifa ya muziki wa hip-hop,Hip-Hop-Dance.Net.Pamoja na kuwapatia wasomaji wa blogu hii nafasi ya kuwafahamu Watanzania wenzetu wanaotangaza jina la nchi yetu kwa namna moja au nyingine,dhumuni jingine la mahojiano hayo lilikuwa kutangaza vipaji vinavypatikana nchini kwetu. Japo mahojiano hayo yanaelekea kuzua mjadala mwingine ambao binafsi nautafsiri kama uhuru wa mawazo,ninaishukuru sana tovuti ya Hip-Hop-Dance kwa "kutoa shavu" kwa mahojiano hayo hasa kwa vile Mtanzania mwenzetu mmoja aliamua kuyabania licha ya kumpa ombi ayaweke "kiwanjani" kwake.Again,naamini alifanya hivyo kwa kutumia uhuru wake kuchagua nini kinastahili kuwepo hapo kwake.
Kuhusu suala la elimu ya Mwana FA,ninaomba kumtetea,sio kwa vile nilimhoji,bali kwa sababu naamini anastahili zaidi pongezi kuliko criticism.Naomba niweke wazi kuwa Mwana FA hakuomba mahojiano hayo bali ni mimi niliyemwomba (na namshukuru sana kwa kukubali ombi hilo).Pili,kama alivyosema mwenyewe,mtu haihitaji kuwa na Masters ili aweze kufanya vizuri kwenye bongoflava.Alichukua uamuzi wa kujiendeleza kimasomo kwa vile,kwa mujibu wa maeleoz yake nayoafikiana nayo,fani ya muziki (hasa wetu) haitoi mwamana wa mafanikio katika maisha.Kwa amaan nyingine,alimua kuongeza elimu yake kama hatua ya kimaendeleo mbali na mafanikio yake katika Bongoflava.
Na hata kama angekuwa anadanganya kuhusu elimu yake (which he absolutely doesn't) ingemsaidia nini wakati tayari ana jina kubwa ndani na nje ya nchi yetu?Nadhani baadhi ya wasomaji wanaomtaka "aeleze ukweli" wanapaswa kwanza "kueleza uongo wake" kabla ya kumtaka aseme "ukweli".Nasema hivyo kwa maana kama nasema jina langu ni Evarist,halafu mtu anasema hilo sio jina langu ,basi ni muhimu kwake kuthibitisha jina langu halisi ni nani.
Binafsi,kama mwanafunzi,nimekumbana na zahma kama hiyo ya Mwana FA.Nimekuwa napokea barua pepe na hata SMS za watu wanaoulizia lini namaliza shule.By the way,shule huwa haimalizwi bali mtu anahitimu hatua moja na anaweza kuendelea na hatua nyingine.Kadhalika,katika mfumo wa elimu ya juu hapa,mwanafunzi anaweza kuahirisha kozi yake pale atapoona umuhimu wa kufanya hivyo.In my case,majibu yangu kwa watu wanaoniuliza kistaarabu ni kuwa kuchelewa kumaliza kozi yangu kumesababishwa na A,B,C na kadhalika kisha nawafahamisha hatua niliyofikia.Kwa wale wanaouliza kwa minajili ya "kudhani nauhadaa umma kuhusu elimu yangu" jibu langu huwa jepesi: Mind your own damn business.
Kuna wanaojiuliza inakuwaje mtu atoke IFM na kuja kufanya Masters University of Coventry,nawasihi wafanye utafiti kidogo kwenye mfumo wa elimu ya Uingereza,na pengine hata huko nyumbani.Inawezekana kabisa kupata admission kwenye vyuo vya hapa kwa kigezo cha "sifa linganifu" (equivalent qualifications).Ni kama ambavyo baadhi ya wanafunzi wanavyojiunga na MBA pale Mzumbe au kwingineko baada ya kumaliza masomo ya stashahada kutoka IFM,Nyegezi,Ustawi wa Jamii (pale Sayansi),nk.Kwa kifupi,mifumo mingi ya elimu duniani iko so "accommodating" kwa watu wenye nia ya dhati ya kujiendeleza kitaaluma.
Nimalizie kwa kutoa shukrani kwa wote wanaoendelea kutoa mawazo yao kuhusu mahojiano hayo.Sipingani na mawazo yoyote bali huu ni mchango na mtazamo wangu binafsi (ambao pia unaweza kuwa si sahihi kwa mujibu wa mitizamo mingine).Huo ndio uhuru wa mawazo,alimradi tunatumia lugha za kiungwana na "hatutiani vidole machoni".Kwa Mwana FA,hizi ndio changamoto za Tanzania yetu.
Stay tuned for the next interview na Mtanzania mwingine anayetuwakilisha vilivyo.Can you make a wild guess?Au una pendekezo lolote?