24 Oct 2008

SERIKALI ipo katika hatua za mwisho za kuingia ubia na Kampuni ya Sonangol kutoka nchini China kwa ajili ya kuendesha Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL).
Nia hiyo ya serikali ilitangazwa jana kwenye ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, Mohamed Misanga, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupokea taarifa ya utendaji kazi wa ATCL.
Alisema ATCL, hivi sasa ipo katika hali mbaya kiuchumi kutokana na kuelemewa na madeni sambamba na kutokuwa na mtaji ambao utawezesha kuingia katika soko la ushindani.
Alisema awali serikali ilipozindua upya kampuni hiyo iliahidi kuchukua madeni yote na kutoa mtaji kwa kampuni hiyo, ili iweze kufanya biashara ya ushindani, lakini imeshindwa kutekeleza ahadi yake.
“Hali ya kiuchumi kwa ATCL ni mbaya, serikali imeamua kuinusuru kwa kuingia ubia na Kampuni ya Sonangol International ambayo wakati wowote kuanzia sasa watasaini mkataba,” alisema Misanga.
Alisema wabunge wameionya serikali kuwa makini na mwekezaji huyo, ili ubia huo usije ukawa kama wa kampuni ya SAA ambayo kwa kiasi kikubwa ndiyo iliyosababisha ATCL iwe hoi na kuidai madeni makubwa.
Alisema lengo la wabunge ni kuona serikali haiingi tena katika uingiaji mikataba mibovu ambayo imekuwa isainiwe na wataalamu wa serikali kila kukicha,” alisema Misanga.
Alisema ni jambo la kusikitisha kuwa hivi sasa ATCL imekuwa ikinunua mafuta kwa siku kila ndege inapotaka kufanya safari badala ya kununua mafuta ya muda wa miezi mitatu au minne.
Aliongeza kuwa shirika hilo halikopesheki na kila kinachopatikana hutumika kwa madeni na shughuli za uendeshaji, jambo ambalo hulidhoofisha shirika hilo kununua na kukodisha ndege.
Alibainisha kuwa Serikali tayari imeamua kuiandikia barua Kampuni ya SAA kuitaka iache kuidai ATCL na badala yake iidai serikali ambayo ndiyo iliyoyachukua madeni.
Aidha, alisema ATCL ipo katika mchakato wa kuuza ndege yake aina ya Boeing 737-200 ambayo inadaiwa kutumia mafuta mengi sambamba na kupitwa na wakati.
“Uamuzi huu utasaidia kupunguza gharama zisizo za lazima kwa shirika lakini pia itasidia kupatikana kwa fedha kidogo zitakazotumika kwa mambo mengine,” alisema Misanga.
Aidha, alikanusha kuwa ATCL hakuna ndege mbovu zilizoletwa hivi sasa kwani kuna Mamlaka mbalimbali ambazo huzithibitisha ndege hizo kabla ya kuanza kazi.
CHANZO: Tanzania Daima
Hivi hatuwezi kuwauliza wenzetu Wakenya au Waethiopia kwanini wao wameweza lakini sie tunashindwa?Well,pengine Kenya na Ethiopia ni mbali,if so kwanini tusiwadadisi wazalendo wenzetu wa Precision Air?

Soma kwa makini stori hizi kisha make your own conclusion
STORI YA KWANZA:
Waziri Membe akana kuubeba msalaba OICNa Ramadhan SemtawaWAZIRI wa Mambo Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernad Membe, amekuja juu akisema baadhi ya watu wamekuwa wakimtwisha mzigo kwamba, ameingiza Tanzania katika Jumuiya ya nchi za Kiislam Duniani (OIC), kitu ambacho si kweli.Kauli hiyo ya Membe ni ya kwanza kuitoa hadharani tangu kuibuka kwa kasi kwa mjadala huo, ambao unaonekana kuigawa nchi katika misingi ya kiitikadi.Akizungumzia hilo jijini Dar es Salaam jana, Membe alisema si kweli kwamba Tanzania imekwishajiunga na OIC na wala yeye hajasema lazima ijiunge.Membe akifafanua huku akionekana kuguswa na tuhuma hizo dhidi yake kutokana na kutamka hilo bunge katika hotuba ya bajeti ya wizara yake, alisema uamuzi wa kujiunga au la, uko kwa wananchi."Nimekuwa kimya, kuachia na kusikiliza watu waseme, jamani, Tanzania haijajiunga na OIC wala sijasema lazima ijiunge," alisema na kuongeza:"Uamuzi wa kujiunga au kutojiunga utakuwa chini ya wananchi, wasomi, NGOs na ninyi waandishi wa habari, ndiyo mtakaoamua."Membe alikuwa akifafanua kuhusu uhusiano kati ya Tanzania na Iran, ambao unaonekana na baadhi ya watu kama wenye nia ya kuingiza nchi OIC.Akifafanua zaidi, alisema watu wasiingize vitu visivyokuwa na msingi kwa ajili ya kutunga na kuzungumzia hisia, na kushauri wasome historia kufahamu uhusiano kati ya nchi hizo mbili.Membe huku akionekana kuchukizwa na fikra mbovu za kupandikiza udini katika nchi, alisema Watanzania ni watu wanaoheshimika duniani kwa umakini wao, ni aibu na haipendezi kujadili udini.Alisema kama ni kujiunga na OIC ni jambo la kuamua, kwani Uganda ambako kuna Waislam asilimia 10 imeweza kujiunga huku Wakristo wakiwa ni asilimia 66 na wengine wapagani."Sasa jamani, msitake kunichinganisha na watu wangu, nawaambieni tena na tena, Tanzania haijajiunga na OIC na haitaweza kujiunga uamuzi huo ni ridhaa ya wananchi," alisisitiza.CHANZO: Mwananchi
STORI YA PILI KUHUSU SUALA HILOHILO:
Waziri: Tanzania kujiunga OIC ni dhahiri
23 Oct 2008
By Muhibu SaidTanzania inatarajia kujiunga na Jumuiya ya Kimataifa ya Nchi za Kiislamu (OIC) wakati wowote katika siku zijazo baada ya serikali kuweka bayana azma hiyo jana.Azma hiyo ya serikali iliwekwa bayana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Seif Ali Iddi, alipozungumza na Nipashe jana, ikiwa ni wiki chache tangu Waziri wa Wizara hiyo, Bernard Membe, aliambie Bunge kwamba, hakuna madhara yoyote kwa Tanzania kujiunga na jumuiya hiyo.
Balozi Iddi alisema mchakato kwa Tanzania kujiunga na OIC, unatarajiwa kuanza wakati wowote na kwamba, hatua ya mwanzo ya mchakato huo, viongozi wa serikali ya Jamhuri ya Muungano watakutana na wenzao wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kwa ajili ya kupata msimamo wa pamoja kuhusu suala hilo.Naibu Waziri huyo alisema hayo alipoulizwa na Nipashe kama mchakato kwa Tanzania kujiunga na OIC umeshaanza au la tangu Waziri Membe atoe kauli hiyo bungeni, mjini Dodoma, Agosti 22, mwaka huu.``Bado hatujaanza mchakato. Kuna kikao tunachotaka kwanza kufanya kwa ajili ya kushauriana na wenzetu wa Zanzibar ili tuwe na msimamo mmoja kuhusu hilo. Ilikuwa tuanze sasa, lakini Mheshimiwa Waziri (Membe) hayupo na Bunge linatarajiwa kuanza,`` alisema Balozi Iddi.Alisema mchakato kwa Tanzania kujiunga na OIC ni mrefu, ambao unatarajiwa pia kulishirikisha Baraza la Mawaziri kufikia maamuzi.Balozi Iddi alisema hatua nyingine ya mchakato, ambayo serikali inatarajia kuichukua, ni kutoa elimu kwa umma ili kuwaondoa uoga wote walioonyesha hofu iwapo Tanzania itajiunga na jumuiya hiyo.``Hao wanaopinga, ni waoga tu, hawajaeleweshwa kwani haina maana Tanzania itakuwa nchi ya Kiislamu. Zipo nchi kama vile Uganda zimejiunga na OIC, lakini hazijabadilika kuwa nchi za Kiislamu. Tutawaelewesha wakati ukifika, tunavyo vyombo vya kuelimisha hilo,`` alisema Balozi Iddi.Agosti 22, mwaka huu Waziri Membe wakati akifunga mjadala wa hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake, alisema hakuna madhara yoyote kwa Tanzania kujiunga na IOC.Waziri Membe alisema serikali mwaka huu, ilifanya kikao na Baraza la Wawakilishi kuhusu suala hilo na kugundua kuwa nchi 21 zimejiunga na jumuiya hiyo.Alisema kati ya nchi hizo, zimo pia nchi za Wakristo ambazo zimejiunga na hazijapata madhara yoyote.``Tumeshakusanya takwimu za nje na kuona hakuna madhara yoyote ya kujiunga na IOC, bora tu kufuata taratibu,`` alisisitiza Waziri Membe.Alisema suala hilo lilileta utata awali kwa sababu aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wakati huo, marehemu Ahmed Hassan Diria, alipeleka ombi la Zanzibar kujiunga kwenye jumuiya hiyo bila kuishirikisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Hata hivyo, alisema suala hilo limefanyiwa kazi na serikali na kuona kuwa hakuna madhara kujiunga na IOC.Siku chache baada ya Waziri Membe kutoa kauli hiyo bungeni, viongozi wa makanisa na baadhi ya wasomi, akiwamo Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Dk. Methodius Kilaini, walipinga vikali kauli hiyo ya serikali.Wengine waliopinga suala hilo, ni Askofu Stefano Msangi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Pare, Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT Tanzania, Dk. Alex Malasusa, Mhadhiri Mwandamizi wa Sheria wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Sengodo Mvungi.Hata hivyo, Imamu Mkuu wa Msikiti wa Mnyamani, Buguruni, jijini Dar es Salaam, Sheikh Mohammed Iddi, amekuwa akijitokeza kuwapinga maaskofu kuhusu kauli zao za kupinga suala hilo.CHANZO:Nipashe
23 Oct 2008

BATAVIA, Ohio (AdAge.com) -- Conventional polls this year are fraught with doubts -- from the "Bradley Effect" to the elusive cellphone-only households. But one poll based in the all-important swing state of Ohio has never failed since its inception in 1984, and it has Barack Obama with an almost insurmountable lead over John McCain.
The Busken Cookie Poll, in which the chain of Cincinnati-area retail bakeries sells cookies bearing cartoon images of each candidate, as of Thursday morning had Mr. Obama ahead 6,477 to 3,090 -- a 68% to 32% margin. Daily updates can be found at www.busken.com.
Unscientific? Perhaps. But Brian Busken, VP-marketing of the family business, said that since the poll's inception in 1984, it has accurately predicted the winner of the presidential election every four years and never been further than 4 percentage points from the final popular vote tally nationwide. (Note: While the website shows a smiling Obama cookie and a frowning McCain cookie, the cookies sold in stores have both smiling.)
"We've never seen a spread like this before in the numbers," Mr. Busken said. "I don't know if there's going to be a crumbslide or not. ... We may still predict the winner, but probably by way too many cookies."
Already there are allegations of irregularities. Commenters on a story at the website of the Cincinnati Business Courier allege some bookstores have Obama cookies up front, McCain cookies in the back, and that Remke stores in Northern Kentucky had run out of the McCain cookies.
Mr. Busken said wholesale sales such as those referenced in the comments don't count. Nor does a recent bulk purchase of 400 McCain cookies by Rob Portman, former Republican congressman and White House budget director. If Acorn buys cookies online for the Dallas Cowboys and their cheerleaders, those don't count either. Only cookies sold in the 11 Ohio stores tracked by the poll count.
Busken milks the poll, of course, for all the publicity it can get, and has incorporated it into outdoor ads from the Creative Department, Cincinnati. The chain will advertise cookie-poll results on the Norton Digital Network in the area during the four days leading up to the election.
SOURCE: Advertising Age

Serikali imeionya Taasisi ya HakiElimu kuacha kutumia matangazo yake katika vyombo vya habari, kueneza chuki miongoni mwa watoto na vijana nchini na badala yake ingetumia nafasi iliyonayo katika kuwafundisha utawala bora.
Aidha, imewatahadharisha wote wanaoanzisha taasisi za elimu kwa minajili ya kupata fedha bila kuchangia lolote katika sekta ya elimu, ikiwa ni pamoja na shule zinazotoza wazazi fedha nyingi ambazo hazilingani na mazingira na kiwango cha elimu kinachotolewa.
Akizungumza wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii katika ofisi za Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk. Lucy Nkya, alisema HakiElimu pamoja na kuonywa na kusimamishwa hivi karibuni kutokana na utendaji wake, bado imeendelea kutoa matangazo ambayo yanaeneza chuki kwa vijana.
“Hili tangazo tena linalorushwa hata televisheni ya TBC1 la watoto wa sekondari wanazungumzia EPA, wanafanyiwa hesabu na kisha wanaambiwa waseme hizi hela zingefanyia hili na lile, kumbukeni samaki mkunje angali mbichi, huku ni kueneza chuki kwa watoto hawa,” alisema Dk. Nkya.
Alisema taasisi hiyo ya HakiElimu inakosea kutumia matangazo hayo kwa upande mmoja tu wa kukosoa. “Mimi nimesomea saikolojia, huu mtindo wa kukosoa serikali kwa namna hii, kunawajengea vijana wetu chuki, badala ya kuwafundisha utawala bora, sasa watoto wanafikiri serikali yote ni mafisadi,” alisema.
Alisema kutokana na matangazo na vitendo hivyo kwa sasa, hata watoto wa baadhi ya viongozi wamelazimika kuhamishwa katika shule za kawaida na kupelekwa shule nyingine kwa vile wanaitwa watoto wa mafisadi na wenzao.
Aliitaka taasisi ya TEN/MET kufikisha ujumbe kwa HakiElimu kuwa wanayo nafasi nzuri kuelimisha jamii juu ya masuala ya sekta ya elimu na si kueneza chuki pekee, kwani serikali itafika mahala italazimika kutumia meno yake.
“Msiisingizie serikali haina demokrasia pindi itakapotumia meno yake, haitokuwa kibogoyo tena,” alionya. Naye Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar, Haroun Ali Suleiman, alitaka kufahamu uwezo wa kiutendaji wa mtandao huo wa elimu kwa kuwa haujitangazi, kwani pamoja na yeye kuwa Waziri wa Elimu ndio anausikia.
Kwa upande wake, Mratibu wa TEN/MET, Joseph Kisanji, alikiri kuwa mtandao huo umejificha na kwamba wanajitahidi kwa sasa kuutangaza kwa kutumia mtindo wao bila kuiga HakiElimu.
Alisema awali wakati HakiElimu ilipokabiliwa na serikali, takribani asasi nyingi za elimu ziliwatetea ukiwamo mtandao huo. “Hata hivyo, kuna mipaka yake katika kutumia media (vyombo vya habari) kwani zina nguvu na tuliwaambia wenzetu juu ya hilo ila hatuna maamuzi, kazi yetu ni kushauri,” alisema.
Alisema kama suala la tangazo la EPA limeleta athari hadi kufikia watoto wa viongozi kuhamishwa shule ni jambo hatari, hivyo aliahidi kulifikisha katika Bodi ya Mtandao huo ili walijadili na kulifikisha kwa taasisi hiyo ya HakiElimu.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya TEN/MET, Antoine Gizenga, alisema watalivalia njuga suala la HakiElimu kwani mtandao wao unaitazama taasisi hiyo kama asasi inayosaidia kuibua yaliyojificha.
Mwaka jana, Ofisi ya Waziri Mkuu ilipiga marufuku machapisho na matangazo yanayotolewa na HakiElimu kupitia vyombo vya habari na kutishia kulichukulia hatua kali za kisheria iwapo itakiuka amri hiyo.
CHANZO: HabariLeo

23.10.08
Evarist Chahali
TANZANIAN ECONOMY
No comments
By Samuel KamndayaAnnual inflation surged to a 10-year high point of 11.6 percent in September owing to soaring food prices, official data from the National Bureau of Statistics show.The inflation rate hit the double digit for the first time in a decade due to skyrocketing food prices in the Holy month of Ramadhan.In August this year, the inflation rate was 9.8 percent. The recent surge indicates a 1.8-point increase within a month. In February this year, inflation was 8.9 percent.Analysts say the Government would not be able to bring down the inflation rate to seven percent by the end of the current financial year."The seven per cent goal is now unrealistic since, under the current system, Tanzania has nothing in place to control food and fuel prices, the two most dominant factors in the country's inflation basket," said Dr Honest Ngowi who lectures at Mzumbe University.He said since the inflationary spiral was mainly on food, fuel and other production factors, it would be very difficult for the country to control it in the short-term."It could be easily contained if it was caused by excess money supply on the market. However, this is due to production factors," he said.He said this could worsen considering that the holiday season was just around the corner.Dr Semboja Haji of the University of Dar es Salaam's Economic Research Bureau (ERB) also said: "Inflation will now be fluctuating between 10 and 12 percent. It requires magic for the government to bring it back to seven per cent," he said.He criticised the government for having no mechanism in place to protect the country from the negative effects of economic developments outside.Food makes over 55 percent of Tanzania's inflation basket. But Dr Semboja suggested that the development was due to bad policies."I find no reason why food prices in Tanzania should be going up while we have a capacity of producing enough to meet the local demand as well for exports," he said.He urged the government to have price mechanisms for sensitive products like food and fuel.He cited the Energy and Water Utilities Regulatory Authority (Ewura), saying it should understand that local companies were colluding to increase prices even when there was nothing to force them to increase the prices.In that respect, the don said, there was no reason to stick to the concept of market pricing while companies were conspiring among themselves to increase prices willy-nilly.
SOURCE: The Citizen
22 Oct 2008

Barack Obama akifanikiwa kushinda urais hapo Novemba 4 atakuwa ameweka historia kwa kuwa Mweusi wa kwanza kuwa rais wa Marekani.Lakini mafanikio ya Obama yanawasumbua wachambuzi wa siasa (hususan za tabia za uchaguzi wa Marekani).Hayawasumbui kwa vile Obama na wao ni wabaguzi.La hasha,bali ni namna hisia kwamba Bradley effect ingemwangusha zinavyoelekea kuwa wrong.
Nilishakiri katika post yangu moja huko nyuma kwamba awali nilitamani Hillary Clinton apitishwe kuwa mgombea wa Democrats.Sababu yangu kuu ilikuwa ni katika hofu kwamba Obama angeshinda nomination basi Weupe wangeungana bila kujali itikadi zao kuhakikisha mtu mweusi haingii White House.Baada ya kumbwaga Hillary,nililazimika kukubaliana na busara za stadi za siasa kwamba lolote linawezekana katika fani hiyo.
Tukirejea kwenye kinachowasumbua wachambuzi wa siasa ni namna Bradley effect inavyoelekea kushindwa kuwa na impact kwa Obama,hasa kipindi hiki ambacho sio tu anapambana na Mweupe bali Mweupe kutoka chama cha weupe wahafidhina (Republican).Kuna wanaoamini kwamba Bradley effect ni uzushi (myth) wa aina flani.I dont.Lakini kama sio myth basi kwanini Obama anazidi kupaa kwenye opinion polls?
Binafsi nadhani hii ni REVERSE BRADLEY EFFECT.Yaani,wapiga kura Weusi hawaonyeshi dhamira zao hadharani (kwa wanaochukua opinion polls) kwamba watamsapoti Mweusi mwenzao.Kwa lugha nyingine,wanashusha matarajio ya support ya Weusi kwa Mweusi mwenzao.Lakini kwa vile Weusi ni wachache Marekani,na hata kama wangefanya nacho-hypothesize hapo juu bado wasingeweza kuifanya hali kuwa kama ilivyo sasa,nachoamini zaidi ni tabia "mpya" ya Weupe kudai hadharani kuwa hawajaamua wampigie kura nani (undecided) au Weupe (hasa wa Republicans) kuongopa hadharani kwamba wanamsapoti McCain ilhali dhamira na sapoti yao ni kwa Obama.
Weusi wa Obama ni issue kwenye uchaguzi huu,nami ni muumini wa hoja kwamba kama Obama angekuwa Mweupe basi muda huu tungeshafuta uwezekano wa McCain kuwa rais hapo Novemba.Kwanini nasema hivyo?Wamarekani wengi wamechoshwa na Republicans na uhafidhina kwa ujumla.Bush ameendelea kuwa one of the most unpopular US presidents ever,na Democrats wanaonekana kama ndio watakaoleta ufumbuzi wa matatizo ya Marekani.Sababu zote hizo ni tosha kumfanya mgombea anayekubalika wa Democrats kuwa mbali sana kwenye kura za maoni.Kwanini Obama anamwacha McCain kwa wastani wa kura 10 tu?Jibu la haraka ni Weusi wake.
Whether Bredley effect ni hype au ndio ujio wa Reverse Bredley effect itajulikana baada ya exit polls hapo Novemba 4.However,no matter what happens to Obama,alipofika ni historia tosha,japo itanoga zaidi akishinda kiti hicho.
22.10.08
Evarist Chahali
SIMBA, SOKA LA TANZANIA, YANGA
No comments

HII ya Yanga haijapata kutokea kwenye historia ya soka ya Ligi Kuu Tanzania Bara. Ndio kauli nyepesi unayoweza kuitumia kama ukipata nafasi ya kupita karibu na kambi ya Yanga jijini Dar es Salaam.
Yanga imeweka kambi kwenye Hoteli ya Lamada Ilala, jijini Dar es Salaam chini ya ulinzi mkali wa askari ambao haujapata kutokea kwa timu yoyote ya Tanzania pengine tangu Ligi Kuu Bara ianzishwe.
Ulinzi huo ambao wachezaji wa Yanga wamesema kwamba hawajapata kuuona, unadaiwa kuwekwa na mdhamini mkuu wa klabu hiyo, Yusufu Manji kutokana na kikosi hicho kukabiliwa na pambano gumu dhidi ya Simba Jumapili kwenye Uwanja Mkuu wa Tanzania jijini Dar es Salaam.
Walinzi hao wengine wakiwa na silaha ambao wametapakaa kila kona mpaka kwenye korido za kwenda vyumbani, walimwagwa hotelini hapo juzi Jumapili jioni wakati mechi baina ya Yanga na Polisi Dodoma ikiendelea kwenye Uwanja wa Taifa. Yanga ilishinda 3-1.
"Tuliporudi tu ile jioni tukashangaa mazingira yamebadilika ghafla, kila kona ina walinzi na wengine wamebeba silaha na wengine wana virungu pamoja na baadhi ya wanachama ambao walikuwa wanapitapita huku na huko kutulinda," alidokeza mchezaji mmoja.
"Sijapata kuiona hali hii, mpaka wachezaji tunashangaa kwa jinsi walinzi walivyomwagwa huku nje wapo kama 12, kwenye korido za vyumbani wapo na kwenye ngazi za kushukia pia wapo.
"Huruhusiwi kutoka nje ya geti na hata ukikaa nje mazungumzo yako yanafuatiliwa kila hatua, yaani mpaka wageni wanaoingia wanaulizwa maswali kama ni mtu mwenye chumba chake lazima waende mpaka chumbani wakahakikishe kama kweli ana chumba.
"Sisi wenyewe wakati unatoka chumbani unaulizwa unakwenda wapi, ukitoka nje kwenye ngazi unawakuta pia hawa walinzi wanafanana na wale wa ile kampuni inayolinda kule ofisni kwa Manji."
Mchezaji mwingine alisema; "Huku ni mitutu tu kila upande bwana, hata kama unaenda nje kununua vocha au kitu chochote kuna walinzi.
"Kwa jinsi palivyo huku utafikiri tunacheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika tena na Real Madrid, ni kasheshe tupu ndugu yangu lakini ndio soka," alisema mchezaji mwingine.
Mwanaspoti ilipojiri kwenye kambi ya timu hiyo jana, askari hao walicharuka mithili ya mbogo wenye njaa na hawakutaka kusikiliza chochote.
"Unakwenda wapi? Wewe ni mteja hapa au unakwenda kuwaona wachezaji wa Yanga?" Walisema walinzi hao wakiwazuia waandishi wa Mwanaspoti kuingia ndani ya hoteli hiyo.
"Huwezi kuingia humu hotelini mpaka upate kibali cha Yanga, wasiliana na mwenyekiti au meneja wa timu," alisema askari mmoja wa kampuni ya Group 7 Security aliyekuwa ameshika rungu.
"Ondokeni eneo hili haraka, usije ukatusababishia matatizo makubwa au tukakufanya chochote baadaye ikawa matatizo, ondoka bwana kwa usalama wako," alisema mlinzi mwingine aliyekuwa amekunja sura.
Waandishi wa Mwanaspoti wamekuwa wakienda mara kwa mara katika hoteli hiyo kufanya mahojiano na wachezaji wa timu hiyo, lakini kila kitu sasa kimebadilika na mawasiliano pekee yaliyobaki ni kwa njia ya simu.
Yanga ambayo imekuwa ikinyanyaswa na Simba kwenye Ligi Kuu Bara kwa takribani miaka saba sasa, inaonekana kujizatiti na kutaka kulipiza kisasi na hasa kutokana na hali kutokuwa shwari ndani ya Simba.
Viongozi wa Yanga wameapa kufanya mauaji makubwa Jumapili kwa madai kuwa dalili za kuimaliza Simba zilianza mwishoni mwa wiki wakati Toto wenye urafiki na Yanga walipoifunga Simba mabao 4-1
22.10.08
Evarist Chahali
UFISADI
No comments
Daniel Mjema na Ally Sonda
Siku saba zikiwa zimebaki kabla ya kile kinachoelezwa kuwa ni kiama cha mafisadi kutimia, mwananchi mmoja mkazi wa Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, jana alichomoza na kumuhoji Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuhusu ukimya wa serikali katika kuwashughulikia watuhumiwa wa ufisadi.
Hali hiyo ilijitokeza jana nje ya jengo la ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Rombo wakati waziri mkuu aliposimama kwa muda kuwasalimia wananchi waliokuwa wamefurika nje ya ofisi hizo kwa lengo la kumuona.
Wakati waziri mkuu aliporuhusu maswali machache ndipo mwananchi mmoja alipomhoji Waziri Pinda akimuuliza kwa nini wanawaacha bila kuwashughulikia mafisadi hadi Bunge lilipoamua kuchukua jukumu hilo.
Mwananchi huyo, ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, alitaka serikali itunge sheria kali ya kuwashughulikia mafisadi.
Mbali na kumhoji Waziri Mkuu kuhusu ukimya huo wa serikali katika kuwashughulikia mafisadi, pia alitaka uteuzi wa Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) na makanda wa mikoa, uthibitishwe na Bunge.
Alisema kuwa hiyo itakuwa rahisi kwa chombo hicho cha wawakilishi wa wananchi kuweza kuwawajibisha viongozi watakaothibitika kujihusisha na vitendo vya ufisadi.
Akijibu swali hilo na mengine, Waziri Pinda alisema suala la ufisadi linapaswa kupigwa vita kuanzia ngazi ya familia kwa sababu viongozi wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu wanatoka katika familia.
Waziri Mkuu alisema hali sasa imebadilika na kwamba suala la kuwachukulia hatua mafisadi lazima lifuate taratibu na sheria za nchi, ikiwamo kuheshimu haki za binadamu na utawala wa sheria.
Suala la kutochukuliwa hatua kwa mafisadi limekuwa mdomoni mwa watu wengi baada ya Rais Jakaya Kikwete kulieleza Bunge la Muungano kuwa watu waliochota Sh133 bilioni kutoka kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) warejeshe fedha hizo ifikapo Oktoba 31, la sivyo wafikishwe mahakamani Novemba mosi.
Kauli hiyo ilionekana kama kuwapa ahueni mafisadi hao kuwa iwapo watarejesha fedha hizo ambazo zilichotwa kati ya mwaka 2005/06, hawatachukuliwa hatua zozote.
Kauli hiyo ilifanya watu kuwa na maoni tofauti, wengi wakihoji sababu za serikali kuwapa ahueni watu waliochota mamilioni ya fedha na wengine wakitaka wezi hao watajwe majina yao, lakini serikali imekuwa ikisema kuwa imeshachukua hatua, ikiwa ni pamoja na kuzuia akaunti zao na kushikilia mali zao.
Hadi sasa serikali inadai kuwa mafisadi hao wamesharejesha kiasi cha Sh61 bilioni, lakini haijataja waliokwisha rejesha fedha hizo wala wale ambao hawajarejesha, ikisema kuwa kufanya hivyo kutaharibu mikakati yao.
Akianza ziara yake mkoani Mbeya, Rais Jakaya Kikwete alikumbana na umati wa watu waliozuia msafara wake maeneo ya Mwanjelwa na wengi wakipiga kelele kutaja neno mafisadi, huku wakihoji maisha bora na ajira.
Mapema wiki hii, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kilisema kuwa kitaifungulia serikali mashtaka ya kuwalinda mafisadi iwapo haitawafikisha mahakamani wale wote wanaohusika na tuhuma za uchotaji wa mabilioni hayo ya fedha.
Kashfa ya wizi wa fedha hizo ilibainika wakati kampuni ya Ernst and Young ilipopewa kazi ya kukagua mahesabu ya Benki Kuu (BoT) ya kipindi cha mwaka 2005/06. Kampuni hiyo iligundua kuwepo na malipo ya kasi ya mamilioni ya fedha kwa wafanyabiashara wa ndani katika kipindi hicho na hivyo kutoa ripoti iliyofichua wizi huo.
Fedha hizo, zilizohamishiwa kwenye akaunti hiyo maalum BoT kutoka NBC, ni zile zilizokuwa zikilipwa na wafanyabiashara wa ndani ambao walinunua bidhaa kutoka makampuni ya nje kwa dhamana ya serikali, ambayo ilikuwa inakabiliwa na uhaba mkubwa wa fedha za kigeni.
Akijibu swali la upungufu wa mbolea ya ruzuku, Waziri Pinda alikiri kwamba mbolea hiyo haitoshelezi mahitaji, hivyo akawashauri wakulima wajiunge na vyama vya akiba na mikopo ili waweze kupata mikopo.
Baadaye waziri mkuu alizindua awamu ya tatu ya mradi wa maji unaosimamiwa na kampuni ya Kiliwater ambao baada ya kukamilika utagharimu zaidi ya Sh10 bilioni.
Aliwataka wananchi kuutunza mradi huo dhidi ya hujuma zozote huku akiiagiza Bodi ya Wakurugenzi kuhakikisha wanaifanyia matengenezo ya mara kwa mara miundo mbinu yake ili iwe endelevu.
Katika ziara hiyo ya siku tano mkoani Kilimanjaro, waziri mkuu anafuatana na viongozi mbalimbali wa serikali, akiwemo Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Dk. Cyrill Chami.
Wengine ni mkewe, Tunu Pinda, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mohamed Babu na Mwenyekiti wa CCM mkoani Kilimanjaro, Vicky Nsilo Swai na watendaji wengine wa serikali na mashirika ya umma.
Wakati huohuo, ziara ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambayo leo inaingia Siku ya tatu mkoani Kilimanjaro, imegeuka msumari wa moto kwa vijana wa mji wa Moshi ambao wengi wao wanashikiliwa na polisi baada ya msako mkali uliofanywa jana.
Taarifa zilizoifikia Mwananchi jana, zimedai kuwa vijana wengi waliokamatwa ni wafanyabiashara ndogondogo (machinga) kwenye maeneo ya sokoni, Mtaa wa Kiusa ambako Waziri Pinda amepangiwa kuhutubia wananchi leo jioni.
Haikufahamika haraka kiini cha polisi kuendesha operesheni hiyo kali ambayo imesababisha vijana wengi kushindwa kumuona Waziri Pinda jana, lakini taarifa zisizo rasmi zimedai kuwa huenda vyombo vya ulinzi na usalama vina hofu na yale yaliyomkumba Rais Jakaya Kikwete mkoani Mbeya.
"Hivi sasa watu waliokata tamaa ni wengi…….hii kamatakamata inayofanywa na polisi leo (jana) ni kuweka mambo sawa ujio wa Waziri Mkuu, Pinda, bila hivyo yapo majitu yanaweza kumzomea," alisema kiongozi mmoja wa dini.
Mwananchi ilipotembelea mitaa ambayo polisi wanasemekana kufanya msako huo ilielezwa kuwa, baadhi ya vijana waliokamatwa walikuwa wakifanya biashara zao za kujiajiri zikiwemo za kuuza vocha za simu.
''Hatukatai Polisi kufanya kazi zao, lakini misako hii isiwaonee vijana kwa kuwa siyo kila kijana ni mwizi au mkorofi……..mimi nadhani Polisi wanatumika kujenga chuki kati ya serikali na wananchi na kitendo hiki ni hatari kwa amani ya nchi,'' alisema mfanyabiashara wa Soko Kuu la mjini Moshi.
Alipohojiwa kuhusu kamatakamata hiyo, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Ramadhani Baruti alisema operesheni hiyo haikufanywa kwa ajili ya ujio wa Waziri Pinda, bali ni ya kawaida na kwamba baada ya uchunguzi wapo watakaofikishwa mahakamani.
Subscribe to:
Posts (Atom)