2 Feb 2012


Tumeuona wa madaktari, lakini mingi yaja

NI sababu zipi zinazomsukuma mwanafunzi kuchagua mchepuo fulani wa masomo anapopewa nafasi ya kufanya hivyo?
Pengine kwa wanafunzi wengi sababu ya msingi ni jinsi mchepuo huo unavyoweza kupelekea kufikia malengo ya taaluma au ajira tarajiwa.
Lakini kwa wengine, sababu inaweza kuwa uwezo wao kimasomo, yaani kama wanaweza kumudu mchepuo husika au la. Binafsi, nilikuwa na ndoto za kuwa tabibu (daktari). Nilipokuwa kidato cha kwanza hadi cha nne niliwekeza nguvu kubwa kwenye masomo ya elimu ya viumbe na kemia. Na niliyamudu vema masomo hayo ambayo niliamini yangeweza kufanikisha dhamira yangu ya kuwa tabibu.
Hata hivyo, ndoto yangu ilipata pigo kubwa baada ya mtihani wa kuhitimu kidato cha nne, ambapo japo nilipata alama A katika kemia na C katika baiolojia, nilifeli katika fizikia kwa kupata alama F, huku nikaambulia D kwenye hisabati.
Kwa maana hiyo, japo nilipata daraja la kwanza na kuchaguliwa kuingia kidato cha tano, uwezekano wa kusoma mchepuo “wa udaktari” wa PCB (Fizikia, Kemia na Baiolojia) ulikuwa hafifu.
Kabla ya kuanza masomo ya kidato cha tano nilipewa ushauri kuwa licha ya kushindikana kuchukua mchepuo wa PCB kuna uwezekano wa kuchukua mchepuo mwingine (unaoikwepa fizikia) wa CBG unaojumuisha Kemia, Baiolojia na Jiografia.
Lakini katika kile nilichokitafsiri kama haikuwa majaliwa yangu kuwa tabibu, licha ya shule kuwa na uhaba wa mwalimu wa jiografia nilipoangalia mtaala wa kemia niligundua ina mada kadhaa zilizojumuisha hisabati na maeneo mengine yenye ugumu kama wa fizikia, hususan katika physical chemistry.
Kufupisha maelezo, nilifikia uamuzi wa kuchukua mchepuo wa HGL (Historia, Jiografia na Lugha ya Kiingereza), ambao niliumudu na miaka kadhaa baadaye ulinisaidia kuchukua michepuo ya Elimu ya Jamii (Sosholojia) na Stadi za Siasa katika ngazi ya chuo kikuu.
Miongoni mwa mada za mwanzo kabisa za Elimu ya Jamii kuna mada ya kanuni za sosholojia (sociological theories).Na moja ya kanuni hizo ni ile inayoiangalia jamii kama mfumo kulingana na kazi za kanuni, desturi, mila na vikundi katika jamii. Kanuni hiyo ijulikanayo kama functionalism inaviangalia vipengele hivyo kama namna mwili unavyofanya kazi kwa ushirikiano wa viungo mbalimbali. Katika miili yetu, moyo unaletewa damu na mapafu na mapafu yanategemea damu inayosukumwa kwake na moyo.
Kadhalika, mfumo wa fahamu unaletewa ujumbe na viungo kama macho, ngozi, pua, nk lakini ili viungo hivyo viweze kupelekea ujumbe husika vinategemea ufanisi wa ubongo.
Kwa kifupi, ni vigumu-na pengine haiwezekani kabisa-kudai kiungo fulani katika mwili ni muhimu zaidi ya kingine. Vyote ni muhimu na kila kimoja kinakitegemea kingine katika utendaji kazi wake. Ni ushirikiano wa viungo mbalimbali ulikuwezesha wewe msomaji kuwa unasoma makala hii muda huu. Macho yaliona gazeti kwa muuzaji na kupelekea ujumbe kwenye ubongo ambako maamuzi yalifanyika ulinunue. Ubongo pia ulitumia maelekezo kwa mkono kutoa fedha mahali ilipowekwa (baada ya kukumbuka mahali husika), sambamba na kutofautisha kati ya fedha (ya kunulia gazeti) na funguo za ofisini au nyumbani.
Na pengine muda huu unatabasamu kwa ‘kukumbushwa jinsi mwili unavyofanya kazi na ufanisi wa ushirikiano wa viungo mbalimbali’, tabasamu hilo ni ushirikiano wa viungo mbalimbali mwilini.
Pengine hadi kufikia hapa nimekuchanganya na huelewi makala hii inaelekea wapi. Lengo la makala hii ni kuzungumzia mgogoro unaoendelea kati ya madaktari na serikali huko nyumbani.
Hadi wakati ninaandika makala hii, kulikuwa na taarifa kwamba mgomo huo unaelekea kusambaa katika hospitali mbalimbali. Kadhalika, kuna taarifa kwamba manesi nao wametoa tishio la kugoma iwapo serikali haitayapatia ufumbuzi matatizo ya madaktari yaliyosababisha mgomo huo.
Inawezekana wakati unasoma makala hii mgomo huo utakuwa umeshamalizika lakini kuna kila dalili kuwa hata kama madaktari watamaliza mgomo wao au/na manesi hawatogoma, kitakachokuwa kimemalizwa ni dalili tu za tatizo na wala si kupatikana kwa tiba yake.
Nilipotoa maelezo ya kanuni ya functionalism kwenye Sosholojia nililenga kuonyesha jinsi taaluma/ajira mbalimbali katika jamii zilivyo na umuhimu sawa na jinsi ushirikiano kati ya fani ya taaluma/ajira hizo unavyoleta ufanisi kwa manufaa ya jamii husika.
Je, wabunge ambao taarifa zinaeleza kuwa wameongezewa posho kutoka shilingi 75,000 kwa siku ni muhimu zaidi kuliko madaktari? Jibu la wazi ni hapana, kama ambavyo madaktari si muhimu zaidi ya walimu au viongozi wa dini si muhimu zaidi ya wanausalama.
Wote hawa ni muhimu kwa jamii na kwa namna moja au nyingine, ushirikiano wao (wa moja kwa moja au vinginevyo) ndio unaotuwezesha Watanzania kuwa hai.
Labda nifafanue. Ili tuwe salama, tunawategemea wanausalama. Lakini ili wanausalama waweze kutimiza majukumu yao ipasavyo wanapaswa kuwa na afya salama pia, na hapo unaona umuhimu wa watumishi wa afya (madaktari, manesi, nk).
Lakini ili mtu awe daktari au nesi ni lazima afundishwe, na hapo tunaona umuhimu wa walimu. Lakini mwalimu nae akiugua ni lazima aende kwa daktari. Hata hivyo, ili daktari aweze kufanya kazi zake ipasavyo ni lazima mazingira ya hospitali (na nchi kwa ujumla) yawe salama, na hapo tunarejea kwenye umuhimu wa wanausalama wetu.
Kadhalika, ingekuwa vurugu isiyoelezeka kama kila daktari, mwalimu, mwanausalama, nk angeenda bungeni kuwakilisha maslahi ya jamii yake au kuwa waziri au kiongozi serikalini. Na ndiyo maana licha ya kuepusha vurugu ya aina hiyo na pengine kuepusha uhaba wa wanataaluma kwenye fani husika, unakuwa na mtu mmoja kama waziri au mbunge mwenye jukumu la kuongoza na kuwakilisha makundi mbalimbali katika jamii.
Lakini viongozi au wawakilishi hao si muhimu zaidi ya wanaowaongoza au kuwawakilisha. Waziri hawezi kabisa kutimiza wajibu wake iwapo yeye mwenyewe ni mgonjwa na hakuna daktari wa kumtibu, au kuwa na wasaidizi ambao hawajatia mguu shuleni kwa vile hakuna walimu. Kadhalika, ili waziri atie mguu ofisini sharti nchi iwe salama, na hapo anatambua umuhimu wa wanausalama.
Kwa wabunge wetu pia, kuwa kwao bungeni kunategemea sana taaluma na nyanja nyingine katika jamii, achilia mbali nani waliowapigia kura kuingia bungeni. Japo picha inayojengeka baada ya ongezeko la posho za wabunge ni kama wapo kwa maslahi yao binafsi, ukweli unabaki kuwa hawawezi kuwa wawakilishi wa hewa. Wanawakilisha wananchi ambao wanaojumuisha watu wenye taaluma na majukumu mbalimbali katika jamii.
Kama daktari ni muhimu kama mbunge, kwanini basi kundi hili dogo (lakini linalosaka kila aina ya nguvu katika jamii ikiwa ni pamoja na kuitwa ‘waheshimiwa’) lipendelewe kwa marupurupu yasiyoendana kabisa na hali ngumu ya uchumi wetu? Kama waheshimiwa wabunge ni muhimu kama madaktari, manesi, walimu na watumishi wengine, kwanini basi wapewe shilingi 200,000 kwa siku huku watumishi wengine wakiwa na mahitaji lukuki ambayo yamekuwa yakipuuzwa na serikali?
Hivi kuwaongezea posho wabunge kutasaidiaje afya za Watanzania? Je, ongezeko hilo la posho litasaidiaje kuinusuru sekta ya elimu inayokwazwa na mishahara kiduchu ya walimu, uhaba wa nyumba na vitendea kazi huku wanafunzi wakisoma katika mazingira magumu?
Je, ni vipi ongezeko hilo la posho za wabunge litawasaidia askari polisi kuepuka vishawishi vya rushwa ambavyo kwa kiasi kikubwa vinachangiwa na maslahi duni?
Lakini tatizo kubwa zaidi linalosababishwa na ongezeko la posho za wabunge ni hili: kama serikali ina uwezo wa kutoa nyongeza ya posho kwa wabunge inamaanisha kuwa fedha si tatizo kwake.
Ninaandika hivi kwa sababu sidhani kama kuna mtu yeyote (ukiondoa wabunge wetu) anaamini kuwa maslahi ya wabunge wetu ni duni. Hatujawahi kusikia kuna mbunge ametishia kujiuzulu au kugoma kwa vile kipato chake cha mamilioni hakitoshelezi mahitaji yake, na wala hakuna mbunge aliyekonda kwa vile mshahara wake haumwezeshi kumudu gharama za chakula. Sana sana tunashuhudia vitambi vya baadhi ya waheshimiwa wetu vikizidi kuongezeka sambamba na kasi ileile ya malalamiko kuwa “maslahi ya wabunge ni duni.”
Hakuna anayependa kuona madaktari wakigoma hasa kwa vile wahanga wakubwa wa migomo ya aina hiyo ni walalahoi wasioweza kwenda India (au kwingineko) kupata matibabu. Na tungependa sana kuiunga mkono serikali katika maelezo yake ya kila siku kuwa haina fedha za kuboresha maslahi ya watumishi wake lakini tutaonekana wendawazimu tukifanya hivyo wakati serikali hiyohiyo inayodai iko hoi kifedha inamudu matumizi makubwa yasiyo ya lazima kwa kuwaongezea posho wabunge.
Sipendi kubashiri hili lakini kuna uwezekano mgomo wa madaktari ni mwanzo tu wa mlolongo wa migomo mingine ya watumishi katika sekta mbalimbali za umma huko mbele. Japo sina hakika serikali itamudu vipi mzigo wa posho za wabunge, kilicho wazi ni kwamba kelele za makundi mbalimbali ya jamii pamoja na wananchi kwa ujumla kupinga ongezeko hilo la posho kimepuuzwa na serikali, na kwa kuzingatia uzoefu itakuwa miujiza kama serikali itabadilisha uamuzi huo usiozingatia hali halisi ya nchi yetu (hasa kwa vile ilikuwa na fursa ya kukataa maombi ya wabunge lakini ikaamua kuyaendekeza).
Nihitimishe makala hii kwa kuitahadharisha serikali kuwa ‘imefungua kopo la minyoo’ kwa kutoa nyongeza ya posho kwa wabunge katika kipindi ambacho watumishi wa sekta mbalimbali za umma wanaelekea kuishiwa na uvumilivu wa kusubiri ahadi hewa za kuboreshewa maslahi yao.
Wakati nyongeza hiyo ya posho kwa wabunge inaweza kuwaongezea nguvu ya kuiunga mkono serikali (hata pale maslahi ya wanaowakilishwa na wabunge hao yanapowekwa shakani) hali itakuwa mbaya pindi harakati za watumishi wa umma kudai maslahi bora zinatakapomaanisha migomo zaidi.




Mkulo ‘amgomea’ Spika kujibu swali bungeni
 
Tuesday, 31 January 2012 22:07
Habel Chidawali, Dodoma
WAZIRI wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo jana ‘alimgomea’ Spika wa Bunge, Anne Makinda kujibu swali lililomtaka aeleze kama chenji iliyorejeshwa na Uingereza kutoka kwenye ununuzi ya rada, ingetumika kununua madawati kwa ajili ya wanafunzi shuleni.

Hata hivyo, baadaye Mkulo alisema hakufanya hivyo makusudi, bali alikuwa hajasikia akiitwa na Spika kujibu swali hilo na kuahidi kuwa makini zaidi katika siku zijazo.

Ilikuwa kichekesho bungeni baada ya Spika kumwita Waziri Mkulo kwa takriban mara nne, akimtaka ajibu swali hilo lililoulizwa na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Martha Mlata lakini hakusimama kujibu.

Kitendo hicho kiliwafanya baadhi ya wabunge waduwae huku waziri huyo akiendelea kuwa kimya.
Tukio hilo lilitokea baada ya Mlata kuuliza swali hilo la nyongeza lililotokana na swali na msingi ambalo liliulizwa na Mbunge wa Musoma Mjini (Chadema), Vicent Nyerere.

Katika swali hilo, Mlata alitaka kujua namna Serikali ilivyojipanga katika matumizi ya fedha hizo za rada na kama kuna mpango wowote wa kuzitumika katika kupunguza tatizo la uhaba wa madawati shuleni.
Swali la msingi la Nyerere lilijibiwa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Elimu), Kassim Majaliwa.

“Swali hilo naomba Waziri wa fedha ujibu, waziri tafadhali jibu swali hilo. Waziri wa Fedha… namtaka waziri ajibu si yupo?” alisema Spika Makinda lakini, Mkulo hakusimama.

Makinda alisisitiza: “ Hilo swali anatakiwa kujibu waziri mwenyewe na asijibu naibu wake. Jamani Waziri wa Fedha hayupo? Vipi mbona kimya kuna nini? Haya endelea naibu waziri.’’

Wakati wote ambao Spika Makinda alikuwa akimtaka Mkulo kusimama na kutoa majibu, waziri huyo alikuwa akiteta jambo na Waziri wa Tamisemi, George Mkuchika ambaye alisimama pia kutaka kutoa majibu lakini, Makinda alimzuia awali kabla ya kumruhusu kutolea ufafanuzi jambo hilo. 

Baada ya kuona hali hiyo, Majaliwa alilazimika kusimama na kusogelea kipaza sauti na kulieleza Bunge kuwa zaidi ya Sh18 bilioni zitapelekwa huko kwa ajili ya kununulia madawati. 

Alipotafutwa baadaye na gazeti hili ili aeleze kwa nini hakutii amri ya Spika ya kusimama na kujibu swali hilo, Mkulo alisema: “Sikumsikia na kwa kuwa maswali yanaulizwa bungeni basi subiri kesho (leo) nitajibu ili irekodiwe.”
Makinda alishawahi kutangaza bungeni kuwa Mawaziri wanatakiwa kuwa makini kwa kila swali au jibu linalotolewa ndani ya ukumbi kwani wakati wowote anaweza kumtaka yeyote kujibu swali au kutoa ufafanuzi.

Serikali ya Uingereza ilikubali kuilipa Tanzania Pauni 29.5 milioni wastani wa Sh75bilioni, ambazo zilizidi katika biashara ya rada kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya BAE Systems.

BAE Systems ilikiri mahakamani kwamba pamoja na kupoteza kumbukumbu, lakini rada hiyo iliuzwa kwa bei kubwa ikilinganishwa na thamani halisi.

Fedha hizo ziliwahi kuibua mvutano kati ya Serikali ya Tanzania na Uingereza, baada ya kutaka fedha hizo zipelekwe kwa asasi za zisizo za kiserikali nchini.

Baadaye Uingereza ilikubali kuzikabidhi fedha hizo zifikie mikononi mwa Serikali ya Tanzania na kuelekezwa katika sekta ya elimu, ikiwa ni pamoja na kununulia vitabu na vifaa vingine ikiwemo madawati.

Sakata hilo la rada bado linaendelea kuitikisa nchi baada ya uchunguzi wa Taasisi ya Makosa Makubwa ya Jinai ya Uingereza (SFO), kuchunguza baadhi ya vigogo wa Serikali ya Awamu ya Tatu akiwemo aliyekuwa Mwanasheria Mkuu, Andrew Chenge ambaye anadaiwa kukutwa na kiasi cha Dola za Marekani 1.2 milioni katika Kisiwa cha Jersey.  

CHANZO: Mwananchi


1 Feb 2012


Moja ya mambo ambayo ninajitahidi sana kuepukana nayo ni malumbano.Hata hivyo,kwa vile kila binadamu ana mtizamo wake na sote tuna uwezo wa akili unaotofautiana,kuna nyakati nalazimika kuingia kwenye malumbano hususan unapotokea upotoshaji wa makusudi dhidi yangu au kazi yangu.

Jana niliweka makala moja fupi yenye kichwa cha habari "EXCLUSIVE TO KULIKONI UGHAIBUNI: Rais Kikwete Azungumzia Kauli ya Pinda Kuhusu Posho za Wabunge." Katika makala hiyo niliambatanisha picha za mazungumzo (yasiyo rasmi) kati yangu na Rais Kikwete kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter.

Sasa jamaa mmoja huko Twitter anayetumia 'handle' ya @majaliwa68 ameamua kushikia bangu makala hiyo,hususan matumizi ya neno 'Exclusive.' Alianza kwa kuandika 


Sasa sijui tatizo la ndugu yangu huyu lilikuwa nini hadi hapo.Lakini ukidhani kuwa aliishia hapo,subiri usome hukumu yake zaidi kuhusu makala hiyo,kama picha zifuatazo zinavyoonyesha (pamoja na majibu yangu)



Sijui kama muungwana huyu anajua lolote kuhusu uandishi,uwe ni wa makala au wa kuandika kwa minajili ya kujifurahisha tu.Ninaandika hivyo kwa sababu laiti angejihangaisha kutafuta maana ya habari ambayo ni 'Exclusive' angemaizi kuwa ni "habari ambayo awali imetolewa kwa chapisho moja tu." Ninaamini nilikuwa na kila sababu ya kuiita habari hiyo 'Exclusive' kwa sababu chanzo chake kilikuwa mazungumzo yangu (yasiyo rasmi na Rais kwenye Twitter.Lakini kwenye elimu ya maneno (Semantics), 'Exclusive' pia inamaanisha "kwa ajili ya mtu/kundi au kitu/vitu fulani tu,pasipo kuwa kimefanywa na watu mtu mwingine au kundi jingine/kitu kingine/vitu vingine."

Kwa upande mmoja,kama mwandishi niliona mazungumzo hayo yasiyo rasmi na Rais kuhusu jambo linalotawala akilini mwa Watanzania wengi (kauli ya Pinda kuwa Rais ameridhia ongezeko la posho za wabunge lakini Rais kupitia Ikulu amekanusha hilo) ni habari yenye umuhimu wa kipekee (na katika Semantics,upekee pia ni exclusive kwa Kiingereza).

Kwa upande mwingine,habari hiyo ilikuwa maalum kwa wasomaji wa blogu hii na ndio maana kichwa cha habari kilikuwa "EXCLUSIVE TO KULIKONI UGHAIBUNI..." Kwa kuwajali na kuwathamini wasomaji wa blogu hii niliona habari hiyo inaweza kuwa yenye interest kwao,hasa ikizingatiwa si kila aliyepo Twitter anadiriki kumuuliza Rais maswali mbalimbali (na si kila anayeuliza anajibiwa).Sasa sijui ndugu yangu @majaliwa68-ambaye ninaamini si mosmaji wa blogu hii-alikerwa na nini baada ya mie kufanya jitihada hizo za kuwapatia wasomaji wa blogu hii kile ambacho laiti kingekuwa kwenye vyombo vya habari 'conventional' kingeitwa SCOOP.

Ndio.Hiyo ni mithili ya Scoop kwani Rais kutolea ufafanuzi kukinzana kwa msimamo wake na Waziri Mkuu wake si jambo dogo.Na habari husika haikubeba 'tweets' zangu na Rais tu bali nilijaribu kuwasilisha 'background' ya tukio zima-kuanzia habari iliyochapishwa na gazeti la Mwananchi na tamko la Ikulu.

Kabla sijaendelea zaidi,naomba niwasilishe shutuma zaidi kutoka kwa Ndugu @majaliwa68


Sasa sijui kama 'EXCLUSIVE' maana yake ni "kuongea na mtu kwa kina" neno la Kiingereza 'INDEPTH' litakuwa na maana gani!Na sijui by "kuongea kwa kina" Ndugu @majaliwa68 alitaka niandike makala ndefu kama thesis ya PhD au alitamani iwe na maneno mengi kama makala zangu kwenye jarida la Raia Mwema!

Hakujihangaisha kutambua kuwa lengo la makala yangu halikuwa kutoa hukumu,kukosoa,kurekebisha au kuchangia 'tweets' za Rais.Nilichofanya ni kuwasilisha kauli zake kama zilivyo (na nilifanya hivyo kwa kutumia picha ili isionekane nimepandikiza maneno yangu mdomoni mwa kiongozi mkuu wa nchi.)

Bwana @majaliwa68 akaendelea na 'busara' zake kama ifuatavyo:

Well,ameshasema hapo juu kwamba kwa uelewa wake, 'EXCLUSIVE' ni 'kuongea kwa kina.' Ukimuuliza 'kina' ni urefu wa kiasi gani sidhani kama atakuwa na jibu la maana.

Akazidi kuchambua


Sijui amehesabu mara ngapi kuona kila 'tweet' ya Rais Kikwete imewekwa bloguni hapa kama 'EXCLUSIVE'!!!Halafu,ni upuuzi wa hali ya juu kudai "kila aliyejibiwa na Rais wakimbilie exclusiveness." Ni upuuzi kwa sababu,kwanza,si kila anayejibiwa na Rais ni mwandishi au bloga,na pili,suala la kuandika au kutoandika ni uamuzi wa mtu binafsi.Lakini pengine hoja ya msingi zaidi ni kwamba mtu ataandika vipi kama HWEZI KUANDIKA?Ninasema hivyo kwa sababu kuna wanaodhani uandishi ni suala la kukurupuka tu.Hii ni fani na ina utaalamu wake.Na licha ya kuwa fani yenye utaalamu wake,si kila anayeweza kuandika atamudu kuandika kitu cha msingi.Kwa lugha nyingine,uandishi ni kipaji kwani japo takriban kila anayejua A,B,C...Z  anaweza kuandika lakini kuandika makala yenye hoja za msingi ni kunahitaji zaidi ya uwezo wa kuandika tu.

Hakuishia hapo,akaendelea

Ndio maana nilisema huyu mtu si msomaji wa blogu hii na wala hana idea yoyote kuhusu uandishi.Kadhalika,nadhani Bwana @majaliwa68 bado ana mtizamo mithili ya ule wa Zama za Mawe (Stone Age) ambapo 'kuzungumza' lazima iwe 'mdomo kwa mdomo.' Yaani kwake,uki-tweet chat na mtu au ukiibua mjadala huko Facebook basi huko sio kuzungumza.Kwa faida yake ninapenda kumfundisha kuwa chanzo cha habari kinaweza kuwa chochote kile alimradi kinaaminika na habari husika ni ya kweli.Sasa sijui mtu huyu alitaka mpaka Rais aongee nami kwa simu au ana kwa ana ndipo niwe na haki ya kuandika "Rais amezungumza..." Jamani fani nyingine si zenu na ni vema kuwaachia wanaojaribu kuzimudu au wanaozimudu kabisa.

Kwa leo amemalizia na 'tweet'  ifuatayo

 Mdau Kelvin Manaseh (@kmanaseh) akachangia hoja hii


Nami nimehitimisha mjadala kwa 'tweets zifuatazo




Kama nilivyotanabaisha hapo mwanzo,sipendelea malumbano lakini nimelazimika kukabiliana na upotoshaji wa Bwana @majaliwa68 ambao kimsingi ninaamini ni matokeo ya kukurupukia jambo asilolielewa.Hajui 'EXCLUSIVE TO...' inamaanisha nini,na kwa uelewa wake fyongo,mazungumzo yanayotokana na vyombo vipya vya mawasiliano kama Twitter hayana sifa ya kuitwa mazungumzo.

Hizi ni baadhi ya changamoto tunazokumbana nazo mabloga na wengineo tulioamua kutumia muda wetu kuuhudumia umma kwa njia ya uandishi.

Katuni kwa hisani ya Said Michael na Global Publishers

31 Jan 2012


Rais Jakaya Kikwete amekiri kuwepo kwa mkanganyiko uliojitokeza kufuatia kauli ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuwa Rais ameridhiria nyongeza ya posho za Wabunge.Rais alisema hayo katika majadiliano kati yangu na yeye kupitia mtandao wa Twitter kama inavyoonyesha picha hapa juu na hapa chini


Awali,Rais Kikwete alifafanua kuwa ni kweli alitoa maelekezo kuhusu suala la posho hizo lakini maelekezo hayo hayakuwa kuridhia jambo hilo.Kadhalika,Rais alibainisha kwamba alikubali haja ya kuangalia upya posho za wabunge na aliwataka wabunge kutumia hekima na busara katika kutafakari.Vilevile aliwataka wabunge kutumia Kikao cha Februari cha Bunge kulizungumzia upya suala hili,na kusistiza ni muhimu.Picha ifuatayo inaonyesha maelezo hayo ya Rais Kikwete kwenye mtandao wa Twitter.


Jana,gazeti la Mwananchi lilikuwa na habari iliyobeba kichwa 'JK ABARIKI POSHO MPYA ZA WABUNGE' ambapo pamoja na mambo mengine habari hiyo ilieleza kuwa Waziri Mkuu Pinda amesema kuwa tayari Rais Kikwete amesaini kuridhia ongezeko la posho za vikao (sitting alllowances) kwa wabunge kutoka shilingi 70,000 hadi shilingi 200,000 kwa siku.Picha ifuatayo inaonyesha sehemu ya habari hiyo:


Hata hivyo,mapema leo Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu ilitoa taarifa ya maandishi kukanusha habari hizo, kama inavyosomeka hapa chini

Taarifa Ya Ikulu

Blogu hii inaendelea kufatilia kwa karibu kuhusu suala hilo.

JK abariki posho mpya za wabunge 
Monday, 30 January 2012 20:54
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
KILA MMOJA KULIPWA 330,000 KWA SIKU, ZITTO, MAKAMBA, KIGWANGALA WASULUBISHWA KWA KUZIPINGA
Waandishi Wetu, Dodoma  
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amesema tayari Rais Jakaya Kikwete amesaini kuidhinisha ongezeko la posho za vikao (sitting allowance) kwa wabunge kutoka Sh70,000 hadi Sh200,000 kwa siku.  Kupitishwa kwa posho hizo ambazo ziliandikwa kwa mara ya kwanza na gazeti hili, kunafanya sasa mbunge kupokea Sh330,000 kwa siku; Sh200,000 zikiwa ni posho ya kikao, Sh80,000 posho ya kujikimu na Sh50,000 nauli.  

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya kikao cha utanguzi cha wabunge jana, zilidai kuwa baada ya Pinda kutoa taarifa hiyo, wabunge walishangilia huku Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, akisimama na kudai kuwa taarifa alizonazo ni kwamba Rais Kikwete alikuwa hajasaini kuidhinisha posho hizo.  

Hatua hiyo ilisababisha Mbunge wa Kondoa Kaskazini, Juma Nkamia (CCM), kusimama na kuhoji iwapo Zitto ni miongoni mwa wasemaji wa Rais kabla ya Pinda kusimama na kuthibitisha kusainiwa kwa posho hizo akisema siyo ajabu kwani hata watumishi wa Serikali wanalipwa kati ya Sh150,000 na Sh200,000.  Hata hivyo, Zitto alitetea msimamo wake kwamba alitarajia baada ya kusainiwa kwa posho hizo na Rais, angepewa masharti mapya ya kazi za ubunge.  

Katika kikao hicho baadhi ya wabunge wanadaiwa kuwashambulia Zitto, Mbunge wa Bumbuli (CCM), January Makamba na Mbunge wa Nzega (CCM), Dk Khamis Kigwangwala kwamba wamekuwa mstari wa mbele kupinga posho hizo hadharani.  Spika wa Bunge, Anne Makinda ambaye anadaiwa kwamba aliungana na Pinda kuthibitisha kwamba Rais Kikwete ameidhinisha posho hizo mpya, pia aliwashambulia wabunge wanaozipinga akisema kwamba wanafuta umaarufu wa kisiasa.

“Wanachotafuta ni umaarufu wa kisiasa tu, mimi ninavyojua umaarufu wa kisiasa unakuja kwa kufanya kazi za kibunge za wananchi lakini siyo kupinga posho,” chanzo chetu cha habari kilimnukuu Makinda.

Mbunge wa Gando (CUF), Khalifa Suleiman Khalifa anadaiwa kwamba alitumia mafumbo  kuwashambulia wabunge hao ambao wamejitokeza kupinga nyongeza hiyo ya posho.  Kauli hiyo inadaiwa kuungwa mkono na Mbunge wa Sikonge (CCM), Said Nkumba ambaye alidai kuwa hawezi kumsemea Zitto kwa sababu ni kawaida yake kupinga, lakini akaelekeza shutuma zake kwa Makamba kwamba ameanza kupinga baada ya kugharamiwa na CCM. “Januari anapinga posho hizo kutokana na CCM kumpa gari, nyumba na analipwa na chama,” kilisema chanzo chetu kikimkariri Nkumba.

 Pia, Mbunge wa Kilindi, Beatrice Shelukindo (CCM), anadaiwa kumshambulia Zitto kuwa lazima apinge posho hizo kwa sababu, anapewa fedha na wafadhili kutoka nchi za nje.  “Shelukindo anasema amefanya ziara nje na kuhakikisha kuna wahisani wanamfadhili Zitto kwa hiyo ana haki ya kupinga posho hizo,” chanzo chetu hicho kilimkariri Shelukindo.
 
Hata hivyo, inadaiwa kuwa baada ya mashambulizi hayo, Dk Kigwangwala alisimama kutetea msimamo wake kwamba ongezeko hilo halina ‘mashiko’ na haliwezi kuelezwa mbele ya umma likaeleweka, lakini alizomewa na wabunge wengi huku wakimtaka kukaa chini.  

Hatua hiyo ilisababisha Zitto kusimama na kueleza kuwa tatizo la wabunge kwamba wana fikra finyu, kauli ambayo alitakiwa na wenzake kuwaomba radhi kuwa amewatukana.  “Zitto ametumia Kiingereza kuwa tatizo la wabunge ‘we think small’,  Shelukindo na (John) Komba wakaja juu wakitaka kuwaomba radhi kwa kuwatukana,” chanzo chetu kilieleza.  Zitto anadaiwa kusema wabunge walitakiwa kujenga hoja ya kuongeza fedha za mafuta ya gari wanayolipwa hivi sasa Sh2.5 milioni kwa mwezi, kutokana na kupanda kwa nishati hiyo, lakini siyo posho.  

Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika alinukuliwa akisema matatizo ya posho yamefikia hapo baada ya kuonekana ni ya watu binafsi siyo mfumo hivyo, wanaopinga wanaonekana kama wanatafuta umaarufu na wana vipato vya fedha, akaitaka kamati ya uongozi ijadili na kupata mwafaka badala ya wajumbe kutofautiana mbele ya umma.  Wabunge wengine wanaodaiwa kutetea posho hizo ni Mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini na Jenister Mhagama (Peramiho CCM).

 Msimamo wa January
Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Makamba alijibu: “Si sahihi kwangu kutoa taarifa za kikao cha ndani. Lakini msimamo wangu kwenye suala hilo unajulikana na haujabadilika.  Msimamo wa CCM ulishawekwa wazi na sote tunaujua. Nitalizungumzia suala hili kwa kirefu katika siku zijazo.”

Kuhusu taarifa kwamba anagharamiwa na CCM, alisema hawezi kuzungumzia suala hilo na badala yake kutaka kiulizwe chama hicho.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alipoulizwa kuhusu taratibu za kuwagharamia viongozi wa chama chake ambao ni wabunge alisema: “Mbunge au kiongozi yeyote wa chama mwenye nafasi nyingine anagharamiwa na chama pale anapokwenda kufanya shughuli za chama tu na si vinginevyo.”

“Kwa hiyo kama ni mbunge suala la mafuta, dereva, mahali pa kulala na mahitaji mengine anagharamiwa na taasisi anayoifanyia kazi na siyo chama.”

“Kwa mfano, mimi kwenye sekretarieti hata posho za vikao huwa sichukui, nadhani na mwenzangu January naye sidhani kama huwa anachukua posho, kwa sababu tukifanya hivyo ni kama tunakiumiza chama, huo ndiyo msimamo wetu na uko wazi wala siyo kificho.”

Kwa upande wake, Zitto alisema jana kwamba hakuwa katika nafasi ya kuzungumzia suala hilo na badala yake kuahidi kwamba atalizungumza leo atakapokutana na waandishi wa habari.

Wabunge walia njaa
Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho zilisema wabunge hao walilalamikia kucheleweshwa kulipwa posho zao za wiki mbili walizokaa Dar es Salaam wakati wa vikao vya kamati.

Walidai hivi sasa wanaishi kwa shida huku wakihoji sababu za kucheleweshewa.

Imeelezwa kwamba Spika Makinda alidai kuwa fedha hizo zipo na kwamba  kilichochelewesha ni uhakiki wa wabunge waliohudhuria vikao.

Makinda alisema baadhi ya wabunge wamekuwa wakilipwa posho za vikao bila kuhudhuria, hatua ambayo imesababisha Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG), kuhoji maswali mengi.

CHANZO: Mwananchi

Blandina Nyoni

Lucy Nkya

Default Kituko Wizara ya Afya, Blandina Nyoni haivi na Lucy Nkya. Hawasalimiani hata wakikutana kwenye kordo

Ndugu zangu hii taarifa nimeipata kutoka kwa wandani wangu aliopo pale Wizara ya Afya. Kwamba Katibu Mkuu wa Wizara Bi Brandina Nyoni haivi na Naibu Waziri wake, Bi Lucy Nkya. Na inadaiwa kuwa hata wakikutana kwenye kordo huwa hawasalimiani. Kinachowazungumzisha ni Madokezo tu. 


Taarifa inasema kwamba ugomvi wao ulitokana na kitendo cha Katibu Mkuu kutaka kumlazimishia kumpa Dereva (Elias Mkumbo) ambae ni Informer wake. Mama Nkya alipotonywa na watumishi wa pale akamkataa huyo Dereva na ali command alitewe dereva aliyekuwa nae kutoka Wizara aliyokuwepo kabla kama sivyo abadilishiwe. Tangu wakati huo Wakuu hawa wa Wizara wamesusiana (Kama wanavyosema watu wa Pwani). 


Blandina Nyoni amekumbwa na matukio mengi ya kususiana na Wakubwa wenzako toka alipokuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii ambapo alikuwa haivi na hasalimiani na Waziri wake Bi Shamsi Mwangunga. Alipohamishiwa Afya mwishoni mwa 2008 pia akagombana na Naibu Waziri wa wakati huo Bi Aisha Kigoda na hadi anaondoka Wizarani hapo bado walikuwa hawaivi. Sijui huyu Mama ni Mtu gani? Maana hata watumishi wake kuazia alipokuwa Hazina, Maliasili na Sasa Afya wamekuwa wamkimkataa kutokana na Uongozi wake Mbovu wa kutojali maslahi halali ya watumishi wake mfano malipo ya likizo, uhamisho, extra duty allowances, etc!
CHANZO: Jamii Forums 


Kwa hisani ya  King Kinya na Global Publishers

29 Jan 2012

Hello to everyone, first and foremost thank you to the blogging community for supporting my family though the past couple of years. 
Growing Up African Season II is coming up bigger & better than ever before. As you know sponsorship takes a while so we are working through it. 

Sema Ukweri is a New Blog created by myself Johnson Lujwangana. It's presents my LIFE and my viewpoint living in both Tanzania & America.
The Blog will take you from a street corner in the Bronx to a busy restaurant in Sinza. From a party in las Vegas to a mellow dinner at Sea Cliff. 
Depending on my location and it changes everyday, you'll always get to read a mind scratching article. 
Is Man City the best team? Is college even worth it anymore? Who's the sexiest celeb in Bongo? What's the best trends in the industry?
What hairstyles workout for men? When should a man think about proposing? Is it okay to have a child out of wedlock? Am I my father's MIRROR! 

The BLOG is different and presents a real perceptive on today's issues. We all have issues, so I hope by being truthful it can help some of my readers in theirs.
CLICK ON the LINK BELOW, you thank me for it. 


PS: I decided to spell Ukweri instead of UKWELI just out of respect. 


Problem Solving Flowchart
CHADEMA ndio wamesababisha mgomo wa madaktari

Wanabidii
TAARIFA za kiintelijensia zimebaini kuwa CHADEMA ndio wamesababisha mgomo wa madaktari, mgomo ambao umeendelea kwa siku kadhaa sasa na umehatarisha maisha ya wagonjwa wengi na umesababisha hata madaktari kuvuana uanachama kwenye chama chao cha madaktari.

CHADEMA ndio hao hao wamekuwa wanaratibu migomo mingi kwenye vyuo vikuu, ndio haohao wameratibu mgomo wa madereva wa malori kule Mbeya lakini pia ni CHADEMA walio hakikisha Naibu Waziri wa Afya anagoma kwenda kuonana na madaktari pale kwenye ule ukumbi walioandaa wao maana protokali na
usalama wake ulikuwa hatarini.

Hawa CHADEMA hawafai, maana wanataka nchi isitawalike, Wanafanya haya wakijua kuwa Rais Kikwete yuko kwenye mkutano wa uchumi duniani na kule anakutana na kuongea ikiwa ni pamoja na kupiga picha na Bill Gates na matajiri wengine wa dunia ili watusaidie kujikwamua kutoka kwenye mkwamo wa njaa na uchumi mbovu.

CHADEMA ndio hawa hawa wamesababisha sasa hivi shilingi yetu imeshuka thamani maana muda mwingi wanautumia kuwasumbua watu waliokuwa wanajua matumizi ya shilingi na sasa wamekasirika na matokeo yake shilingi imeshuka thamani.

CHADEMA ni watu wabaya sana, maana baada ya mgomo huu wa madaktari wataandaa mgomo mwingine waliouahirisha na walimu mwaka jana, wanachowaza CHADEMA ni migomo tu ili serikali idorore na nchi isitawalike, CHADEMA ni chama cha fujo na maandamano.

Chama hicho kimewezesha mgomo mpaka ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na kusababisha wale makada wenye magamba kugoma kuvua magamba yao! Hiki chama ni kibaya sana kinawanyima usingizi viongozi na makada wa chama cha magamba.

Watanzania mtambue kuwa CHADEMA ni chama kibaya sana maana ndicho kimesababisha minong’ono, eti Dk. Harrison Mwakyembe amewekewa SUMU! Nani amuue kiongozi huyo?

Mwakyembe hana tatizo kubwa anaugua tu mafua na hata ripoti yake ni CHADEMA hao hao ndio wameizua, maana wanajua kuwa ikiwekwa hadharani italeta tena mambo yake yenye harufu ya ki - Richmond.

CHADEMA ni watu wabaya sana, maana wamesababisha maisha magumu kwa kila Mtanzania, tofauti na ahadi za CCM kutaka kuwapa maisha bora kila Mtanzania, chama hicho kimesababisha mpaka umeme unatolewa kwa mgawo na unakatika katika mara kwa mara.

Tusiwaamini watu hawa, maana wanataka kuiondoa serikali iliyoko madarakani kwa maandamano kwa madai kuwa imeshindwa kuboresha huduma za msingi kwa Watanzania.

Nadhani sasa ni wakati muafaka kwa CHADEMA kimsababishe Rais Jakaya Kikwete agome kuingia IKULU, ili nchi iingie kwenye uchaguzi kabla ya mwaka 2015, kwakuwa huko kote kutakuwa mbali sana.

Hii ni siri yako! Hata yale mafuriko yaliyotokea jijini Dar es Salaam na kusababisha ndugu zetu kuhamia kwenye majumba ya nguvu kule Mabwepande, ni jamaa hawahawa wakiongozwa na makamanda wao. Hawa jamaa ni nuksi!


CHANZO: Tanzania Daima



Although this guy claims "I know anytime you sing for god [sic] it doesn't matter how you sound..." this kind of singing could very well annoy God


28 Jan 2012



Kwa niaba ya wasomaji wa blogu hii naomba kukutakia heri kwa siku yako ya kuzaliwa.Ni matumaini yangu kuwa utaendelea kuwa accessible na kudumisha dhana ya uongozi ni pamoja na kuwa karibu na wananchi.Ninatumaini pia kuwa tutaendeleza mijadala mbalimbali kwenye 'kijiwe chetu' cha Twitter.

Enjoy your big day!


Rais Barack Obama akiwa na wageni wake,Rais Mstaafu George H.W. Bush  na mwanae Gavana wa zamani wa Florida  Jeb Bush,walipomtembelea Ikulu ya Marekani Ijumaa iliyopita

CHANZO (na kwa habari kamili): Politico

25 Jan 2012


Rais Kikwete amefungua milango

Rais Kikwete msibani kwa Marehemu Mbunge Regia
Rais Kikwete msibani kwa Marehemu Mbunge Regia
KWA mara ya pili ndani ya takriban kipindi cha wiki moja, Tanzania imepoteza wabunge wawili. Kabla majonzi hayajatuisha kutokana na kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu kupitia CHADEMA, Regia Mtema, taifa likapatwa na msiba mwingine wa Mbunge wa Arumeru Mashariki kwa tiketi ya CCM, Jeremiah Sumari.
Kila kifo kinaacha pengo lakini kifo cha kiongozi (awe wa familia kama mzazi au wa jamii) kinaacha pengo linalowagusa na kuwaathiri wengi. Japokuwa yayumkinika kuhisi kuwa katika zama hizi za siasa za kuendekeza maslahi kuna wanaofurahi vifo vya viongozi kwa vile vitatoa nafasi ya wao kugombea, ukweli unabaki kuwa ni vigumu kupata mrithi atakayelingana kwa kila kitu na marehemu (hasa katika utekelezaji wa majukumu).
Kama nilivyoandika katika makala ya wiki iliyopita kuhusu kifo cha Regia, njia bora ya kumuenzi marehemu Sumari ni kudumisha mema yote aliyofanya wakati wa uhai wake. Kwa wanaofikiria kumrithi nafasi yake (na kwa atakayeteuliwa kumrithi nafasi ya Marehemu Regia) changamoto kubwa itakuwa kwenye kuwaenzi viongozi hao kwa kuwajibika ipasavyo. Japo utendaji kazi bora wa kiongozi anayerithi madaraka kutoka kwa kiongozi marehemu hauwezi kurejesha uhai, kwa kiasi fulani unasaidia kupunguza machungu ya wananchi walioathiriwa na pengo lililotokana na kifo husika.
Katika mila na desturi za kiafrika, shughuli ya msiba inatawaliwa na majonzi na kwa kiasi kikubwa ni kumbukumbu kwa kila aliyehai kuwa sote “tulitoka kwenye udongo na tutarejea kwenye udongo.” Misiba inapaswa kutukumbusha kuwa sote ni wasafiri na kila nafsi ya mmoja wetu itaonja mauti.
Moja ya matukio yaliyotawala msiba wa Regia ni habari kwamba Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willbroad Slaa, alikwepa kusalimiana na Rais Jakaya Kikwete. Habari hiyo ilichukua uzito mkubwa kiasi cha kukaribia kufunika tukio la huzuni lililowakutanisha viongozi hao huko Ifakara.
Kwa sababu anazozijua mwenyewe, jamaa mmoja aliamua kusambaza waraka katika blogu kadhaa ndani na nje ya nchi kukemea kitendo hicho cha Dk.  Slaa. Mtu huyo ambaye hakufanya jitihada za kuficha itikadi yake ya siasa, akaenda mbali zaidi na kudai kuwa kilichosababisha Katibu Mkuu huyo wa CHADEMA kutosalimiana na Rais ni amri iliyotolewa na mwenza wa Dk. Slaa (Josephine).
Pengine kwa kuelewa kuwa kukalia kimya jambo hilo kungeibua maneno zaidi, hatimaye Dk. Slaa alieleza kilichomfanya ashindwe kusalimiana na Rais Kikwete. Kwa wanaojua protokali, mtu hakurupuki tu na kwenda kusalimiana na kiongozi mkuu wa nchi hasa ikizingatiwa kuwa kumkaribia kiongozi huyo (hata kama ni kwa nia nzuri) kunawafanya walinzi wake watafsiri kama tishio la usalama kwake.
Kadhalika, Dk. Slaa alieleza bayana kuwa kilichompeleka Ifakara ni kumzika Regia na si vinginevyo. Kwa lugha nyingine, alimaanisha kuwa isingehitaji kutokea kifo cha mbunge au kiongozi wa chama ndipo “mahasimu wawili” (kama ‘wazushi’ wa habari hiyo walivyojaribu kutuaminisha) wakutane na kupeana mikono.
Lakini kama kuwasuta wanaokuza matukio madogo, siku chache baadaye vyombo vya habari vilitawaliwa na picha inayomwonyesha Rais Kikwete na Dk. Slaa wakipeana mikono baada ya mazungumzo kati ya Rais na viongozi wa CHADEMA yaliyofanyika Ikulu ya Magogoni, Dar es Salaam.
Sijui waliozusha kuwa Josephine alimkataza Dk. Slaa wanasemaje kuhusu hilo. Labda watazusha kuwa alimtoroka mwenza wake kama sio kuzusha kuwa kiongozi huyo wa CHADEMA aliamua kuambatana na viongozi wenzie Ikulu ili kujisafisha kutokana na tukio la Ifakara.
Inasikitisha kuona mambo ya msingi yakigubikwa na porojo zisizo na mashiko. Binafsi, moja ya mambo ya msingi yaliyonigusa na kunipa matumaini mapya ni jinsi Rais Kikwete na takriban uongozi wake mzima (serikalini na huko CCM) walivyoweza kuweka kando tofauti za kiitikadi na kumzika Regia kama kiongozi wa Watanzania na si mbunge wa CHADEMA pekee.
Mara kadhaa nimekuwa nikishutumiwa kwa kumkosoa au kumlaumu Rais Kikwete. Lakini siku zote nimejitahidi kusisitiza kuwa lawama hizo na kukosoa hakumaanishi chuki au husuda bali ni kwa minajili ya ustawi wa taifa letu.
Natambua kuna uwezekano wa baadhi ya wasomaji kuhisi nimefikia hatua ya kumpongeza Rais Kikwete kwa vile tukio husika linaihusu CHADEMA (ambayo nimekuwa nikituhumiwa kuipendelea na baadhi ya watu, huku wengine wakidai mimi ni mwanachama wa chama hicho.)
Yeyote aliyesoma salamu za rambirambi zilizotolewa na Rais Kikwete kwenda kwa familia ya marehemu Regia na CHADEMA hatoshindwa kubaini kuwa zilikuwa zimetoka moyoni kwa dhati. Hakukuwa na hata chembe ya tofauti za kiitikadi bali hisia za kibinadamu pindi zinapopatikana habari za kifo.
Naomba nisisitize kuwa tukio hilo sio pekee au la kwanza kwa Rais Kikwete kuonyesha kile wanachokiita Waingereza ‘human side’ (ubinadamu wake, kwa tafsiri isiyo rasmi). Mara nyingi mkuu huyo wa nchi ameonyesha kuguswa kwa dhati kila anapokuwa kwenye matukio ya huzuni.
Japo wakati mwingine huishia kulaumiwa kuwa ‘haisaidii kuonyesha uchungu ilhali janga husika lingeweza kuzuilika’ (kwa mfano kwenye matukio ya milipuko ya mabomu huko Mbagala na Gongo la Mboto), hiyo haindoi ukweli kuwa ameguswa na matukio hayo.
Lakini pamoja na pongezi hizi kwa Kikwete na CCM kwa ujumla pengine ni muhimu kukumbushana kuwa kama tunaweza kushikamana wakati wa misiba kwa nini basi iwe vigumu kufanya hivyo nyakati nyingine?
Kwa lugha nyingine, kwa nini tusubiri hadi kiongozi wa chama cha upinzani afariki ndipo tuonyeshe kuwa tofauti za kiitikadi haziondoi ukweli kuwa sote ni Watanzania tunaoweza kutofautiana kimtizamo au kiitikadi pasipo umuhimu wa ‘kuong’oana’ macho.
Japo Kikwete si mahiri katika kuendekeza siasa za uhasama (aidha kwa vile si muumini wa dhana hiyo au anatumia wasaidizi wake kukwepa lawama zinazoweza kuelekezwa kwake), kiujumla chama anachoongoza, yaani CCM, kimekuwa kikifanya jitihada kubwa kuuaminisha umma kuwa vyama vya upinzani ni mithili ya mikusanyiko ya maharamia wasioitakia mema nchi yetu.
Ukisikiliza hotuba za baadhi ya viongozi wa CCM wanapovizungumzia vyama vya upinzani unaweza kabisa kutamani kwenda Idara ya Uhamiaji kuhoji iwapo viongozi hao wa upinzani ni raia halisi wa nchi hii. Hivi haiwezekani kukosoana pasipo kupandikiza chuki ya uadui miongoni mwetu?
Katika tafiti za kitaaluma, kuna hatua ambapo mtafiti huwezi kubashiri matokeo ya utafiti husika kwa kuzingatia dhana alizotengeneza (hypothesis). Japo makala hii si sehemu ya utafiti lakini ningependa kutengeneza dhana kuu mbili zinazoweza kubashiri matokeo fulani.
Ya kwanza, kwa vile Rais Kikwete na CCM wameweza kututhibitishia kuwa tofauti zao za kiitikadi na CHADEMA si za kiadui, na ndio maana wameshiriki kikamilifu katika msiba wa marehemu Regia, Tanzania inaingia kwenye zama mpya za siasa za upendo na kukosoana kistaarabu.
Ya pili, kwa vile siku chache baada ya msiba wa mbunge wa CHADEMA, Rais Kikwete aliwaalika viongozi wa CHADEMA kufanya majadiliano nao, tunaanza kushuhudia ukurasa mpya wa ushirikiano kati ya Rais (na pengine CCM kwa ujumla) katika uongozi wa nchi.
Matokeo yanayotarajiwa ni kwamba badala ya muda mwingi wa ujenzi wa taifa letu kutumika kunyoosheana vidole, kuitana majina ya ajabu ajabu na upuuzi mwingine, sasa tunaweza kuona uongozi wa nchi ukifanya kazi bega kwa bega kwa lengo la kuikomboa Tanzania yetu kutoka katika lindi la umasikini (licha ya rasilimali lukuki tulizojaliwa) na kuunganisha nguvu kukabiliana na kundi la maharamia walioigeuza nchi yetu kuwa ‘shamba la bibi’ kwa ufisadi.
Unaweza kudhani labda aya tatu za hapo juu nimeziandika nikiwa ndotoni. La hasha. Kila nililoandika linawezekana kwani sababu (ya kushirikiana) ipo, na uwezo wa kufanya hivyo upo (kama ilivyothibitika katika tukio hilo la msiba wa marehemu Regia), ila kinachokosekana ni nia tu.
Ni matarajio ya safu hii kuwa Rais Kikwete (ambaye naamini anasoma makala hizi au anasimuliwa na wasaidizi wake) hatorudi nyuma katika kufungua sura mpya ya siasa za maelewano na ushirikiano kwa manufaa na ustawi wa Tanzania yetu. Penye nia pana njia.




Tim Gunn reveals he hasn't had sex in 29 years, but doesn't feel like 'less of a person' for it 

The 'Revolution' host says he's been celibate since the end of a 'very intense relationship'

Wednesday, January 25 2012, 12:10 PM

 Fashion consulant Tim Gunn arrives for the finale of the Bravo TV reality show "Project Runway" at the Tribeca Grand Hotel.

JAMES KEIVOM/NEW YORK DAILY NEWS

Tim Gunn revealed his celibacy Tuesday, but added, 'I don't know what's around the corner.'

Tim Gunn made it very clear Tuesday that nothing will be off limits on his new daytime talk show, "The Revolution" — including himself.
The "Project Runway" mentor opened up about his nearly 30-year sexual dry spell on the show, but said he had nothing to be ashamed of.
"I haven't had sex in 29 years," he revealed. "Do I feel like less of a person for it? No. Not even remotely."
Gunn, 58, explained that a former lover had so scarred him in all matters intimate that he just hasn't had a sexual relationship since.
"I was in a very intense relationship for a long time and my partner ended it, saying quite frankly that he was impatient with my sexual performance," he said. "It was at the cusp of AIDS, and I think a lot of people simply retreated because they were concerned about their health.
"I'm a perfectly fulfilled person ... but it's very psychological," he said.
Gunn, who is openly gay, added that just because he has gone nearly three decades without sex doesn't mean he isn't open to possibilities down the line, however.
"I have feelings. It's not as though I am some barren forest," he said. "I don't want to imply to anyone that I have a mandate that says no sex. I don't know what's around the corner.
"I'm happy to be healthy and alive, quite frankly."
SOURCE: NYDaily News


Jasusi ChatBot

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.