11 Mar 2008

Mmoja wa polisi wa ngazi za juu hapa Uingereza,Chifu Konstebo wa Greater Manchester Police,Michael Todd,amekutwa amekufa.Habari zaidi zinapatikana hapa

MAKALA HII YANGU ILITOKA KATIKA GAZETI LA MTANZANIA TAREHE 07 MACHI 2008

Unafiki wa viongozi wetu wa dini

na evarist chahali, uskochi

MADA yangu ya leo, najua dhahiri itawakera wateule wachache wa aina fulani. Lakini kabla ya kuwapasha, naomba nizungumzie suala la imani na dini hapa ninapoishi Ughaibuni.

Nilipofika hapa kwa mara ya kwanza, nilionyeshwa majengo kadhaa ambayo huko nyuma yalikuwa Makanisa, lakini sasa yamegeuzwa kuwa kumbi za disko na klabu za usiku.

Na hao walioyageuza Makanisa hayo kuwa sehemu za starehe, wala hawakujishughulisha kabisa katika kubadili mwonekano wake, bali wameyaacha yatoe ushuhuda kuwa huko nyuma yalikuwa sehemu za ibada.

Nilipofanya udadisi kwa wenyeji, niliambiwa kwamba makanisa hayo yaliuzwa baada ya kuwa matupu kutokana na ukosefu wa waumini. Wengi wa waumini wa makanisa ya mji huu ninaoishi, ni ama wahamiaji waliotoka nje ya nchi hii kama mimi, na au vikongwe vya hapa hapa.

Binafsi, sina majibu ya moja kwa moja kwamba tatizo la hawa wenzetu ni nini. Hata hivyo, ninachofahamu ni kwamba kuna watu kadhaa ambao wanajitambulisha kuwa hawana dini, na au hawaamini kuwapo kwa Mungu.

Imani ni suala la mtu binafsi, na hivyo pengine si mwafaka kuhoji kwa nini fulani anaamini, ama haamini kuwapo au kutokuwapo kwa Mungu.Ingawa binafsi, ni muumini kwa aina fulani, huwa sisiti kuwasifu wale wasiowaumini wa dini yoyote, lakini wasioona aibu kuelezea msimamo wao wa kidini. Kwa lugha nyingine, watu hao si wanafiki. Wanaeleza bayana kile wanachokiamini na kutokiamini.

Kuna tatizo la msingi huko nyumbani, ingawa natambua dhahiri kwamba watu wengi hawapendi kujadili mambo ya dini kwa sababu ile ile ya unafiki!

Baadhi ya viongozi wetu wa dini, wamekuwa mstari wa mbele kukemea wale ambao wanakwenda kinyume na imani zao, lakini viongozi hao hao wakishiriki kwenye maovu wanayoyakemea.

Ndiyo, tunatambua kwamba mara nyingi viongozi wetu wa dini wana wafadhili wao nje ya nchi. Lakini hicho si kigezo cha wao kuishi maisha tofauti kabisa na wafuasi wao.

Utakuta katika kijiji fulani ambacho kimegubikwa kabisa na umasikini, kiongozi fulani wa dini yeye akiishi kama yuko peponi. Na bila huruma, huyo huyo anayeishi maisha kama ya peponi katikati ya waumini masikini, kwa kutumia kisingizio cha maandiko matakatifu, anawashurutisha waumini wake kujipigapiga ili kuongeza sadaka wanazotoa.

Kinachokera zaidi, ni hili suala la baadhi ya viongozi wa madhehebu fulani kuwa na watoto mitaani, huku sheria za madhehebu yao zikiwa haziwaruhusu kufanya hivyo.

Tatizo hili ni sugu sana, hususan maeneo ya vijijini. Kinachosikitisha ni ukweli kwamba waumini wanafahamu kwamba kiongozi wao wa dini, anaishi kinyume na maadili ya huduma yake, lakini hawachukui hatua yoyote zaidi ya kulalamika chini chini.

Binafsi, ninayo mifano hai ya baadhi ya viongozi wa madhehebu yangu ambao wana watoto lukuki mitaani. Baadhi yao wanatoa huduma kwa wazazi wa watoto wao hao, lakini wengine wamewatelekeza kabisa.

Hawa watu ni wanafiki ambao hawastahili kuachwa waendeleze uhuni kwa kisingizio kwamba daraja walilofikia, haliwezi kutenguliwa.

Mitume wetu waliishi maisha ya uadilifu, ambayo yalishabihiana kwa asilimia 100 na kile walichokuwa wakikihubiri. Na si katika suala la uzinzi pekee, bali hata kwenye dili za kibiashara.Majanga kama ya ukimwi yataondoka vipi iwapo baadhi ya wale wanaopaswa kukemea vitendo vya ngono, kwa vile vinavunja amri ya Mungu, nao ni washirika wa vitendo hivyo?

Pamoja na mapungufu waliyonayo baadhi ya viongozi wa dini, hivi karibuni tumeshuhudia wengi wakijitokeza kuungana na Watanzania wenzao kukemea masuala yanayohatarisha umoja wa kitaifa.

Suala ambalo baadhi ya viongozi hao wa dini wanastahili pongezi, ni katika kukemea vitendo vya kifisadi, ingawa tatizo linakuwapo, pale msimamo huo unapokuwa wa kiongozi mmoja zaidi, badala ya kuwa msimamo wa taasisi ya dini.

Katika hili, napenda nichukue fursa hii kumpongeza Askofu Mkuu mpya wa Kanisa la Anglikana Tanzania, ambaye ameweka bayana msimamo wake dhidi ya vitendo vya kifisadi. Hiyo inatia moyo sana!

Licha ya kukemea ufisadi na maovu mengine katika jamii, asasi za dini zinaweza kubadili tabia za waumini wao kwa kuwawekea vikwazo vya aina fulani. Taratibu za aina hiyo, zipo katika baadhi ya imani, kwa mfano, Wakatoliki, ambao muumini akikiuka kanuni fulani, anazuiwa kushiriki baadhi ya sakramenti.

Kwa nini basi tunaendelea kujumuika na mafisadi makanisani, na au misikitini ilhali matendo yao yanalenga kutuumiza kimaisha? Nafahamu kuwa dini zote zinahimiza upendo, lakini hiyo si sababu ya kutowabana wale wasio na upendo kwa Watanzania wenzao.

Inawezekana kwamba kikwazo kikubwa kwa dini zetu kuwa mstari wa mbele katika kukemea maovu na kubadili tabia za wanaokwenda kinyume na maadili ya kimwili na kiroho, ni hofu ya usafi wa baadhi ya viongozi wa dini hizo, kama nilivyoeleza mwanzoni mwa makala haya.Tatizo hilo linaweza kupatiwa ufumbuzi iwapo viongozi wa madhehebu wataepuka mtindo wa kulindana, na hivyo kuchukua hatua kali kwa walio chini yao, ambao wanakwenda kinyume cha kanuni na taratibu za madhehebu.

Ni wazi kwamba viongozi waadilifu wa dini, hawawezi kuogopa kumnyooshea kidole fisadi fulani, kwa kuwa hata kama fisadi huyo atataka kulipa kisasi, atajikuta hana jambo lolote analoweza kulitumia kushusha heshima ya kiongozi wa dini aliyemkemea.

Busara za Kiswahili zinatueleza kwamba kujikwaa si kuanguka, na hata kuanguka si mwisho wa safari. Wito wangu kwa viongozi wetu wa dini, ni kuongeza jitihada za kuwahudumia waumini wao kiroho na kimwili.

Ni muhimu kwa viongozi hao kuishi kama Mitume ambao mafundisho yao yalikubalika na kuvuta watu wengi, kwa vile wao wenyewe walikuwa waadilifu na mifano bora ya kuigwa na wanadamu.




10 Mar 2008

Weka kando (japo kwa muda) habari zinazovuma za ufisadi,kuna habari njema za warembo wetu wanaotufanya tuamini kuwa nasi tulipendelewa pia na Muumba kwa kutupatia mabinti warembo.Hao wote pichani wanavutia na kumeremeta,ingekuwa ni kuchagua nani bora zaidi ya mwenzie basi majaji wangelazimika kufumba macho na kuchagua kwa kugusa,yaani atakayeguswa kwanza ndio mshindi wa kwanza.Ila binafsi haiba,pozi na mvuto wa huyo model wa tatu kutoka kulia-mstari wa mabinti-vinanishawishi nimpe nambari wani (numero uno)...Yaani utadhani anakuita!!!Au wewe msomaji unaonaje?Big up to Dollywood na wadau wengine wa mambo ya urembo kwa kuvumbua vipaji
Picha kwa hisani ya foto-bloga tishio HAKI

9 Mar 2008


NIMETUMIWA BARUA-PEPE IFUATAYO NAMI NAOMBA KUIWASILISHA KAMA ILIVYO

Sun, Mar 9, 2008 18:24

Subject: Tanzania joined world largest online soccer game!
Date: Sunday, March 9, 2008 15:08
From: Franc de Bok
To:
Conversation: Tanzania joined world largest online soccer game!
Dear Sir/Madam,
I am Franc de Bok a student from The Netherlands and I’d like to bring you something to your
attention.
Since a week Tanzania has joined the community of Hattrick, http://www.hattrick.org , a free online soccer simulation game. It was the 120th nation to do so. Today nearly 1 million people around the world are part of Hattrick and the game has been mentioned in articles in newpapers in many countries.
In Hattrick you can manage your own football team, train players, transfer players, talk to other people in the much praised community. There are also the national teams in each country to which a player can be selected to play in the World Cup.
For the Hattrick community of Tanzania and their national teams it is really important that many people join hattrick and train players. People who join now, will play on a high level and
have a good opportunity to become the National Champion of Tanzania. At the moment 168 people in Tanzania can start a team, 16 people have decided to do so in less than a week.
As I am the National Coach of Tanzania Under 20’s, I’d love to help people with their questions. It would be great If your blog could run an article about this fascinating story of a global internet community around a football game.
We also made a promotional video: http://www.youtube.com/watch?v=uuOUQ0IQqjM in case you want to see some footage about it.

Thank you very much in advance,
more questions are very welcome,
Kind Regards,
Franc de Bok (nickname PolCaf-Bokmans)
U20 National Coach of Tanzania,
The Netherlands
Blijf onderweg online met Windows Live for Mobile! Download 't nu op jouw mobiele

telefoon.

8 Mar 2008

Mzimu wa uhuru wa Kosovo unaendelea kuisumbua Serbia na sasa serikali yake imesambaratika kutokana na tofauti za kimsimamo kati ya Waziri Mkuu,Vojislav Kostunica mwenye mtizamo wa kitaifa (nationalist) na Rais Boris Tadic mwenye mtizamo wa kimagharibi zaidi.Habari zaidi,soma HAPA.

PIA KUNA HABARI MOJA IMENIGUSA SANA KUHUSU BIASHARA YA "UNGA" KATIKA NCHI YA GUINEA BISSAU.UNAWEZA KUISOMA HAPA



Ama kweli Dunia haijaishiwa vituko.

7 Mar 2008

Wengine wanasema Ukimwi ni miongoni mwa dalili kuwa mwisho wa dunia u-karibu.Huwezi kuwalaumu wanaodhani hivyo kwani tatizo hili limekuwa likiendelea kusumbua miaka nenda miaka rudi pasipo dalili ya ufumbuzi.Ni nafuu zaidi kwa waathirika walio kwenye nchi zilizoendelea ambao licha ya kupatiwa misaada ya tiba na ushauri nasaha,wana nafuu zaidi katika matatizo mengine yanayozizunguka jamii katika nchi masikini ikiwa ni pamoja na ufisadi wa raslimali na ngono,masangoma matapeli,unyanyapaa,nk.Inawezekana tiba ya ukimwi ikapatikana mapema kabla ya tiba ya ufisadi huko nyumbani?Anyway,blogu ya Illseed ina habari inayoweza kuleta matumaini kwa mamilioni ya waathirika wa HIV/AIDS.Soma habari hiyo kwa KUBONYEZA HAPA.

5 Mar 2008

Makala yangu ndani ya toleo la wiki hii la gazeti la Raia Mwema inatoa lawama kwa wale ambao baada ya kutajwa kwenye Ripoti ya "Tume ya Mwakyembe" wamekuja na ngonjera za ukabila,eti kuna mpango wa ethnic cleaning dhidi ya kabila flani.Pia makala hiyo inatoa changamoto kwa Bunge kutumia kasi ile ile ya "mwewe" (kama iliyomshukia Zitto Kabwe) kuwashukia wale wote wanaoikejeli Ripoti hiyo ilhali hilo ni kosa kisheria.Kadhalika,wito unatolewa katika makala hiyo kuharakisha uchukuzi wa hatua pindi yanapoibuka mambo yanayohitaji actions dhidi ya wahusika.Sambamba na hilo ni changamoto kwa wansheria "kununua kesi" dhidi ya mafisadi na vikundi vya kijamii kutoishia kulalamika tu bali kuchukua hatua dhidi ya mafisadi.Makala inamalizika kwa wito kwa CCM kutodhani taarifa kwamba kuna kundi la "Agenda 21" ni hadithi za kuvuta muda tu.Onyo la makala kwa chama hicho ni kwamba wakizembea,basi itakuwa kilio pindi maji yatakapozidi unga usiku wa manane wakati maduka yote yashafungwa.Pamoja na habari za makala nyingine zilizofanyiwa utafiti wa kina,soma makala yangu hiyo kwa KUBONYEZA HAPA



















Hillary Clinton amefanikiwa kuibuka mshindi kwenye kinyang'anyiro cha kugombea nafasi ya urais kupitia chama cha Democrats katika majimbo muhimu ya Ohio na Texas na pia Rhode Island  huku mpinzani wake,Barack Obama, akishinda jimbo la Vermont.Pengine ushindi huo wa Hillary unaendana na mtizamo wa baadhi ya wachambuzi wa siasa za Marekani,kama vile David Gergen,ambao wamekuwa wakionya not to count out Hillary mapema hasa kwa kuzingatia namna Clinton political machine inavyofanya kazi.Ni muhimu pia kukumbuka kwamba kwa muda mrefu sana hakuna mgombea aliyewahi kushinda urais wa Marekani pasipo kushinda Ohio,na hiyo inaweza kuelezea umuhimu wa ushindi wa Hillary katika jimbo hilo

Hatimaye Seneta wa Arizona (Republican) John McCain ameshinda nomination ya chama chake kugombea Urais wa Marekani baadaye mwaka huu baada ya kufanikiwa kupata delegates 1195.Kwa mujibu wa Breaking news hii ya CNN,inatarajiwa kuwa kesho (kwa saa za US of A,maana hapa tayari ni Jumatano) Rais George W.Bush atam-endorse rasmi McCain.Kazi kubwa iliyobaki mbele ya Seneta huyo ni kuwaunganisha Republicans wenzie,hususan wale wanaodai kuwa he's not conservative enough kama Rush Limbaugh,Sean Hannity,Ann Coulter na wengineo.Baada ya hapo kinafuatia kimuhemuhe cha kuingia 1600 Pennsylvania Avenue NW dhidi ya Barack Obama au Hillary Clinton.

Jasusi ChatBot

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.