
Heri ya Mwaka Mpya.Well,so far hakuna jipya katika mwaka huu ukiondoa mabadiliko kwenye tarakimu 2010,ambapo sasa inasomeka 2011.Kitu pekee kitakachofanya upya wa mwaka huu (na pengine hapo baadaye) ni mabadiliko.Iwe ya mtu binafsi au ya jamii.Na baraka za Mungu,ofkozi
Nimesoma hotuba ya Rais Jakaya Kikwete kuaga mwaka jana na kukaribisha mwaka huu "mpya".Naomba niwe mkweli.Hotuba hiyo imethibitisha kwa mara ya elfu kidogo kuwa Kikwete is out of touch.Najua hadi hapa msomaji mpendwa unaweza kusema "ah ee bwanaee,kweli wewe unamchukia JK.Yani hata alivyoahidi Katiba mpya bado unamlaumu?".Well,simchukii huyu Mkwere bali siridhishwi na udhaifu wake kiuongozi.
Hotuba ya Kikwete jana inatoa picha wa kiongozi wa nchi ya kufikirika.Badala ya kuwa mkweli kwa anawaowaongoza,anarejea usanii wake wa kwenye kampeni za uchaguzi ambapo yayumkinika kusema aliweka historia kwa kutoa rundo la ahadi,ilhali nyingi ya zile alizotoa mwanzo zikiwa hazijatekelezwa.
Kuna bloga mmoja ameandika makala ya kumpongeza JK kwa kuanzisha mchakato wa Katiba mpya.Tatizo la ndugu yangu huyu ni kuweka busara zake kando kila linapokuja suala linalomhusu JK.Anasahau kuwa umuhimu wa Katiba mpya sio matakwa ya Rais,na hasa ikizingatiwa bayana kuwa Katiba mpya si miongoni mwa vipaumbele vyake (if he has any at all).Lakini pia anapuuza ukweli kuwa tamko la jana ni matokeo ya moto unaowaka kwenye jamii kushinikiza jambo hilo muhimu.Sasa hata kiongozi anapofanya kile anachopaswa kufanya-yaani kusikiza matakwa ya jamii- ni sababu ya kiongozi huyo kuingizwa kwenye vitabu vya historia?This is way too low hata kwa magwiji wa kujipendekeza.
Lakini ili uelewe vema mantiki ya post hii,jaribu kusikia baadhi ya kauli za viongozi wa mataifa yenye hali njema zaidi ya Tanzania,Waziri Mkuu wa Uingereza,David Cameron,kwa mfano wa karibu na ulio mwafaka.Katika salamu zake za mwaka mpya,Cameron amekuwa mkweli kwa Waingereza na kuwaambia licha ya jitihada za serikali yake ya mseto (wa vyama vya Conservative na Liberal Democrats),mwaka 2011 utakuwa mgumu,hususan kutokana na utekelezaji wa hatua za kubana matumizi.Waziri Mkuu huyo alibainisha kuwa hakuna njia ya mkato ya kukabili mwenendo tete wa uchumi wa Uingereza ( sambamba na kuyumba kwa uchumi wa dunia) bali kufanya kinachostahili sasa ili kuepusha madhara makubwa mbeleni.Pia,Cameron,aliwafahamisha Waingereza kuwa tishio la ugaidi bado lipo juu,na akawaomba Waislam wa nchini hapa kusaidia katika mapambano dhidi ya msimamo mkali wa kidini.
Tofauti na Kikwete ambaye sehemu kubwa ya hotuba yake ilikuwa inatoa picha kuwa Tanzania iko shwari kabisa-kisiasa,kiuchumi,kijamii,nk,mwenzie Cameron hakuumauma maneno bali alifanya kile kinachopaswa kufanywa na kiongozi anayejali ncbi na watu wake.Wafadhili wetu wanakuwa wakweli kwa walipakodi wao,sie wafadhiliwa tunavishana vilemba vya ukoka kuwa mambo si mabaya.
Ukisikia namna Kikwete anavyozungumzia uchumi wa Tanzania,unaweza kudhani nchi yetu iko kwenye ngazi ya developed nations,hatutegemei fadhila za wahisani kutosheleza bajeti yetu na tunamudu kwa ufanisi huduma muhimu kwa umma.Uchumi pekee unaoleta maana kwa Mtanzania wa kawaida sio takwimu,kwa vile baba hawezi kuilisha familia yake kwa takwimu.Hakuna mwenye nyumba atakayemwelewa mpangaji wake kwa takwimu,au muuza duka atakayekuuzia bidhaa kwa takwimu badala ya fedha.Umasikini unazidi kuongezeka miongoni mwa Watanzania lakini hilo halimsumbui Kikwete kwa vile takwimu zinaridhisha.
Hebu angalia alivyozungumzia ishu ya umeme!Ahadi juu ya ahadi kama ilivyokuwa wakati wa kampeni.Lakini kingine cha msingi ni ni ahadi kuwa tatizo la umeme linatarajiwa kumalizwa within miezi 36 kutoka sasa.I wish iwe hivyo,lakini itawezekanaje kuwa hivyo katika hali tuliyonayo sasa ambapo sekta ya nishati ni kitegauchumi cha kuaminika zaidi kwa mafisadi?Je dhamira hiyo ya Kikwete ina baraka kutoka kwa akina Rostam?Je wamemwahidi kuwa hakutakuwa na Richmond na Dowans nyingine mara baada ya kulipwa shilingi bilioni 185 kama zawadi ya kutufisadi?Halafu yule bloga wa kujipendekeza anasema JK atakumbukwa kwa historia njema (kuhusu Katiba)!!!
Na wakati ameweza kutetea ongezeko la bei ya umeme,JK alijifanya hajasikia kuwa kampuni ambayo hadi leo hatujui mmiliki wake-Dowans- italipwa shs bilioni 185 licha ya utapeli na ujambazi waliotufanyia.JK alijifanya hakumbuki kauli ya Mwanasheria wake Mkuu,"Mura" Jaji Werema ( pumzika kwa aibu huko Ukuryani,bosi wako JK kakuumbua),kwamba suala la kuilipa Dowans halina mjadala.Kikwete ameshindwa kuwaambia ukweli Watanzania kuwa bei ya umeme inabidi iongezeke ili kupata fedha za kuwalipa wanaharamu wa Dowans.
Kuna wanaoweza kudai JK asingeweza kuongelea ishu ya kuilipa Dowans kwa vile ni suala la kisheria.Je alipozungumzia uwezekano wa serikali yake kukata rufaa dhidi ya hukumu ya Zombe haikuwa jambo la kisheria?
Ndio maana kichwa cha habari cha post hii kinahoji JK amejulia wapi kuwa Watanzania wanahitaji Katiba mpya ilhali yeye anaonekana kuishi nchi tofauti na wanayoishi walalahoi?Amejuaje kuhusu Katiba lakini ameshindwa kujua kuhusu Dowans?Jibu ni rahisi.He is completely out of touch with reality.Anazungumzia kubana matumizi wakati serikali yake inaendeleza matumizi ya anasa na akina Mkulo wanakodi ndege kwa shs milioni tano kuhudhuria mahafali huku shangingi lake likipelekwa "tupu".Au anajigamba kuhusu kubana matumizi kwa vile the so-called "Mtoto wa Mkulima",Waziri Mkuu,Mizengo Pinda alikataa shangingi (lakini akashindwa kuzuwia shangingi hilo kukabidhiwa mtu mwingine!)
Sijawahi kuongelea suala la Katiba mpya,na leo sintoongelea hilo.Ila kwa wanaoanza kudai kuwa yaani kwa KUAHIDI tu mchakato wa Katiba basi JK ataingia kwenye vitabu vya historia,ni vema wakatambua kuwa JK ni GWIJI LA AHADI.Pia wanapaswa watambue kuwa hii top-bottom model of constutitional reforms inaweza kutuletea kilekile tunacholalamikia kuhusu Tume ya Taifa ya Uchaguzi: vitu vinavyofanywa kiujanja ujanja kuendeleza maslahi ya makundi flani.Kinachohitajika sio tume ya mchakato wa mabadiliko ya katiba bali tume HURU ya kushughulikia mchakato huo.








