16 Oct 2011




Tuhuma za kuuawa kwa Mwakyembe na wenzake kwa IGP na Mwandishi wetu FEBRUARI 8, mwaka huu, Dk. Mwakyembe alizungumza na baadhi ya viongozi waandamizi wa Jeshi la Polisi makao makuu ya jeshi hilo jijini Dar es Salaam. 

Baada ya maelezo hayo, polisi walimtaka aweke madai yake kwenye maandishi na siku moja baadaye Dk. Mwakyembe aliwasilisha taarifa yake ya maandishi. 

Dk. Mwakyembe amesema kwenye barua hiyo, “Pamoja na kwamba taarifa hii ni mpya yenye matukio ya takriban mwezi moja tu, naamini kwa dhati kuwa msingi wake (kwa maana ya wahusika na maudhui) hautofautiani na ule wa matukio mengine ya awali ambayo baadhi yake yalisharipotiwa polisi na vyombo vingine vya usalama kwa lengo la kuchunguzwa. 

Maelezo ya Barua ya Mwakyembe “Bado nina imani kubwa na Jeshi letu la Polisi kwamba litaifanyia kazi taarifa hii bila kujali nguvu ya ukwasi na ya kisiasa ya watuhumiwa na kwa kuzingatia misingi ya haki na ukweli. 

“Msingi wa mimi kushtuka na kuamua kulivalia njuga suala hili kwa kuwataarifu watu mbalimbali wenye uelewa na kuvitaarifu vyombo vya dola, ni taarifa nilizozipata kutoka Songea Januari 22, 2011 kuhusu kundi la watu saba lililoingia mjini humo usiku wa Januari 21, 2011 kwa gari iliyodaiwa kuwa ya wizara yangu (Ujenzi) aina ya Land Cruiser yenye usajili nambari STK 68… (ambayo kipindi fulani katika safari hiyo ilibadilishwa namba yake kuwa STK 68…). 

Gari hiyo iliwateremsha “abiria” hao saba sehemu iitwayo Madaba na baadaye kuchukuliwa na gari nyingine (Hardtop Land Cruiser yenye namba za usajili T7…BDU) hadi Top Inn ya mjini Songea. “Majina ya baadhi ya watu hao saba ni Wasomali wawili Hafidh na Faraj; kijana wa Kichagga kwa jina Mustafa a.k.a “Master”; Mkusa, jamaa ambaye wenzake wanaamini kuwa yuko Usalama wa Taifa; na mtu mwingine (jina tunalo) kutoka Tanga anayedaiwa kuwa na utaalamu mkubwa wa kukaba watu. 

“Mwenyeji aliyewapokea Songea watu hao saba ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya (kaitaja) akiongozana na mtu aitwaye Manya. Kilichowafanya baadhi ya watu waanze kulidadisi kundi hili ni dhamira ya safari yao. Tetesi zilisema walikuwa wanaelekea Mbunde kwa mganga maarufu wa kienyeji kwa jina (linahifadhiwa). Hivyo, udadisi ukaongezeka kujua nani anakwenda “kulogwa” safari hii. 

Tetesi zikarejea na jina langu na msululu wa majina mengine: Dk. Slaa (Willibrod), Anne Kilango - Malecela, Reginald Mengi, Profesa Mwandosya na Benard Membe. “Pamoja na kwamba sina imani na ushirikina au nguvu za giza, kutajwa kwa jina langu na fursa ya pekee niliyokuwa nayo ya kujua kilichokuwa kinafanyika, kukanipa ari, nguvu na shauku ya aina yake kutaka kulielewa zaidi suala hili ili ikibidi, niwataarifu wenzangu nao waelewe. 

“Usiku wa Jumamosi Januari 22, 2011 kundi hilo lilielekea Mbunde, wilayani Namtumbo, (kwa gari aina ya Defender STK 26…, likiendeshwa na (jina tunalo) kukutana na ‘mganga’ …ambaye anaishi ndani ya Selous Game Reserve With Impunity. Defender hiyo iligeuza kurejea Songea siku mbili baadaye na kuwaacha ‘wageni’ hao kwa mganga ambako walikaa siku saba ‘wakitengenezwa’. Walirejea Songea Januari 29, 2011 na kesho yake Januari 30, 2011 wakaanza safari ya kurejea Dar es Salaam. 

“Kutoka Songea hadi Mafinga walitumia ile Hard Top iliyowatoa Madaba hadi Top Inn ya Songea (T7… BDU). Walifika Mafinga milango ya saa mbili usiku na kukuta gari mbili zikiwasubiri: Hilux Mayai ya (kampuni moja) na Defender iliyowaongoza hadi Morogoro. Walipokewa Morogoro na askari (jina tunalo). 

Hapo kundi likagawanyika: watu wanne wakiwemo wale Wasomali wawili wakaingia kwenye Nissan Patrol (T8… ADH) mali ya (kampuni jina tunalo) na wengine wakabaki Morogoro. “Kufuatana na ‘mganga’ mwenyewe, ambaye wapelelezi wako wanaweza kuongea naye kama walivyofanya walionipa taarifa hizi, aliwapa masharti ya kutotumia silaha za moto ila njia nyingine kumuua kwanza Mwakyembe, baadaye Slaa, n.k., n.k, n.k. kwa zamu; alitengeneza dawa ya kuwapooza wale wengine (wanaosubiri) kwenye orodha ya kuuawa (Dk. Slaa, Anne Kilango, Mengi, Mwandosya na Membe) wasitaharuki na kupiga kelele za nguvu hata kuamsha hasira za wananchi mauaji yakitokea; aliwazindika vilivyo wasiweze kudhuriwa na tendo la kuua na alitengeneza dawa ya kuwapumbaza “waliohukumiwa kifo” (wawe mfano wa mbwa mbele ya chatu). 

“Jijini Dar es Salaam ‘wahitimu’ hao walifikia Kiwalani karibu na kiwanda cha Mohamed Enterprises. Jirani na kiwanda hicho kuna jengo la ghorofa: Februari 5, 2011, wageni wawili zaidi waliwasili kwa ndege kutoka Uganda; mwanaume mmoja (aliyechanganya rangi) na mwanamke mmoja (mweusi vilivyo). Walipokewa na gari mbili: moja ya polisi (PT 02…) na ya pili yenye namba za kibalozi (aina ya RAV 4). 

Ushiriki wa Al Shabaab “Jioni wakawa na mazungumzo ya kina na Wasomali wawili niliowaelezea awali ambao inadaiwa ni wapiganaji wa Harakat al-Shabaab al- Mujahideen (kwa kifupi Al- Shabaab). “Niliweza kupata picha pana zaidi kwa nini wapiganaji wa kikundi hicho (kinachopambana na wanaodhaniwa kuwa maadui wa Uislamu) wameingizwa nchini. 

Nimeweza kukusanya taarifa zinazodai kuwa awali walifikiriwa kuletwa wapiganaji kutoka Rwanda, lakini wazo hili lilikataliwa na wafadhili wa mpango huu ambao walitaka ‘wanaharakati’ wa aina hiyo watoke Somalia. Ndipo kikundi hicho kikashawishiwa kwamba Tanzania kuna tatizo la udini la Uislamu kutishiwa. 

Mimi na wenzangu hao watano tumejengewa hoja kuwa maadui wa Uislamu tunaotumiwa na makanisa, hivyo hatuna budi kukatishwa maisha yetu. “Niliweza vilevile kupata picha kuwa wafadhili wa kundi hili, wana mahusiano ya karibu na Sheikh …(jina tunalo) ambaye baadhi ya utabiri wake unatokana na agenda za wafadhili hao. 

Inadaiwa kuwa utabiri wa sheikh … mwaka jana ulimlenga Dk. Slaa ambaye alidaiwa kubebwa na makanisa. “Utabiri” huo haukutimia kwa kuogopa kuiingiza nchi kwenye machafuko makubwa ya kisiasa/kidini ambayo yangewaweka pabaya hata wafadhili wa mpango huo. “Inadaiwa kuwa Sheikh … ameombwa tena kutoa utabiri wa mwanasiasa na kiongozi mmoja kupoteza maisha mwezi huu (Fabruari). 

Inadaiwa kuwa mwanasiasa huyo anayetembea na kifo ni mimi na tayari maandalizi ya ‘hukumu yangu’ yamefanywa: “(a) Kijana mmoja kwa jina la Hassan alitumwa kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma siku ya Jumamosi Februari 5, 2011 kwa “maandalizi” hayo (mahali pa kufikia kikosi hicho cha mauaji, utambuzi wa nyumba ya kuishi niliyopangiwa na kumtafuta mhudumu mmoja wa Bunge ili ile ‘portion’ ya mganga ya kunipumbaza kabla ya hukumu, iweze kunyunyizwa kwenye kiti changu Bungeni); “(b) Kesho yake (Jumapili) Februari 6, mnamo saa nne usiku, kikosi hicho cha mauaji kikiwa na watu watano kiliondoka Dar es Salaam kwenda Dodoma kwa gari aina ya Land Cruiser nyeupe ya mkongo (T3… AKU) na kimejichimbia Dodoma mpaka leo (Februari 9). 

“Waliomo kwenye kikosi hicho ni Wasomali wale wawili, mgeni moja (wa kiume) kutoka Uganda, Mustafa a.k.a “Master” na kijana mmoja ambaye Januari 19, 2011 aliwabeba Wasomali hao kutoka Morogoro hadi Ununio kupitia Kibaha na Baobab kwa gari aina ya VX Land Cruiser (T6…APF). Kijana huyo ana shepu ya Kitutsi na anaongea Kifaransa. 

“Utabiri atakaoufanya Sheikh … (pengine aamue kuachana nao sasa baada ya kubaini kuwa tunaujua) utakuwa na lengo la kuwapumbaza wananchi waelekeze macho na masikio yao zaidi kwenye utabiri wake kuliko kwenye njama za kundi hilo za muda mrefu za mauaji. “Kila siku ya Mungu napata taarifa za ziada kutoka kwa raia wema kuhusu suala hili. 

Naziingiza kwenye taarifa hii ili ziwasaidie katika upelelezi: “Inadaiwa kuwa Wasomali hao waliingia nchini kutokea Kenya na wakaja kwa barabara hadi Dodoma. Walitumia gari aina ya RAV4 (new model – T8… AQS) Januari 8, 2011 na kusafirishwa hadi Morogoro ambako walipokewa na askari niliyemtaja awali… wa polisi Morogoro. “Mjini Morogoro, walikaa hoteli mbili tofauti: Hilux Hotel Morogoro na Top Life. 

Aliyewafanyia Wasomali hao booking hapo Top Life ni mmiliki wa hoteli ya….(jina la hoteli na mmiliki tunalo). “Magari waliyotumia wakiwa Morogoro ni RAV4 T8… AQS, VX Land Cruiser STK 1…, Mercedes Benz (Station Wagon) T8… BDT, Toyota Mark II GX100 nyeupe T2… BKR na wakiwa Dar es Salaam wametumia magari VX Land Cruiser T6… APF, Nissan Patrol T8… ADH.” 

“Naomba nihitimishe maelezo haya kuwa nimekuwa muwazi kwa asimilia 100 na hata vyanzo vyangu vya habari ni miongoni mwa watu hao niliowataja katika taarifa hii ambao naamini utachukua hatua ya kuwahoji kulipatia ufumbuzi suala hili. 

“Suala la msingi hapa, si uhai wangu, kwani iko siku lazima nitakufa kama ambavyo hao mafisadi wanaodhani wanaweza kufadhili vifo vya wenzao watakavyokufa hata wao hatimaye, watake wasitake, hakika ni suala la muda tu. Suala la msingi hapa ni mustakabali wa taifa letu, taifa aliloliasisi Mwalimu Nyerere na kulilea kwa misingi ya usawa, haki, umoja, amani na utulivu. 

“Nimejieleza awali kuwa nina imani kubwa na Jeshi letu la Polisi kwamba litaifanyia kazi taarifa hii bila kujali nguvu ya ukwasi na ya kisiasa ya watuhumiwa na kwa kuzingatia misingi ya haki na ukweli. 

“Hata hivyo nalazimika kusema nitasikitika sana ikiwa taswira ya ‘ukorofi’ niliyopewa kwenye kesi moja ya awali (2009) itapewa nafasi kwenye suala hili, hivyo kuninyima fursa ya kusikilizwa vizuri na ulinzi ninaostahili kama raia Kikatiba na kisheria. Niko tayari wakati wowote na mahali popote kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi litakaponihitaji.”

CHANZO: Jamii Forums

Kitu cha karibu na taaluma ya uchumi nilichomudu kukisoma ni Book Keeping(ambayo niliambulia C kwenye mtihani wa Kidato cha Nne) na Commerce (ambayo niliachana nayo Kidato cha Pili).Naomba nikiri,mie ni kilaza wa hesabu,na alama D niliyoipata katika Hisabati kwenye Mtihani wa Kidato cha Nne ilikuwa ni kama A kwangu kwani nilikuwa natarajia F.Sasa kwenye uchumi kuna mambo ya Statistics,which means namba (hesabu).Kuashiria udhaifu wangu kwenye namba,wakati ninasoma shahada ya pili ya uzamili (Shahada ya Uzamili ya Utafiti katika Utafiti wa Siasa-Master of Research in Political Research) nililazimika kuomba ku-drop somo la Quantitative Analysis.Aibu?No,ni ukweli huo!

Anyway,lengo la post hii sio kuzungumzia udhaifu wangu wa namba wala kuelezea kuhusu shule yangu bali ni swali linalonisumbua kuhusu kinachoendelea katika sehemu nyingi za nchi zilizoendelea ambapo kumekuwa na upinzani mkali dhidi ya uroho wa taasisi za fedha (mabenki,nk).

Lakini pengine kabla ya kuelekea huko,swali la msingi linaweza kuwa hili.Inakuwaje nchi kama Ugiriki ikumbwe na msukusuko wa kiuchumi ilhali akina sie (Tanzania) tunaonekana kama "tunapeta" tu?Pamoja na Ugiriki,nchi nyingine ambazo zinasumbuliwa na kuyumba kwa uchumi ni pamoja na Hispania,Ureno,na Italia (ambazo pamoja na Ugiriki zinaunda kinachoitwa PIGS-Portugal,Italy,Greece na Spain).

Hebu wachumi nifahamisheni.Hivi hao PIGS si wapo bora zaidi kiuchumi ukilinganisha na nchi kadhaa za Afrika?Sasa mbona sie tupo kama hakuna tatizo la uchumi?Au sie ni sugu?Au uchumi wetu ni kama haupo?

Halafu kuna hili la harakati dhidi ya uroho wa taasisi za fedha ambazo kwa kimsingi zimeanzia mtaa wa Wall (Wall Street) jijini New York na kupewa jina la Occupy Wall Street,na sasa zinaelekea kusambaa sehemu mbalimbali duniani kama picha zifuatazo zinavyoonyesha.Je,kwanza,kuna uwezekano wa harakati hizo kuhamia nchi masikini?Pili,kwani hazijatugusa hadi sasa?Au ni yale yale ya uchumi usiokuwepo na hivyo kutokuwa na umuhimu wa kuulalamikia?

Nitashukuru sana kama kuna mchumi yeyote atakayeniandikia kwa barua pepe [email protected], kisha nitachapisha hapa,na ninaahidi kuandika makala kwenye jarida la Raia Mwema na kumtaja mchumi mwenye jibu mwafaka

Enewei,hebu tuangalie picha za harakati za "Occupy Wall Street" zilivyosambaa sehemu mbalimbali duniani



 Wall Street,New York,Marekani

 Tokyo,Japan

 Seoul,Korea ya Kusini

 Sydney,Australia

  Sydney,Australia

 Hong Kong

 Zurich,Uswisi

 Seoul,Korea ya Kusini

 Roma, Italia

 Hong Kong

 Frankfurt,Ujerumani

 Roma, Italia

 Stockholm, Sweden

 London,Uingereza

 London,Uingereza

 Sydney, Australia

 Hong Kong

 Julian Assange na waandamani jijini London
 London
London

15 Oct 2011


Simba,Nyati,Faru,Chatu....haya ndiyo majina ya wanyama yanayoweza kukujia akili pindi ukiulizwa MNYAMA YUPI NI HATARI ZAIDI KWA MWANADAMU.Well,amini usiamini,kiumbe hatari zaidi ni mdogo mara elfu kadhaa akilinganishwa kiumbo na hao majabali tunaowafahamu.Na udogo wake si katika umbile pekee bali pia hata sauti yake ni ndogo kulinganisha na mbwa,paka au mbuzi,achilia mbali wababe kama Simba,Chui au Faru.Kiumbe huyo hatari wa kuogopwa kwa gharama yoyote ile ni MBU.

Kwa mujibu wa takwimu,Mbu ni kiumbe hatari zaidi kuliko wote duniani.Kiumbe huyo hatari ni maarufu kwa kuambukiza rundo la magonjwa,kubwa zaidi ikiwa ni homa ya malaria.Lakini pia mbu hueneza homa ya matende (elephantiasis), homa ya manjano (yellow fever),kindiga popo (dengue fever) na homa ya Mto Nile.

KESI DHIDI YAKE: Mbu anawajibika kusababisha kati ya vifo milioni2 hadi 3 kwa mwaka.

VIJIWE (Hangout) VYAO: Takriban dunia nzima lakini zaidi barani Afrika, Asia na Amerika ya Kaskazini

ANAVYOSABABISHA MAAFA:Mbu huambukiza maradhi ya kuuma kwenye ngozi ya binadamu na kumwaga mate yake yenye vijidudu vinavyosababisha homa husika.Ukiweka kando vipele vidogo vinavyotokea mahala alipouma mbu,anayeambukizwa na mbu hatambua maambukizo hadi pale kinga za mwili inaposhtuka (na kuleta dalili mbalimbali).

JINSI YA KUMKWEPA: Njia ya kupambana na mbu na maambukizo ni pamoja na  kutumia chandarua kilichomwagiwa kinga,kuangamiza sehemu za mazalio ya mbu na vidonge vya kinga.
------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Nyoka Wenye Sumu Kali

Japo kuna zaidi ya aina 2,000 za nyoka, 450 kati yao wenye sumu,ni aina 250 tu kati yao ndio wenye uwezo wa kuua binadamu.

KESI DHIDI YAO: Nyoka wenye sumu kali husababisha kati ya vifo 50,000 na 250,000 kwa mwaka.

VIJIWE VYAO: Zaidi ni Afrika,Asia na Amerika ya Kaskazini

WANAVYOSABABISHA MAAFA: Nyoka wana kasi sana na sehemu yoyote katika mwili wa binadamu inaweza kuwa kugongwa na kiumbe huyo hatari.Lakini ni hatari zaidi nyoka anapomgonga mtu kwenye mshipa wa damu kwani hiyo huharakisha kusambaa kwa sumu ya kiumbe huyo.Nyoka hutumia sumu yao kumlegeza mtu na pengine kumpotezea fahamu.Majoka makubwa kama Mfalme Kobra (King Cobra) yanaweza kusimama hadi usawa wa kichwa cha binadamu,huku wengine wakiweza kutema na kurusha sumu yao kutoka mbali kwenda kwenye macho ya mwanadamu.

JINSI YA KUWAKWEPA: Mara nyingi nyingi nyoka hushambulia pale tu pale anapobughudhiwa.Kwahiyo ushauri muhimu wa kuepuka shambulizi kutoka kwa viumbe hao ni kujiepusha nao (Stay away!).Pia ni muhimu kuvaa mabuti kwenye mazingira yanayoweza kuwa na nyoka.Epuka mapori yanayoweza kuwa makazi ya nyoka.Na ikitokea umeomwona nyoka,inashauriwa urudi kinyumenyume taratibu kwani anaweza kujirusha mara nusu ya urefu wake,na mtikisiko kidogo tu unaweza kumasha hasira za kiumbe huyo hatari. 
------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Nge 

Ni kiumbe hatari mwenye sura mbaya maradufu.Inaaminika kuwa ng'e anaweza kuwa anasababisha vifo vingi zaidi ya vile vinavyorekodiwa rasmi,sababu ya kuhisi hivyo ikiwa ni mazingira wanayoishi viumbe hao na ugumu wa kupatikana tiba dhidi ya sumu yao.Hata hivyo,japo kuna aina tofauti 1500 za ng'e ni 25 tu kati yao ambao ni hatari kwa uhai wa uhai wa binadamu.

KESI DHIDI YAO: Ng'e husababisha kati ya vifo 800 hadi 2,00 kwa mwaka

VIJIWE VYAO: Duniani kote hususan Afrika,America ya Kusini na Kaskazini na Asia ya Kati.

WANAVYOSABABISHA MAAFA: Ng'e humlegeza binadamu baada ya kumdunga sumu kwa kutumia "vijisindano" vilivyopo kwenye mikia yao.Kama ilivyo kwa sumu nyingine za wadudu/wanyama,binadamu walio hatarini zaidi ni wale wenye aleji,japo ng'e wengi wenye sumu wanaopatikana Afrika wanaweza kumdhuru mtu yeyote yule.

JINSI YA KUWAKWEPA: Ng'e huwa active zaidi nyakati za usiku na hupendelea kujipumzika mchana.Kwahiyo ni muhimu kuhakikisha sehemu ya kujilaza ipo salama kabla ya kuubwaga mwili.Kadhalika ni muhimu kupunga mavazi na/au soksi kuhakikisha hakuna ng'e humo,vinginevyo itakuwa balaa.
---------------------------------------------------------------------------------------------------------
WENGINEO KWA KIFUPI

Paka Wakubwa (Simba,Chui,nk)


Paka Wakubwa (kwa mfano yaani Simba,Chui,nk) husababisha takriban vifo 800 kwa mwaka
---------------------------------------------------------------------------------------
Mamba
Mamba husababisha kati ya vifo 600 na 800 kwa mwaka
-------------------------------------------------------------------------------------
Tembo
Pamoja na upole wao,Tembo husababisha kati ya vifo 300 na 500 kwa mwaka
---------------------------------------------------------------------
Kiboko
Mwamba huyo wa majini mwenye sura mbaya husababisha vifo kati ya 100 na 150 kwa mwaka
--------------------------------------------------------------------------------------
Konyeza (jellyfish)
Kiumbe huyu wa baharini husababisha takriban vifo 100 kwa mwaka
-----------------------------------------------------------------
Papa
Kiumbe huyu hatari wa baharini husababisha takriba vifo 100 kwa mwaka
----------------------------------------------------------------------
Panda
Husababisha kati ya vifo 5-10 kwa mwaka
-------------------------------

CHANZO: Habari hii imetokana na vyanzo mbalimbali mtandaoni

14 Oct 2011





Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla (wenye suti) akiangalia uzio uliowekwa na mwekezaji katika Kitongoji cha Kinyenze, Kijiji cha Kipera, Wilayani Mvomero, Mkoa wa Morogoro na kuziba njia inayokwenda katika mtaa wa Mwanga  na katika mashamba. Pia mwekezaji huyo raia wa kigeni amechukua sehemu ya mashamba ya wananchi hao bila ya taarifa yeyote kwa Halamashauri ya Kijiji na wananchi.

--
*Mroki Mroki
*
*Director MD Digital Company*
*General Secretary PPAT*
*Professional Photojournalist & BLOGGER
P.O.BOX 110097,*
*Mob: +255 755 373999 */*+255 717 002303,*
*DAR ES SALAAM, TANZANIA*
**

13 Oct 2011


Kuna tofauti kati ya kujipa ujiko na kuongea ukweli.Na japo kujipa ujiko si dhambi as long as ujiko huo ni stahili,lakini ukweli ni shurti usemwe hata kama utaleta tafsiri ya kujipa ujiko,which as pointed out earlier sio kosa la jinai.

Nimekuwa kwenye ulingo huu wa kublogu kwa kitambo sasa.Mara ya kwanza niliandika post ya kwanza bloguni mwezi April mwaka 2006-yaani miaka mitano iliyopita.Lakini mie si muumini sana wa maadhimisho na ndio maana hata blogu hii ilipotimiza miaka mitano nilisahau kuandika chochote kile.Kwa kawaida siku zangu za kuzaliwa husherehekewa kwa sala na simu kwa mzazi,na zaidi ni tafakuri ya wapi nimetoka,nilipo na niendako.Kuna maana gani ya "kusumbua dunia nzima" kwa vifijo na vigeregere kisa umetimiza miaka 50 ilhali akili yako ni haba zaidi ya mwenye miaka 10? (huo ni mfano tu,don't get me wrong).

Anyway,leo nimeamua kuweka flashback ya makala yangu ya kwanza kabisa katika blogu hii.Kimsingi,makala hiyo haikuwa kwa minajili ya kuwekwa bloguni kwa sababu niliiandika kwa ajili ya makala zangu kwenye lililokuwa gazeti maarufu la kila wiki huko nyumbani la KULIKONI.Na ni makala hizo ndizo zilizozua jina la KULIKONI UGHAIBUNI (ie safu hiyo ilibeba jina hilo la Kulikoni Ughaibuni)

Anyway,makala husika ni hii hapa chini

KULIKONI UGHAIBUNI


Asalam aleykum waungwana.

Nadhani kabla ya kubwabwaja mengi ingekuwa ni vema tukatambuana. Lakini kabla ya hapo, ngoja nikunong’oneze kitu kimoja kuhusu gazeti hili mwanana la KULIKONI.Hili sio gazeti la kawaida. Japokuwa hili ni toleo la pili tu, lakini nimeshuhudia kwa macho na masikio yangu maelfu kwa maelfu ya wapenda habari wakisema kwamba gazeti hili tayari limeshakidhi kiu ya wasomaji japo ndio kwanza linaanza. Na nawahakikishia wenye mtizamo huo kuwa hawajakosea. Ama kwa hakika huu ni mwanzo wa tofauti na mazoea. Japokuwa yapo baadhi ya magazeti yanayotoka mara moja kwa wiki ambayo ukilikosa linapotoka usitarajie kulipata siku inayofuata, kwa KULIKONI ukilikosa Ijumaa basi uwezekano wa kulipata kesho yake ni finyu sana. Kwa kifupi, ni gazeti linalokidhi matakwa ya kila aina ya msomaji: mtu mzima kwa kijana, kinababa kwa kinamama, waliojiajiri kwa walioajiriwa, na kadhalika na kadhalika.

Nirejee kwenye kujitambulisha. Mimi ni Mtanzania mwenzenu, na hadi naandika makala haya nipo hapahapa nchini, lakini nitakuwa nikiwaletea makala kutoka huko Ughaibuni ninakoishi. Naamini kuna mengi yanayotokea huko Ughaibuni ambayo ninyi wasomaji watukufu mngependa kuyapata sio kwa mtizamo wa CNN, Newsweek au Times, bali kwa mwenzenu ambae anayaona katika macho ya ki-Tanzania. Labda nifafanue. Mara ya kwanza nilipoombwa sigara na Mzungu nilidhani ni utani. Nilipompatia alinishukuru nusura anilambe miguu.Kumbe yule Mzungu alikuwa ombaomba kama rafiki yangu Matonya (japo ile staili ya Matonya inaweza kuwa kali kuliko zote ulimwenguni).Nilipokutana kwa mara ya pili na jamaa yule alieniomba sigara ,ambapo safari hii aliniomba pauni moja,ndipo nilipogundua huenda akawa ni ombaomba kweli.Uthibitisho niliupata nilipokutana nae kwa mara ya tatu lakini safari hiyo nikiwa na rafiki yangu mmoja Mghana ambae alikuwa hapo Ughaibuni kabla yangu.Huyo mjukuu wa Kwame Nkrumah ndiye alienithibitishia kuwa hapo Uingereza kuna ombaomba lukuki.Niliposimulia hadithi hiyo kwa jamaa zangu hapa baadhi walinibishia.Na walikuwa na hoja.”Mbona tunaangalia BBC kila siku na tunaowaona ni wazungu wanaoonekana kuwa hawana shida hata kidogo”,ilikuwa hoja ya mmoja wao.Ukweli ni kwamba hawa wenzetu wanapenda zaidi kuonyesha yale wanayoyaona kuwa yanaleta picha nzuri ya nchi zao.Angalau balaa la Katrina lilisaidia kuwafumbua macho watu kwamba hata huko kwa George Bush kuna masikini kama hapa kwetu,na wamesahaulika.

Kwa hiyo basi,makala hii itawasaidia Watanzania wenzangu kujua mambo mbalimbali-mazuri kwa mabaya-yanayojiri huko Ughaibuni ambayo ni nadra kwa mtu wa kawaida kuyapata.Naahidi wasomaji watukufu kwamba kama ambavyo hamtopenda kukosa nakala za KULIKONI basi ndivyo hamtotaka kukosa uhondo nitakaokuwa nawaandalia kutoka huko nje.Kama azma ya gazeti hili ilivyo-kuupatia umma chakula cha kila wakati-nami nitahakikisha nawapatia mlo wa kila wakati.Labda tofauti itakuwa ni kwamba mlo huo unaandaliwa kutoka nje.Lakini ugali si ugali tu.Ukitoka Uingreza au ukipikwa Manzese si bado ni ugali.Cha msingi upikwe kwa kuzingatia kanuni za upishi wa ugali.Pengine kingine ni kwamba mapishi haya ya kutoka nje yatakuwa tofauti ni yale uliyoyazowea.Haya yatamlenga mlaji wa kawaida.Kwa ufafanuzi,ni kwamba utofauti wa makala hii ni kwamba kama lilivyo gazeti lenyewe,itakuwa tofauti ni makala mlizozizowea katika baadhi ya magazeti ya kila wiki.Na tofauti yenyewe ni kwamba kipaumbele kitawekwa kwa watu wa kawaida na mambo ya politiki yatakuja tu pale yanapowagusa watu wa kawaida.

Basi hadi Ijumma ijayo,nawaomba make mkao wa Kula ambapo makala motomoto zitaanza kuwajia kutoka Ughaibuni.Ahadi yangu na ya timu nzima ya KULIKONI ni kubeba sauti za watu wa kawaida,na kwahakika hilo linawezekana.

Alamsiki





Kabwe ZuberiZitto, Mb



WaziriKivuli wa Fedha na Uchumi



TAARIFA KWAVYOMBO VYA HABARI



Waziri wa Fedha ndugu Mustafa Mkulo akae pembeni kupishauchunguzi dhidi yake kuhusu Shirika la CHC.

Katika Mkutano wa Nne wa Bunge la Kumi kulitokea malumbano makali kati ya Serikali na Wabunge wajumbe wa Kamati yaHesabu za Mashirika ya Umma kuhusu kuongezwa muda wa Shirika la CHC. WakatiWaziri wa Fedha alileta Azimio la kulivunja Shirika hili lenye taarifa nyingina nyeti kuhusu zoezi la Ubinafsishaji, Kamati ya Bunge ya POAC kutokana nauzoefu wake wa kukagua mahesabu ya Mashirika ya Umma na kufuatilia zoezi laUbinafsishaji wa Mashirika ya Umma, ilipinga hatua hii na kulitaka Bungekukataa Azimio la Serikali na kulifanyia marekebisho makubwa.

Hatimaye Bunge liliridhia kufanya mabadiliko makubwa katika Azimio la CHC, kwa kuamuru Shirikalipewe uhai wa miaka 3 na kuagiza uchunguzi wa namna bora ya kuendesha shughuliza Shirika la Consolidated Holdings. Mapendekezo ya Kamati ya POAC ni kulifanyaShirika hili kuwa la kudumu na kulipa jukumu la kumiliki na kusimamia uwekezajiwa Serikali kwenye kampuni binafsi (National Investment Agency) kama ilivyo Shirikala Tamasek ya Singapore na Shirika la Khazana ya Malaysia. Kwa sasa Uwekezajiwa Serikali katika Kampuni binafsi unasimamiwa na Hazina na usimamizi wake nimbovu na hauleti tija kwa Taifa.

Kitendo cha kushindwa kwahoja Bungeni kiliifedhesha Serikali na hivyo kwa kupitia Wizara ya Fedha kuamuakulihujumu Shirika kwa kumsimamisha Mkurugenzi wake Mkuu kwa makosa ya kimajungumajunguna kwa kuzusha kwamba CHC iliwahonga wabunge ili kuitetea. Waziri wa Fedha ndugu Mustafa Mkulo alilitaarifuBunge kuwa Bodi ya CHC imeomba ukaguzi maalumu kuhusu tuhuma za ubadhirifundani ya Shirika hilo. Niliitaka Serikali ichunguze pia tuhuma kwamba Kamati yaPOAC ilihongwa na kuahidi kuahidi kujiuzulu nyadhifa zangu zote ikithibitika.

Katika Uchunguzi wakeMdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Heabu za Serikali kwa kupitia Kampuni ya Ernest andYoung walitaka kufanya mahojiano na Waziri wa Fedha juu ya tuhuma mbalimbalizinazomkabili ndani ya CHC. Waziri Mkulo alikataa kuhojiwa na wakaguzi nabadala yake akaandika barua (kumb TYC/B/70/2/03 ya Oktoba 8, 2011) yenye kujibutuhuma moja, tena kwa juu juu, kuhusu yeye kuliamuru Shirika kuuza kiwanja cha Shirikabila kufuata taratibu za sheria.

Wakati Waziri anakanusha kuliagiza Shirikakuuza kiwanja kwa mtu aliyemtaka yeye, mimi nina ushahidi tosha wa Nyarakakutoka Hazina, kwa mfano barua TYC/A/290/13/4 ya Machi 9, 2011 ambayo inawagizaCHC kutekeleza agizo la Waziri la Fedha kuhusu kiwanja na. 10 barabara yaNyerere. Vilevile, nina ushahidi wa mkutano uliofanyika huko Morogoro Hotelkati ya Waziri wa Fedha na Mwenyekiti wa Bodi ya CHC kuhusu jambo hilo.

Siku mbili baada yakumjibu CAG, Waziri wa Fedha ndugu Mustafa Mkulo aliamua kutengua uamuzi wakewa kuongeza muda wa Bodi ya Shirika la CHC mpaka mwezi Disemba 2011 na hivyokuivunja. Uamuzi huu wa Waziri una lengo la kuficha ukweli kwani CHC bila Bodiya Wakurugenzi inaendeshwa na Hazina na hivyo taarifa ya ukaguzi itabidiipelekwe Hazina ambayo Waziri wake ni mtuhumiwa.

Uchunguzi wa kina
Ninapendekeza uchunguzi wakina ufanyike kwa kutumia vyombo vya dola na hasa TAKUKURU kuhusu tuhuma hizidhidi ya Waziri wa Fedha na alazimishwe kisheria kujibu maswali ya wakaguzi (Auditors) kuhusu tuhuma dhidi yake.

Wakati uchunguziunaendelea ndugu Mustafa Mkuloasimamishwe kazi ya Uwaziri wa Fedha hadi hapo uchunguzi utakapokamilika.Kitendo chake cha kuiamuru Bodi kumsimamisha kazi aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu kwatuhuma za kutunga na majungu na baadaye kuvunja Bodi ya CHC wakati inasubiritaarifa ya uchunguzi kutoka kwa CAG ni kuingilia uchunguzi na pia ni matumizimabaya ya Ofisi ya Umma ili kulinda maslahi binafsi. Ni dhahiri akiendelea kuwaWaziri wa Fedha ataharibu uchunguzi.Vilevile, Rais wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania ndugu Jakaya Kikwete aangalie kama anaitendea haki nchina Uchumi wa nchi kwa kuwa na Waziri wa Fedha ambaye anasema uwongo Bungenibila kuogopa na mwenye kutumia Ofisi yake vibaya kwa kuchukua maamuziyanayoingilia uchunguzi unaomhusu ili kujilinda.

Taarifa ya Uchunguzi ikabidhiwe kwa Spika
Kutokana na ukweli kwambasuala la CHC lilianzia Bungeni na hata Waziri mwenyewe kukiri kuwa taarifa yauchunguzi inapaswa kuwekwa wazi. Kutokana na matokeo ya sasa ambapo Waziri waFedha mwenyewe ana tuhuma za kujibu na kwamba hivi sasa hakuna Bodi yaWakurugenzi ya Shirika na hata itakayoundwa itateuliwa na Waziri mtuhumiwaninashauri kuwa taarifa ya uchunguzi wa Shirika la CHC sasa ipelekwe kwa Spikawa Bunge kwa hatua zaidi.

KZZ
Dar es Salaam, 13 Oktoba,2011.


Nadhani unaweza kuhoji kwanini kichwa cha habari kimeanza na "KIKWETE UPO..." Well,kama tunavyoelewa,utamaduni wa kijiuzulu ni msamiati wa kigeni kwa viongozi wetu.Kutaraji kuwa Waziri Mkulo atatekeleza ushauri wa Zitto ni ndoto ya mchana.Kinachopaswa kufanyika ni kwa Rais Jakaya Kikwete kumpumzisha Mkulo hadi uchunguzi wa suala hili utakapomalizika.By the way,hatuwezi kuruhusu uwepo wa Waziri wa Fedha anayeandamwa na tuhuma za ufisadi.MTIHANI MWINGINE KWA KIKWETE.Let's wait and see!


Kama nilivyobashiri kwenye MAKALA HII,Kaimu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Benno Malisa ameundiwa zengwe zito kufuatia kauli zake jijini Arusha ambapo pamoja na mambo mengine aliwataka viongozi wenzie wa CCM kuacha kuiandama Chadema.

Kwa mujibu wa habari iliyochapishwa kwenye jarida la Raia Mwema,Malisa anadaiwa kuwa amekuwa akiandaa mazingira mazuri kwa ajili ya Edward Lowassa endapo harakati za kuvuana magamba ndani ya chama hicho zitamkumba.

Japo tuhuma dhidi ya Malisa zinahusishwa zaidi na kitendo cha yeye kufungua mashina ya UVCCM (ambapo anadaiwa kufanya hivyo pasipo kushirikisha uongozi wa umoja huo ngazi ya mkoa) yayumkinika kuamini kuwa kilichomponza kiongozi huyo wa UVCCM Taifa ni kauli zake za kutaka demokrasia ya kiutu-uzima,sambamba na kuikumbusha CCM wajibu wake kuwatumikia Watanzania.

Na hili ndilo tatizo litakalopelekea mauti ya chama hicho kingongwe.Kiongozi au mwanachama yeyote yule atakayeamua kuongea ukweli ataanza kusakamwa na si ajabu akajikuta anavuliwa madaraka,CCM imekuwa ikiongoza nchi kwa namna ya uchawi wa kuwafumba macho Watanzania.Licha ya vyama vya upinzani (hususan Chadema) kuwaamsha Watanzania kuwa chama hicho tawala kinaendesha nchi kwa siasa za kimafia,CCM imekuwa ikijitetea kwa kuwaita wapinzani wachochezi na watu wa majungu,huku ikitumia taasisi za dola kupandikiza migogoro kwenye vyama hivyo.

Sasa anapotokea kiongozi au mwanachama wa kawaida wa chama hicho kuakisi yale yanayosemwa na wapinzani (aambayo kimsingi ni mtizamo wa Watanzania wengi) basi ataandamwa huyo hadi aonekane kama mhaini flani.

Wanachojisahau CCM ni ukweli kwamba kuficha ugonjwa hakuwezi kuwa sehemu ya tiba ya ugonjwa husika.Hata akina Malisa wakikaa kimya na kufuata porojo za "mshikamano wa chama" au "umoja wa kitaifa" ukweli unabaki kuwa ipo siku umma utaamka na kuking'oa chama hicho kwa nguvu kwani wanaweza kudanganya umma wote kwa muda fulani lakini hawawezi kuudanganya milele.

Anyway,soma habari husika hapa chini


Wakati huo huo, hali ya kisiasa ndani ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) ni tete ikibainika kuwa Makamu Mwenyekiti wa umoja huo, Benno Malisa, ameanza kucheza hadharani siasa uasi zinazoendeshwa na kambi inayotajwa kuwa ni ya kigogo mmoja wa CCM mkoani humo. 
Malisa sasa anahusishwa na tukio la hivi karibuni linalohusisha na ufunguzi wa mashina ya chama hicho Arusha mjini, unaotajwa kuratibiwa kinyemela bila viongozi wa chama hicho ngazi ya wilaya na mkoa kutoa kufahamishwa na kwamba, sehemu ya waratibu wa tukio hilo ni vijana waliosafirishwa kutoka wilayani Monduli. 
Taarifa za uhakika ambazo gazeti hili limezipata zinaeleza kuwa tukio hilo halikushirikisha viongozi wa UVCCM mjini Arusha na viongozi wengine wa chama hicho. 
“Mipango yote kwa kiasi kikubwa imeratibiwa na watu wa kutoka wilayani Monduli. Inasemekana kuwa hii ni sehemu ya mkakati wa maandalizi ya watu hao kumhami Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa endapo atabanwa kwenye mkakati wa kujivua gamba wa CCM, basi wajifanye kushusha bendera za CCM kwenye mashina hayo ili kuuonyesha umma kuwa anakubalika sana ndani ya chama,” anasema mmoja wa watoa taarifa wetu ambao ni vijana waliohusika kuratibu mpango huo. 
Hali kama hiyo ya kujiandaa kwa ajili ya mchakato wa kujivua gamba ilijitokeza wakati aliyekuwa Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz pale alipotangaza kujiuzulu baadhi ya vijana waliandaa mabango yenye ujumbe unaomtaka ajisiuluzu na wengine wakihoji hatua hiyo huku taarifa zikisema mabango hayo yaliandaliwa muda gani wakati alikuwa bado kutangaza kujiuzulu. 
Kiongozi mmoja wa UVCCM Arusha anaeleza; “UVCCM Arusha mjini walikataa utekelezaji wa mkakati huo haramu kupitia kikao chake cha Kamati ya Utekelezaji kilichoketi Oktoba 7, mwaka huu, kwa kumwandikia barua Katibu wa Vijana CCM mkoani Arusha.” 
Inaelezwa kuwa barua hiyo ilimjulisha kiongozi huyo kuwa wao kama wilaya hawajapata taarifa rasmi za uzinduzi wa mashina hayo ya wakereketwa na hivyo kwa muda uliobaki wasingeweza kufanya maandalizi mazuri ikizingatiwa wao ndio wenye jukumu la kuandaa mashina hayo na si Wilaya ya Monduli. 
“CCM Mkoa baada ya kupata nakala ya barua hiyo waliamua kuitisha kikao cha sekretariati ya mkoa pamoja na kamati ya utekelezaji ya vijana Mkoa wa Arusha na Wilaya Arusha mjini, Oktoba 8, 2011. 
“Katika kikao hicho maazimio yalikuwa ni kusitisha zoezi hilo hadi hapo taratibu za chama zitakapofuatwa. Chama Mkoa walimwandikia barua hiyo Katibu wa UVCCM Mkoa wa Arusha ili aweze kuwataarifu na viongozi wengine pamoja na wanachama wa umoja wa vijana wa CCM. 
“Baada ya kupata barua hiyo Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha, James Millya, alifanya kikao cha faragha na Mbunge wa Viti Maalumu, Catherine Magige na Benno Malisa. Baada ya kikao chao hicho, waliamua kufanya shughuli hiyo iendelee kama walivyokusudia pamoja na chama kukataza. 
“Jumatatu, Oktoba 10, 2011 walianza kushughulikia kibali cha maandamo na uzinduaji mashina hayo. Hadi saa nne asubuhi polisi waliwanyima kibali cha kazi hiyo,” alisema mtoa habari wetu mwingine ambaye naye amekataa kutajwa jina lake gazetini. 
Inaelezwa kuwa mkutano huo wa kufungua mashina uliofanyika 10/10/2011, ulihudhuriwa na vijana kutoka Monduli na vijana wengine wa vyama mbalimbali vya siasa. 
Katika shughuli hiyo, Benno Malisa ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, alishambulia wazi wazi chama chake akitetea Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( Chadema) chini ya mwavuli wa demokrasia na utawala bora. 
Katika hotuba yake hiyo, Benno Malisa amekejeli hata kauli ya viongozi wenzake wa CCM wanaoonyesha kwamba CCM ni chama tawala na kuonya dola kuingilia mambo ya siasa, hali inayozidi kuashiria mgawanyiko mkubwa ndani ya chama hicho tawala.

CHANZO: Raia Mwema


Rejea taarifa ya msiba wa Mzee Said Muhammad Sikamkono mazishi yatafanyika kesho tarehe 13/10/2011 katika makaburi ya Hainalt Garden of Peace saa nane mchana. Ila kabla ya makaburini tunaombwa wote tufike msikiti wa Sakina Walthamstaw (basi namba 179) saa sita na nusu mchana. Msiba uko nyumbani kwa marehemu Woolwich Dorkyard ambako wote tunakaribisha muda wowote kujumuika na familia ya marehemu wakati huu wa majonzi .Wakina mama pia wanaweza kufika msikitini au nyumbani kwa marehemu kwa ajili ya kutoa pole.

Address ya sehemu ya msiba ni;

Woolwich Ferry
405,Frances Street, London.
SE18 5JU.

Kwa maelezo zaidi  tafadhali wasiliana na;

07813539025 - Haruna mbeyu.Katibu Jumuiya ya Watanzania -london

07766454596 - Abdallah Mdidi

12 Oct 2011


Hello to all you lovely people,

Miss Jestina George Blog has been nominated for the Blog of the Year category at the 2011 (BEFFTA) Black Entertainment Film Fashion Television and Arts Awards. Please show your support by voting through this link, http://www.beffta.com/voting, under category select News 4. Blog Of the Year & Under Nominee select Miss Jestina George then submit your vote. Voting closes on 14th October and your vote would be very much appreciated. If you have any questions please feel free to contact this email.

Thank you for your time,


--
Jestina George
CEO & Founder - MISS JESTINA GEORGE BLOG
Telephone: +447404332910
Facebook: JestinaGeorge


MSIBA WA MTANZANIA MWENZETU MZEE SAID MUHAMMAD SIKAMKONO

Tunaskitika kuwataarifu kuhusu kifo cha Mtanzania mwenzetu Mzee Said Muhammad Sikamkono kilichotokea jana tarehe 11/10/2011 mchana katika hospitali ya Queen Elizabeth, Woolwich, London.
Mipango ya mazishi inaendelea na mtaendelea kujulishwa. Kwa wakati huu ambao tutakuwa tunasubiri kupata taarifa ya mazishi, mwenye kuweza kuchangia chochote au mwenye kuhitaji kujua zaidi kuhusu msiba huu, tunaomba awasiliane na;
Sheikh Ayub kwa namba; 07944930708
AU
 Said Surur kwa namba; 07538063536
AU
Mr. Haruna Mbeyu kwa namba; 07813539025.

“MWENYEZI MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU SAID MUHAMMAD SIKAMKONO MAHALI PEMA.  MUNGU AMETOA NA MUNGU AMETWAA, JINA LAKE LIBARIKIWE”

11 Oct 2011


Nyakati za Ujamaa na Kujitegemea tulifundishwa kuwa maadui wakubwa wa maendeleo ni ujinga,maradhi na umasikini.Na tuliaswa kuhakikisha tunapambana nao kwa nguvu zote.Lakini mambo haya matatu si binadamu bali ni hali ya kimaisha.

Kibinadamu,tulifundishwa kuwa maadui wakubwa ni wanyonyaji-makupe,makabaila,mamwinyi,ma-mangi meza,na viumbe wengine kama hao.

Baada ya itikadi ya Ujamaa kuzikwa hai na aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili,Ali Hassan Mwingi na kundi lake,utambulisho wa maadui zetu ulibaki wa kusuasua.Lakini tulipoingia kwenye siasa za vyama vingi,wakazuka maadui wapya.Kundi moja-ambalo na akina sie (waropokaji au vimbelembele-kama wanavyotuita watawala) lilikuwepo hata zama za Ujamaa.Uzuri au ubaya ni kwamba nyakati hizo haikuwa rahisi kupingana au kuwa na mawazo tofauti na watawala.Na 'vimbelembele' na 'waropokaji' waliishia jela kama si kusumbuliwa kwa muda wao wote wa uhai wao.

Baada ya mageuzi ya kisiasa na kiuchumi,kundi hili limeendelea kunyanyaswa japo kwa wakati huu sio waziwazi.Akina Marehemu Katabalo,Kolimba na wengineo ni majeruhi wa hasira za watawala na washirika wao dhidi ya kundi hili.Na hadi leo wapo wenzetu wengi tu ambao wananyanyaswa na vyombo vya dokla kwa kosa la kusema ukweli ambao watawala na washirika wao hawataki usemwe.

Lakini kundi jipya la maadui baada ya ujio wa mageuzi ni vyama vya upinzani.Pamoja na CCM kuridhia kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi,wapinzani wameendelea kujengewa picha kwenye jamii kama watu wa kuogopwa kama ukoma.Wanahujumiwa kwa fedha za walipa kodi,wanasemwa vibaya na kupachikwa majina mabaya kuliko makupe,makabaila,nk.

'Kosa' kubwa  la wapinzani ni kutaka kuwanyang'anya watawala na washirika wao fursa ya kuendelea kutukandamiza.Wanaonekana kama walafi na waroho wa madaraka (watakuwaje waroho wakati wameingia juzi tu ilhali kuna watu wanazeekea madarakani?).Hoja inayojengwa ni kwamba walikimbia CCM na kujiunga na upinzani si kwa minajili ya kuutumikia umma kwa siasa bali kutokana na tamaa,ulafi na uroho wao wa madaraka.

Ukimsikia mtu kama Nape Nnauye akiwazungumzia wapinzani unaweza kabisa kuhisi kuwa anawazungumzia Taliban au Al-Shabaab.Picha inayojengwa ni ya viumbe hatari kuliko virusi vya ukimwi.

Kwa muda mrefu CCM imekosa sauti za kusisitiza mshikamano wa kitaifa (ambapo hata wapinzani wana jukumu hilo) na badala yake nguvu nyingi zimeelekezwa katika kupanda mbegu ya chuki.Wapinzani wanaonyeshwa kama sio Watanzania,na pale inapobidi kuwakubali kuwa ni Watanzania wenzetu basi jitihada zinafanywa kujenga picha kuwa wenzetu hao wanataka kuitumbukiza nchi yetu kwenye shimo lenye kina kirefu.

'Kosa' jignine la wapinzani ni kutumia nafasi waliyonayo kupigania maslahi ya wananchi,ambao kwa kiasi kikubwa wanaendelea kutapeliwa na watu wanaolipwa mshahara kwa kazi ya kuwawakilisha-I mean Wabunge wetu.Hatuhitaji kuingia kwa undani kuhitimisha kuwa wengi wa wabunge wetu ni sawa na majambazi tu ambao wanalipwa mishahara minono pasipo kuwatumikia wapiga kura wao ipasavyo.Nasisitiza,NI BAADHI TU ya wabunge.

Sasa katika pitapita zangu mtandaoni nimekutasna na habari ifuatayo ambayo kwa hakika imenitia nguvu sana.Kaimu Mwenyekiti wa UVCCM, Benno Malisa ameonyesha ukomavu wa hali ya juu kisiasa kwa kuongea masuala ambayo kwa hakika ni kwa maslahi ya taifa na si ya kichama.

Najua kuna watakaomsema vibaya-hususan ndani ya chama chake-lakini uzuri wa ukweli ni kwamba ukishawekwa hadharani,atakayeumia na aumie lakini hakuna wa kuufuta.Wapo watakaodai Malisa ameanza kumpigia debe mmoja wa wanaotajwa kutaka Urais 2015 (nadhani itakuwa ni Lowassa) na wengine wanaweza kumtuhumu kuwa huenda hata yeye (Malisa) ana nia ya kugombea urais.

Sijawahi kumsifia Malisa lakini kwa hili NINAMPA TANO.Namsihi apuuze tuhuma zote zitakazoelekezwa kwake kwa 'kosa' la kusema 'yasiyopaswa kusemwa.' Laiti tukiwa na viongozi wanaodiriki kueleza hisia zao pasi kuhofia kuwachukiza watu fulani (na wanachokiongea kuwa chenye maslahi kwa umma) basi kwa hakika tunaweza kufanya mijadala muhimu kuhusu taifa letu na kuzika chuki zisizo za msingi dhidi ya wale wanaoongea tusiyopendezwa nayo.

Nisiandike mengi,hebu soma habari ifuatayo:

UVCCM yataka CCM isiifuatefuate Chadema
Monday, 10 October 2011 22:27
Waandishi wetu, Arusha 
KAIMU Mwenyekiti wa Umoja Vijana wa CCM (UVCCM), Benno Malisa amewataka vigogo ndani ya chama hicho tawala kuacha kuingilia mambo ya chama kikuu cha upinzani nchini, Chadema hasa mgogoro wake na madiwani wa Arusha Mjini na badala yake watafute suluhu ya matatizo ya msingi yanayoikabili nchi kama mfumuko wa bei na tatizo la ajira.Akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Hospitali ya Mtakatifu Thomas, Malisa alisema wapo baadhi ya watu ndani ya CCM ambao siyo wana Chadema lakini wamekuwa wakijihusisha na mgogoro wa chama hicho pinzani. 
Alisema wana CCM hao wamekuwa wakiingilia mgogoro kati ya Chadema na madiwani wake ambao tayari chama hicho kilikwishaamua kuwafukuza na kusisitiza kuwa mambo ya chama hicho pinzani yaachwe yasiingiliwe. 
Kauli hiyo ya Malisa inakuja kipindi ambacho Chadema kimekuwa kikilalamikia baadhi ya mawaziri wa Serikali kupuuza uamuzi wake wa kuwatimua madiwani wake.
Chadema imewahi kumnyooshea kidole Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi,) George Mkuchika kwamba alikuwa na ajenda ya siri baada ya kuendelea kuwatambua madiwani hao.
Pia Chadema kimekuwa kikituhumu baadhi ya makada wa CCM mkoa wa Arusha na taifa, kujaribu kuingilia uamuzi huo wa Chadema wa kutimua madiwani hao kutokana na uamuzi wao wa kuingia muafaka wa Umeya wa Arusha. 
Kaimu Mwenyekiti huyo wa UVCCM, alisema si sahihi kwa CCM kutumia hata vyombo vya serikali kudhoofisha demokrasia kwa vyama vya upinzani akionya kwamba
mwisho wa siku matokeo yake hayatakuwa mazuri kwa taifa. 
Alisema demokrasia inapaswa kuachwa ichanue kwa vyama vya upinzani ili kujenga ustawi mzuri wa nchi.

“Nitumie nafasi hii kumuomba Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), kaka yangu (Godbless) Lema kuwa mstari wa mbele katika kuleta umoja na mshikamano hapa mjini na kumaliza tofauti za UCCM na UCDM (U - Chadema) ili wakazi wa Arusha wapate maendeleo. Sasa uchaguzi umekwisha tujenge nchi yetu.” 
Alisema CCM kinapitia katika wakati mgumu hivi sasa na kuonya kwamba badala ya kuisimamia Serikali wapo wanaohangaika kutafuta wachawi na kutuhumu watu. 
“Tuache kabisa. Hili jambo halisaidii chama wala taifa letu, kumekua na dhana na fikra potofu juu ya ushindi wetu wa 2010 matokeo yale na tuliyoyaona Igunga ni funzo kwetu na hasa vijana,” na kuongeza kuwa vijana wengi wameanza kukosa imani na CCM kwa sababu: 
“Tunashindwa kuwaonyesha kuwa tuna majibu ya matatizo yao. Tumebaki tunaimba historia na kumtaja Baba wa Taifa na kutumia nukuu zake bila kuwapa matumaini vijana kuwa Tanzania yao itakua njema, watapata elimu nzuri, afya na itakua ya uhakika.” 
Alisema vijana wanataka kusikia uchumi umekua, ajira zinapatikana, fursa za kujiajiri zipo, mikopo inapatikana na kusisitiza: “Tusipotoa matumaini haya na kuyafikia 2015, wapiga kura milioni sita wapya watatukataa, uelewa wa vijana wa Kitanzania sasa umekua mkubwa. Wanajua haki na wajibu wao tuache kufanyia siasa maisha ya Watanzania.” 
Wanaotaka urais 2015
Akizungumzia mbio za urais kwa mwaka 2015 ndani ya CCM, Malisa aliwataka makada wa chama hicho wanaotaka kuwania nafasi hiyo kuacha kuwagawa vijana na kuvuruga chama akisema kufanya hivyo ni hatari kwa uhai wa chama. 
“Wapo baadhi ya watu wanaopita wenzangu msiishi kwa kutarajia madaraka ya kupewa wapo wengine wanapita wanakusanya CV za vijana na kuwaahidi vyeo vya U-DC. Msipotoshwe na wala msifungwe fikra kwa sababu mmepewa ahadi ya kuteuliwa U DC. Tuna bahati mbaya wapo ambao mpaka leo wanaishi kwa kusubiri U DC wamegeuka kuwa ndiyo mzee na watumwa kifikra, tuukatae utumwa huu UVCCM.” 
“Tusiwe ndiyo mzee. Nawaagiza wenyeviti na makatibu wa mikoa na wilaya zote Tanzania, wafuatilie katika halmashauri zao kujua mipango ya maendeleo inayohusu vijana na kufuatilia utekelezaji wake wakiona hakuna utekelezaji, watumie kamati za siasa za wilaya kuwabana wenyeviti wa halmashauri. Nazitaka wilaya zote zifuatilie zituletee taarifa juu hili jambo. Tusikubali kuwa ndiyo mzee lazima tusimamie maslahi ya Vijana.” 
Alisema huu si wakati Serikali ya CCM kukaa likizo badala yake ifikirie namna ya kufikia matarajio ya Watanzania. 
Dowans
Akizungumzia suala la mitambo ya Dowans Malisa alisema: “Watu waliosababisha hasara wawajibike, walitudanganya. Kama taifa leo tumeshindwa kesi mitambo ile waliyosema haifai leo inatumika na kampuni ya Symbion. Wanatufanya Watanzania mazuzu. Walisema heri tukae giza wakati wao wanatumia majenereta na wanalipiwa na Serikali huku wakinunua aspirini kwa mamilioni.” 
“Leo wanajifanya wazalendo. Nilitarajia wawajibike walidanganya taifa, Serikali ikavunja mkataba. Wakasema mitambo haifai mibovu leo imenunuliwa na Wamarekani na wanatuuzia umeme... wanafiki wametufikisha hapa niwaombe UVCCM na vijana wa vyama vyote tuungane hawa wawajibike.” 
Watunishiana misuli na polisi
Kabla ya kuhutubia, Malisa na msafara wake waliingia katika mgogoro na vyombo vya dola, baada ya kufanya maandamano na mikutano ya uzinduzi wa matawi mapya ya UVCCM ambayo awali, yalizuiwa na polisi kabla ya kuruhusiwa baadaye. 
Mamia ya vijana wa CCM walianza kukutana kuanzia asubuhi katika Ofisi za UVCCM mkoani hapa, lakini walipoanza matembezi walizuiwa na polisi mbele ya Jengo la CCM Mkoa. 
Sababu ya kuzuiwa inaelezwa kuwa ni mgogoro ndani ya chama hicho katika Wilaya ya Arusha. Viongozi wa umoja huo wanadaiwa kupinga ziara ya viongozi hao wa kitaifa. Hata hivyo, maandamano hayo yaliendelea baada ya mazungumzo baina ya polisi na viongozi hao wa UVCCM huku wakikubaliana njia za kupita. 
Lakini, mara baada ya kukamilika kwa uzinduzi wa matawi hayo viongozi wa umoja huo walionyesha kukerwa kwao na hatua ya polisi na baadhi ya viongozi wa chama hicho kutaka kuzuia kazi hiyo. 
Habari hii imeandikwa na Mussa Juma,Peter Saramba na Moses Mashalla


CHANZO: Mwananchi



Ubinafsi hauwezi kukusaidia kutengeneza marafiki wengi lakini inaelekea utakusaidia kupata mafanikio kazini.

Utafiti mpya umebaini kwamba watu wasio wabinafsi na wenye roho nzuri ndio wanaopendwa zaidi lakini wakati huohuo wameonekana kama wasiofaa kufukiriwa kwa ajili ya kupandishwa vyeo makazini.

Utafiti huo umeonyesha kuwa ujeuri na kiburi ni ishara za uwezo (nguvu) ilhali upole na wema unachukuliwa kama dalili za udhaifu.

Utafiti uliofanywa na Chuo cha Utawala ya Kellogg,Chuo cha Masomo ya ngazi ya juu ya Biashara cha Stanford na Chuo cha Biashara cha Tapper katika Chuo Kikuu cha Carnegie Mellon ulilenga kuchunguza aina ya maisha ya mtu tunayoihusisha na uongozi.

Katika mlolongo wa majaribio matatu,watafitiwa waliwekwa kwenye makundi,kisha watafiti walichambua tabia zao katika matumizi ya ishara zilizotumika kama fedha; jinsi gani baadhi waliamua kubaki na ishara hizo kwa ajili yao binafsi huku wengine wakiziingiza ishara hizo kwenye hazina ya kundi.

Wale wenye tabia za kibabe walionekana kama wenye tabia 'alpha' (alpha personalities).

Mhariri mwenza wa ripoti ya utafiti huo, Rober Livingston wa Chuo cha Biashara cha Kellog alieleza, "Kuwa mbinafsi kunafanya mtu aonekane anatawala,na kuonekana unatawala kunakufanya uonekana unafaa kuwa kiongozi,hususan pale penye ushindani."

"Akilini,watu wanalinganisha wema kuwa sawa udhaifu."

Dr Livingston anaamini kwamba tabia hii ya kuhusisha ubabe na uongozi inaweza kutoa maelezo kwani tunakuwa na rushwa.

"Watu wenye maadili,wema na wapenda watu wana nafiasi finyu ya kuteuliwa kushika majukumu ya uongozi," alisema msomi huyo.

"Hiyo inaongeza uwezekano wa rushwa na utendaji kazi kinyume cha sheria kwa sababu tunakuwa na watu wasiofaa kwenye nafasi za uongozi."

Lakini Bob Kaplan,Makamu Mwenyekiti wa Zamani wa taasisi ya fedha ya Goldman Sachs,na sasa Profesa wa kanuni za utawala katika Chuo Kikuu cha Harvard haafikiani na hoja ya utafiti huo.

Aliieleza tovuti ya Today.com kwamba maadili mema ndio kigezo kinachoweza kushauri kuhusu kiongozi anayefaa.

"Sisemi kwamba ili kuwa bosi lazima uwe mtu 'poa' lakini nadhani inabidi uwe na maadili,uadilifu na kushirikiana vema na watu, na kuwajenga watu," alisema.

CHANZO: Tafsiri isiyo rasmi kutoka gazeti la Daily Mail


9 Oct 2011


Tuipende,tuichukie lakini ukweli unabaki kuwa CCM ndio chama tawala.Kwa mantiki hiyo kila Mtanzania,including sie tusiokuwa wananchama wa chama chochote kile cha siasa tunalazimika kuwa na interest na hali ya mambo ndani ya chama hicho.Afterall,tofauti zetu za kiitikadi hazimaanishi uadui kama unavyohubiriwa na akina Nape.Sote ni Watanzania,na iwe CCM,Chadema,CUF,nk vyote ni vyombo tu vya kutushirikisha katika siasa za nchi yetu kwa namna moja au nyingine.

Anyway,niende kwenye mada.CCM inakabiliwa na changamoto kubwa katika kumpata mgombea wake anayetarajiwa kumrithi Rais Jakaya Kikwete atakapomaliza muda wake mwaka 2015.Naomba kuorodhesha changamoto hizo kama ifuatavyo

MGOMBEA KUTOKA ZANZIBAR

Japo Katiba ya Jamhuri ya Muungano na ile ya CCM hailazimishi utamaduni usio rasmi wa kupokezana nafasi ya mgombea urais kati ya CCM Bara na Zanzibar,yayumkinika kuamini kuwa baada ya miaka 20 (1995-2015) ya CCM Zanzibar kutotoa mgombea kwenye nafasi ya Urais wa Muungano upande huo utakuwa unatarajia kuwa sasa ni zamu yao.Baada ya Rais Mzanzibari Ali Hassan Mwinyi,alikuja M-Bara Benjamin Mkapa aliyetawala kwa miaka 10 kabla ya kurithiwa na M-Bara mwingine Jakaya Kikwete ambaye kufikia mwaka 2015 atakuwa ametawala kwa miaka 10.

Kwa vile katika utamaduni mwingine usio rasmi ndani ya CCM mgombea atakayepitishwa mwaka 2015 (na ikitokea akashinda) anaweza kuwa madarakani kwa miaka 10 (kwa maana kuwa anatarajiwa kupitishwa tena mwaka 2020-kama ilivyokuwa kwa Mwinyi,Mkapa na sasa Kikwete), Wazanzibari wakikubali mgombea ajaye wa CCM atoke Bara itamaanisha wakose nafasi kwa miaka 30 mfululizo.

Tofauti na ccm Bara ambapo uongozi wake una sauti kuliko wanachama,kwa Zanzibar wanachama na viongozi wa kawaida wana influence kubwa ndani ya chama hicho.Wakati uongozi wa CCM Zanzibar unaweza kuridhia mgombea ajaye ataoke Bara,ni vigumu kuhisi wanachama na viongozi wa kawaida wakakubali miaka mingine 10 pasipo Mzanzibari mwenzao kushika urais kupitia CCM.

Iwapo CCM Bara watashinikiza lazima mgombea atoke Bara basi Wazanzinari wanaweza kutumia turufu ya "tunatoka nje ya Muungano" na hili linaweza kuzua sokomoko kubwa.

MGOMBEA/RAIS MUISLAM KISHA MKRISTO (na vice versa)

Utamaduni mwingine ndani ya CCM ni kuzungusha nafasi ya urais (au mgombea wa urais) kati ya Waislam na Wakristo.Baada ya miaka kadhaa ya utawala wa Mwalimu Nyerere ikaja zamu ya Muislam Mwinyi,ambaye naye alirithiwa na Mkristo Mkapa,kabla ya ujio wa Muislam Kikwete.Katika mambo ambayo CCM inapaswa sifa nyingi ni pamoja na umakini wake katika kudili na ishu nyeti ya dini (japo wanasiasa mufilisi wameanza kutumia udini kwa minajili ya kusaka mafaniko yao binafsi kisiasa).Chama hicho kimejitahidi sana kuzingatia ukweli wa mgawanyo wa kiimani miongoni mwa Watanzania ambapo Waislam na Wakristo wanatengeneza takriban robo mbili za wakazi wote wa nchi yetu (robo nyingine ni wanaofuata imani nyingine pamoja na wapagani)..

Sasa,kwa kuzingatia ukweli kuwa Kikwete ni Muislam,inatarajiwa mgombea urais wa CCM mwaka 2015 awe Mkristo ili kudumisha utamaduni huo usio rasmi.Iwapo mgombea huyo atatoka Bara,haitokuwa vigumu kumpata.Tatizo ni iwapo mgombea atatakiwa kutoka Zanzibar.Kama tujuavyo,takriban asilimia 99 ya Wazanzibari ni Waislam,na hali ni kama hiyo kwenye uongozi wa CCM visiwani humo.Uwezekano wa kumpata mgombea urais kutoka Zanzibar ambaye ni Mkristo ni mgumu pengine kuliko uwezekano wa Gaddafi kuwa mgombea urais wa Marekani kuchuana na Rais Barack Obama hapo mwakani.

Kwa mantiki hiyo,kama changamoto ya kwanza itapatiwa ufumbuzi,yaani CCM kufanikiwa kupata mgombea wake kutoka Zanzibar,tatizo litabaki kwenye changamoto ya pili,yaani kupata mgombea Mkristo kutoka visiwani humo.

CHAGUO LA KIKWETE

Ni wazi Rais Kikwete angependa kupata mrithi atakayeweza kumpa amani baada ya kustaafu.Baada ya kuonjesha ladha ya 'ujeuri' pale baadhi ya vigogo wa chama hicho wanapodaiwa kutaka kumng'oa kwenye kiti cha uenyekiti wa chama hicho kwa kigezo cha kutenganisha kofia ya urais na uenyekiti wa CCM,yayumkinika kuamini kuwa asipokuwa makini kumpata mrithi atakayehakikisha anakula pensheni yake bila usumbufu wala hofu ya kukumbana na yaliyomkuta Chiluba...

Lakini Kikwete kulazimisha chaguo lake kutategemea namna atakavyoweza kumpromoti kuanzia sasa.Wachambuzi wengi wa siasa zetu wanafahamu kuwa Kikwete hana sauti kubwa ndani ya chama hicho.Kimsingi,mtu kama Edward Lowassa ana nguvu takriban mara mbili ya alizonazo Kikwete ndani ya chama hicho.Nguvu pekee ya mwenyekiti huyo ni kutoka kwa watu wa Idara ya Usalama wa Taifa ambao licha ya kumpatia dossiers zenye "machafu" ya viongozi wenzie wa CCM,pia wanaweza kulazimisha matakwa ya Kikwete yakatimia kwa mbinu chafu za kiintelijensia.Hilo linafanyika sehemu nyingi tu duniani ambapo siasa na intelijensia zimefunga ndoa isiyo rasmi.

Lakini hili la mashushushu kuingilia siasa za ndani ya CCM linategemea zaidi siasa za ndani za Idara ya Usalama wa Taifa.Wajuzi wa mambo wanafahamu mgogoro wa chini chini ndani ya Idara hiyo kuelekea mchakato wa CCM kumpata mgombea wake mwaka 2005.Tofauti za kimaslahi miongoni mwa viongozi waandamizi wa Idara hiyo zilitishia kwa kiasi kikubwa jina la Kikwete kupitishwa,na hata alipofanikiwa kupitishwa na hatimaye kushinda urais baadhi ya viongozi waandamizi wa Idara hiyo walijikuta majeruhi.

LOWASSA NA 'PIGA UA' YAKE

Mpende au mchukie, lakini Edward Lowassa ameendelea kuwa mwanasiasa mwenye nguvu na ushawishi mkubwa ndani na nje ya CCM.Licha ya uwezo wake mkubwa wa kifedha,Lowassa amewasaidia viongozi wengi wa CCM kuwepo madarakani,iwe kwa misaada ya kifedha au kimkakati.

Japo hajaweka msimamo wake hadharani,wachunguzi wengi wa siasa wanaamini kuwa ndoto za mwanasiasa huyo kumrithi Kikwete bado zipo hai.Inaaminika kuwa chanzo cha ndoto hizo ni mkataba usio rasmi kuwa Kikwete angemwachia Lowassa jahazi la kuongoza Tanzania baada ya kumaliza miaka yake 10 ya Urais.Mahesabu yalikwenda vizuri hadi pale ilipoibuka skandali ya Richmond iliyopelekea Lowassa kuachia ngazi.Laiti hilo lisingetokea basi muda huu wala nisingeandika makala hii kwa vile ingekuwa wazi kuwa Lowassa ndiye Rais ajaye baada ya Kikwete.

Kinachomsaidia Lowassa ni jinsi anavyotumia kila nafasi ipasavyo kuhakikisha jina lake linaendelea kuwa masikioni mwa Watanzania.Mwanasiasa huyo yupo radhi hata kuwaunga mono wanasiasa wa vyama vya upinzani alimradi kufanya hivyo kunamweka karibu zaidi na wapiga kura.

Kadhalika,pamoja na kuhusishwa na ufisadi,Lowassa anakubalika kama mtu anayemudu kufanya anachoamini,jambo linalomtofautisha na Rais Kikwete ambaye anaelemewa zaidi na kutaka kuwafurahisha watu wake wa karibu.Lowassa yupo tayari aonekane mbaya ndani ya CCM lakini aishie kuonekana mkombozi kwa Watanzania.

Na katika kumtendea haki,Lowassa ana 'u-Sokoine' wa namna flani.Hasiti kutoa maamuzi na anaweza kusimamia maamuzi yake.Laiti mwanasiasa huyu asingekuwa na mawaa ya ufisadi basi Tanzania ingeweza kupata carbon copy ya Sokoine.

Kuna wanaomwona Lowassa kama mwanasiasa anayeweza kubadilika kwa sababu kuu mbili.Kwanza,utajiri mkubwa alionao unaweza kabisa kumshawishi asitumie madaraka yake kuendeleza utaratibu wa kuifanya Tanzania kuwa shamba la bibi.Japo utajiri sio kigezo cha fisadi kutotamani fedha zaidi lakini madaraka kama ya Urais yanaweza kumfanya mtu apate huruma kwa anaowaongoza.Kikwete ana huruma lakini tatizo ni kwamba huruma yake kwa mafisadi ni kubwa ziadi ya ile aliyonayo kwa walalahoi.Hilo halina mjdala na mwenyewe anajua hilo.

Kingine kinachoweza kumpa faida Lowassa ni network yake ambayo inaweza kabisa kupenya Zanzibar kuwashawishi wamuunge mkono.Ukichanganya na advantage nyingine kwamba yeye ni Mkristo (ambayo inamfanya awe eligible kwa mujibu wa changamoto ya pili hapo juu),

Lakini pengine faida nyingine aliyonayo mwanasiasa huyu ni ukaribu wake na Idara ya Usalama wa Taifa,ambayo penda usipende itacheza nafasi muhimu kwa mgombea mwana-CCM yeyote anayetaka kumrithi Kikwete.Japo sina hakika kwa sasa ukaribu huo upo katika hali gani lakini unaweza kuwa na faida kubwa kwake.

Kubwa zaidi ya yote ni ukweli kwamba Lowaasa anamfahamu Kikwete in and out.Kwa mantiki hiyo,anaweza kumwandama Kikwete hata atakapomaliza muda wake wa Urais.Na kwa vile by then Kikwete hatokuwa na nguvu za kutosha ukilinganisha na hali ilivyo sasa ambapo yeye ni mkuu wa nchi, yayumkinika kuamini kuwa angependa kuwa na maadui wachache wenye nguvu na uwezo wa kumwangamiza.Kikwete anaweza kujikuta anakabiliwa na mzimu uleule ambao yeye na wanamtandao wenzake walimsababishia Rais Mkapa.

Inafahamika kuwa Kikwete na timu yake waliweka wazi kwa Mkapa kuwa laiti asingepitishwa basi aidha angegombea (na pengine kushinda) kupitia tiketi ya chama cha upinzani.Sasa ukizingatia Kikwete hakuwa karibu kihivyo na vyama vya upinzani kwa wakati huo,ukaribu wa Lowasaa kwa wapinzani unaweza kulifanya tishio la aina hiyo kuchukuliwa kwa uzito mkubwa.Ikumbukwe kuwa nafuu pekee kwa Kikwete atakapostaafu ni kwa CCM kubaki madarakani kwani kuna kila dalili kuwa kama chama cha upinzani kikishinda basi anaweza kabisa kupandishwa kizimbani kujibu tuhuma lukuki za ufisadi.

Je CCM wanawezaje kukabiliana na changamoto hizi?Moja ya njia mwafaka ni kujaribu kuiga utaratibu wa siasa za uchaguzi nchini Marekani ambapo wananchama wenye nia ya kuwania kupitishwa kugombea urais wanatangaza dhamira zao mapema.Pamoja na faida ya kumfanya mwanachama mwenye dhamira hiyo kufahamika vema kwa wapiga kura,utaratibu huo unaambatana na hatari zake.Kwa mwananchama kujitambulisha hadharani mapema anaweza kuwapatia maadui zake wa kisiasa ammunition ya kutosha kumteketeza mapema,na ikifika wakati wa kupiga kura za kumpitisha mgombea anaweza kuwa amekwisha kabisa.

Anyway,kwa leo naomba kuishia hapa.Nitaendelea na mada hii wakati mwingine

Jasusi ChatBot

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.