Mambo hayo!Habari yenyewe iko HAPA4 Mar 2008
3 Mar 2008

It's every Blackman's dream to see a fellow Black person in the White House.And for that matter,every Black person has is supposed to wish Barack Obama success in his attempt to rewrite American history by becoming the first non-White President of the US,the first Black President of the US of A.However,I just wish Obama does not win the Democratic Party nomination.Sounds weird,doesnt it?Well,simple reason is he would make too soft a target for Conservative smear campaign.And I believe that's why they pretend to admire his performances in the Dem's Primaries and Caucuses:they pray that Hillary Clinton loses to Obama,and that offers a Republican candidate an easy ride to the White House.I'm not suggesting that Obama is a weaker candidate than Hillary,he's shown over and over how strong,determined and likable he is.Conservatives are scared of competing AGAINST Hillary,who they paint as a divisive and controversial figure,because they know how strong and effective the Clinton's political machinery is.Why then is Hillary trailing in some polls?Well,it's not hard to see that she isn't only competing WITH Obama for a Dem's presidential spot but also AGAINST the Republicans and conservatives who knows what to expect should she emerge the winner in the Dem's race.The clips below might give you an idea as what to expect come a day when Obama is the Dem's Presidential candidate.If it's started this early while he isnt yet nominated to run for the presidency,imagine how dirty and vile swiftboat campaigns would be against Obama.
2 Mar 2008
2.3.08
Evarist Chahali
CCM, LOWASSA, MTANZANIA, MWAKYEMBE, MWINYI, NYERERE, OLE NAIKO, RICHMOND, SALMIN AMOUR, TABORA BOYS
No comments
MTANZANIA UGHAIBUNISakata la mkataba wa Kampuni ya Richmond linaelekea kuchukua mwelekeo mpya kila kukicha. Ni rahisi kutafsiri kwamba suala hili lisipopatiwa ufumbuzi wa kudumu linaweza kuwa na madhara makubwa kwa nchi na kwa chama tawala, CCM.
Tangu ripoti ya “Tume ya Mwakyembe” ilipowekwa hadharani katika kikao kilichopita cha Bunge la Jamhuri ya Muungano, kumejitokeza kauli kadhaa za utatanishi ambazo japo zinaweza kuwa ni za kawaida tu, tafsiri ya ndani inaashiria matatizo makubwa huko tuendako.
Naomba niwe muwazi zaidi katika makala hii, na ningependa kutamka bayana kwamba sina nia ya kumshushia heshima yeyote nitakayemtaja. Lengo kuu la makala hii ni kuikumbusha kila pande inayoguswa na sakata hilo kutambua kwamba taifa letu ni muhimu zaidi kuliko maslahi ya mtu mmoja.
Naikumbuka sana siku taifa lilipotangaziwa kifo cha Baba wa Taifa.Watanzania wengi walitokwa na machozi sio tu kwa vile hawangemwona tena Mwalimu bali pia ni ile hali ya kutokuwa na uhakika taifa letu lingekuwaje bila Nyerere.Naamini kwamba laiti Mwalimu angekuwepo, baadhi ya upuuzi kama huo wa mkataba wa Richmond wala usingetokea, lakini ndio hivyo tena, hatuko naye duniani.
Wanaoilaumu “Tume ya Mwakyembe” kuwa imewaonea wanasahau kwamba tume hiyo haikuundwa baada ya Mwakyembe na wenzake kutuma maombi ya kuwa kwenye tume hiyo.Inashangaza wanaolalamika sasa kwamba ripoti ya tume hiyo ilikuwa na ajenda za kumalizana kisiasa,ilhali hawakuipinga wakati inaundwa na pale ilipokuwa ikitimiza majukumu yake.Ina maana ajenda hizo za kisiasa zilianza baada ya akina Mwakyembe kuwa wajumbe wa tume au zilikuwapo kabla.Kama zilikuwapo kabla,kwanini basi waliotajwa kuhusika na kuliingiza taifa katika hasara kubwa kwa mkataba huo wa kizembe hawakulalamika?
Na iwapo ajenda hizo zilianza baada baada ya wajumbe hao kuingia kwenye tume,kwanini basi watajwa walikimbilia kujiuzulu (huku wengine wakigoma waziwazi kujiuzulu kwa kuendelea kung’ang’ania madaraka) badala ya kudai haki itendeke?Ni rahisi kuhitimisha kuwa kelele zinazoendelea hivi sasa ni za mfa maji.
Nakumbuka kwenye miaka ya tisini nilipokuwa mwanafunzi wa sekondari ya wavulana ya Tabora (Tabora Boys) tulibahatika kutembelewa na Komandoo Salmin Amour.Nayakumbuka baadhi ya maneno yake ambayo kimsingi yalikuwa na lengo la kutupa changamoto ya mafanikio ya kielimu na hatimaye kufanikiwa maishani (japo sio kila mara kufanikiwa kielimu ni tiketi ya moja kwa moja ya kufanikiwa kimaisha).Alitueleza kwamba madaraka ni mazuri na kutupa mifano ya namna yeye kama rais alivyokuwa na wasaidizi kibao wa kuhakikisha kila kitu kinakwenda vema.
Nilikubaliana na Komando wakati huo,na nakubaliana nae sasa,kwamba madaraka ni mazuri na matamu,na ndio maana tunashuhudia hizi kelele zinazoendelea kutoka kwa waliokumbwa na zahma ya kisiasa baada ya skandali ya mkataba wa kampeni ya Richmond.Hakuna dhambi kwa madaraka kuwa matamu kwani hata njia ya kuyafikia sio nyepesi.Inahitaji jitihada na juhudi za kutosha kufikia hatua ya kuongoza watu wenye akili timamu.Na inatarajiwa kwamba mtu akishapata bahati ya kuwa kiongozi atatambua kwamba wengi,kama sio wote,wa aliokuwa akiwaongoza ni watu wenye akili timamu,uwezo wa kufanya maamuzi na wanaostahili heshima.Waziri Mkuu aliyepita,Edward Lowassa,ameendelea kuonyesha kwamba japo aliamua kubwaga manyanga kwa hiari yake,alifanya hivyo huku roho ikimuuma.Nasema hivyo kwa sababu kauli zake za hivi karibuni zinaashiria wazi kwamba bado ana kinyongo kikubwa na matokeo ya uchunguzi wa “Tume ya Mwakyembe.”
Lowassa anaamini kwamba atarejea tena kwenye ulingo wa juu wa kisiasa kama Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi ambaye alipokuwa Waziri alilazimika kujiuzulu kutokana na skandali iliyoikumba Wizara yake.Tofauti ya msingi kati ya Mwinyi na Lowassa ni ukweli kwamba wakati Mwinyi alijiuzulu kutokana na tukio lililotokea mbali kabisa na mahala alipokuwa akifanyia kazi (lilitokea Shinyanga wakati ofisi ya Mwinyi ilikuwa Dar es Salaam),Lowassa alijikuta akikumbwa na shutuma kuhusu mkataba huo kwa vile katika hatua flani ulipita machoni mwake na akaamua “kusikiliza maamuzi ya wataalamu.”

Uongozi ni pamoja na kuwa na maamuzi ya haraka na yanayoangalia athari zinazoweza kujitokeza mbeleni iwapo yatafanyika maamuzi potofu.Haiyumkiniki kwamba Waziri Mkuu mzima anaweza kusikiliza ushauri mbovu na kuafikiana nao pasipo kujiridhisha iwapo ushauri huo ni wa manufaa kwa taifa.Hilo pekee linamvua sifa ya uongozi mtu yeyote aliye katika nafasi ya juu kitaifa.
Hivi kama mkataba wa Richmond ungekuwa na madhara ya moja kwa moja kwa familia ya Lowassa,kiongozi huyo angeendelea kusikiliza ushauri asio na uhakika na matokeo yake au angetaka kujiridhisha kwamba kilichokuwa kikifanyika hakingekuwa na madhara kwa familia yake?
Tukimweka kando Lowassa kwa muda,tumeshuhudia vituko vingine kutoka kwa Mkurugenzi wa TIC Emmanuel Ole Naiko ambaye anadai kuna dalili za “mauaji ya halaiki” dhidi ya watu wenye asili ya wilaya ya Monduli.Hizi ni hoja mufilisi ambazo kama zitaachwa bila kudhibitiwa zinaweza kuliingiza taifa kwenye matatizo yasiyo na msingi.

Hivi Ole Naiko amefanya utafiti wa kutosha kiasi gani kuthibitisha kwamba kuna mpango wa “ethnic cleansing” dhidi ya watu wa Monduli?Kwa hakika serikali inapswa kumhoji kwa undani mtu huyu mwenye heshima kubwa ndani na nje ya nchi kutokana na matamshi hayo ambayo yanaweza kabisa kuathiri hata utendaji wa ofisi yake (hakuna mwekezaji aliye tayari kuwekeza kwenye nchi inayoelekea kwenye “ethnic cleansing.”)
Kuna tetesi kwamba upo mkakati mkubwa wa “kujibu mashambulizi” dhidi ya ripoti ya “Tume ya Mwakyembe.” CCM imekuwa ikituaminisha kila siku kwamba vikao nje ya chama ni majungu,sasa basi inapaswa kuhakikisha kwamba wote wenye kudhani hawakutendewa haki wawasilishe malalamiko yao kwa ngazi hsuika katika chama hicho au hata bungeni.
Kama taarifa tunazozisoma katika vyanzo mbalimbali kwamba kuna mgawanyiko mkubwa ndani ya CCM kutokana na skandali la Richmond zina ukweli, basi ni muhimu kwa uongozi wa juu wa chama hicho kuachana na itifaki zake za kawaida za kuwasifia hata wanaostahili kukemewa na badala yake kuwawekwa “kiti moto” waeleze malalamiko yao mbele ya vikao halali badala ya kuendeleza mbinu za chini chini ambazo zinaweza kabisa kuathiri hali ya usalama wa nchi yetu.
Tusirejee makosa yaliyojitokeza katika mkataba wa Richmond ambapo baadhi ya watu walitahadharisha mapema kuhusu uhalali wa kampuni hiyo lakini wakapuuzwa.Kuna watu wanataka urais kwa kutimia njia yoyote ile hata kama kwa kufanya hivyo wanahatarisha uhai wa chama.
Lakini wakati tunawalaumu wanaolalamika kwamba wameonewa na “Tume ya Mwakyembe” tunapaswa pia kujiuliza kama hawapati jeuri hiyo kutokana na uzembe unaendelea wa kutowachukulia hatua wahusika.Pengine jeuri waliyonayo inatokana na ukweli kwamba wanaamini kuwa hakuna mwenye jeuri ya kuwachukulia hatua hasa ikizingatiwa kuwa baadhi yao wameishia kupongezwa kwa “ushujaa wao” badala ya kushutumiwa kwa hasara waliyoisababisha kwa taifa.
Nadhani anachopaswa kufanya Lowassa,Ole Naiko na wengine wote waliohusishwa na mkataba wa Richmond ni kutafuta msaada wa kisheria kuona haki inatendeka upande wao iwapo wanaamini kuwa hawakutendewa haki,badala ya kuendeleza hizi porojo ambazo kwa hakika zinaweza kuua kabisa ndoto zao za kurejea kwenye ulingo wa juu wa siasa za nchi yetu.Mahakama zipo,vikao vya chama vipo,sasa kwanini kelele za kuonewa zisipelekwe huko?TANZANIA NI MUHIMU ZAIDI KULIKO MASLAHI YA MTU BINAFSI.
BAADA YA KUMALIZA KUSOMA MAKALA HII,UNAWEZA KUANGALIA VITUKO VYA SIASA ZA URUSI AMBAVYO VIMEZAA TERM MPYA YA NANO PRESIDENT (as in iPod Nano).BONYEZA HAPA
HALAFU KWA WALE AKINA DADA "WENYE ULIMI MZITO",CLIP IFUATAYO INAWEZA KUWA YA MSAADA WA INA FLANI
29 Feb 2008
29.2.08
Evarist Chahali
WAR ON TERROR
No comments
Hivi ukiwa na glasi yenye maziwa yenye ujazo unaofikia nusu ya glasi hiyo,utasema iko HALF FULL au HALF EMPTY?Au,unapokwenda kazini,shuleni,kwenye mizinguko,nk je unakuwa umetoka NJE ya makazi yako au umetoka NDANI ya makazi yako?Haya ni maswali yanayohusiana na mantiki na maana ya kauli.Nimekuchokoza ili utafakari hoja hii:je vita dhidi ya ugaidi (war on terror) imefanikiwa-hata kama ni kwa kiasi kidogo-huko Mashariki ya Kati na Ghuba au ndio imeifanya dunia kuwa sayari hatari zaidi kwa maisha ya binadamu?
Hebu tuangalie Iraki ya Saddam Hussein na hii ya baada ya uvamizi wa Marekani na washirika wake.Wakati wa utawala wa Saddam,hakukuwa na demokrasia ya aina yeyote ile,kauli ya dikteta huyo ilikuwa na nguvu pengine zaidi ya kauli ya Mungu.Lakini pamoja na hayo,Wairak kwa kiasi kikubwa hawakuwa na hofu ya kuwa kwenye mkusanyiko kwa kuhofia kulipuliwa na suicide bombers,hatukuwahi kusikia jina la mtu aitwaye Muqtada al Sadr,hakukuwa na kitu kiitwacho Al Qaeda in Iraq,huduma za muhimu kama maji,umeme,barabara,nk zilikuwa zikipatikana kwa wingi,utajiri wa mafuta ulisaidia kuifanya nchi kuwa yenye nguvu,na kadhalika na kadhalika.Baada ya uvamizi wa Marekani na washirika wake,demokrasia imepatikana na watu wamepiga kura japo kwa hofu ya suicide bombers na snipers waliotapakaa nchini humo.Hata hivyo,uvamizi huo umezaa "majimbo mapya" ikiwa ni pamoja na lile lililopachikwa jina la "pembetatu ya kifo" (Triangle of Death),umeibua vikundi kama Mehdi Army,uliwavutia watu kama Zarqawi,umekosesha huduma nyingi muhimu kama maji,umeme,barabara na uhaba wa mafuta licha ya nchi hiyo kuwa mzalishaji mkubwa wa mafuta na,kama Obama alivyomjibu McCain-baada ya kutupiwa kijembe kwamba (Obama) ni dhaifu kwa kudai kwamba hakuna Al-Qaeda nchini Irak-hivi sasa kuna kitu kiitwacho Al-Qeada in Iraq.Je Iraki chini ya Saddam ni bora zaidi kuliko hii ya sasa au ni vice versa?Tunarudi kulekule kwenye "mwenye nyumba ametoka ndani au ametoka nje."
Bush na neocons wenzake walikuwa na sababu muhimu za kuivamia Afghanistan baada ya mashambulizi ya Septemba 11,2001.Hakuna wakati ambao kiongozi wa nchi anatakiwa kuonyesha msimamo kama pale linapotokea jambo la kutikisa nchi.Kama utamaduni huu utazingatiwa basi si ajabu kelele za wanaolialia kuwa wameonewa kwenye sakata la Richmond na BoT/EPA zikasikika kutoka Segerea,Keko,Ukonga au hata wakiwa deathrow huko Isanga,japo I doubt).Nadhani kila Mmarekani alisapoti uvamizi dhidi ya Taliban huko Afghanistan hasa kwa kuzingatia usemi "akuanzae mmalize."Lakini kabla mission ya Afghanistan haijazaa matunda yaliyotarajiwa,na Osama bin Laden na mpambe wake Zawahiri wakiendeleza ngebe zao,Bush na neocons wenzake wakaamua kumalizia kiporo cha Joji Bush Mkubwa cha kumng'oa Saddam kwa kisingizio cha WMD.Haya,Saddam aliondoka madarakani na hatimaye kunyongwa lakini Irak imetokea kuwa sumaku ya magaidi kuliko ilivyokuwa kipindi cha dikteta huyo.Pia chuki dhidi ya taifa la Marekani imekua maradufu katika Muslim World.So far,taarifa kutoka Afghanistan zinaonyesha dalili za mission impossible.
Anyway,hiyo ndio siasa:ubabaishaji,udanganyifu,utapeli,uzushi,kuzinguana na lolote lile linaloweza kumfanya mwanafunzi wa siasa kama mie kujiuliza nyakati flani kama hiki nachosoma kina umuhimu wowote.Well,at the end of the day,"kinacho-matter" ni shahada uliyonayo na si shahada kwenye fani gani (in most cases,watu huwa hawaulizi Profesa Othman Haroub,Issa Shivji au Mwandosya ni wahitimu wa fani gani....)In simple words,Politics sucks!
29.2.08
Evarist Chahali
BLACK RHYNO, CLIP
No comments
BLACK RHYNO-Mistari.Mie si mtaalam wa videography,lakini naona kuna ubunifu unaostahili pongezi ktk video hii.Kingine kinachonifanya kuupenda wimbo huu ni sababu ya ki-binafsi zaidi.Nilipokwenda TZ 2005,ndipo nilibahatika kunisikia kipindi cha Planet Bongo kwa mara ya kwanza.Sasa huu wimbo ndio uliokuwa ukitumika kama "intro" ya kipindi (sijui ktk lugha ya utangazaji ule wimbo unaotambulisha kipindi unaitwaje?Is it jingle au....?)
27 Feb 2008
27.2.08
Evarist Chahali
AMERICAN GANGSTER, ARUSHA, BLACK AMERICANS, CONVERSATIONA, DAWACO, EPA, JAY-Z, KKKT, LAIZER, LOWASSA, MWANDOSYA, RAIA MWEMA, UNAFIKI
No comments
Makala yangu ndani ya toleo la wiki hii la gazeti la Raia Mwema inazungumzia UNAFIKI: Ule wa Profesa Mwandosya kuitaka Dawasco isiwataje hadharani mawaziri wanaodaiwa maji na Mamlaka hiyo;ule wa Askofu Thomas Laizer wa KKKT Dayosisi ya Arusha kutumia neno la Bwana kuwapiga vijembe wanamwandama Lowassa,na ule wa "mabilioni ya EPA yanayorejeshwa kwa kasi."Makala hiyo imeanza kwa stori za hapa na pale,mambo ya muziki wa kufokafoka na albamu ya Jay-Z ya American Gangster ilivyosahau matatizo ya Black Americans.Stori hizo ni zinaunganishwa katika namna ile ile ya conversational style,napenda sana makala iwe mithili ya kupiga stori na msomaji,iwe kijiweni,kwenye pub,au hata barazani.Pamoja na habari na makala zilizokwenda shule,bingirika na makala hiyo kwa KUBONYEZA HAPA26 Feb 2008
26.2.08
Evarist Chahali
SOME VIDEOS
No comments
ASHANTI ft CRROKED I-Baby Remix
SNOOP ft PHARELL-Beautiful
YOUNG JEEZY ft AKON-Soul Survivor
SHAGGY ft OLIVIA-Wild 2Nite
CHINGY-One Call Away
KEISHA WHITE FT CASSIDY-Dont Care Who Knows
OUTKAST-Ms Jackson
AKON ft SNOOP-I Wanna Love You
BONE THUGS-N-HARMONY ft AKON-I Tried
24 Feb 2008
24.2.08
Evarist Chahali
JAMBOFORUMS, POLISI
No comments
Hatimaye ukumbi wa majadiliano katika mtandao (web forums) wa Jambo Forums umerejea hewani baada ya kujitokeza matatizo kati ya baadhi ya wanachama wa Jambo na jeshi la Polisi.Habari zaidi soma hapa
Subscribe to:
Posts (Atom)