29 Jul 2009


BARAZA LA MAASKOFU KATOLIKI TANZANIA
(TEC)

Mpendwa Msomaji,

Tume ya Haki na Amani ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania inayo furaha kukuletea Ilani hii.
Madhumuni ya matini hii ni kukualika tutafakari pamoja juu ya masuala muhimu yanayotukabili kama Taifa.
Tunawashukuru Wanataaluma Wakristo wa Tanzania walioandaa hati hii.
Kwasababu chaguzi za mwaka 2010 haziko mbali mnaona ni muhimu kupendekeza vipaumbele vyetu kama jamii tukiwaambia viongozi wetu wajao yale ambayo tungependa yafanyike kwa ajili ya jamii yetu. Katika uchaguzi hatupigi kura tu, tunapaswa kueleza makusudio yetu kwa yale tunayofikiri kuwa muhimu sana kwa Taifa.

Kwa kuchapisha Ilani hii tunataka kutekeleza haki yetu ya uzalendo ili kujenga maisha yaliyo mema zaidi kwetu sote katika siku zijazo.

Askofu Mkuu P. Ruzoka
Askofu Mkuu wa Tabora
MWENYEKITI
Tume ya Haki na Amani - TEC


WANATAALUMA WAKRISTO TANZANIA (CPT)

ILANI

MAPENDEKEZO YETU YA VIPAUMBELE VYA KITAIFA


A: Fikra Msingi

Maswali ya msingi

Uchumi na Siasa vipo kwa madhumuni gani?
Chimbuko la uwepo wa mfumo wa kisiasa ni nini?

Dira yetu

Maadili ndio dira yetu msingi ambapo kiini chake ni wanadamu walioumbwa katika sura na mfano wa Mungu, wakiwa na hadhi katika utu wao, haki yao na wajibu zao. Watu ndio kusudio na sababu ya shughuli zote za kiuchumi na kisiasa. Tunu za Ujamaa ambazo ndizo zilizojenga utamaduni wa nchi yetu zinakubaliana kabisa na maoni haya ya kimaadili. Tunu hizo ambazo ni umoja mshikamano, maelewano, mtazamo wa kifamilia (familyhood) zinabeba maana pana zaidi ya itikadi ya kisiasa. Uamuzi wetu wa kuchagua kufuata uchumi wa ujamaa wa kisoshalisti kulituletea matokeo mazuri na mabaya (chanya na hasi), kwa hiyo basi sio vema kudharau na kutupilia mbali kila kitu.

Marekebisho ya sera yanayofanyika sasa ni mengi, na baadhi ni ya lazima na ni mazuri. Lakini sio yote ambayo ni ya kujenga jamii yetu. Tunaweza kuona kuna ukuaji mzuri wa uchumi, lakini panakosekana usawa kwa kiwango kikubwa katika kunufaika na ukuaji huo wa uchumi. Kimsingi kanuni za uchumi wa soko huria sio tu kwamba zina kasoro za kiuchumi na kijamii tu, bali pia kasoro zake zinajionyesha katika maisha ya watu kiutamaduni na kimaadili. Watu wanaona mabadiliko haya kuwa yameingizwa kwa nguvu kutoka nje na hivyo yananufaisha matajiri na wenye uwezo.

Kumekuwa na ongezeko kubwa mno la tofauti/pengo kati ya wenye nacho na wasio nacho, wanaosonga mbele kimaendeleo na wanaoachwa nyuma. Sera zetu nyingi za sasa zinajiridhisha kuwa msukumo wa maendeleo ni katika ukuaji wa uchumi kwa kutazama fedha taslimu (monetary terms). Kwa hiyo tunatilia mkazo shughuli na mambo yanayoonekana kusaidia ukuaji uchumi. Mtazamo huu ni wa kibepari kabisa.

Matokeo ya kubaki katika mtazamo wetu finyu, kutengeneza sera zetu kwa kuzingatia sekta chache zenye kulenga ukuaji uchumi tu, kumewaacha nje watu wetu wengi. Kuweza kuwachukulia watanzania wote kuwa ndio msingi wa sera zetu za kiuchumi na maendeleo yetu, sio suala la kimaadili tu bali pia inaleta maana kamili kiuchumi. Ni pale tu taifa zima litakaposhiriki katika uzalishaji na katika matumizi ya bidhaa na huduma (faida ya ukuaji uchumi) ndipo tu soko litakapopanuka.

Nchi za Magharibi zimeweza kupiga hatua mbele katika maendeleo ya kiuchumi pale tu walipoweza kupanua na kuimarisha soko lao la ndani, katika maana ya uzalishaji na matumizi. Vile vile kwa uzingatiifu huo huo nchi za Mashariki zimefanikiwa (kama vila Japani, Korea, Vietinam) na hali hiyo hiyo inaonekana wakati huu katika nchi za China, India, Brazil.

Katika Tanzania sisi tunaonekana kufanya kinyume chake. Kuweza kufanya maboresho yenye manufaa, ni lazima tubadili mtazamo wetu kutoka ule wa kukazania ukuaji uchumi tu na badala yake lengo liwe kuinua maisha ya watu wa kawaida: wake kwa waume. Hatuwezi kuwa na matumaini ya kutatua tatizo la umaskini kwa kufikia ukuaji katika sekta chache tu kama ya utalii na madini. Mtindo tunaotumia sasa hauwezi kutusaidia kupunguza kiwango kikubwa cha umaskini uliopo ambao pia umeenea nchi nzima.

Kuzungumzia sekta rasmi na isiyo rasmi ni mfano mmoja wa fikra finyu tuliyo nayo ya kugawa katika matabaka mfumo wetu wa kiuchumi. Kwa kuwa wengi miongoni mwa watanzania wamo katika sekta isiyo rasmi, kwa sababu hiyo wamegeuzwa kuwa watu wasio na umuhimu, ambao kiuchumi thamani yao ni ndogo.


Kitendawili msingi cha Tanzania

Tanzania ni tajiri katika rasilimali na bado watanzania wengi ni maskini. Kwa nini? Hiki ni kitendawili kikubwa ambacho tunapaswa kukijibu.

Umaskini katika Tanzania sio ugonjwa ambao tiba yake haipatikani kwa urahisi. Kwa kweli umaskini tulionao huku tukiwa tumejaliwa rasilimali nyingi na utajiri mwingi unaotokana na mchakato wa mambo mengi yanayokuwepo kwa wakati mmoja.

Hali tuliyo nayo imeletwa na mchanganyiko wa mambo mengi. Tunapaswa kuchunguza na kuchanganua mambo hayo na hasa tukijiangalia sisi wenyewe, mienendo yetu, na kisha tuelewe ukweli wetu, mazuri na kasoro zetu. Kuondokana na umaskini, ni lazima kufuata mchakato wa kubadilika. Mwenye wajibu katika kuongoza mchakato huo ni sisi wenyewe. Ni lazima tuwe viongozi wa mchakato huo. Haifai kuwaachia watu wa nje, wafadhili, ama fedha kutoka kwingine popote. Hatuwezi kufaulu kwa kujifunza na kupokea njia zilizosaidia nchi nyingine. Kikwazo cha maendeleo yetu ni utegemezi na kukosa uwajibikaji miongoni mwa mawakala katika jitihada za kuleta maendeleo. Kukosa uwajibikaji ndio sababu kuu na jambo kuu linalosababisha umaskini wetu. Ni lazima, kwa hiyo, tujiwajibishe wenyewe katika kujinasua na mtego huu. Lazima tujisumbue na tuhangaikie kutafuta ufumbuzi wa matatizo yetu tukitumia ubunifu wetu wenyewe na rasilimali zetu wenyewe.


Madhumuni/Lengo la Ilani

Mipango tunayo, sera, taratibu na kanuni tunazo na pia mikakati mingi imewekwa. Licha ya hayo, ujuzi wa kinadharia juu ya ufumbuzi wa matatizo yetu tunao. Na bado hatufanyi vizuri katika kupambana na matatizo yetu. Kimsingi kinachokosekana ni uwajibikaji wetu katika utekelezaji wake. Tunakosa ujasiri na utashi katika utendaji, kujitoa kweli na kufanya kazi kwa bidii: kutimiza majukumu na kujitoa katika kutoa huduma yetu kwa ajili ya manufaa kwa wote; kuwa mawakala na wafanyakazi wazalendo waaminifu kwa jamii yetu. Tukubali kuukabili ukweli kuhusu sisi wenyewe. Alisema Mtume Yohane “Ukweli utawaweka huru” (Yh. 8: 32).

Kwa ilani hii, tunatoa mwaliko kwa wote na kuwasihi watanzania wote kufikiri kwa makini changamoto kuu zinazokabili nchi yetu na wananchi wake wengi ambao ni maskini wa mali, waliotengwa na wasio na uwezo. Kuzishughulikia changamoto hizi kunahitaji kuweka vipaumbele sahihi na njia sahihi za ufumbuzi ambazo zinashughulikia kikamilifu matatizo ya umaskini, utenganisho wa kijamii na hali ya kukosa uwezo kwa watanzania wengi. Ilani hii itakuwa mwongozo kwa mtu binafsi kuchagua chama na mgombea katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2009 na Uchaguzi Mkuu wa 2010.

B: Vidokezi vya vipaumbele katika sera

Katika kuzingatia maoni yetu ya msingi juu ya jamii yetu, na uchunguzi wetu wa jumla juu ya utendaji na mfanikio, hapa sasa tunawasilisha mawazo yetu juu ya vipaumbele kwa taifa letu. Huu ni mchango wetu kwa ajili ya watu kutafakari na kuchangia katika mijadala kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2010.

1) Hadhi ya Utu wa Mwanadamu

Lengo na sababu ya mahusiano yote katika jamii ni kumpa kila mtu hadhi ya kiutu ambayo ni stahili yake. Maana yake ni kwamba, kila mtu apatiwe mahitaji msingi kumwezesha kuishi maisha yanayostahili mwanadamu. Hicho ni kipaumbele namba moja. Watu wote wameumbwa na Mungu katika usawa. Kwa hiyo kila mtu ni sawa na mwingine.
Hapa tunapendekeza:

- Lazima tunu za kimaadili ziwe ndio msingi wa taifa letu, haya yakiwa yamehifadhiwa katika Katiba na kuongoza kanuni na taratibu zote za uendeshaji na utendaji.
- Kutengeneza na kutekeleza programu ya elimu ya uraia kwa watu wazima wengi juu ya haki msingi za binadamu na wajibu kwa kila raia.
- Kuwafundisha watu umuhimu na njia za uchunguzi wa malalamiko ya watu ili kusukuma huduma ambazo ni stahili ya watu zitolewe kikamilifu. Huduma hizo ni pamoja na zile za utawala wa umma. Hapo ni pamoja na kuwapa watu nafasi na kuweka njia fanisi za kupeleka malalamiko yao ngazi za juu.
- Ni haki ya msingi kwa kila raia kupatiwa fursa ya kutoa malalamiko yake na kusikilizwa. Haki hii lazima iweze kutendeka kwa kuiwekea mifumo ya kisheria na kiutawala.
- Kanuni na taratibu za kimaadili na weledi (meritocracy) viwe ndio vigezo au sifa za kuwapa watu kazi na kupandishwa cheo.


2) Marekebisho ya Katiba

Katiba inaeleza Mkataba Msingi wa Kijamii wa watu kuhusiana na namna ya kujipanga katika maisha yao ya pamoja. Katiba ni zaidi ya hati ya kisheria. Ni dira ya kimaadili na maelezo ya kifalsafa ya tunu na kanuni watu wanazotaka kuzizingatia katika maisha yao ili kuwahakikishia amani, haki na vile vile kuheshimiana na kuvumiliana katika kuwa na maoni tofauti. Hakuna chama cha kisiasa wala serikali ya wakati huu wanaoweza kihalali kutumia Katiba kwa faida zao za kisiasa.

Katiba inamilikiwa na watu na ni ya watu katika anuwai (diversity) na katika upokeaji wa watu wenye tofauti mbalimbali (plurality). Kwa kuwa taifa ni kitu kinachoishi ni jambo la kiasili na la muhimu hivyo ni sharti kuruhusu mapitio ya vipindi kwa vipindi yafanyike ili kuwapa watu fursa kueleza maoni yao. Haifai kuachia kundi moja kushinikiza au pande/kundi/chama chenye maslahi (kijamii, kiuchumi au kidini) kuchochea mabadiliko. Tangu Tume ya Nyalali imetoa ripoti yake (1991), ombi la marekebisho ya Katiba halijapokelewa kwa namna na kiwango cha kuridhisha. Kuhusiana na suala hili tungependa masuala haya yapewe kipaumbele:
- Tamko dhahiri juu ya tunu msingi za maadili ya kitaifa ambayo yapasa yazingatiwe katika mchakato wa kurekebisha Katiba.
- Pana haja ya kuunda Baraza la Mapitio ya Katiba. Katika mifumo mbalimbali ya kisiasa, kuna njia kadhaa za kuwezesha suala kutekelezwa: Mahakama ya Kikatiba, Chamba ya pili katika Bunge, Mkutano wa Katiba.
Tunapendekeza paundwe baraza la wazee, wanaoteuliwa na sekta za kijami, ama wanaochaguliwa na taasisi mbalimbali za kijamii, kidini na wanazuoni. Chombo hiki kingechaguliwa na kuhakikishiwa uhuru watendaji wake kulingana na Katiba yenyewe. Kiwe huru, na kisibanwe na serikali.
- Kanuni za marekebisho na udhibiti (regulations) na kuwezesha uwazi kisheria kuhusiana na upatikanaji wa fedha za chama ama mgombea.
- Kanuni za udhibiti na marekebisho ya kuchagua wagombea kutoka ndani ya chama kwa lengo la kusaidia mchakato mzima. Kufanyika kwa uwazi na kwa kidemokrasia zaidi.
- Kuanzisha mfumo wa kiuwiano katika uwakilishi badala ya huu wa sasa wa mwenye kupata kura nyingi kuwa ndiye mshindi.
- Kuruhusu wagombea binafsi (isipokuwa katika nafasi ya Urais).
- Kuheshimu kanuni ya kuwa Serikali haina dini na kutoruhusu taasisi za kidini kuwa sehemu ya mfumo wa nchi (mfano. Mahakama ya Kadhi na uanachama wa OIC).
- Kulinda haki ya watoto ambao hawajazaliwa.




3) Uongozi wa Umma

Kwa kiongozi, huduma kwa umma ni dhima muhimu sana kwa jamii yoyote ile ya wanadamu. Ndio maana lazima pawepo uangalifu mkubwa kwa jamii yoyote katika njia na namna (means) inavyochagua viongozi wake na namna inavyoweka taratibu za kusimamia na kudhibiti mienendo ya viongozi wao. Mamlaka mikononi mwa wanadamu kwahitaji uangalifu mkubwa ikiwa tunataka madaraka hayo yasiegemee upande mmoja yawe na uwiano, yasitumike vibaya na hata kuwa ya rushwa.

Kwa wakati huu, tumesikia matukio mengi ya ufisadi, maamuzi yanayopendelea upande fulani kwa sababu ya maslahi ya kiuchumi (kwa watu wa nje na wa ndani). Hapa tunaweka kipaumbele katika yafuatayo:

- Uwazi zaidi katika michakato yote ya uteuzi katika huduma na ofisi za umma, Tume za umma na bodi za utawala.
- Kufanya mapitio ya mamlaka ya Rais katika kuwateua mawaziri, idadi ya wizara, na pia uwezo na uhuru zaidi wa bodi za usimamizi wa mashirika ya huduma za umma.
- Kanuni na taratibu za uongozi ikiwa ni pamoja na kutafuta njia za kuondoa wale wanaothibitika kutumia vibaya nafasi zao.
- Kuhimiza na kuunga mkono kazi halali ya uandaaji wa ripoti zilizofanyiwa uchunguzi na kutafuta taarifa juu ya utendaji fanisi katika huduma za umma kama huduma msingi kwa raia wote.
- Kuhimiza utamaduni wa kufanya tathmini makini juu ya utendaji fanisi wa viongozi, kwa kuweka njia ya kuwezesha wasomi, vyombo vya habari, jumuiya za kiraia na vikundi vya kiraia kushiriki katika tathmini hiyo ya umma.


4) Mfumo wa Kisheria

Kutenda haki ni zaidi ya kufuata sheria na taratibu. Sifa ya uadilifu kwa wale wanaosimamia uendeshaji wa taasisi za sheria na taratibu, na msingi wa mawakala hao wa kuheshimu utu wa kila mtu na kwa ajili ya manufaa kwa wote na kutunza amani na utulivu na maelewano, ni mahitaji ambayo kamwe hayapaswi kupuuzwa, na yafaa liwe ni somo la kila mara katika malezi yao endelevu.

Polisi, maafisa wa mahakama, mawakili, maofisa magereza, watunga sheria, na watawala sio “mabosi” mbele ya watu. Wao ni walinzi wa taratibu nzuri za jamii yetu.

Lazima hawa wajali sana wigo mpana wa mahitaji ya jamii yetu, na sio wawe na ufinyu wa kujiona kuwa wasimamia sheria tu. Kwa ulingo huu tunaleta vipaumbele hivi:

- Lazima kuweka na kudumisha uwiano mzuri zaidi katika mgawanyo wa madaraka katika mihimili mikuu mitatu ya Dola, Serikali, Bunge na Mahakamu. Ilivyo sasa uwiano hakuna na kuna uegemeo upande wa mkono wa Utawala/Utendaji (Executive). Sio kweli kudhani kwamba kudhibiti uwezo wa maamuzi ya madaraka kutaleta ucheleweshaji na kukosa ufanisi, bali kinyume chake ndio kweli. Maamuzi mengi mabaya na ubishani wenye mvutano yangeweza kuzuilika. Ni muhimu pia kuachia madaraka ya maamuzi katika masuala ya kiutawala kwa ngazi za kati na chini yakiandamana na haki ya kukata rufaa kwa ngazi za juu.
- Dhima ya Bunge ya kudhibiti Serikali Kuu inapaswa kuiimarishwa. Pamoja na hatua njema iliyopigwa hapa karibuni, udhibiti makini unatakiwa kwasababu Bunge likiwa ndilo mwakilishi wa majimbo yote linatarajiwa kutoa tathmini yakinifu ya maamuzi yanayofanywa na Serikali.
Wabunge nao wawe na mawasiliano ya karibu na wapiga kura wao wakiwa na ziara zilizopangiliwa majimboni mwao ambako watu wataweza kukutana nao. Wabunge wajizuie kujipendelea kwa kujipangia marupurupu na mapato maalumu pamoja na bonasi nyingi.
- Kupunguza usiri katika mchakato wa maamuzi yanayofanya katika ngazi za juu. Uwazi huboresha maamuzi yanayofanyika.
- Maamuzi yanayofanywa na utekelezaji unaohitajika vinazuiwa na kukosekana matumizi ya kanuni ya auni, badala yake mfumo unategemea maamuzi ya viongozi wa juu wanaohusika. Watu wa chini yake wanaweza kukatishwa tamaa katika uwajibikaji. Kwa hiyo wakubwa lazima wajifunze kugawa madaraka yao kwa walio chini yao. Kwa kufanya hivi, mfumo wa kisiasa unaweza kufikia maboresho makubwa.
- Kupunguza kiwango cha wanasiasa kuingilia mambo ya utawala na huduma.
- Hasira ya kijamii yapasa ishughulikiwe na taasisi za kisiasa na wakala wa sheria na taratibu. Tunaunga mkono sera ya ulinzi shirikishi na kupendekeza kuongeza idadi ya njia mbadala ya adhabu kwa watenda makosa madogo madogo (mfano; huduma kwa jamii, kulipa fidia, kemeo/karipio/onyo rasmi la umma). Pia kuanzisha vituo zaidi kwa ajili ya majaribio kwa wakosaji vijana kuishi bila kufanya kosa.
- Magereza yetu yanapaswa kuendesha programu za mafunzo kwa ajili ya marekebisho ya wafungwa kimaadili, kutoa fursa kwa wafungwa kuwa na mawasiliano na upande wa pili (mshtaki/mhanga) kwa lengo la kufikia usuluhishi.
- Mfumo wetu wa kisheria uchunguzi na kutafiti, na kutekeleza nyenzo na taratibu zinazoongeza ufanisi na utendaji wenye kuleta mafanikio yanayotakiwa kufikia matarajio ya watu. Ucheleweshaji na uzembe/uchovu (lethargy), kukosa uwajibikaji na kukosekana utendaji mzuri wa mahakama kunawafanya wananchi wakose matumaini na kukatishwa tamaa (frustrating) na kuwakosesha imani katika mahakama kama chombo cha kuwasaidia kupata haki kwa njia ya mfumo wa kisheria. Watu hawaoni uwezekano wa kushughulikiwa kesi zao kwa wakati na hivyo kujenga mazoea ya kujichukulia sheria mkononi.
Lazima mfumo wenyewe wa sheria uanzishe njia za kujinidhamisha na kujitathimini utendaji wake na kutumia kanuni za kisasa zaidi za kusimamia utendaji.
- Mahakama inapaswa kutumia sehemu kubwa ya fedha na mali zake zilizopo kwa ajili ya Mahakama za Mwanzo na za Wilaya na za Hakimu Mkazi (kwa mishahara, majengo, kutengeneza ofisi ziwe za kisasa na vifaa na huduma nyinginezo, kuongeza idadi na ujuzi wa mahakimu na makarani). Ni kweli kwamba ni katika ngazi hizi za mahakama ndipo watanzania wengi wanapoijua (wanapofika) mahakama.

5) Viwanda, Biashara na Fedha.

Ni vivutio vingi mno vinatolewa kwa wawekezaji wakubwa na hakuna jitihada na kujali vya kutosha wawekezaji katika uzalishaji mdogo. Wawekezaji wa nje pamoja na makampuni makubwa sio ufumbuzi katika kupunguza umaskini wa watanzania wengi. Upande mwingine wanataaluma wengi wanavutiwa na “mambo makubwa na ya kisasa na ya ughaibuni.” Wanakimbilia mitaji ya nje na njia za nje ya nchi wakati fedha ya ndani inabaki tu pasipo kutumika vizuri katika taasisi zetu za fedha.
Hatua hizi tunazipendekeza ziwekewe kipaumbele:
- Kabla ya yote kabisa, lazima tuangalie suala la utu katika kazi na wajibu wa kimaadili wa kila mmoja kuchangia katika jamii na sio kuwa mnyonyaji wa jamii. Kukaa bure bila kufanya kazi na uvivu ni dhambi mbele ya Muumba na pia ni kosa mbele ya macho ya jamii. Uzururaji ni kosa kisheria. Kutofanya chochote ni tabia isiyoridhisha, malipo sio kitu pekee kinachosukuma mtu kufanya kazi. Utu wa mtu wenyewe unamtaka mtu afanye kazi.
- Kuhusisha taasisi zinazosaidia uwekezaji (huduma za mikopo, miundo mbinu na huduma za ushauri, utafiti wa masoko) kwa ajili ya sekta ya uzalishaji mdogo.
- Kuweka kipaumbele katika kutengeneza soko la ndani na kuongeza uwezo wa watumiaji wa ndani na hapo tutawezesha uzalishaji wa ndani kuwa ndio nguvu ya kukuza uchumi wetu. Viwanda na biashara zetu lazima zikue kutoka ndani ya nchi yetu.
- Kuingilia kati uzalishaji katika sekta ya kilimo ili kuwahakikishia mapato wakulima wadogo wadogo kwa kuweka sera za bei ambazo zinawapa wazalishaji wadogo kipato cha uhakika kutokana na mazao yao. Njia za kuwalinda wakulima dhidi ya anguko la bei ya soko la dunia lazima ziwekwe.
- Maslahi ya wafugaji, haki zao na wajibu wao yanahitaji kufikiriwa kwa makini zaidi na kuwekewa njia nzuri zaidi za kisheria na kiutawala ambazo zitawahakikishia haki zao msingi na uhuru kwa mujibu wa Katiba.
- Kuweka njia imara za marekebisho ya kifedha kwa ajili ya faida ya wawekezaji na kunufaika na upendeleo zaidi kwa watu wetu badala ya kuwajali zaidi wawekezaji wa nje.
- Kufanya mapitio makini ya kuongoza vigezo vya vivutio kwa wawekezaji wa nje. Ni lazima tusiwachukulie kama wahisani wetu.
- Serikali iingilie katika kudhibiti soko la fedha ili kuwajali wakopaji wadogo. Kuna haja ya kuchukua hatua za kusaidia huduma za mikopo na akiba kuwafikia watu vijijini.
- Waendesha maduka madogo yasiyo rasmi sio kero kwa jamii. Tunakubaliana kuwa sekta hii inahitaji mabadiliko, lakini sio kwa njia ya polisi, bali kwa njia ya kuweka jitihada za kiuchumi zinazowawezesha watu wawe mawakala wenye thamani na faida. Hivyo lazima kuwaingiza katika sekta nzima ya biashara ikiwa ni pamoja na mambo ya huduma za mikopo, kuchangia kodi, huduma zilizo katika kiwango, utoaji leseni na mahala pa kuendeshea biashara ndogo ndogo na sio tu katika bustani za majumba makubwa.
- Kuimarisha upatikanaji wa mikopo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za kuishi. Kuanzisha sera ya dhamana au rehani kwa kuwalinda na kutoa upendeleo kwa wenye kipato cha kawaida. Ujenzi wa majengo na barabara ni kichochea muhimu katika kukuza uchumi wan chi.


6) Uchumi

Kwa kuangalia changamoto za sasa kufuatana na ukubwa wa tatizo la umaskini, kuangalia mahitaji ya kiuchumi katika upeo mpana zaidi ya ukuaji uchumi. Tunahitaji kuweka mkazo katika watu wengi zaidi kuzifikia fursa, hasa kwa watu maskini na wasio na uwezo. Ukuaji uchumi lazima unufaishe watu kwa kuangalia walio maskini zaidi, kunufaisha wengi badala ya kuangalia wachache tu wenye kupewa upendeleo.

Kwa hiyo watu yapasa wapewe fursa ya kushiriki katika shughuli za uzalishaji na katika mchakato wa ukuaji ili wanufaike kwa njia ya ushiriki wao wenye kuleta tija na kuweza kufikia maendeleo ya jumla ya nchi yetu. Watu wanahitaji kuwezeshwa ili ushiriki wao uwe wa tija. Uwezeshaji huu unaweza kufanyika kwa njia ya kuwekeza katika elimu, afya, miundo mbinu n.k.

Panahitajika mfumo sahihi uandaliwe kuhakikisha matumizi mazuri na ya kisheria juu ya urithi wa pamoja wa rasilimali zetu. Hapa panahitajika kuimarisha uwezo wa utawala na taasisi zenye wajibu huo. Pawepo uwiano kuhusiana na dhima ya Dola na soko.

Lingine muhimu ni juu ya namna tunavyojenga mahusiano yetu na jumuiya ya kimataifa. Ushirikiano wenye tija lazima uwekwe na kulindwa kwa misingi ya kuheshimiana, na maslahi ya taifa lazima yawe ndio yanaongoza ushirikiano huo. Hivyo umiliki wa nchi yetu na uongozi katika kutengeneza sera, mikakati, programu na menejimenti ya mchakato wa bajeti yapasa ziwe ndio kanuni zinazoongoza.

Sasa tunaelewa kwamba kinachotupatia lengo la uchumi na sera za kiuchumi sio tu uzalishaji na upatikanaji wa bidhaa na huduma. Uchumi lazima uwe chombo cha kutuhakikishia ubora wa maisha ya raia wote, ukiwa unahudumia manufaa kwa wote na uhalali na usawa wa kupata mali na huduma zilizopo. Sera yetu ya kiuchumi inaangalia mno upande mmoja, upendeleo ukiwa ni kwa wale ambao wana uwezo tayari. Masuala ya kijamii yanahitaji kutiliwa mkazo upya. Hapa maoni yetu ni haya:

- Tunapendekeza kwamba huduma ya afya na elimu ziwe ndio kipaumbele namba moja katika kupanga uchumi wetu.
Rasilimali kubwa ya taifa letu ni watu wake. Kushughulikia afya na elimu ya watu, kwanza kabisa ni wajibu wa kimaadili, kutunza maisha na kuongeza ustawi wa watu. Lengo hili hili yapasa liwe ndilo la kwanza katika mipango yote ya kisiasa na kiuchumi. Kuacha kujali afya na elimu kwa watu wetu ni kosa kimaadili.

Kwa maoni ya kiuchumi kuzungumzia gharama za huduma hizo ni kupotoka. Ni bora kuzungumzia kuwezesha ubora wa rasilimali watu ili uwezo wao uongezeke. Gawio linalotokana na uwekezaji huu tu linatokea haraka mara tu na ni la muda mrefu na huongeza kiwango cha jumla cha tija katika nchi.
- Watu wanaofanya kazi katika huduma ya afya na elimu wako katika taaluma za kiwito. Ubora wa elimu na afya unatokana kwanza kabisa na kujitoa kimapendo na uwajibikaji wa kitaaluma.
Tunatoa changamoto kwa dhana msingi ya mtazamo wa uchumi wetu wa sasa ambao mkazo wake ni kwamba lazima nia iwe ukuaji uchumi, kisha tutaweza kuongeza matumizi katika huduma za jamii. Maoni yetu ni kwamba tunahitaji kuwekeza zaidi katika afya na elimu ili tija ya kiuchumi na ukuaji wake vitokane na uwekezaji/matumizi hayo.
- Tunapendekeza mapitio katika sera ya kuchangia huduma za jamii. Sera hii ya ushirikiano wa Umma-Binafsi (UBIA) inaleta mambo mengi yasiyoridhisha na inachangia moja kwa moja katika kuyumbisha na kuzidi kuongeza mgawanyo wa matabaka katika jamii yetu, kwa kuwa baadhi wanazimudu gharama za huduma hizo na wengine wanashindwa kwa hiyo hawawezi kupata huduma hizo msingi.

• Sera ya Elimu

Mkazo lazima uwe katika kiwango cha juu katika elimu cha shule zote na kuondoka na kiwango cha chini kwa watu maskini na kwa shule za vijijini.
Ubora huu wa kiwango kizuri na sawa kwa wote, lazima kikubalike katika ufundishaji na kujifunza na vile vile katika usimamizi na utawala wa shule katika ngazi zote za elimu: msingi, sekondari na vyuoni.

 Katika ngazi ya shule ya msingi elimu iwe bure na gharama zibebwe na kodi inayolipwa Serikali kuu na Serikali za Mitaa.
 Kwa ngazi ya Sekondari na vyuo sera nzima ya elimu inahitaji kufanyiwa mapitio na mpango lazima uongozwe na Serikali na hivyo hapatakuwa na mwingiliano wa programu kama ilivyo sasa. Pia hali ya mazingira ya kazi kwa waalimu yafanyiwe mapitio. Tuisheni/mafundisho ya ziada yafanyiwe mapitio pia, ulipaji ada na viwango vyake lazima udhibitiwe, mfumo wa mikopo uwe wazi zaidi na iwe ni juu ya mfumo mzima wa kodi na sio mzigo umwangukie mzazi pekee yake.
 Mapitio katika mfumo wa mitihani na kupima wanafunzi kwa kutumia maendeleo yake, na sio tukio moja la kufanya mtihani.

• Sera ya Afya

 Tunapendekeza kurudi katika huduma bure ya tiba kwa mahitaji msingi ya kiafya katika zahanati na hospitali ngazi zote na kuanza mtindo wa kuzipiga faini hospitali za Serikali ngazi za chini ikiwa huduma hizi za msingi hazipatikani katika eneo lao.
 Kushirikisha kikamilifu hospitali na zahanati zinazotoa huduma bila kujitafutia faida, nazo ni zile zinazoendeshwa kwa kujitolea ama zile za mashirika ya kidini. Hizi ziingizwe katika mfumo wa uendeshaji wa zahanati na hospitali za umma na zipate misaada sawa.
 Kuifanya huduma ya bima ya afya kuwa ni hitaji msingi na la lazima kwa kila Mtanzania.

• Sera ya Kazi na Ajira

 Sera hii inahitaji kufikiriwa upya haraka. Jambo hili limekuwa kitendawili cha hali za kihistoria na maoni na upendeleo na imeathiri sekta mbalimbali na makundi ya watu wa namna mbalimbali. Msingi ungekuwa pato la mshahara ambao unamwezesha mtu kuishi na sio mshahara wa kima cha chini. Malipo ya ziada kama zawadi kwa mafanikio mazuri (bonus), marupurupu (allowances) ya kila namna, gharama maalum sasa yamekuwa sambamba na kipato na wala hayatozwi kodi wala kudhibitiwa. Wale walio katika nafasi za kujipangia upendeleo huu wanafanya hivyo kwa makusudi na hawako radhi kujipunguzia au kujiondolea upendeleo huo. Na hii ni kuanzia na ngazi za juu za nafasi za umma.

Sio tu kwamba sera ya ajira sio ya haki, bali pia sio nzuri na inaleta mtikisiko na hali ya kutoridhika katika jamii kama ambavyo migomo ya waalimu na watumishi wa afya ilivyodhihirisha hivi karibuni. Na njia ya kutumia nguvu iliyotumika kukabili migomo hiyo ni jambo la aibu.

• Mtazamo wa jumla wa sera ya kiuchumi – kijamii

 Lazima tuwe na ujasiri na tuthubutu kutambua mahitaji yetu na kuweka vipaumbele na kujua namna ya utekelezaji wenye kuleta kilichokusudiwa. Wafadhili, Benki ya Dunia, Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), nchi wahisani wanaweza kuwa na la kusema. Lakini wasiwe ndio wanatuamulia namna ya kupanga mahitaji na vipaumbele vyetu na kuwa ndio wasimamizi (take charge) katika mchakato wa maboresho ya kimaendeleo kama ambavyo imeonekana kuwa.

Kwa haya lawama zinatuangukia sisi wenyewe. Kila mara tunavutwa na pesa na hivyo tunakuwa tayari mno kukubali masharti yoyote bila kufikiria matokeo yake na bila kujali sura kamili; bila hata kujifunza mahusiano yaliyomo baina ya hali mbalimbali ya nchi yetu kiuchumi na kimuundo. Mara nyingi mno tunakuwa na mtazamo katika mradi tu (project – focused) na tunashindwa kuwa na mtazamo kamili katika kupanga maendeleo yetu.

 Kilimo na ufugaji yapasa vipewe uzito na kipaumbele kadiri inavyostahili, kwa kuwa bado ni muhimili/uti wa mgongo wa uchumi wetu. Mazao ya kilimo na biashara yanayostawi katika kila sehemu (mkoa au wilaya) yapasa yatambuliwe kisayansi na watu wasaidiwe kushughulikia kilimo kwa njia ya kuwezeshwa kuwekeza katika viwanda vya kusindika mazao ya kilimo na ufugaji, huduma za ugavi wa pembejeo, mashine za kilimo (agri-machinery), masoko na huduma za ugani kwa kulenga kupata mazao mengi na yenye ubora.





7) Hifadhi ya Jamii

Njia ya moja kwa moja inayoweza kuisaidia Tanzania kupunguza umaskini ni kuhakikisha huduma ya hifadhi ya jamii kwa walengwa na makundi ya wasio na uwezo. Sera hii inaweza kupunguza umaskini uliokithiri kwa nusu ndani ya muda mfupi na kwa kutumia gharama tunayoimudu.

• Tunapendekeza:

- Mpango wa mafao ya uzeeni kwa watanzania wote walio na umri wa zaidi ya miaka 60.
- Kuwapatia watoto wote wa shule za msingi chakula cha mchana bure/bila malipo.
- Malipo ya kila mwezi kwa kila mtoto mlemavu.
- Zaidi ya hayo tunapendekeza kuimarisha mfumo wa kijamii wa ustawi (welfare): hifadhi ya jamii inahitaji mambo mengine zaidi ya pesa. Hali ya kukosa uwezo na ulemavu vinahitaji raia wote kumjali mtu huyo. Jamii haiwezi kuwa imestaaribika na kuwa na msimamo wa kimaadili ikiwa inawadharau wale wasio na uwezo ama walio na ulemavu. Kuheshimu hadhi ya utu wao ni sehemu ya kuonyesha mwenendo na tabia ya kiutu. Kuwatendea kwa kiwango kilicho chini ya utu wa mwanadamu ni tabia ya kiuhalifu (criminal) na vile vile ni dhambi kimaadili.

Tunapotoa wito wa kuimarisha mfumo wa ustawi wa kijamii (social welfare) tunapendekeza kupanua ushirikiano baina ya jitihada za vikundi vya kujitolea kama vile vya Jumuiya Ndogo Ndogo za Kikristo na vya Mfumo wa zakat kwa waislamu na vile vya Serikali kuu na Serikali ngazi za chini. Hii inaleta hitaji la kuongeza wafanyakazi (social workers) ambao wataunganisha jitihada za vikundi vya kujitolea na zile za taasisi za Serikali. Kushughulikia na kutunza watu wasio na uwezo na walemavu sio kazi rahisi, na hivyo ili kuweza kufaulu tunahitaji kushirikiana wote miongoni mwetu.

Ni lazima tushawishike kwamba hii ni kazi yenye thamani na maana kubwa. na kwa kweli matokeo mazuri ya jitihada kama hizo za jamii ni kwamba jamii yetu itakuwa ya kiutu zaidi, yenye msimamo wa kimaadili na itaonyesha sifa nzuri ya ubora wa kujali, ambayo itameza au kuondoa tabia na mienendo mibaya kama uchoyo, ubinafsi na rushwa/ufisadi. Kutunza kwa kujali watu wasio na uwezo yapasa, na hatimaye kunaifanya jamii yetu kuwa nzuri zaidi kimaadili na ya kiutu zaidi.



HITIMISHO

Mwisho kabisa tunapendekeza tafakari ya kina juu ya nini na nani wanaongoza uchumi wetu na maslahi ya taifa letu. Na kwa hiyo kwa uwezo mkubwa tuhimize mijadala juu ya kama uchumi wetu unavutiwa na ongezeko la mahitaji ama na kuwezesha ongezeko la upatikanaji vitu? Nini kinasukuma/kuongoza uchumi wetu? Je, ni uwekezaji, au ni ongezeko la fedha, kuongeza ajira na bidhaa na miundombinu? Tuna nia ya kuongeza mahitaji na matumizi ya ndani ili kuchochea uzalishaji wa ndani kukamilisha mahitaji ya ndani na hapo tuweze kuongeza uwezo wetu wa kuzalisha bidhaa zenye thamani zaidi badala ya kuwa na bidhaa za malighafi.

Kwa kusikiliza mjadala huu kuwa mahitaji yetu hasa sio pesa, bali tunachohitaji ni utashi, mawazo na kufanya kazi kwa bidii. Kuna tabia imejijenga katika jamii yetu, nayo ni ile ya kutojishughulisha, na watu wana kiu ya kutaka fedha bila kufanya kazi. Mwenendo huu hautatuletea maendeleo ya kweli.

Naam, nchi ina utajiri mkubwa wa rasilimali na utaalam, na pia kuna fursa nyingi ambazo hazijatumika. Na bado nchi ina vikwazo vingi vya kiurasimu ambavyo huruhusu wachache kunyonya kwa faida yao binafsi. Tunahitaji kuweka mfumo wa kuweka mikakati na kuanzisha chombo cha kujitoa kweli katika kuhamasisha na kulinda manufaa kwa wote na mafanikio mazuri kabisa kwa ajili ya urithi wa kitaifa.

Tunahitaji kufufua maadili, kurudi katika tunu msingi za kimaadili na matashi ya kujenga maelewano, mshikamano, kujali manufaa kwa wote na kumpatia kila mmoja mahali, nafasi, fursa na wajibu.



KAMATI YA TAIFA
CPT





MPANGO WA KUHAMASISHA HUDUMA YA KICHUNGAJI KATIKA JAMII KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2010


Idara ya Kichungaji
TUME YA HAKI NA AMANI - TEC

MPANGO WA KUHAMASISHA HUDUMA YA KICHUNGAJI
KATIKA JAMII KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2010


DIRA

Mungu anakuita, anakuhitaji.
Dunia imeumbwa na Mungu ili iendelee kuwa mahala panapodhihirisha Ufalme wa wake. Ukuu wa uumbaji huu ni mwanadamu ambaye ndiye kiumbe aliyekirimiwa utashi na uelewa ili awe mshiriki na mdhamini wa kazi ya Mungu. Mungu ametuchagua tuchukue wajibu huu, na pamoja naye tupunguze uovu na taabu, na kujenga dunia ambamo upendo na maelewano vinamhakikishia kila mmoja kufurahia utu wake.

Kama wakristo, tunapokea mwaliko wa Kristu uwe mwaliko wetu. “Roho wa Bwana yu juu yangu, kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, na vipofu kupata kuona tena kuwaacha huru waliosetwa, na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa” (Lk 4: 18 – 19).
Kwa kutilia mkazo mwaliko huu, tunaelezwa kuwa Mwana wa Mtu atakaporudi atayahukumu mataifa kwa kigezo cha huduma tuliyotoa kwa wenye njaa, kiu; walio wageni, uchi, wagonjwa na wale walio kifungoni (rej. Mt. 25: 31 – 46).

Mungu alipomuumba Mwanadamu alimpa wajibu wa pekee, sio tu kuwa mlinzi na mdhamini wa dunia/uumbaji, bali pia kuwa mshiriki katika kuumba, na kutunza. Ni wito wa kushirikiana na Mungu katika kupambana ili kuuondoa uovu katika jamii yetu na kujenga ulimwengu ambamo kila mmoja ana wajibu wa kutekeleza na wakati huo huo ana haki ya kufurahia matunda ya dunia yetu.

Programu yetu ya kulihamasisha Kanisa kutekeleza wito wa kichungaji katika mambo ya kijamii ni kuwatia moyo waamini wote kutambua na kukubali wito wao wa Kikristo, wito wa kuwapelekea watu habari njema ya Yesu katika mambo ya kijamii na ya kitaifa. Kutakatifuza malimwengu, kuifanya nchi yetu na watu wetu kuishi pamoja huku manufaa ya kila mmoja yakiwa yanatimizwa: kupata huduma msingi za maisha na kuheshimiwa utu wa kila mmoja. Hapa maslahi na manufaa ya wote na ya kila mmoja katika jamii yanapaswa kuzingatiwa. Huu ni wajibu wa kila mmoja.

Mungu anakuhitaji, haya si maneno tu, bali ni uamuzi wa makusudi wa Mungu anayetukabidhi wajibu huu. Kutopokea mwaliko huu unaotoka kwa Mungu ni kushindwa kutimiza wajibu wetu, ni dhambi ya kutotimiza wajibu wa wito wetu wa Kikristo. Wito wa kutimiza wajibu wa kijamii, ambao ni kutia chachu ya tunu za injili na Mafundisho ya Kristo katika masuala na shughuli za kijamii, kiuchumi na kisiasa ya taifa letu.
Wito huu haujaeleweka vema na jumuiya zetu. Watu wengi wanadhani kwamba mambo ya umma sio sehemu ya majukumu yetu ya kidini na kiimani, na hivyo Kanisa halipaswi kujishughulisha na mambo hayo. Kinyume chake Kristo anatualika kuleta mafundisho ya Mungu, maadili ya asili yetu ya kibinadamu kama tulivyoumbwa na Mungu. Tunaalikwa kuyafanya hayo yawe ndio msingi na mwanga unaoongoza maamuzi na sera zetu.

Tunaona kwamba ikiwa maadili hayo yatakuwa sio msingi wa maisha yetu ya pamoja na kuyashuhudia katika utendaji wetu na mienendo yetu, hapo tutaingia haraka katika uovu na ubinafsi na uchoyo, mambo ambayo yanaangamiza jamii yetu.

Katika miaka ya hivi karibuni sote tumeshuhudia haya yakitokea na tumepata madhara yake katika amani na utulivu katika taifa letu. Kumekuwa na mgawanyiko miongoni mwetu, kumejengeka matabaka ya wenye mali nyingi na watu wengi ambao wana mali kidogo sana, maskini na fukara hasa . Mwelekeo huu unatishia na kuhatarisha amani na moyo wa ujamaa tuliokuwa nao na kushamiri kwa utengano na chuki kati yetu.

Sote tunawajibika kwa nchi yetu na taifa letu. Ndio maana Mungu ametujalia sote kuenzi hadhi ya utu wetu sawa. Kwa hiyo tusiruhusu nchi yetu Tanzania ikawa na watu ambao thamani ya utu wao ni zaidi ya wengine. Tusisahau kila mmoja wetu ameumbwa katika sura na mfano wa Mungu (Taz. Mwa 1: 28).

Ni kwa sababu hiyo tunazindua programu hii ya kuhamasisha jumuiya zetu kuelewa wito wao wa kijamii, kuinjilisha na kuifanya jamii yetu iwe ya kiutu kulingana na mpango wa Mungu wa uumbaji na haswa kwa jamii ya wanadamu. Msingi wa utu wa mwanadamu ni asili yetu ya kwamba tumeumbwa na Mungu. Huu ndio msingi ambao dini zote zinausadiki na kuuheshimu. Kwa hiyo tunaweza kushirikiana na waislamu, wahindu, na watu wenye kufuata dini za jadi. Sote kwa pamoja tujenge dunia yetu kulingana na mpango wa Mungu.


WITO

Tumetumwa katika jumuiya zetu, Parokia na jumuiya ndogo ndogo, kuwahamasisha watu wafanye tafakari juu ya hali halisi ya maisha na kujua ni kwa namna gani mafundisho ya Kanisa na Injili yanatupatia mwanga wa namna ya kuboresha maisha yetu na katika Taasisi za jamii yetu. Tunachukua hatua katika kurekebisha mambo yanayokwenda vibaya na kuimarisha mambo mazuri. Ni mwaliko wa kuwasaidia watu katika kutekeleza maamuzi yaliyothibitishwa katika ahadi yao waliyoweka wakati wa ubatizo.

Hatua zifuatazo zinapendekezwa kutumika katika utekelezaji:
- Kuchunguza hali, kutambua na kubaini tatizo.
- Kutumia Mwanga wa mafundisho ya Kristo na kutoka katika Mafundisho ya Kanisa kuhusu Jamii.
- Kuamua hatua ya kuchukua na namna ya kufuatilia utekelezaji.


UTARATIBU WA KUZINGATIA (METHODOLOJIA)

Programu hii ya kichungaji inahitaji uongozi mzuri na hatua madhubuti za ufuatiliaji. Hapo tutaweza kufanikiwa na kuleta matokeo katika maisha ya Jumuiya ya Kanisa na ya taifa letu.

Katika hatua ya utekelezaji wa programu hii tunapendekeza:

1) Kufanyika mikutano ya makleri na viongozi wa halmashuri walei. Ni lazima katika mkutano huu ijadiliwe programu hii katika ngazi ya Jimbo na kupewa umuhimu unaostahili.
2) Wajumbe wa Mkutano huu: Wakurugenzi wa Kichungaji na Wajumbe wa Tume ya Haki na Amani watakuwa wakufunzi – kueleza na kufafanua mada za programu yetu.
3) Katika kazi ya kuongoza mkutano (no. 1), wajumbe wa CPT na wawakilishi wa Serikali waalikwe kutoa maelezo juu ya hali halisi pale watu wanamoishi.
4) Inapendekezwa paundwe timu ya Jimbo kwa ajili ya ufuatiliaji wa programu hii.
5) Katika ngazi ya Parokia programu ilenge kufundisha wanavijiji/watu mitaani na katika Jumuiya Ndogo Ndogo ili waweze kujadili masuala yaliyomo katika programu.
6) Ripoti za majadiliano hayo zitumwe Parokiani (Paroko na Halmashauri) kila baada ya miezi mitatu. Ripoti hizo zionyeshe mambo yaliyojadiliwa na maamuzi yaliyofikiwa.

Kwa kupata uelewa zaidi mada zilizojadiliwa katika mkutano wa Wakurugenzi wa Kichungaji na Wajumbe wa Tume ya Haki na Amani (TEC) ni:
1) Vipaumbele kwa mujibu wa Mafundisho ya Kanisa kuhusu Jamii.
2) Umuhimu wa uongozi wenye maadili katika kuleta mabadiliko ya kijamii, kiuchumi, kisiasa na kidini katika Tanzania.
3) Mfumo wa Sheria Tanzania: Nguvu na Changamoto.
4) Haki za Binadamu katika sera za biashara na fedha.
5) Mtazamo wa kimaadili katika mfumo wa kisiasa na kiuchumi.
6) Hifadhi ya jamii.

Mada hizi zinapatikana kwa kiswahili na kiingereza, kama unazihitaji wasiliana na:
- Ofisi ya CPT - St. Josephs Cathedral Dar es Salaam
Tel: 022-2127675/0713-329984
E.mail:
[email protected]

Tunaweza pia kukusaidia kupata Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa utatujulisha mahitaji yako.
MADA KUU ZA TAFAKARI


Agenda hizi ndizo zilizoazimiwa katika Mkutano wa Wakurugenzi wa Kichungaji na Wajumbe wa Tume ya Haki na Amani TEC uliofanyika tarehe 20 – 22 Januari, 2009.

1. UTU
Utu aliokirimiwa kila mwanadamu bado haujawa ndio kiini na msingi wa mienendo yetu kama watu binafsi, katika vikundi na kama jamii. Kasoro hii tunaiona katika jumuiya za kidini, katika mila, desturi na tamaduni zetu, katika shughuli zetu za kiuchumi na katika uwanja wa kisiasa.

Kila mwanadamu ana utu sawa na utu wa mwingine na kwa hiyo lazima utu wa kila mmoja uheshimiwe na wengine: watu binafsi, taasisi na utawala. Ikiwa mwanadamu anapewa hadhi kutokana na utu wake, na haki zake atajengeka na kuwa na utu kamili, na yeye mwenyewe atajenga uwezo wake kikamilifu.

Vile vile bila kufanya hivyo jamii yetu haiwezi kamwe kukua na kuwa jamii yenye watu wenye kuenzi ukweli, utu na usawa. Kuigawa jamii katika matabaka ni kosa na ni dhambi, licha ya kuwa huko ni kuzuia jamii kufikia uwezo wake kamili na kuwa jamii yenye furaha. Katiba ya Jamuhuri imeweka bayana kwamba haki, wajibu na uhuru wa binadamu lazima vilindwe, viheshimiwe na kutolewa sawa kwa wote.

Kwa hiyo tunapaswa kufundisha watu dira hii katika:

- Ngazi ya familia, katika ujirani na Jumuiya ndogo ndogo. Ni hapa ndipo msingi wa jamii na kanisa unapojengwa.
- Katika mashule, tuangalie upya sera zetu za elimu na malezi na upande wa kimaadili tuchunguze yaliyo katika mitaala na ratiba katika mashule. Kwa sasa hakuna msisitizo wa kutosha katika malezi ya ubora/sifa za kiutu.
- Katika mambo ya kisiasa na kiuchumi: heshima na utu wa mtu sio suala la kubaki katika maneno na hotuba nzuri na matamko. Taasisi na sheria zetu lazima zikumbuke kuwa kanuni za kimaadili yapasa ziongoze kazi yao.
- Katika ngazi za Kanisa: mkazo zaidi uwekwe katika kuwajenga watu katika mambo ya kiroho ambayo ni ya lazima katika kuongoza tabia ya kijamii. Hapa ni zaidi ya kuweka kanuni na taratibu. Kinachohitajika hasa ni roho ya kiinjili na wito wa kinabii.

Mambo yanayopendekezwa kufanywa katika kufundisha na kuhamasisha utu ni:
- Mafungo katika ngazi ya Parokia na taasisi za Kanisa.
- Mikutano na wazazi ili kuwahamasisha na kutafakari namna ya kufundisha maadili katika ngazi ya familia.
- Semina na Waalimu.
- Kujadili na mamlaka ya elimu ngazi ya wilaya na mkoa.
- Tathmini ya kiroho ili kupima mambo ya kiroho na kupendekeza dhamira za kichungaji ambazo zinaweza kutumika katika mahubiri na miongozo ya katekesi.
- Kufanya utafiti katika ngazi ya Parokia ili kujua nini vijana wanapendelea na kutafuta njia ya kuwajengea hadhi ya utu wao kwa kutumia mambo yanayowavutia vijana.
- Kuchunguza vitabu vinavyotumika mashuleni kama vinahimiza au vinachochea maadili mema.


2. UONGOZI
Dira
Suala la uongozi ni pana. Kuna aina nyingi za uongozi (kiroho, kiutamaduni, kielimu, kiutawala, kisiasa, kiuchumi). Vile vile zipo ngazi mbalimbali za uongozi (familia, ujirani, vijiji, taasisi, kidini, kitaifa). Uongozi unahitaji watu wenye sifa ya huduma, wanaojali, walio wazi, wanaowajibika, wanyenyekevu, wenye hekima na upendo. Uongozi kila mara unashawishika kutenda kinyume na hayo na kuwa na uchoyo na kutumia madaraka vibaya. Kwa hiyo ni muhimu kuandaa viongozi, kushirikiana nao na kushikamana nao na kuwadhibiti kwa lengo la kuwasaidia kuwa jasiri walio waaminifu katika kazi zao.

Hali yetu inadhihirisha kuwa:
- Katika miaka ya hivi karibuni tumeona matatizo mengi ya uongozi. Kwanza kabisa yapasa tujadili kiini chake na kisha tutafute tiba yake.
- Katika uwanja wa kisiasa tunapaswa kuangalia namna wagombea wa na vyoteuliwa na vyama vyao. Tunahitaji kutafuta taarifa ya njia na vyanzo vya upatikanaji wa fedha za vyama vya siasa na namna wanavyozitumia. Watu wajadili kama mfumo wa uwakilishi kiuwiano (proportional representation system) haungeweza kuwa bora kuliko ule wa sasa. Kuna haja kubwa pia ya kusaidia watu kuijua Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
- Ni lazima katika mambo ya kijamii tuwahimize watu kueleza matatizo wanayokumbana nayo katika maisha yao na kuyatolea taarifa katika ngazi ya Parokia hadi Jimbo/Wilaya. Tuwasaidie kushiriki katika utawala tangu ngazi ya Serikali za kijiji/mitaa hadi ngazi ya halmashauri ya wilaya na kutafuta taarifa kisha kufuatilia nini watumishi wa umma wanafanya katika kuhudumia watu. Njia nzuri ni kuanza na kundi mahalia kushughulikia matatizo ya hapo walipo.
- Katika Kanisa tuhimize watu kutoa maoni yao katika Jumuiya ndogo ndogo na kusaidiana kuwa waaminifu katika wito wa Kikristo. Jumuiya ya Kanisa ni mahala ambapo mtu anakuwa na nafasi ya kutimiza wajibu wake wa kushiriki vilivyo katika shughuli za jumuiya. Hiarakia ya Kanisa haimaanishi kuwa ni kutoa amri tu kwa watu wa ngazi ya chini, bali kazi ya Hiarakia ni kuongoza namna ya kutimiza ahadi tuliyoweka wakati wa ubatizo.

Kwa agenda hii tunapendekeza:

Katika ngazi ya kisiasa: kuunda timu ya CPT na wajumbe wa halmashauri kutengeneza maswali maalum, kuendana na hali mahalia, watu wajadili na ili kutoa mawazo na maoni mazuri, wapatiwe habari zinazohitajika kwa ajili ya tafakari. Hapa tusiwape nafasi wale ambao ni wagombea wa kisiasa kutawala mjadala.

Kijamii: Watu watafute ni mashirika gani yapo hapo na huduma zipi hutolewa, na wangeweza kupata msaada gani katika kutatua matatizo yao. Ni taarifa gani tunapaswa kuwapatia watu ili waweze kufanya tafakari katika Jumuiya ndogo ndogo.

Kanisa: Tunawezaje kuimarisha tafakari katika jumuiya juu ya namna Parokia inavyoendeshwa. Halmashauri inafaa iwe chombo ambamo tathmini hiyo inaweza kufanyika. Ikumbukwe Parokia sio chombo cha utawala, bali lazima iwe ni jumuiya hai ya kusaidiana katika kuleta ubora wa maisha ya kiimani, matumaini na mapendo. Kwa pendekezo hili tufanye tathmini ya kiroho katika dhamiri na kuweka ahadi ya uwajibikaji katika kuwa zaidi mashahidi wa ujumbe wa Kristo katika hali halisi ya Tanzania leo.

3. HAKI

Dira
Lazima mfumo wa sheria uwe ni kwa ajili ya jumuiya ya watu katika kulinda na kudumisha amani, ukweli, haki, uhuru, mshikamano na usalama. Mfumo huu unapoleta ukosefu wa haki, watu wanapoteza imani nao.

Tutafute:
- Kwa njia gani tutawasaidia watu kujua haki zao na kuelewa sheria zinazoathiri maisha yao.
- Kuona kama shule zetu zinafundisha Katiba ya nchi na umuhimu wake.
- Tuone kama Wabunge wanawasiliana na majimbo yao na kuwa kweli wawakilishi wao. Kujadili kama wanadhibiti ya kutosha utendaji wa serikali. Ni kwa vipi watu wanapeleka masuala yao katika vyombo vya serikali na kusikilizwa?
- Mahakama za mwanzo zinahudumia watu wengi lakini ziko katika hali mbaya. Je, tunaweza kuziboresha vipi?
- Watu wanaona adhabu zinatolewa kwa makosa madogo, lakini wenye makosa makubwa, wanaachwa tu. Kwa nini watu wanafikiri hivi?
- Lazima tufikiri njia mbadala ya kutoa adhabu na kuona wafungwa kama watu wenye haki pia. Vile vile kutambua kuwa lengo la magereza ni kujenga amani na kurekebisha watu waliofanya makosa.
- Kila mara mfumo wa sheria unafanya kazi taratibu na hivyo watu husubiri mno haki kutendeka. Kukosa ufanisi na utaratibu wa utekelezaji vinasababisha ukosefu mwingi wa haki. Tunawezaje kuboresha hali hii?
Katika mjadala tulenge kuona kwamba “Mamlaka za siasa zichaguliwe na uamuzi wa hiari wa raia, nazo lazima zijali kanuni ya “utawala wa sheria,” ambamo ukuu ni wa sheria na si wa matashi ya watu wasio na sheria.”1

4. BIASHARA NA FEDHA

Dira
Hizi ni taasisi za biashara na fedha na shughuli nyingine zinazotoa huduma katika jumuiya. Biashara zinazotoa mahitaji ya vitu/bidhaa na kubadilishana na bidhaa hizi. Taasisi za fedha zinatunza thamani ya fedha, kwa kuweka kiwango cha kubadilisha fedha.

- Katika biashara, motisha haipaswi kuwa katika faida tu. Biashara inawafikishia watu bidhaa, hivyo isiendeshwe kiunyonyaji.
- Ni vipi tunaweza kuwasaidia watu kutetea maslahi yao na kuzuia wasinyonywe.
- Moyo wa ushirika umepungua mno na matokeo yake watu wameathiriwa na biashara zilizokosa uwaminifu. Tunawezaje kusaidiana.
- Mfumo wetu wa benki unafikisha huduma kwa watu wachache tu, na hasa kwa watu wa mijini na kwa wale wenye kiwango kizuri cha kipato. Lazima tusaidiane, hasa wale ambao hawana kipato cha kutosha, kuunda SACCOS na vikundi vya kusaidiana. Kanisa lazima lifanye bidii kuhamasisha hayo.
- Wachache walio katika mamlaka au katika nafasi za juu za utawala wana marupurupu mengi mno. Tusukume kupunguziwa hayo ili wawe na maisha ya kawaida.
- Tuwe makini na uporaji wa ardhi unaofanywa na makapuni makubwa na watu binafsi, matajiri. Tukumbuke ardhi ni ya thamani na ni hitaji la lazima kwa kila mmoja.
- Rushwa katika biashara, huduma duni, bidhaa duni vinaleta sifa mbaya, na hii ni tabia iliyo dhambi. Miongoni mwa watu hali hii inawajengea hasira na kukosa uaminifu na vile vile watu hujitetea kwa nguvu na kujengea watu fikra ya kulipiza kisasi.
- Udanganyifu katika biashara ni kushusha sifa mmiliki kwa wateja.
- Serikali iwe makini katika kuweka mikataba na wawekezaji wa umma na watu binafsi. Imekwishabainika kuwa katika mikataba hiyo maslahi ya wananchi hayalindwi kikamilifu badala yake wawekezaji hupewa unafuu mkubwa kwa kisingizio kuwa ni kivutio kwao.
- Makapuni ya ndani ni lazima yatiwe moyo na kuungwa mkono ili yaweze kuboresha utendaji wao uwe wenye tija.


5. UCHUMI.

Dira
Uchumi ni kwa ajili ya kuhudumia watu ili wawe na maisha mazuri: wapate mahitaji msingi na walindwe dhidi ya hali zinazowakuta na kutishia usalama wao na majanga mengine yanayoadhiri ubora wa maisha. Maadili katika shughuli ya kiuchumi na kuhakikisha mahitaji haya muhimu katika kumpatia mtu maisha mazuri yanapatikana. Sera za kiuchumi ni lazima ziweke kipaumbele kwa kuzingatia maadili na hivyo kufikia manufaa kwa wote na kulinda utu wa kila mmoja. Kwa hiyo tujadili pamoja na kama jumuiya za kanisa ni lazima tujifunze kuhimiza mahitaji yetu yazingatiwe na wenye maamuzi. Maoni yetu yasikilizwe na kufanyiwa kazi, tunu za kikristo tunazosimamia zionekane katika sera na katika mgawanyo wa bajeti ya serikali.

- Tunaweza kupunguza umasikini kwa kiasi kikubwa katika nchi yetu ikiwa watu wataelewa wajibu wao na kushiriki katika kutatua matatizo yetu: kwa mfano: kushiriki katika namna ya kupata huduma ya maji vijijini, namna ya kudhibiti matumizi ya fedha zinazotumwa katika serikali za mitaa.
- Ni kwa njia gani madiwani watafikisha maombi ya watu wao katika mgawanyo wa bajeti ngazi ya wilaya.
- Je, matumizi katika serikali ngazi ya chini yanawekwa wazi kwa wananchi kujua?
- Wabunge na viongozi katika ngazi ya Mkoa wanatoa fursa ya watu kuwauliza na kuwaeleza mahitaji yao? Tunawezaje kuboresha hali hiyo?
- Je, wakristo wetu wanazielewa fursa zilizopo; huduma zinazotolewa na serikali, mipango ya kusaidiana kama SACCOS, MVIWATA, vyama vya ushirika, jitihada za TASAF. Kwa nini wakristo wetu hawafanyi bidii kuanzisha vikundi/mipango ya kusaidiana? Pia parokia zetu ziwajibike vema katika kujenga ushirikiano na kujenga uwajibikaji wa kijumuiya ili kuboresha maisha.
- Kwa nini watu wetu hawaaminiani? Na tunawezaje kujenga moyo wa uaminifu miongoni mwetu?
- Kwa nini wakristo wetu wanaogopa kuzungumza na wenye mamlaka na walio katika huduma za utawala ili kupeleka malalamiko na kufuatilia utekelezaji wa maamuzi yaliyofanyika. Pia tutafakari namna ya kupambana na tabia ya uvivu.
- Tuna mali nyingi, lakini kila mara tunasubiri “wengine “ au “Serikali” kufanya kitu au kutuletea fedha. Lazima tujifunze kutumia vipaji vyetu na uwezo wetu katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo yetu. Kusaidiana kwa kuunganisha nguvu zetu na uwezo wetu ni wajibu wa kikristo. Mungu ametupa vipawa, lazima tuvitumie.
- Umaskini wa fikra, umaskini wa utashi duni na uwajibikaji ndio hasa husababisha umaskini. Ni kwa vipi jumuiya ya wakristo wanaweza kuwa mahala pa uwajibikaji ili kuweza kuboresha hali yetu.


6. HIFADHI YA JAMII

Dira
Mungu ametujalia uhai na anatupa mwaliko wa kutunza maisha na kuongeza ubora wa maisha. Mungu pia anatutaka kujali kwa namna ya pekee watu wasio na uwezo katika jamii yetu: yatima, wajane, walemavu, wagonjwa, watoto wa mitaani na wazee.

Hifadhi ya jamii maana yake ni kuweka mipango ya kuwahakikishia watu mahitaji na huduma ili wasiishi katika hali ya kukosa hifadhi/ usalama. Tunapozungumzia hifadhi ya jamii haswa tunamaanisha mifuko ya pensheni, elimu, bima ya afya na misaada ya kijamii.

Watu wengi miongoni mwetu hawafikiwi na huduma hii na familia zao zinakwama wanapoingia katika kuhitaji huduma hizo. Tunapaswa kuwa na mtazamo fikiriki ili kuweza kupata njia za kusaidiana. Mipango rasmi iliyoanzishwa na serikali au mashirika ya umma ama makampuni binafsi zinawafikia watu wachache tu ambao ni kama asilimia sita (6%) ya kundi la wafanyakazi.
- Jumuiya ndogondogo wangeweza kuwa chombo cha kusaidiana katika mahitaji ya kila siku ya wanajumuiya wao. Tunawezaje kuzifanya jumuiya zetu zitimize wajibu huu?
- Kutoaminiana ni kikwazo kikubwa katika kuwa na mipango na mifuko endelevu ya jumuiya. Tunawezaje kujenga moyo wa uaminifu? Viongozi wazuri walio tayari kuhudumia wanawezaje kupatikana na tutawawajibishaje viongozi wabovu?
- Lazima tutafute taarifa juu ya huduma na fursa zilizopo. Katika ngazi ya Parokia iundwe timu kwa ajili ya kutafuta taarifa na kuzifikisha katika Jumuiya ndogo ndogo. Taarifa hizo ni pamoja na zihusuzo mfuko wa afya ya jamii, sera ya serikali juu ya karo ya shule, sheria zinazohusu huduma ya tiba kwa mama na mtoto, wazee.
- Katika jamii yetu kuna watu walemavu wengi: Takwimu zinaonyesha kuwa walemavu ni 10% ya watu wote. Hawa ni wenye ulemavu wa namna moja ama nyingine. Kwa kawaida wahitaji hawa wanabaki kutegemea wanafamilia wao wachache, hasa mama au bibi. Kundi hili ndio maskini kupindukia kwa sababu jitihada za kuwainua ni ndogo sana.

Tatizo hili sio rahisi kulitatua. Lakini kwa kutegemea mifumo rasmi ya hifadhi ya jamii tu haitoshi na huduma hii kwao haitakuwa endelevu. Kwa hiyo tunapaswa kutafuta njia ambazo misingi yake ni katika njia za kizamani za kusaidiana, tuzitumie katika mazingira yetu ya leo kwa namna ya kisasa. Wazo hili linaweza kutekelezekaje?


PROGRAMU YA KUHAMASISHA HUDUMA YA KICHUNGAJI KATIKA JAMII KUELEKEA
UCHAGUZI MKUU 2010

(2009 - 2011)


TUKIO

WALENGWA
WAPI/NGAZI
LINI
MHUSIKA/MWEZESHAJI
Mkutano wa Taifa wa kutengeneza Programu
- Wakurugenzi wa Kichungaji
- Wajumbe wa Tume ya H & A (Majimbo)


TEC
20 – 22 Januari, 2009
- Katibu wa Idara ya Kichungaji TEC
- Katibu Tume ya Haki ya Amani – TEC
+ CPT (T)
Kukamilisha programu (booklet form)

TEC
Februari 2009
,,
Kutuma Programu Majimboni
- Maaskofu
- Wakurugenzi wa Uchungaji – Majimbo
- Viongozi wa Tume Majimbo


TEC
Machi 2009
,,
Mkutano wa Jimbo kuzindua Programu
- Mapadre, Watawa
- Halmashauri na vyama vya Kitume
- Taasisi


Jimbo
Aprili 2009
I. Kuanza Mapadre na Watawa, wa
II. Walei
- Askofu
- Mkurugenzi
- Tume (Jimbo)
Mkutano wa Makatekista
Makatekista

Jimbo
Aprili 2009
- Mkurugenzi Uchungaji
- Tume/Mkurugenzi Katekesi
Semina/Mikutano ya Walei/Vyama
Halmashauri (Viongozi wa JNN & Vyama, Kamati)

Parokia
Mei - Juni 2009
- Paroko/mjumbe kutoka Jimboni
- Kamati Tendaji, Viongozi wa vyama
Kufikisha Programu JNN
Waumini/Wakazi
JNN
Julai – Sept. 2009
- Paroko
- Halmashauri ya Parokia
Mijadala na utekelezaji
,,
- JNN
- Vyama vya Kitume
Okt – Des. 2009
- Paroko, Kamati tendaji
- Viongozi wa Jumuiya
Mkutano wa Taifa
(Tathmini ya I)
- Wakurugenzi wa Kichungaji
- Wajumbe wa Tume

TEC
Januari 2010
- Katibu Mtendaji Idara ya Kichungaji
- Katibu Tume – TEC
+ CPT (T)

Mwendelezo wa Mijadala na utekelezaji
Waumini na Wakazi
- Jimbo
- Parokia
- JNN
Febr. – Sept. 2010
- Askofu
- Paroko
- Walei

Kushiriki Uchaguzi kwa tathmini
Waumini na Wakazi
- Taifa
- Jimbo
- Parokia, JNN
Okt – Des. 2010

,,
Mkutano wa Taifa (Tathmini ya II) + kubainisha agenda
- post election
- post synodial
- Wakurugenzi wa Kichungaji
- Wajumbe wa Tume


TEC

Januari 2011
- Katibu Mtendaji Idara ya Kichungaji
- Katibu Tume
+ CPT (T)
Mwendelezo wa Programu
- Post Election
- Post Synodial
Waumini na Wakazi
- Jimbo
- Parokia
- JNN
Febr. - Sept. 2011

- Askofu
- Paroko
- Walei

Kuandaa Ripoti ya Majimbo na kutuma Taifa

Jimbo
Oktoba 2011
- Mkurugenzi wa Uchungaji
- Viongozi wa Tume
Kuandaa Ripoti ya Kitaifa ya utekelezaji wa Programu.


TEC
Novemba 2011
- Katibu Mtendaji Idara ya Kichungaji
- Katibu Tume ya H & A – TEC

(Picha kwa hisani ya MJENGWA)

Wenzetu wa huku Magharibi wanasifika kwa kuwajali watoto. Licha ya serikali zao kutunga sheria zenye kulenga kuzuia na kukomesha uonevu, unyanyasaji, ukatili na unyama mwingine dhidi ya watoto, kuna mlolongo wa taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali zinazojihusisha na suala hilo. Hiyo sio kusema watoto wote wako salama.Ni vigumu katika ubinadamu wetu kufanya kitu kiwe absolutely perfect.

Pamoja na sifa hiyo ni shutuma kwamba upendeleo huo wa hali ya juu kwa watoto unachangia “kuwaharibu” watoto hao. Yayumkinika kusema kwamba miongoni mwa time bombs katika jamii za Magharibi ni watoto wanaodekezwa kupita kiasi. Kama ilivyo kwenye nyanja nyingine, uhuru usipokuwa na mipaka unaweza kupelekea matokeo yasiyopendeza.Hatahivyo, katika hili, uzuri (kuwajali watoto) unazidi ubaya (kuwadekeza).

Ni katika minajili hiyo kunajitokeza hofu kwa baadhi ya watu kutoa misaada kwa watoto kwa kuhofia misaada hiyo inaweza kutafsiriwa tofauti. Hivi karibuni niliona kwenye runinga mtunzi mmoja wa vitabu akilalamikia utaratibu wa kufanyiwa background checks (uchunguzi wa kiusalama,kwa tafsiri isiyo rasmi) kila anapokwenda kwenye shule za watoto kuwasomea vitabu anavyotunga.Mtunzi huyo analalamika kwamba kitendo hicho kinamfanya ajisikie kama mhalifu licha ya ukweli amekuwa akijihusisha na usomaji vitabu kwa watoto kwa miaka kadhaa sasa. Mamlaka husika zinajitetea kwamba utaratibu huo unalenga kuwalinda watoto.

Zamani kidogo niliwahi kukutana na simulizi moja kwamba jamaa flani (mwanaume) alimwona mtoto wa kike anakaribia kuzama kwenye bwawa la kuogelea.Kwa huruma, akajitosa majini kumwokoa mtoto huyo ambaye kwa bahati mbaya chupi yake ilimvuka katika hekaheka hiyo ya kukaribia kuzama.Alipomwokoa na kumpeleka mtoto huyo kwa mama yake akapigwa swali la kutatanisha: “Chupi ya mtoto iko wapi?”Kabla hajatafakari jibu akatandikwa kigongo kingine, “Hivi lini mibaba kama wewe mtaacha kunyemelea watoto wetu kwenye sehemu za kuogelea huku mkisubiri wakumbwe na matatizo kisha muwatomasetomase kwa kisingizio cha kuwaokoa? Hebu nipe chupi ya mwanangu kabla sijakuripoti kwa polisi”.Sijui ungekuwa wewe ungefanyaje!

Tafiti zisizo rasmi zinadokeza kwamba wanaume wengi wamekuwa waoga kusaidia watoto, hususan wa kike, kwa kuhofia kwamba ukarimu na msaada wao usije kuwaingiza matatizoni kwa tuhuma za child molestation.

Nadhani kufikia hapa unajiuliza naelekea wapi! Well, nataka kuzungumzia namna mamlaka zetu zinavyowadekeza mafisadi, lakini nataka kwanza nikupe mifano ya kuiweka akili yako vema kabla hatujaivaa hoja ya ufisadi.Twende kwenye mfano mwingine. Katika miaka ya hivi karibuni baadhi ya watu wanaoporwa na vibaka wameishia kupata vipigo kutoka kwa raia baada ya washirika wa kibaka aliyepora kupiga ukelele wa “mwiz,mwizi...” dhidi ya aliyeporwa.Na kama kanuni za mob justice zilivyozoeleka,hakuna muda wa kuhakiki iwapo aliyepigiwa ukelele ni kibaka halisi au victim.

Back to hoja kuhusu mafisadi. Inaelekea mamlaka husika huko nyumbani zimeamua kuwalinda mafisadi mithili jamii za Magharibi zinavyowalinda watoto dhidi ya suspected/potential/career child molesters.Na anayediriki kupiga kelele dhidi ya mafisadi anakumbana na yaleyale ya anayeporwa na kibaka na kisha kupigiwa ukelele wa “mwizi,mwizi...” na washirika wa kibaka mhusika, na kuishia kupewa kipigo cha haja katika mtindo wa mob justice.

Wachunga kondoo wa Bwana walipobaini kwamba kondoo wao wanakamuliwa hadi damu baada ya maziwa kumalizika miilini mwao wakaamua kuja na kinachoitwa roughly muongozo wa kanisa kuhusu elimu ya uraia hususan uchaguzi wa viongozi. Tuliyekuwa tukimwamini kuwa swahiba wa karibu wa Baba wa Taifa, Kingunge Ngombale Mwiru,akatuthibitishia his true colours kwa kuwakemea wachunga kondoo wa Bwana.Hata kama Kingunge aliasi Nyumba ya Bwana (tukiaminishwa kuwa ni matokeo ya kuamini Ujamaa kupitiliza hadi kuufanya kuwa dini yake) tunapaswa kumshangaa babu huyu ambaye hivi karibuni ameibuka kuwa mtetezi mahiri wa mafisadi. Gazeti la Taifa Letu limemnukuu mtumishi mmoja wa Mungu akim-describe Kingunge kama BABA WA TAIFA WA MAFISADI.

Walioliibia taifa kwa kununua mgodi wa Kiwira kwa bei ya kutupa kana kwamba wanachonunua ni kifusi wameishia sio tu kusafishwa bali kufidiwa kwa wizi wao. This is more than crazy! Yaani tunawafidia majambazi!?Tunalipeleka wapi taifa letu? Wakati hatujui hizo milioni kadhaa walizotumia kununulia mgodi huo walizitoa wapi (lakini kwa vile hawakuwa wafanyabiashara basi yayumkinika kuhisi ni fedha za kifisadi),tuna uhakika wa asilimia zaidi ya 1000 kwamba hayo mabilioni watakayolipwa kama “fidia za kutufisadi” ni fedha zangu, zako na zetu walalahoi,walalawima,walala kichwa-chini miguu-juu, na wanyonge wengineo.

Kinachosikitisha ni kwamba kuna waungwana wanalipwa mishahara minono kuzuia upuuzi wa namna hii lakini badala ya kutumia nguvu za kikatiba walizonazo kustopisha ujambazi wa aina hii, wanakuwa bize zaidi na wale wanaowasaidia (waungwana hao) kupiga kelele dhidi ya ufisadi na mafisadi. Kama hufahamu basi naomba nikujulishe kwamba shughuli ya hatari kabisa kwa Mtanzania ni kudiriki kukemea ufisadi.Utaandamwa,utatishwa,utafanywa ujione mhaini,na kufanyiwa kila anachopaswa kufanyiwa Osama bin Laden pindi akikamatwa!Na shughuli yenye uhakika wa kipato, heshima na ulinzi kuliko zote ni ufisadi. Correct me if I’m wrong!

Siku zote nimekuwa nafahamu kwamba kimbelembele changu (according to how those in the know describe it) dhidi ya mafisadi ni kujiingiza kwenye kundi la dead men walking. I know, you’re thinking I’m scared of my own shadow. Kwa vile hapa si mahala mwafaka kutoa ushuhuda wangu, then ni bora tuliache hilo kwa sasa. Hata hivyo, naamini kwa nguvu zote kwamba ukimya sio suluhisho la matatizo yetu. Silence is not an option at all.

Kinachonisikitisha zaidi ni namna baadhi ya wenzetu wenye nguvu, uwezo na sababu wanapokosa nia au ujasiri wa kuendeleza kelele hizi. Inasikitisha zaidi unapoona wasomi wenye uwezo mkubwa wa uchambuzi wanageuka vibaraka wa kusifia pasipo kugeuza upande wa pili wa shilingi kukemea mwenendo tete wa taifa letu.Hate me or love me, ninachofanya ni kinachopaswa kufanywa na kila Mtanzania mwenye uchungu wa dhati wa taifa letu, na anayefahamu kwamba it’s no use crying over spilled milk. Imani kwamba “hata tukipiga kelele hatuwezi kubadili kitu” ni hatari sana kwa vile japo Ukimwi umekuwepo kwa miongo kadhaa sasa bado jamii inaendelea kuhamasisha vita dhidi ya gonjwa hilo hatari.

Kinachopaswa kuwaamsha wanaochelewa kujiunga kwenye mapambano dhidi ya ufisadi ni ukweli ufuatao.Katika utafiti wangu wa kitaaluma unaoelekea ukiongoni,kuna ushahidi wa kutosha unaoonyesha kwamba vurugu za kidini (utafiti wangu unahusu dini) na nyinginezo katika jamii zinachangiwa sana na jamii kukatishwa tamaa na mwenendo wa watawala kushughulikia matatizo yanayozikabili jamii hizo.Na kwa vile watawala wa aina hiyo hufanya kila wawezalo kuzuia “sauti zisizopendeza masikioni mwao”,kimbilio pekee hubaki kwa nyumba za ibada na dini kwa ujumla.

Tatizo ni kwamba masuala ya dini yanaelemea zaidi kwenye hisia kuliko reasoning. Sote tunafahamu, kwa mfano, kuwa piga ua huwezi ku-reason na Mkatoliki kuhusu ishu “ngumu kuelezeka” kama Utatu Mtakatifu, namna Bikira Maria alivyomzaa Yesu pasipo “kukutana” na Josefu, na maswali mengine kama hayo.Na katika masuala ya dini, ambapo mara nyingi emotions tend to come in front of common sense, hakuna taratibu kama za jeshini kwamba amri ya jenerali lazima iheshimiwe na brigedia, au ya kanali iheshimiwe na meja, au ya kapteni kwa lance corporal. Kwenye dini, kauli ya askofu au shehe haina nguvu sana katika kutuliza hamasa za waumini pindi wanapoamua kupambana na mamlaka za kidunia kwa jina la Mungu.

Kinachoniogopesha zaidi ni vuguvugu linaloendelea huko nyumbani ambapo ishu kama ahadi hewa za CCM kuanzisha mahakama ya kadhi,mwongozo wa Kanisa kuhusu uchuguzi wa viongozi waadilifu,mwendelezo wa madai kuwa Wakristo wanapendelewa na Waislam wanaonewa,nk zimetawala anga za habari. Kibaya zaidi, hayo yanatokea katika kipindi ambacho mafisadi wako tayari kufanya lolote alimradi wafanikiwe kuendelea kutufisadi. Yayumkinika kuamini kwamba hawawezi kusita kutumia fursa hii ya “kuwachanganya Watanzania” kwa misingi ya dini na hivyo ku-deflect attention yao (Watanzania) kuhusu ufisadi na mafisadi kwa vile watakuwa bize zaidi kunyoosheana vidole kwa misingi ya udini.

Tukiunyamazia ufisadi, utatumaliza!

It can be done if you play your part.

It’s now or never!

28 Jul 2009

Picha kwa Hisani ya MJENGWA.Uchambuzi zaidi kesho,panapo majaliwa.

23 Jul 2009







Hiyo sio sanamu,bali "msanii" mmoja ambaye kila wikiendi anavizia mtaa ulio bize na "kuganda kama sanamu" kisha kutoa vijishara vya kuvunja mbavu.Hulazimishwi kutoa asante bali "mchango wako utathaminiwa".Ni mchanganyiko wa ubunifu na "usanii" (i.e. ujanja-ujanja wa kuishi mjini)

Huyu nae ni mtaalam wa cover versions,or sort of off.Ukiskia muziki wake pasipo kumtia machoni unaweza kudhani The Killers,Coldplay,au rockers flani wanafanya concert mtaani minus makelele ya kawaida ya rock stars.Kipaji?Usanii? Well,katika zama hizi za recession,credit crunch na vitu kama hivyo,si serikali na taasisi za fedha pekee zinazohitaji kuwa na mikakati ya kujinusuru.Nahisi "wasanii" hawa wanatumia vipaji-au ujanja ujanja-kukabiliana na hali hiyo.At the end of the day,kinacho-matter ni kono kwenda kinywani.

22 Jul 2009



Riot police have broken up a tense standoff between black and white protesters in a town in Texas.


The conflict began with a march by 100 mostly African-American activists, who were unhappy at the state̢۪s handling of the case of 24-year-old Brandon McClelland who was run over and killed by a vehicle.

Speaking to US television network ABC, Brandon's mother Jacquiline said: "The reason for today's rally is to let everybody know how the justice system around here is really doing things."
When the protesters reached the town square, the crowd of black demonstrators ballooned to around 200 people on one side of the street.

Approximately a dozen white supremacists, including four skinheads carrying Nazi swastika flags, gathered on the other side.

A skinhead and another white man were arrested on suspicion of disorderly conduct, before the protesters separated peacefully.

No blows were exchanged.


SOURCE: Yahoo! News

15 Jul 2009


na Charles Mullinda

IMEBAINIKA kuwa, Ofisi ya Bunge imetumia vibaya mamilioni ya shilingi yaliyotolewa na serikali kwa ajili ya uendeshaji wa ofisi hiyo katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2007/2008.

Hayo yamebainishwa na baadhi ya wabunge wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) katika mahojiano yao na Tanzania Daima Jumatano yaliyofanyika wiki iliyopita mjini Dodoma kwa wakati tofauti.

Wakizungumza kwa sharti la majina yao kutoandikwa gazetini, kwa kile walichoeleza kuwa ni kuogopa kuandamwa na baadhi ya wabunge wenzao, walisema ushahidi wa maelezo yao umo katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CGA) ya mwaka wa fedha wa 2007/2008.

Mmoja wa wabunge hao alieleza kuwa licha ya ripoti ya CGA kubainisha matumizi mabaya ya mamilioni ya fedha katika Ofisi ya Bunge, Mwenyekiti wa PAC, John Cheyo, alizuia kujadiliwa kwa ripoti hiyo baada ya kushauriana na baadhi ya vigogo wa Ofisi ya Bunge, jambo ambalo linazuia kuchukuliwa hatua zozote za kisheria au kurekebisha hali hiyo hadi sasa.

Alisema Ofisi ya Bunge imekuwa ikifanya jitihada za makusudi kuhakikisha ripoti hiyo haijadiliwi na PAC, kwa hofu kwamba inaweza kusababisha baadhi ya watendaji kuwajibishwa na baadhi ya wanasiasa kuchafuka majina yao.

Cheyo, Mwenyekiti wa PAC na Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP), alipoulizwa na gazeti hili kuhusu madai hayo, alisema ni kweli ripoti ya CAG kuhusu matumizi ya fedha za serikali katika Ofisi ya Bunge si nzuri, kwa sababu inaonyesha upungufu mkubwa wa urejeshaji masufuru pamoja na matumuzi mengine mabaya ya fedha za ofisi hiyo.

Hata hivyo, alikana kuikalia ripoti hiyo kwa namna yoyote na kueleza kuwa, aliamua kuiweka pembeni baada ya kushauriana na kukubaliana na wajumbe wote wa kamati hiyo kuwa hawawezi kuijadili, kwa sababu walishindwa kumhoji Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, ambaye wakati kamati hiyo akikutana kujadili ripoti mbalimbali za CGA kuhusu hesabu za taasisi za serikali, alikuwa hajaapishwa na rais kushika wadhifa huo.

“Ni kweli ripoti ya CAG kuhusu matumuzi ya fedha katika Ofisi ya Bunge si nzuri, inaonyesha upungufu mkubwa katika urejeshaji wa masurufu, na ripoti zote ambazo zinaonyesha hivyo kihasibu huwa ni mbaya. Sasa kwa Spika hii si nzuri, inamtia doa, anaweza asiaminike tena iwapo itawekwa wazi, kwa sababu ataonekana hafanani na kauli zake.

“Siyasemi haya kwa sababu nina kisasi na Spika, bali ni kwa sababu umeniuliza. Unajua Spika amenijeruhi hivi karibuni, sasa sitaki nionekana kama ninalipa kisasi. Lakini ukweli unabaki pale pale kwa sababu umeandikwa vitabuni kuwa kuna kasoro katika Ofisi ya Bunge ambayo inasimamiwa na Spika,” alisema Cheyo.

Spika Sitta alipoulizwa kuhusu kauli hiyo ya Cheyo, alisema hahusiki kwa namna yoyote na uchukuaji wa masurufu, hivyo hapaswi kunyooshewa kidole iwapo imebainika kuwapo kwa kasoro zozote za matumuzi mabaya ya fedha za serikali katika ofisi yake.

Spika alisema taratibu ziko wazi kuwa wanaochukua masufuru kwa ajili yake ni wasaidizi wake wanaohusika kumuandalia safari zake zote, ndani na nje ya nchi.

“Mimi sihusiki kuchukua masurufu, wanaohusika ni wasaidizi wangu, sasa kama kuna kasoro, wao ndio wanajua. Nina ofisi yangu binafsi kama viongozi wengine wakuu wa kitaifa, sitembei na fedha mfukoni, wasaidizi wangu wa ofisi hiyo ndio wanaoniandalia safari na ziara zangu zote. Wao ndio wanaonilipia kila kitu, walinzi, maradhi, kila kitu, ndio wanaochukua fedha za masurufu kwa niaba yangu,” alisema Spika Sitta.

Alipoulizwa kuhusu madai kuwa alitumia fedha nyingi za Ofisi ya Bunge kugharamia vikao na tafrija zilizokuwa zikifanyikia nyumbani kwake wakati mkewe, Margaret Sitta, ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, akiwania nafasi ya kuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC), alisema madai hayo inabidi yafafanuliwe.

“Ninachokijua mimi kuhusu hili, ni kweli kulikuwa na vitu vya aina hiyo wakati huo, lakini ninachokumbuka ni kwamba gharama nyingi za mikusanyiko hiyo nilikuwa ninatumia fedha zangu za mfukoni, nilikuwa nalipa mwenyewe. Lakini hili ili nilielewe vizuri, inabidi lifafanuliwe,” alisema.

Naye Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah alipoulizwa kuhusu hali hiyo, alisema hawezi kuzungumza jambo hilo, kwa sababu alipoingia katika wadhifa huo alikuta hali hiyo imeshatokea.

Alibainisha kuwa ni kweli hakuhojiwa na Kamati ya PAC kwa sababu alikuwa hajaapishwa na rais, lakini kwa sasa kamati hiyo inaweza kuendelea na kazi zake kama kawaida, bila kupata kipingamizi kutoka kwa mtu yeyote.

“Mimi nilipoingia katika ofisi hii, hali hiyo niliikuta, hivyo siwezi kusema kitu, kwa sababu sikuwapo, siwezi kuizungumzia. Ninachoweza kukitolea maelezo ni kile ambacho kimefanyika wakati wa kipindi changu.

“Lakini suala la ripoti hiyo kukaliwa halipo, PAC ikitaka kukaa kuijadili hata kesho ni sawa tu, hakuna tatizo, waje wakae, wao wana ratiba zao za vikao, kuna ripoti nyingi tu hazijajadiliwa, hizi hazijakaliwa, naomba kwa sababu linahusu Ofisi ya Spika, isichukuliwe kuwa linazimwa,” alisema Dk. Kashililah.

Ripoti ya CAG, ambayo Tanzania Daima Jumatano imeiona, katika ukurasa wake wa 43, fungu la 42, inaitaja Ofisi ya Bunge katika orodha ya taasisi za serikali zilizopewa hati zenye shaka, kwa kukiuka taratibu za kihasibu.

Ripoti hiyo inabainisha kuwa Ofisi ya Bunge ilifanya malipo ya matibabu nje ya nchi ya zaidi ya sh milioni 101 bila kuidhinishwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, uhamisho wa fedha wa zaidi ya sh milioni 63 kutoka kifungu kimoja kwenda kingine bila kibali na malipo yenye thamani ya sh milioni 7.8 yalifanyika bila kibali.

Upungufu mwingine uliotajwa katika ripoti hiyo ni malipo yenye nyaraka pungufu ya sh milioni 526, malipo yasiyo halali ya sh milioni 102.5, malipo yenye shaka ya sh milioni 63.9, mishahara isiyolipwa na ambayo haikurejeshwa Hazina sh milioni 17.1, sh milioni 3.4 za mishahara ya watumishi walioachishwa kazi inayoendelea kulipwa kwenye akaunti zao benki na usuluhisho wa tofauti ya sh milioni 1.1 kati ya bakaa ya benki na bakaa inayoonyeshwa katika daftari la mapato na matumizi haukufanyika.

Marekebisho yasiyostahili yaliyojumuishwa kwenye hundi ambazo hazijawasilishwa benki ni sh milioni tano, masurufu maalumu ya sh milioni 50.2


KINACHOKWAMISHA VITA DHIDI YA UFISADI NI HUU MTINDO WA KUENDESHA MAMBO KISHKAJI.UKITAFAKARI KAULI YA CHEYO KUHOFIA KUHUSISHA HABARI ZA UFISADI HUO NA HATUA YA SPIKA KUMTOA NJE YA BUNGE HIVI KARIBUNI UTAGUNDUA KUWA BADALA YA MBUNGE HUYO KUSHUGHULIKIA SUALA HILO KAMA MWENYEKITI WA KAMATI HUSIKA,YEYE ANAJIONA KAMA JOHN MOMOSE CHEYO ALIYETOLEWA NJE NA SAMUEL SITTA,BADALA YA OFISI YA BUNGE ILIYO CHINI YA SPIKA NA WATENDAJI KADHAA.

NA UNAFIKI MWINGINE NI WA HAO WABUNGE WALIONUKULIWA KATIKA HABARI HII AMBAYO HAWATAKI KUTAJWA MAJINA KISA WANAOGOPA KUANDAMWA NA WABUNGE WENZAO.KWANI WALIINGIZWA BUNGENI NA HAO WABUNGE WENZAO WANAOWAOGOPA AU WANANCHI HUKO MAJIMBONI?

WIZI MTUPU!


12 Jul 2009


Kizitto Noya na Habel Chidawali, Dodoma

WAZIRI wa Maliasili na Utalii Shamsa Mwangunga, amekiri kukithiri wizi wa nyara za serikali hasa pembe za ndovu na kueleza kuwa sio rahisi kudhibiti vitendo hivyo kwa kuwa vinafanywa na mtandao wa watu wenye fedha nyingi.

Mwangunga alisema hayo bungeni jana alipokuwa akihitimisha mjadala wa bajeti ya wizara yake mjini na kufafanua wizi wa makontena mawili ya pembe za ndovu yaliyokamatwa Machi, mwaka huu nchini Vietnam.

“Kukithiri kwa wizi huo kumetokana na Wizara ya Maliasili na Utalii kutohusishwa na ukaguzi wa mizigo bandarini na soko kubwa la nyara hizo liko katika nchi za Asia. Mtandao wa watu wenye fedha nyingi ndio unaendesha biashara hiyo kwa kushirikiana na maafisa wa bandari,” alisema Mwangunga.

“Ninasema maafisa wa bandari wanahusika kwa sababu bandarini ndiko kwenye lango la kupitisha nyara hizo na maafisa wake ni miongoni mwa watuhumiwa katika matukio hayo.”

Mwangunga alikuwa akijibu hoja ya mbunge wa Same Mashariki Anne Kilango Malecela ambaye juzi alitishia kutoa hoja binafsi kutaka iundwe Kamati teule ya Bunge kuchunguza wizi wa makontena hayo yaliyokamatwa Machi 25, mwaka huu nchini Vietnam.

Mbunge huyo alitaka kamati hiyo ichunguze jinsi makontena hayo yalivyopita kwenye bandari za hapa nchini baada ya kukaguliwa na mamlaka husika na kufika Vietnam bila kujulikana kuwa yalibeba pembe za ndovu.

"Mheshimiwa Spika, naomba nizungumzie kuhusu jambo ambalo kwa kweli limenisikitisha sana ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii ambao ni wizi wa nyara; wizi wa pembe za ndovu. Wizi huu Mheshimiwa Spika, unafanyika kama vile nchi yetu hakuna ulinzi," alilaumu Kilango na kuongeza:

"Nimefanya utafiti nina faili zima; Mheshimiwa Spika nilikwenda kufanya utafiti, baada ya kusoma kwenye magazeti kuhusu makontena mawili yaliyokamatwa Vietnam, nikaona nisiishie hapo niende ndani mpaka nipate faili zima.

"Nasikitika sana. Nilikwenda kuhoji; nikaelezwa; nikapewa na faili; nikasoma kontena zile mbili zilipitia bandari yetu kama kawaida".

Kilango aliomba atumie kanuni ya 117 ya Bunge kuwasilisha hoja binafsi kutaka iundwe kamati teule kwa ajili ya kuchunguza jambo hilo.

Hata hivyo, jana Spika wa Bunge Samuel Sitta ambaye juzi aliahidi kufanyia kazi suala hilo, alitupa hoja hiyo baada ya Kilango kushindwa kuwasilisha kusudio lake hilo kwa maandishi kwa wakati.

”Kulikuwa na hoja ya kuundwa kamati teule jana, lakini niseme kwamba, hoja hiyo sijaipata hapa kwa maandishi, nimwombe Katibu aendelee na shughuli za leo,” alisema Sitta muda mfupi kabla ya bunge kukaa kama kamati.

Kabla ya Sitta kusema hivyo, aliingia bungeni akikimbia akiwa ameshika bahasha ya kaki ambayo ilisemekana kuwa ilikuwa na hoja yake hiyo kimaandishi ambayo alitarajia kuiwasilisha.

”Naona kuna kitu kinataka kunifikia sijui kama ndio hiyo hoja, ah, lakini kwa mujibu wa kanuni za Bunge siwezi kuipokea hoja hiyo na kusema kweli itakuwa ndiyo basi, sitaipokea tena hivyo tunaendelea waheshimiwa,” alisema Sitta.

Akizungumza na gazeti hili katika viwanja vya Bunge jana, Kilango alisema alichelewesha kupeleka hoja yake baada ya awali kushauriwa na Spika kuwa suala hilo liachwe liendelee kushughulikiwa na Polisi wa Interpol chini ya makubaliano ya Lusaka (Lusaka Agreement).

”Mimi hoja nilishaandaa, lakini Spika alinishauri kuwa kwa vile suala hilo linashughulikiwa na Interpol, tuache kwanza.

Lakini hii haina maana kwamba, hoja imekufa. Nitaiibua tena wakati wowote baada ya interpol kumaliza kazi yake,” alisema.

Awali akizungumzia wizi huo Mwangunga alisema ulitokea Machi 25 mwaka huu na tayari watu tisa wamekamatwa na kuhojiwa.

”Kati yao, watu wanne wamefunguliwa kesi mahakamani mkoani Tanga,” alisema Mwangunga na kutaja majina ya watuhumiwa hao.

Alisema mbali na tukio hilo, kontena lingine lilikamatwa Machi Mosi, mwaka huu katika Bandari ya Manila Ufilipino ambako pembe za ndovu zenye uzito wa tani tano lilikamatwa.

Siku nne baadaye maafisa Forodha wa Vietnam walikamata kontena lingine namba ESU 1174 lililokuwa na tani 6.2 za pembe za ndovu.

Hata hivyo, Mwangunga alishindwa kusema pembe hizo za ndovu zilitoka wapi kama alivyotakiwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe.

Kabwe alitaka waziri huyo aeleze endapo shehena hiyo ni ndovu wanaoendelea kuuawa au zimekwapuliwa kutoka kwenye ghala la serikali.

”Siwezi kusema kuwa zilitoka wapi kwani katika ghala za serikali hakuna wizi uliotokea na namna zilivyopangwa na kama ingechukuliwa hata moja ni rahisi sana kujua, hivyo inawezekana zilitoka katika maeneo yetu au hata nchi jirani waliamua kusafirisha kwa kupitia bandari zetu kutokana na udhaifu uliopo katika bandari za hapa nchini,” alisema Mwangunga.

CHANZO: Mwananchi

INA MAANA WIZARA INGEWEZA KUWADHIBITI MAFISADI HAO LAITI MTANDAO WAO UNGEKUWA NA FEDHA KIDOGO AU HOHEHAHE?HII WIZARA IMEKUWA KICHAKA CHA MAFISADI MIAKA NENDA MIAKA RUDI.BY THE WAY,KAMA MAFISADI WANAWEZA KUTUIBIA BENKI KUU (THRU EPA,etc) AMBAPO KUNA ULINZI WA HALI YA JUU,TUTEGEMEE NINI HUKO MBUNGANI?TUTAJUA MENGI PINDI IKIFANYIKA "SENSA" YA RASLIMALI ZETU HUKO MBUGANI.HOPEFULLY,BY THEN MAFISADI HAWA HAWATAKUWA WAMEKOMBA KILA KITU!


<

11 Jul 2009


Pamoja na sifa zake nyingi ikiwa ni pamoja na kuwa jiji la tatu kwa ukubwa (kwa idadi ya watu idadi ya watu,nyuma ya London na Birmingham) hapa UK,Glasgow,unabeba historia ya "Simba na Yanga" za Scotland,yaani klabu mbili za soka zenye upinzani wa kupindukia:Glasgow Rangers (almaaruf RANGERS) na Celtic.Tofauti na upinzani wa Simba na Yanga,au Manchester City na Manchester United,au kwingineko kwenye "mafahali wawili wanaopigania ubabe kwenye mji mmoja",upinzani kati ya Celtic na Rangers umevuka mipaka ya soka.Wakati Celtic ni,generally speaking,Wakatoliki,Rangers ni Waanglikana.Zamani hizi,ilikuwa jambo lisilowezekana kabisa kwa mchezaji Mkatoliki kusajiliwa na Rangers,au Muanglikana kusajiliwa na Celtic.

Sasa,moja ya tahadhari wanazopewa wageni katika jiji la Glasgow ni rangi za timu hizo mbili.Ukirogwa kuvaa "jezi" za Rangers kwenye maeneo ya wapenzi wa Celtic,au kutinga rangi za Celtic kwenye maeneo ya kujidai ya Rangers,tarajia yasiyotarajiwa.






In his first visit to Africa since taking office, Barack Obama said today that the continent of his ancestors must overcome tyranny and corruption if it is to flourish.

Speaking in Ghana's parliament, Obama said the key to Africa's future prosperity was democratic and accountable government.

"Development depends upon good governance. That is the ingredient which has been missing in far too many places, for far too long. That is the change that can unlock Africa's potential," he said.

In an tough speech aimed at politicians across the continent, he gave an unsentimental account of squandered opportunities since the end of colonial rule. "No country is going to create wealth if its leaders exploit the economy to enrich themselves, or police can be bought off by drug traffickers," he said.

"No business wants to invest in a place where the government skims 20% off the top ... No person wants to live in a society where the rule of law gives way to the rule of brutality and bribery. That is not democracy, that is tyranny, and now is the time for it to end.

"Africa doesn't need strongmen, it needs strong institutions."

Obama conceded that colonialism had left a legacy of conflicts and arbitrary borders. "But the west is not to blame for the destruction of the Zimbabwean economy over the last decade, or wars in which children are enlisted as combatants.

"Africa is not the crude caricature of a continent at war," he said. "But for far too many Africans conflict is a part of life, as constant as the sun. There are wars over land and wars over resources. And it is still far too easy for those without conscience to manipulate whole communities into fighting among faiths and tribes."

Earlier, after meeting Ghana's president, John Atta Mills, Obama praised the country's record of democracy and economic growth as a rare success in a continent beset by corruption and poor governance.

"We think that Ghana can be an extraordinary model for success throughout the continent."

This morning, Obama was given a hero's welcome in the country's capital, Accra. Thousands of people wearing Obama T-shirts thronged the streets, cheering and waving as his motorcade swept past.

Walls and utility poles were plastered with posters of Obama and Mills, as well as the word "change" – the mantra of Obama's presidential election campaign. Other posters showed the president and his wife, Michelle, with the greeting "Ghana loves you".

Obama and his family arrived late last night from the G8 summit in Italy, where the world's richest nations agreed on a $20bn (£12.4bn) food security plan to help poor nations feed themselves during the global recession.

Speaking in Italy before he left, Obama said: "There is no reason why Africa cannot be self-sufficient when it comes to food."


The Obamas will visit Gold Coast Castle, a former British slave trading post. Michelle Obama is a great-great granddaughter of slaves.

The visit comes as the US plans a much more assertive policy in Africa, using both diplomacy and the threat of force to end the protracted conflicts in Democratic Republic of the Congo and Nigeria, which are seen as two of the main obstacles to the continent's progress.

"This is both a special and an important visit for him personally as president, but also for our country to articulate a vision for Africa," said Robert Gibbs, the White House spokesman.

Despite the enthusiastic reception from ordinary Ghanians, no major public events have been planned during Obama's 21-hour visit, for fear it could cause a celebratory stampede, as almost happened during a 1998 stop by Bill Clinton.


SOURCE: The Guardian

10 Jul 2009

Rais Barack Obama anaonekana kama "analipiga jicho" bunda (makalio) la binti wa Kibrazili,Mayara Tavarez,huku Rais Nicholas Sarkozy akishika tama!Yes,He can!


9 Jul 2009


A British diplomat in Russia, James Hudson, has quit after being filmed having sex with two blonde prostitutes.Hudson, 37, resigned from his posting to the Urals over the video, which is thought to have been secretly shot by Russian spies.

The footage apparently shows Mr Hudson, wearing a dressing gown, kissing the two semi-naked girls while drinking champagne in a brothel
...CONTINUES



8 Jul 2009


Neo-Nazis are plotting a 'spectacular' terrorist attack on Britain to fuel racial tension, Scotland Yard's counter-terrorism officers fear.

Senior officers have increased their surveillance of suspects to monitor their ability to carry out a deadly attack aimed at causing a 'breakdown in community cohesion'.

The chilling warning comes after last month's startling gains by the BNP in the local and European elections which many fear may 'embolden' violent Far-Right extremists.

Commander Shaun Sawyer, from the Met's specialist operations wing told a meeting of British Muslims last night: 'I fear that they will have a spectacular ...

'They will carry out an attack that will lead to a loss of life or injury to a community somewhere. They're not choosy about which community.'

His comments came after Commissioner Sir Paul Stephenson asked officers to examine what effect the recession could have on far-right violence.

And the news mirrors similar warnings of the threat from far-right sympathisers issued in America in recent months.

While countering a threat from Islamic extremists remains the priority many officers now believe that funds need to be funnelled towards preventing a possible strike by the Far-Right.

Threat level in the UK may be downgraded, says terror chief

Despite the warning, Assistant Commissioner John Yates today warned that counter terrorism police face budget cuts.

He admitted savings must be made in two years time despite the risks posed by the looming London 2012 Olympic Games.

The senior officer, who took control of Scotland Yard's specialist operations wing three months ago, said it would be "naive" to think counter terrorism work would escape the recession.

Last weekend it was revealed that a network of suspected extremists with access to 300 weapons and 80 bombs has been uncovered by counter- terrorism detectives.

Thirty-two people were questioned by police and 22 properties were raided over an alleged plot to bomb mosques.

It was the biggest terrorist arms haul since the IRA mainland bombings in the 1990s.

Sir Norman Bettison, the chief constable of West Yorkshire, said: 'The big bad wolf is still the Al-Qaeda threat.

'But my people are knocking over right-wing extremists quite regularly. We are interdicting it so that it doesn't first emerge into the public eye out of a critical incident like an explosion.'

It is more than 10 years since neo-Nazi nail bomber David Copeland attacked three targets in London in 1999.

Three people died at the Admiral Duncan gay pub in Soho.

Copeland also targeted the Muslim community in Brick Lane, east London, and a supermarket in Brixton, south London.

Abdurahman Jafar of the Muslim Safety Forum, where the concerns were raised, said:

'Muslims are the first line of victims in the extreme right's campaign of hate and division and they make no secret about that.

'Statistics show a strong correlation between the rise of racist and Islamophobic hate crime and the ascendancy of the BNP.'

Mark Gardner, of the Community Security Trust, which monitors violence against Jews, said there has been a surge in right-wing incidents.

He said: 'Ten years after the Nazi nail bombings in London, we are seeing increasing numbers of neo-Nazis being arrested in their attempts to start some kind of so-called race war.

'It is the Muslim community that appears to be most targeted, but all of society is at risk, and we are in regular discussion with police about the problem.

'Worse still, the recent electoral successes for the BNP may cause some would-be terrorists to be further emboldened in their actions.'

Last year neo-Nazi Martyn Gilleard, 31, was convicted of three terrorism offences and jailed for 16 years.

Gilleard idolised Adolf Hitler and urged sympathisers to act to preserve the 'purity of the white race'.

When police raided his flat they found bullets, swords, knives and four nail bombs under a bed used by his five-year-old child.

Officers also found DIY bomb manuals, a guide on making a sub-machine gun and internet instructions on carrying out assassinations by poison.

A speech he had recorded in a notebook mentioned 'killing Muslims, blowing up mosques and fighting back'.

No one at the Muslim Safety Forum was available for comment. The Metropolitan Police declined to comment.

Last month a white supremacist with links to the BNP shot dead a security guard at Washington's Holocaust Museum in a racially-motivated killing.

Before launching the attack, 88-year-old James von Brunn sent out an email claiming: 'It's time to kill all the Jews.'

Von Brunn was shot and wounded by museum security officers after he walked into the packed tourist attraction and began firing indiscriminately.

4 Jul 2009



KWANZA Merged

Picha kwa hisani ya KENNEDY

Wanasema siasa ni mchazo mchafu.Lakini siasa katika bara letu la Afrika ni zaidi ya mchezo mchafu.Ni mchanganyiko wa kanyaboya,songombingo,mbinde,usanii,ufisadi na what have you.Hiyo sio kumaanisha kuwa siasa katika maeneo mengine,kama Ulaya na kwingineko ni safi kihivyo.Lakini angalau hawa wenzetu check-and-balance mechanism zinafanya kazi kwa kiasi kikubwa.Sie tunazo lakini aidha wenye majukumu ya kuzitumia wako bize sana na posho au nyumba ndogo au hawajui kwa nini wapo mahala panapopaswa kufanya hiyo check na balance.

Hivi CCM walikuwa wanafikiri nini mwaka 2005 kuahidi kuwa wangeshughulikia uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi?Binafsi sina tatizo na uanzishwaji wa mahakama hiyo as long as suala hilo linafanywa kwa uangalifu.Sio priority kwa sasa lakini kwa vile ni haki kwa Waislamu,then hakuna budi kuangalia uwezekano huo.Kwahiyo,CCM hawakufanya kosa "kukubali" kuanzisha Mahakama ya aina hiyo baada ya uchaguzi mkuu wa 2005.Hawakufanya kosa kwa vile wazo hilo sio baya au la hatari kama baadhi ya watu wanavyofikiria.Nitatafuta wasaa mwafaka siku nyingine kuelezea kwanini Waislam wako sahihi kudai mahakama hiyo na kwanini uanzishwaji wake hauna madhara kwa wasio waislam.In fact,suala sio "kuanzisha" bali "kurejesha" kwa vile mahakama za aina hiyo zilikuwepo wakati wa ukoloni na muda mfupi baada ya uhuru.

Kosa la jinai (yes,ni jinai) la CCM ni kutoa ahadi nyeti kama hiyo wakati inafahamu fika kwamba haina muda wa kuishughulikia.Ni kosa pia kwa vile pamoja na ahadi hiyo ya kuanzisha mahakama ya kadhi tayari chama hicho kilikuwa kimeshatoa ahadi nyingine lukuki kana kwamba kinaomba kutawala kwa miaka 100 na sio mitano (2005-2010)!Kulikuwa na ahadi za kuwakalia kooni wala rushwa,kushughulikia kero za Muungano,kuboresha maisha ya Watanzania,na ahadi nyingine kedekede.Si tu kwamba wakati tunaelekea mwishoni mwa miaka hiyo mitano rushwa imeshamiri na ku-mutate into ufisadi (kumbuka,neno hili limejitokeza katika kipindi hiki),kero za Muungano sio tu kuwa bado zipo ila tumeshuhudia "kibiriti kikitikiswa mpaka kinataka kulipuka",na hayo maisha bora kwa kila Mtanzania sanasana yamewezekana kwa mafisadi na washirika zao....

Hili la kuahidi kushughulikia masuala yanayogusa imani (ya kiroho) ilhali hakuna dhamira au uwezo wa kufanya hivyo ni jambo hatari mno.Dini ni hatari zaidi ya ukabila kwani inahusisha uhai na kifo (mtu akifa kwa ajili ya dini ni martyr,at least dini nyingi zinaamini hivyo).

Kauli za viongozi kuhusu suala hili sio tu zimekuwa za kujichanganya bali zimechangia kukuza tatizo hilo.Mara mchakato unaendelea,mara sheria za kiislam zitaingizwa kwenye sheria za mahakama za sasa (hicho tayari kinafanyika),mara hili,mara lile.Kama kawaida,wahusika wanasubiri lilipuke ndio watafute chanzo cha mlipuko.Unfortunately,milipuko mingine ikianza hata huo muda wa kutafuta chanzo hautokuwepo.Waulize Nigeria!

Tuiombee nchi yetu.












Michael Jackson mithili ya chura!?The Jacko mithili ya Bikira Maria!?Ukishangaa yanayohusu maisha na kifo cha the King of Pop basi hujakutana na "kazi za sanaa" zinazomhusu the Jacko.Picha za juu ni baadhi tu ya "kazi" hizo.Unajua,fani yenyewe ya sanaa imetawaliwa na ujanja ujanja wa namna flani.Kwa mfano nenda maeneo ya Msasani kwa wauza vinyago wa Kimakonde.Utakutana na kinyago cha Nyerere,kwa mfano,lakini zaidi ya ukweli kuwa kinyago hicho ni cha mpingo (kama alivyodai mchonga kinyago),the rest havifanani kabisa na Nyerere,unless uwe hujawahi kuona sura ya Baba wa Taifa.Pita pita mitaani,utakutana na wasanii wanaodai wanaweza kukuchora na wakikamilisha mchoro utadhani unajiangalia kwenye kioo.Of course,wapo wenye vipaji vya namna hiyo.Lakini kuna " wasanii" pia.Atakuchora,kisha akikupatia "picha yako" unaweza kuishia kutamani kumkaba loba (kabali) ya mbao!

Na kifo cha Michael kinaelekea kuwa dili la nguvu kwa WASANII kwa maana ya ARTISTS na WASANII kwa maana ya CONFIDENCE ARTISTS (con artists).Ama kweli kufa kufaana!



3 Jul 2009


Mufti Simba aagiza Waislamu waikatae CCM

Mufti Issa bin Shaaban Simba, amekasilishwa na uamuzi wa serikali kuhusu Mahakama ya Kadhi.

Na Ummy Muya

BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) limesema kutokana na serikali kutupilia mbali ombi la kunzisha Mahakama ya Kadhi, Waislamu hawataipigia kura CCM katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

Katika taarifa yake, Bakwata ilifikia hatua ya kusema Waislamu wasimchague Rais Jakaya Kikwete iwapo atasimamishwa na CCM kugombea urais, ikiwa ni pamoja na wabunge na madiwani watakaosimamishwa na chama hicho tawala kutokana na kitendo cha serikali kutupilia mbali hoja ya Mahakama ya Kadhi.

Kauli hiyo imetolewa jana wakati Mufti Issa bin Shaaban Simba alipokuwa akitoa tamko kupinga uamuzi wa serikali kutaka kutumia sheria za dini ya Kiislamu katika mahakama za kawaida badala ya kuanzisha Mahakama ya Kadhi, kitu ambacho alisema anaamini kitawanyima haki Waislamu.

Alisema serikali imedhihirisha kuwa inaendeshwa na Wakristo na si kweli kama serikali haina dini na akamtaka Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe kubatilisha kauli hiyo kwa kuwa inamchafua Rais Jakaya Kikwete mbele ya umma wa Waislamu.

Waziri ametuthibitishia kama Rais Kikwete alikuwa akitulaghai ili tumpigie kura kwa kigezo kuwa suala hilo litashughulikiwa na kupatiwa ufumbuzi na sio kuchanganywa kama ilivyokuwa mwaka 1970 katika Sheria ya Ndoa na kuwanyima haki Waislamu,alisema.

Alisema kwa muda mrefu sana Waislamu wamekuwa kimya wakitumia hekima na busara kudai haki zao, lakini katika hatua hii ambayo serikali imefikia hawapo tayari kuendelea kudhalilishwa na kuwa kitendo hicho ni dhalimu.

Mufti alisema wamekuwa wakiiomba Mahakama ya Kadhi kwa zaidi ya miaka 20 na hivyo hawezi kuendelea kuwa kimya na kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa kwa kuwa mahakama hiyo ni haki yao.

Alisema kauli ya Waziri Chikawe imedhihirisha kuwa serikali ina wenyewe na Waislamu wamewekwa katika tabaka la pili pamoja na Rais Jakaya Kikwete kuwatuliza kwa ahadi kuwa watalipatia ufumbuzi suala hilo.

Natoa wito kwa Masheikh wote nchini na Waislamu wa madhehebu yote kupinga vikali kauli iliyotolewa na Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe na kwamba Waislamu waige mfano wa Waislamu wa Afrika Kusini,alisema Mufti na kuhoji:

Kwa nini iwe Afrika ya Kusini na isiwe Zanzibar, Uganda na Kenya ambazo zipo ndani ya Afrika Mashariki? Kwa niaba ya Waislamu nasema serikali haikututendea haki na imetuchukiza sana,alisema.

Alisema lengo la kuomba mahakama hiyo ni kuhakikisha Waislamu wanashughulikia masuala yao ya ndoa na mirathi na si vinginevyo, hivyo waziri asipotoshe jamii kwa kutumia mifano ambayo haiko sahihi.

Mahakama hii haitawakata wezi mikono kwa kuwa nchi hii ina katiba na sheria na sisi tutazirudisha kesi zote za jinai mikononi mwa serikali. Sifahamu hiyo kamati ambayo waziri alisema alikuwa amekaa na kutoa tamko hilo ilikuwa na watu gani,alihoji.

Aliongeza kuwa kutokana na mapungufu hayo waziri arudi tena na kukutana na masheikh ili apate muongozo wa nini Waislamu wanahitaji na sio kuzungumza bila kuwa na usahihi wa kile anachosema.

Wakizungumza na waandishi wa habari baada ya tamko la Bakwata, masheikh walikuwa na mitazamo tofauti. Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Salum Mussa alisema wapo baadhi ya Waislamu ambao watakubali kutokana na ufinyu wao wa elimu ya dini.

Mussa alisema haoni sababu ya serikali kufanya njia ya mkato katika suala hilo kwani Waislamu wanahitaji Mahakama ya Kadhi kama ilivyo kwa wafanyabiashara ambao wana mahakama yao.

Hukumu inayotolewa katika Mahakama ya Kadhi ni ibada kwa mujibu wa mafundisho ya Mtume Muhammad (S.A.W) hivyo ni lazima kwa atakayetoa hukumu hiyo awe Muislamu na si vinginevyo,alisema.

Namshanga waziri anapotaka sheria hizi zitumiwe katika mahakama za kawaida. Aliona wapi John akawa imamu,alihoji sheikh huyo wa mkoa wa Dar es Salaam.

Naye katibu wa Bakwata wilayani Ilala, Sheikh Issa Ausi alisema historia iko wazi. Waasisi na wanaharakati ambao waliitoa Tanganyika mikononi mwa wakoloni walikuwa Waislamu, na akahoji sababu za serikali kuwa mstari wa mbele kuwafunga midomo leo.

Bakwata imezinduka sasa Waislamu wote tumeungana katika kupigania haki zetu na kutetea maslahi yetu na serikali itambue kuwa Bakwata iko hai hao Wakristo walikuwa wapi wakati sisi tukipigania uhuru,alihoji.

Wakati huohuo, Sheikh Salum Rwambo alisema anawashangaa wabunge Waislamu ambao baadhi ni mahajat na malhaj wanakaa kimya na kushindwa kutetea hoja za msingi na kudai kuwa huo sasa ndio mwisho wao wa kuwaita masheikh na kutaka waombewe dua ili wasipate wepesi katika kampeni zao.

Sheikh Rwambo pia alimsifia mbunge wa Nzega Lucas Selelii kwamba ni miongoni mwa wabunge katika Bunge hilo wanaozungumza ukweli na kwa kujiamini tofauti na wengine ambao wanaenda kukaa bila kufanya kazi zilizowapeleka .


CHANZO: Mwananchi


KWA MWENENDO HUU SI AJABU KUSIKIA HATA WATANZANIA WALIOAHIDIWA MAISHA BORA NAO WAKAJITOKEZA KUDAI HAWAITAKI CCM....HOJA IKIWA MAISHA BORA YALIYOAHIDIWA YAMEISHIA KWA KUNDI DOGO LA MAFISADI PEKEE!



In a recent interview with MTV News, The Game relayed Michael Jackson’s attempts to end the beef between him and 50 Cent. Although the rappers eventually laid the feud to rest (without Jackson’s help) the tension between the two still remained.However, The Game has finally taken it upon himself to give a formal apology, not just to 50, but to the whole Interscope label.“For 50, I’m just gonna apologize to him, just as a man,” he told MTV. “It has nothing to do with music, or beef, or nothing like that. It ain’t about being the bigger man. He can take it and say, ‘Game is apologizing,’ ‘Game’s a sucka, he’s apologizing.’ I’m apologizing for me to him, to [Dr.] Dre, to Jimmy Iovine, to Eminem, to all the fans. Because if you think about what Interscope was when we were gellin’, man we were it. We were an unstoppable force.”

He explained that while he was a member of G-Unit, there were some things he needed to do “for my career to have longevity, and for me to survive in Hip Hop music,” and this may have played a part in the dissolving relationship between himself and 50 Cent. He also expressed some regret that G-Unit and the Interscope label did not get to experience the success that it could have had, potentially.

“Now, four albums in, I can say as a man that G-Unit, Game, Aftermath, Black Wall Street, Interscope, Geffen, Eminem, Shady, from [Lloyd] Banks to [Young] Buck to [Tony] Yayo to Dre to whoever; If it woulda kept going: endless paper. Millions of albums sold. Because we were great together.”

The Game also expressed his strong belief that, had he and G-Unit (and perhaps Young Buck) not parted ways, many things would have been different.

“Me and Fif’s chemistry is what Method Man was to Redman when they get in. Red ain’t from Wu-Tang but you know when Meth gets wit' Redman it’s goin’ down… [Me and 50’s] biggest records were together. Whether I was on them or I wasn’t on them. Whether he was on them or he wasn’t on them. When we were in gellin’ writing together as a family, we had it man. If we never would have [broken] up, I think Detox would have been out and we all would have been selling millions from Banks to Buck, and Tony Yayo. I’m going to apologize for my role.”

50 Cent and the Aftermath camp have not yet issued a response.

SOURCE: Hiphopdx.com


Jasusi ChatBot

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.