9 Oct 2010


Majuzi tumemsikia Mwenyekiti Mwenza wa REDET,Dokta Benson Bana akilipuka tena na utafiti wao wa kuchakachua kuhusu mwenendo wa uchaguzi,ambapo kwa mujibu wao wanadai mgombea wa CCM,Jakaya Kikwete anaongoza kwenye kura za maoni.

Huko nyuma nilishawahi kuandika post moja kuhusu Dokta Bana,na tabia yake ya ulipukaji.Katika post hiyo nilikuwa nazungumzia kauli ya Mhadhiri huyo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwamba tuhuma zilizokithiri dhidi ya ufisadi zinaweza kusababisha taifa kukosa viongozi wazuri.Yani mhadhiri mzima alikosa busara ya kufahamu kuwa kukalia kimya ufisadi hakuwezi kusababisha taifa kupata viongozi wazuri.

Bana na Redet yake wanadhani Watanzania ni wajinga ndio maana wakakurupuka na uchakachuaji huo wakiamini wanaisaidia CCM na Kikwete.Sio ubishi wala kulazimisha matokeo tunayotaka sie bali hali halisi ya mwenendo wa kampeni inaonyesha dhahiri kuwa CCM na Kikwete wamekaliwa kooni na Dokta Wilbroad Slaa na Chadema,huku uthibitisho mkubwa ukiwa kwenye vioja kama kauli ya vitisho ya Mnadhamu Mkuu wa JWTZ Brigedia Jenerali Shimbo.

Hivi huyo Kikwete angekuwa 'anapendwa' na zaidi ya asilimia 70 ya wapiga kura watarajiwa (potential voters) angekuwa anahangaika huku na kule ku-recycle lundo la ahadi zake za mwaka 2005?

Lakini tungetarajia nini kutoka kwa Dokta Bana na REDET yake?Waseme umaarufu wa Kikwete umeshuka?Waseme Dokta Slaa anaongoza kura za maoni?Hayo hayawezekani katika utawala huu wa kifisadi unaotaka kusikia habari njema tu hata kama hazina ukweli.Tunafahamu kuwa Synovate walishindwa kutueleza nani anaongoza kura za maoni kwa vile CCM ilihofia matokeo ya ripoti hiyo yangewaadhiri.Sasa kwa vile REDET 'wameshafungulia mbwa' sintoshangaa Synovate nao wakikurupuka na ripoti yao iliyochakachuliwa itakayoonyesha Kikwete na CCM wanaongoza.

Haina haja ya kuwashutumu wachakachuaji hawa.Dawa yao iko kwa wapiga kura waliochoshwa kuona nchi yao ikigeuzwa maabara ya uchakachuaji kwenye kila eneo.Hebu pata picha iwapo kila Mtanzania aliyechoshwa na ufisadi akipiga kura ya kuwaadhibu mafisadi na hatimaye Kikwete akan'goka madarakani,Dkt Bana na REDET yake watakuwa katika hali gani!

Hilo linawezekana.Wapiga kura wasianze kukata tamaa kuwa CCM wataiba kura.Of course wataiba lakini ili 'kura zitoshe' watalazimika kufanya wizi wa 'mchana mweupe' (day light robbery) jambo ambalo sio rahisi sana,japo linawezekana.Wanaweza tu kuchakachua matokeo kama,kwa mfano Dokta Slaa akipata asilimia 51 na Kikwete asilimia 49.Hapo watarejea uchakachuaji kama ule wa Zanzibar.Lakini kama ni tofauti ya double digits,wanaweza kupatwa na kigugumizi katika kufanikisha ujambazi huo.

Ni muhimu kutovunjwa moyo na hujuma hizi.Yatupasa kufahamu kuwa Kikwete na CCM yake ni kama mgonjwa mahututi ambaye yuko tayari hata kuning'inia kwenye uzi ili asalimike.Tutashuhudia vituko zaidi ya huo uchakachuaji wa REDET au vitisho vya akina Brigedia Shimbo.Cha muhimu ni kusimamia dhamira yetu.

Inawezekana.Timiza wajibu wako

8 Oct 2010

Image and video hosting by TinyPic


Urban Pulse Creative ikishirikiana na Aset Inapenda kuwataarifu wadau wote wa Music wa bongo Flava na Hip Hop kuwa imeandaa tamasha maalum linaloitwa URBAN TOUR ambapo msanii Diamond kutoka bongo anayetamba na kibao chake cha Mbagala atakuwepo hapa ukerewere kuanzia mwezi wa November mwaka huu. Wasanii wengine ni Pamoja na First lady wa Urban Pulse Mish Ze Fyah Sis UK Artist anayetamba na single yake Freedom na I don't give a damn.



Tamasha Hili ni kwa ajili ya kuchangia Vita Dhidi ya Malaria Afrika. Diamond ni ambassador wa Malaria Tanzania na ndiye atakekuwa akiwakilisha.
Shows Hivi zitafanyika tarehe 6th Nov Milton keynes, 12th Nov London and 27th Nov Birmingham.
Stay tune kwa habari zaidi.

Asanteni,

Urban pulse Creative.

Katika toleo la wiki hii la jarida la Raia Mwema nazungumzia kuhusu tuzo ya milenia,msaada tuliopewa na Waingereza baada ya kuridhishwa kwao na "nidhamu na matumizi yetu" na sifa alizomwaga Obama kuhusu "utawala bora".Cheki makala hiyo hapa bila kusahau makala na habari nyingine motomoto ndani ya jarida hilo maridhawa.

6 Oct 2010

BABA BABA BABA HUYO BABA BABA BABA BABA BABA HUYO...TUMBA TUMBA TUMBA TUMBA HILO TUMBA TUMBA HILO TUMBA TUMBA HILO...KIKWETE HOYEEEE...NILISEMA WALA RUSHWA NAWAJUA KAMA WAPIGA TUMBA ILA NAWAPA MUDA WA KUJIREKEBISHA...AKINA CHAHALI WANAOHOJI KUHUSU DEADLINE KWANINI HAWAHOJI PIA KUHUSU DEADLINE YA KUJIFUNZA KUPIGA TUMBA? (ACTUALLY,NIKIREJEA IKULU  NTAMSHTAKI HUYU KIJANA HUKO KIBEREGE KWA MZEE MAGU%^&£$%^)


NIMEISHIWA NA AHADI SASA.NGOJA NIJARIBU HII: NAWAAHIDI WATANZANIA KUWA MKINICHAGUA TENA NITAHAKIKISHA KILA MTANZANIA ATAKUWA NA TUMBA YAKE NYUMBANI AMBAYO UKIPIGA TU UNAPATA MAISHA BORA...SI NILIWAAMBIA KUWA MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA YANAWEZEKANA?

UFISADI OYEEE,TUMBA OYEEEE

MIE NI ZAIDI YA MORIS NYUNYUSA.ACTUALLY,ZILE NGOMA ZA ULE WIMBO WA TAARIFA YA HABARI YA RADIO TANZANIA NI KAZI YANGU.MCD (BADO YUPO TWANGA?)  NA ALI JAMWAKA AJIRA YENU MASHAKANI.

HUYU ZUMA ANATAKA KULETA HABARI ZA VUVUZELA,HAJUI KAMA MIE MTOTO WA MJINI.AI NEMA NEMA,AI NEMAA AAA,AI NEMA NEMA USIPONEMA LEO UTANEMA LINI

NEMA MWANANGU NEMA
SITAKI WATANZANIA WANIKUMBUKE KWA EPA,KAGODA NA RICHMOND PEKEE.NATAKA PIA WAELEWE KUWA MIE MIE KWA KUYARUDI NDIO MWENYE,IWE ENZI ZA NZAWISA,MAYENU AU HATA MSONDO....SHALO SHALO TINA TINA,YAANI SHAA MTU MZIMA (HEHEHEEE NGWEA NA JAY MO MPO?HATA MIE BONGOFLAVA NAZIJUA PIA.SI MNAWAONA WANABONGOFLEVA KWENYE KAMPENI ZANGU?)

UWEZEKANO WA JAKAYA KIKWETE KUMALIZIA MAUMIVU YAKE YA KUBWAGWA NA DOKTA SLAA (KAMA HAWATACHAKUACHUA KURA) KWENYE UALIMU KATIKA CHUO CHA SANAA BAGAMOYO NI MKUBWA (HOME BOY COMES BACK HOME....DON'T FORGET KIKWETE NI MKWERE).TUSICHOWEZA KUWA NA UHAKIKA NACHO NI WHETHER ATAKUWA MWALIMU WA KUPIGA NGOMA (TUMBA) AU DANSI STUFFS HE FANCIES KAMA PICHA ZA HAPO JUU ZINAVYOONYESHA

HAPPY RETIREMENT MR SOON-TO-BE EX-PRESIDENT



Chanzo: Wandima









Tukiwa tunaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu Tanzania ambao utafanyika October 31, 2010, Watanzania wazalendo wanachama na wapenzi wa Chadema mnaombwa kuchangia kwa dhati harakati za Chadema ili tuweze kuwafikia Wananchi wengi zaidi katika kila kona ya Tanzania tukitafuta ridhaa yenu ya kuweza kujenga nchi yetu; nchi yenye usawa, uzalendo, maadili na uwajibikaji katika miaka mitano ijayo.

CHANGIA CHADEMA KUPITIA BANK:
CRDB BANK
CHADEMA - M4C
Account Number: 0J1080100600

National Microfinance Bank [NMB]
CHADEMA
Account Number: 2266600140

Unaweza kuweka pesa kupitia tawi lolote la Benki hizi Tanzania.


CHANGIA CHADEMA KUPITIA SMS (MESEJI):
Tuma neno:

"CHADEMA" kwenda namba 15710
"NAJIUNGA" kwenda namba 15710
"SLAA" kwenda namba 15710

Unaweza kutuma meseji mara nyingi kadri unavyoweza na kila ujumbe utagharimu TZS 350/= tu.
HII NI KWA MITANDAO YA ZAIN, TIGO NA VODACOM TU.

CHANGIA KUPITIA M-PESA:
Kwa watakaotaka kuchangia kwa M-Pesa wanaweza kutumia namba zifuatazo:

0758 223 344
0764 776 673


CHANGIA KUPITIA ZAP:
Kwa watakaotaka kuchangia kwa ZAP wanaweza kutumia namba hii:

0789 555 333

"Ndugu Zangu Watanzania, tunawaomba kwa dhati kabisa tushikamane, tushirikiane bila kujali itikadi zetu kuchangia harakati hizi, tunawashukuru sana. - Dr. Wilbroad Peter Slaa"

CHAGUA MABADILIKO YA KWELI. CHAGUA CHADEMA.









Kwa hisani ya SUBI

4 Oct 2010

France


France


Sweden


Germany

Add caption


3 Oct 2010




Blogu hii inapenda kutoa salamu za pongezi kwa mpambanaji na mwanaharakati mahiri,Mwalimu Nkwazi Mhango (a.k.a Mpayukaji Msemaovyo) mwenye makazi yake nchini Kanada kwa kutuletea mpambanaji mwingine wa kiume.Ujio wa mwanaharakati huyu mchanga unaweza kuwa dalili njema hasa kwa vile tupo kwenye mchakato wa kuwatimua mafisadi wanaofakamia keki ya taifa letu kama hawana akili nzuri.

Naungana na Mwalimu Nkwazi na familia yake kumtakia kijana wetu afya njema na kila mafanikio ili pindi muda utapowadia ajumuike nasi katika harakati zetu za kupigania usawa katika jamii.

1 Oct 2010

"Ufisadi Oyeee.Tupeni tena miaka mitano tuwakwangue kabisa".Of course ni unatarajia nini hapo?

Mgombea wa CCM,Jakaya Kikwete akiendelea na ngwe ya kuwatetea rafiki zake.Alianza na Lowassa,akaenda kwa Mramba,kisha kwa Mzee wa Vijisenti Chenge,na sasa kwa "baba lao" Rostam Aziz.Ama kweli Tanzania bila ufisadi inawezekana!

Wakati "ndege wenye manyoya yanayofanana wakiruka pamoja",Dokta Slaa anaendelea na darasa la kuwahamasisha wenye uchungu na nchi yao kufanya kila liwezekanalo kuwang'oa "ndege hao"


Wananchi mjini Songea wakimsikiliza Rais Mtarajiwa kwa makini
Picha zote kwa hisani ya Jamii Forums

Jasusi ChatBot

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.