6 Apr 2008

Pata burudani ya picha zaidi kutoka Bongo
Lounge ya hoteli ya Kempinski

Kempinski kwa ndani,kwa hakika wanastahili pongezi kwa namna palivyoboreshwa.
Msikiti wa Kichangani Magomeni.Jirani na msikiti huuu,kuna makutano ya barabara za Morogoro na Kawawa.Eneo hilo ni maarufu sana kwa vibaka wababe wanaopora madereva.Ni zaidi ya kosa la jinai kusimamisha gari eneo hilo huku kioo kikiwa chini au nusu.
Makutano ya barabara za Morogoro na Bibi Titi.
Kasi ya majengo mapya ni kubwa katika maeneo mengi ya Dar.Hata hivyo,wananchi wengi wanalalamika kuwa hali ya maisha inazidi kuwa ngumu.
Sehemu hii inapendeza.Kwa muda nilijiskia kama niko Scotland vile.Hapa ni Kilimanjaro Hotel Kempinski.

Kempinski

Hakuna sheria muhimu ya uendeshaji gari mitaa ya Kariakoo zaidi ya ubabe.Ukifuata taratibu za usalama barabarani utaishia kugongwa,kuporwa au kulala hapohapo.
Mbinde za driving mitaa ya Kariakoo
Leo ni Jumapili na foleni katika barabara nyingi ni pungufu
I wish kila siku barabara zingekuwa nyeupe namna hii.
Msikiti wa Kichangani Magomeni
Millennium Towers.Eneo hili kuna internet cafe ambayo ni kimbilio la wengi wanaotegemea wireless connection.Pia ni mahala unapoweza kugongana na jamaa mbalimbali mliopoteana kutokana na kwenda nje kusaka hili au lile
Hii joint inaitwa "SAMAKI SAMAKI".The name tells it all...it's all about fish,fish and even more fish...Jana tulipewa ofa ya bure ya dagaa wa kukaanga.Yaani.... ndio mambo ya home sweet home hayo!However,dont let these nice pics fool you,mapambano ya maisha hapa yanataka ujasiri...na ukiwa jijini hapa inaweza kuwa rahisi kufahamu kwanini UFISADI unashamiri.The going seems to be getting tougher and tougher,forcing some folks to try to make the tough get going.
Barabara nyeupe
Barabara nyeupe pyee
Mitaa ya Kariakoo







Wakati unasubiri batch nyingine ya picha kutoka hapa,hebu pata burudani kutoka kwa Common featuring Dwelle katika track ya The People

5 Apr 2008

Zoezi la kuleta picha za Bongo linaendelea.I'm not trying to become a photoblogger of some sort,hiyo wanaiweza magwiji WA FANI kama rafiki yangu HAKI.Hapa chini kuna kiji-collection kidogo ca picha nilizodhani zinaweza kukupendeza wewe msomaji. Zote zimepigwa kwa kutumia Samsung Armani,na naamini quality ya picha inaridhisha.If not,let me know,plz!















Foleni za magari bado ni tatizo sugu kama Ufisadi.Hapa ni junction ya maeneo ya Namanga.Halafu jana kulikuwa na mvua si utani.Breaking news niliyopata jana mchana ni kuwa maji yalikuwa yanalazimisha kuingia ndani ya "mansion yetu" huko Ifakara (well,kwa level ya kijiji chetu,nyumba ikipigwa lipu nje,na vikorombwezo flani na geti la kizushi basi inapata hadhi ya kuitwa "mansion")

















Hapa ni HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI.Jana nayo ilikuwa imeelemewa na maji.Tatizo la Hospitali hii ni kwamba mazingira ya nje hayaridhishi,ya ndani ni ya kusikitisha na huduma ndani ni za kuvunja moyo. It's like a hospital from hell.



















Niliamua kuwanasa kwa picha hawa wageni waliokuwa wanafanya nini sijui hapo Mbuyuni,barabara ya Ali Hassan Mwinyi.Lilikuwa sio kundi kubwa as such lakini kama ujuavyo Bongo hakuna jambo dogo,muda si muda kukawa na lundo la watu wanawashangaa hao jamaa...I could swear I saw someone cancelling his trip to work just ku-join the party ya kushangaa... More pics hapo chini




















STAY TUNED FOR MORE PICS.

2 Apr 2008

Dar kuna tatizo kubwa sana la foleni.Na kwa kasi magari yanayoingizwa kila siku jijini hapa,nadhani kimeo cha foleni kitaebndelea kwa muda mrefu sana.Na inavyoonekana,hakuna mipango ya kuboresha barabara ili ziweze kumudu wingi wa magari.Sijui quality ya picha hizi ikoje.Ni majaribio ya Samsung Armani kwenye poor light (mida ya saa 12).Location ni Millennium Towers.Will keep on bringing more pics for you guys.






31 Mar 2008

KWA MUDA SASA BLOGU HII IMEKUWA KIMYA.HIYO NI KUTOKANA NA SAFARI YA KUJA HAPA NYUMBANI BONGO.LIBENEKE LITAENDELEA PINDI MAMBO YAKISHATULIA.WILL DO MY BEST TO KEEP YOU GUYS POSTED ABOUT WHAT'S HAPPENING KIPANDE HII

23 Mar 2008

Wakati tunasherehekea sikukuu ya Pasaka ni vema tukifanya tafakuri ya mambo ambayo machoni yanaweza kuonekana madogo lakini yenye uzito mkubwa katika hali halisi.Ni muhimu kumshukuru Mungu kwa mengi au machache aliyo/anayotujalia.Hivi kuna zawadi kubwa kutoka kwa Mungu zaidi ya UHAI?Sambamba na uhai ni uzima/ukamili wa miili yetu.Tuliozaliwa tukiwa kamili (yaani bila ulemavu) tunaweza kujisahau kuuliza maswali magumu kama "ingekuwa vipi kama ningezaliwa nina mkono nusu,au pua iliyozama ndani,au hata jicho lililokaa kisogoni" hadi pale tunapowaona wenzetu kama huyu mtu-tembo (elephant man-sio yule wa dancehall),ambaye stori yake inapatikana HAPA

22 Mar 2008

NAWATAKIENI NYOTE HERI NA BARAKA ZA SIKUKUU YA PASAKA.UFUFUKO WA BWANA YESU KRISTO ULETE AMANI,UPENDO,AFYA NJEMA NA MAFANIKIO KWA KILA MMOJA WETU.PAMOJA NA SALAMU HIZI NI SHUKRANI ZANGU ZA DHATI KWENU NYOTE MNAOTEMBELEA BLOGU HII NA KUSOMA MAKALA ZINAZOTOKA KATIKA BAADHI YA MAGAZETI YA NYUMBANI.BWANA AWABARIKI SANA,AMEEN.

Jana nilishuhudia kituko cha mwaka.Mwanzoni nilidhani ni porojo tu lakini asubuhi hii nimeona tukio hilo limekuwa gumzo mtandaoni.Ilikuwa takriban saa 6 mchana za hapa (hapa saa zitabadilika mwishoni mwa mwezi huu),nikaamua kupoteza muda kwa kuangalia kipindi cha Fox&Friends.Nasema kupoteza muda kwa vile waendesha kipindi hicho huwa wananikera sana kutokana na kauli zao za upendeleo wa wazi kwa wahafidhina na upinzani wao mkubwa dhidi ya Democrats na liberals.Sikujutia uamuzi wa "kupoteza muda" kwani huku watangazaji Steve Doocy na Gretchen Carlson wakishikia bango kauli ya Obama kwamba grandmom wake ni like typical White person,mwenzao Brian Kilmeade aliamua kuondoka kwa muda studioni kutokana na kukerwa na namna wenzie walivyokuwa wakimsakama Obama.Kama hiyo haitoshi,muda mfupi baadaye,mtangazaji mwandamizi wa kituo hicho,Chris Wallace,alionekana hewani wakati Fox&Friends inaendelea ambapo alielezea waziwazi kwamba alikuwa akiangalia kipindi hicho na hakupendezwa na namna kauli ya Obama kuhusu bibi yake ilivyokuwa ikipotoshwa.Wallace alieleza wazi kwamba yeye si msemaji wa kambi ya Obama lakini angependa kuona kipindi hicho kinazungumzia suala hilo ndani ya context,na kwenda mbali zaidi kwa kuwashauri wana-Fox&Friends kuangalia pia habari nyingine za muhimu kuhusu Obama kama vile endorsement ya Bill Richardson na hotuba zake mbili kuhusu uchumi na vita ya Irak.





19 Mar 2008

Makala yangu katika toleo la wiki hii la gazeti la Raia Mwema inajaribu kudadisi chanzo cha ufisadi huko nyumbani.Je tatizo ni mfumo unaozaa na kulea ufisadi au tatizo ni watu wanaosabaisha ufisadi na kuishia kutengeneza mfumo haramu wa maovu?Lakini kabla ya kuingia kwenye mjadala huo,makala hiyo imeanza kwa discussion fupi kuhusu kipindi cha BET cha Hip-Hop vs America.Binafsi,nimetafsiri dhima ya kipindi hicho kuwa ni jamii ya Black Americans kujiuliza adui yao halisi ni nani: wao wenyewe au mfumo dhalimu uliotawaliwa na ubaguzi na nguvu za Corporate America.Basi,pamoja na habari na makala nyingine zilizokwenda shule,bingirika na makala hiyo kwa KUBONYEZA HAPA.

18 Mar 2008

Gazeti la Los Angeles Times lina habari kwamba rapa tajiri na maarufu,Sean "P.Diddy" Combs alikuwa na taarifa za ndani kuhusu mpango wa mauaji ya Tupac Shakur aliyepigwa risasi na hatimaye kufariki Novemba mwaka 1994.
Kwa mujibu wa taarifa za kiuchunguzi za gazeti hilo,watu mbalimbali wamethibitisha tuhuma hizo ambazo zimekanushwa vikali na P.Diddy.Itakumbukwa kwamba kifo cha Tupac kinahusishwa pia na mauaji ya rapa mwingine maarufu Christopher Wallace a.k.a. Notorious B.IG. ambacho kinadhaniwa kuwa ni kisasi cha washirika wa Tupac.


                
              Uchunguzi huo wa L.A.Times unadai kwamba sababu kubwa iliyopelekea kuuawa kwa Tupac ni "adhabu" kwa nguli huyo wa rap kukataa kuwa mshirika wa kibiashara wa lebo ya Bad Boy inayomilikiwa na P.Diddy.

Kwa habari zaidi soma habari hiyo ya kusisimua kwa KUBONYEZA HAPA.Hapo chini ni clip ya B.I.G katika track Mo Money Mo Problems akimshirikisha Puff Daddy na Mase


Pia waweza kuangalia track hii hapo chini ya Tupac  f/t The Outlawz (Caution: Very Explicit Lyrics) Hit Em Up ambapo rapa huyo na vijana wake wanatupa "madongo" makali kwa P.Diddy (enzi hizo akijulikana kama Puff Daddy),B.I.G,Lil' Kim,Lil' Cease,Mobb Deep na lebo nzima ya Bad Boy.Ni dhahiri kuwa track hii ilichangia sana kukuza beef kati ya mahasimu hao wa Pwani ya Mashariki na ya Magharibi huko Marekani.



17 Mar 2008

Hebu toa hukumu mwenyewe katika MAKALA HII

16 Mar 2008

Nawazungumzia wahafidhina.Wanafikiri siku zote wao wako sahihi,lakini licha ya fikra hizo mufilisi,wanataka ku-monopolize haki ya kuwa on the right of the political spectrum.And for that matter,Jeremiah Wright,yule livewire cleric wa Barack Obama yuko wrong ilhali right-wing lunatics like Bill O'ReillySean Hannity,Ann Coulter,Rush Limbaugh,ambao wanasifika kwa maneno machafu kupita kiasi,siku zote wako sahihi...according to them.Anyway,that's politics.Soma makala hii kuhusu uhusiano wa Obama na Rev Wright.

15 Mar 2008



OBAMA:On My Faith and My Church. (CLICK THE LINK TO READ THE ARTICLE)

12 Mar 2008

Makala yangu katika toleo la wiki hii la gazeti la Raia Mwema inatanua wigo wa uchambuzi kuhusu suala la ufisadi na kuangalia eneo jingine nyeti la ufisadi wa ngono.Umeshawahi kujiuliza ma-miss wangapi wanaletwa jijini Dar kutoka vijijini,wilayani au mikoani kisha kushirikishwa kwenye mashindano ya ulimwende na hatimaye kuachwa mikononi mwa fisi-maji wa ngono?Pamoja nahabari na makala nyingine zilizobobea,bingirika na makala yangu hiyo kwa KUBONYEZA HAPA

11 Mar 2008























Kufuatia Gavana wa New York,Elliot Spitzer,au "Client 9", kukumbwa na skandali la kujihusisha na makahaba,The Huffington Post wametoa wanachokiita (kwa tafsiri yangu) Mwongozo wa Kutumia Huduma ya Makahaba (Prostitution:A User's Manual).Soma Mwongozo huo HAPA (you never know when it might become handy!)

Mmoja wa polisi wa ngazi za juu hapa Uingereza,Chifu Konstebo wa Greater Manchester Police,Michael Todd,amekutwa amekufa.Habari zaidi zinapatikana hapa

MAKALA HII YANGU ILITOKA KATIKA GAZETI LA MTANZANIA TAREHE 07 MACHI 2008

Unafiki wa viongozi wetu wa dini

na evarist chahali, uskochi

MADA yangu ya leo, najua dhahiri itawakera wateule wachache wa aina fulani. Lakini kabla ya kuwapasha, naomba nizungumzie suala la imani na dini hapa ninapoishi Ughaibuni.

Nilipofika hapa kwa mara ya kwanza, nilionyeshwa majengo kadhaa ambayo huko nyuma yalikuwa Makanisa, lakini sasa yamegeuzwa kuwa kumbi za disko na klabu za usiku.

Na hao walioyageuza Makanisa hayo kuwa sehemu za starehe, wala hawakujishughulisha kabisa katika kubadili mwonekano wake, bali wameyaacha yatoe ushuhuda kuwa huko nyuma yalikuwa sehemu za ibada.

Nilipofanya udadisi kwa wenyeji, niliambiwa kwamba makanisa hayo yaliuzwa baada ya kuwa matupu kutokana na ukosefu wa waumini. Wengi wa waumini wa makanisa ya mji huu ninaoishi, ni ama wahamiaji waliotoka nje ya nchi hii kama mimi, na au vikongwe vya hapa hapa.

Binafsi, sina majibu ya moja kwa moja kwamba tatizo la hawa wenzetu ni nini. Hata hivyo, ninachofahamu ni kwamba kuna watu kadhaa ambao wanajitambulisha kuwa hawana dini, na au hawaamini kuwapo kwa Mungu.

Imani ni suala la mtu binafsi, na hivyo pengine si mwafaka kuhoji kwa nini fulani anaamini, ama haamini kuwapo au kutokuwapo kwa Mungu.Ingawa binafsi, ni muumini kwa aina fulani, huwa sisiti kuwasifu wale wasiowaumini wa dini yoyote, lakini wasioona aibu kuelezea msimamo wao wa kidini. Kwa lugha nyingine, watu hao si wanafiki. Wanaeleza bayana kile wanachokiamini na kutokiamini.

Kuna tatizo la msingi huko nyumbani, ingawa natambua dhahiri kwamba watu wengi hawapendi kujadili mambo ya dini kwa sababu ile ile ya unafiki!

Baadhi ya viongozi wetu wa dini, wamekuwa mstari wa mbele kukemea wale ambao wanakwenda kinyume na imani zao, lakini viongozi hao hao wakishiriki kwenye maovu wanayoyakemea.

Ndiyo, tunatambua kwamba mara nyingi viongozi wetu wa dini wana wafadhili wao nje ya nchi. Lakini hicho si kigezo cha wao kuishi maisha tofauti kabisa na wafuasi wao.

Utakuta katika kijiji fulani ambacho kimegubikwa kabisa na umasikini, kiongozi fulani wa dini yeye akiishi kama yuko peponi. Na bila huruma, huyo huyo anayeishi maisha kama ya peponi katikati ya waumini masikini, kwa kutumia kisingizio cha maandiko matakatifu, anawashurutisha waumini wake kujipigapiga ili kuongeza sadaka wanazotoa.

Kinachokera zaidi, ni hili suala la baadhi ya viongozi wa madhehebu fulani kuwa na watoto mitaani, huku sheria za madhehebu yao zikiwa haziwaruhusu kufanya hivyo.

Tatizo hili ni sugu sana, hususan maeneo ya vijijini. Kinachosikitisha ni ukweli kwamba waumini wanafahamu kwamba kiongozi wao wa dini, anaishi kinyume na maadili ya huduma yake, lakini hawachukui hatua yoyote zaidi ya kulalamika chini chini.

Binafsi, ninayo mifano hai ya baadhi ya viongozi wa madhehebu yangu ambao wana watoto lukuki mitaani. Baadhi yao wanatoa huduma kwa wazazi wa watoto wao hao, lakini wengine wamewatelekeza kabisa.

Hawa watu ni wanafiki ambao hawastahili kuachwa waendeleze uhuni kwa kisingizio kwamba daraja walilofikia, haliwezi kutenguliwa.

Mitume wetu waliishi maisha ya uadilifu, ambayo yalishabihiana kwa asilimia 100 na kile walichokuwa wakikihubiri. Na si katika suala la uzinzi pekee, bali hata kwenye dili za kibiashara.Majanga kama ya ukimwi yataondoka vipi iwapo baadhi ya wale wanaopaswa kukemea vitendo vya ngono, kwa vile vinavunja amri ya Mungu, nao ni washirika wa vitendo hivyo?

Pamoja na mapungufu waliyonayo baadhi ya viongozi wa dini, hivi karibuni tumeshuhudia wengi wakijitokeza kuungana na Watanzania wenzao kukemea masuala yanayohatarisha umoja wa kitaifa.

Suala ambalo baadhi ya viongozi hao wa dini wanastahili pongezi, ni katika kukemea vitendo vya kifisadi, ingawa tatizo linakuwapo, pale msimamo huo unapokuwa wa kiongozi mmoja zaidi, badala ya kuwa msimamo wa taasisi ya dini.

Katika hili, napenda nichukue fursa hii kumpongeza Askofu Mkuu mpya wa Kanisa la Anglikana Tanzania, ambaye ameweka bayana msimamo wake dhidi ya vitendo vya kifisadi. Hiyo inatia moyo sana!

Licha ya kukemea ufisadi na maovu mengine katika jamii, asasi za dini zinaweza kubadili tabia za waumini wao kwa kuwawekea vikwazo vya aina fulani. Taratibu za aina hiyo, zipo katika baadhi ya imani, kwa mfano, Wakatoliki, ambao muumini akikiuka kanuni fulani, anazuiwa kushiriki baadhi ya sakramenti.

Kwa nini basi tunaendelea kujumuika na mafisadi makanisani, na au misikitini ilhali matendo yao yanalenga kutuumiza kimaisha? Nafahamu kuwa dini zote zinahimiza upendo, lakini hiyo si sababu ya kutowabana wale wasio na upendo kwa Watanzania wenzao.

Inawezekana kwamba kikwazo kikubwa kwa dini zetu kuwa mstari wa mbele katika kukemea maovu na kubadili tabia za wanaokwenda kinyume na maadili ya kimwili na kiroho, ni hofu ya usafi wa baadhi ya viongozi wa dini hizo, kama nilivyoeleza mwanzoni mwa makala haya.Tatizo hilo linaweza kupatiwa ufumbuzi iwapo viongozi wa madhehebu wataepuka mtindo wa kulindana, na hivyo kuchukua hatua kali kwa walio chini yao, ambao wanakwenda kinyume cha kanuni na taratibu za madhehebu.

Ni wazi kwamba viongozi waadilifu wa dini, hawawezi kuogopa kumnyooshea kidole fisadi fulani, kwa kuwa hata kama fisadi huyo atataka kulipa kisasi, atajikuta hana jambo lolote analoweza kulitumia kushusha heshima ya kiongozi wa dini aliyemkemea.

Busara za Kiswahili zinatueleza kwamba kujikwaa si kuanguka, na hata kuanguka si mwisho wa safari. Wito wangu kwa viongozi wetu wa dini, ni kuongeza jitihada za kuwahudumia waumini wao kiroho na kimwili.

Ni muhimu kwa viongozi hao kuishi kama Mitume ambao mafundisho yao yalikubalika na kuvuta watu wengi, kwa vile wao wenyewe walikuwa waadilifu na mifano bora ya kuigwa na wanadamu.




10 Mar 2008

Weka kando (japo kwa muda) habari zinazovuma za ufisadi,kuna habari njema za warembo wetu wanaotufanya tuamini kuwa nasi tulipendelewa pia na Muumba kwa kutupatia mabinti warembo.Hao wote pichani wanavutia na kumeremeta,ingekuwa ni kuchagua nani bora zaidi ya mwenzie basi majaji wangelazimika kufumba macho na kuchagua kwa kugusa,yaani atakayeguswa kwanza ndio mshindi wa kwanza.Ila binafsi haiba,pozi na mvuto wa huyo model wa tatu kutoka kulia-mstari wa mabinti-vinanishawishi nimpe nambari wani (numero uno)...Yaani utadhani anakuita!!!Au wewe msomaji unaonaje?Big up to Dollywood na wadau wengine wa mambo ya urembo kwa kuvumbua vipaji
Picha kwa hisani ya foto-bloga tishio HAKI

9 Mar 2008


NIMETUMIWA BARUA-PEPE IFUATAYO NAMI NAOMBA KUIWASILISHA KAMA ILIVYO

Sun, Mar 9, 2008 18:24

Subject: Tanzania joined world largest online soccer game!
Date: Sunday, March 9, 2008 15:08
From: Franc de Bok
To:
Conversation: Tanzania joined world largest online soccer game!
Dear Sir/Madam,
I am Franc de Bok a student from The Netherlands and I’d like to bring you something to your
attention.
Since a week Tanzania has joined the community of Hattrick, http://www.hattrick.org , a free online soccer simulation game. It was the 120th nation to do so. Today nearly 1 million people around the world are part of Hattrick and the game has been mentioned in articles in newpapers in many countries.
In Hattrick you can manage your own football team, train players, transfer players, talk to other people in the much praised community. There are also the national teams in each country to which a player can be selected to play in the World Cup.
For the Hattrick community of Tanzania and their national teams it is really important that many people join hattrick and train players. People who join now, will play on a high level and
have a good opportunity to become the National Champion of Tanzania. At the moment 168 people in Tanzania can start a team, 16 people have decided to do so in less than a week.
As I am the National Coach of Tanzania Under 20’s, I’d love to help people with their questions. It would be great If your blog could run an article about this fascinating story of a global internet community around a football game.
We also made a promotional video: http://www.youtube.com/watch?v=uuOUQ0IQqjM in case you want to see some footage about it.

Thank you very much in advance,
more questions are very welcome,
Kind Regards,
Franc de Bok (nickname PolCaf-Bokmans)
U20 National Coach of Tanzania,
The Netherlands
Blijf onderweg online met Windows Live for Mobile! Download 't nu op jouw mobiele

telefoon.

8 Mar 2008

Mzimu wa uhuru wa Kosovo unaendelea kuisumbua Serbia na sasa serikali yake imesambaratika kutokana na tofauti za kimsimamo kati ya Waziri Mkuu,Vojislav Kostunica mwenye mtizamo wa kitaifa (nationalist) na Rais Boris Tadic mwenye mtizamo wa kimagharibi zaidi.Habari zaidi,soma HAPA.

PIA KUNA HABARI MOJA IMENIGUSA SANA KUHUSU BIASHARA YA "UNGA" KATIKA NCHI YA GUINEA BISSAU.UNAWEZA KUISOMA HAPA



Ama kweli Dunia haijaishiwa vituko.

Jasusi ChatBot

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.