Mwezi Novemba mwaka 2006,niliandika makala moja iliyotoka katika gazeti la KULIKONI (toleo la tarehe Novemba 3-9, 2006 2006).Katika makala hiyo (BONYEZA HAPA KUISOMA),nilizungumzia kusikitishwa kwangu na habari kwamba ex-PM Edward Lowassa alikuwa akifanya jitihada za kuwanyamazisha wabunge wa CCM kuhusu shinikizo la kujadili mkataba wa Richmond.Pia katika makala hiyo nililaumu staili ya uongozi wa Lowassa ya kuwaumbua hadharani watendaji walio chini yake badala ya kufanya hivyo kimaandishi au ofisini.Nilieleza kwamba japo dhamira ya Lowassa kukosoa utendaji wa subordinates ni njema,njia anazotumia sio mwafaka.Nilihoji kiongozi angejisikiaje iwapo Bosi wake,JK,akitokea kumkosoa hadharani badala ya kufanya hivyo faraghani.Nilipoandika makala hiyo,sikujua kuwa kuna siku,Lowassa atakumbana na fedheha ileile aliyokuwa akiwapatia ma-DC,RAS,Katibu Kata,nk kwa kuwaumbua hadharani (pengine kwa kujitafutia tu umaarufu wa kisiasa).Leo siku hiyo imetimia.Siku chache baada ya makala hiyo kuchapishwa,Mwandishi wa Habari wa Lowassa,aliandika makala kupinga hoja zangu,kabla ya kunitumia barua-pepe ya shutuma na hatimaye aliweka comments kwenye blog hii.Contents za makala,barua-pepe na comments za muungwana huyo zilikuwa na ujumbe unaolingana,ambapo pamoja na mambo mengine alipingana na hoja zangu huku akishutumu kwamba sie wanafunzi tulio nje tukisomeshwa kwa kodi za masikini hatupaswi kukosoa mambo tusiyoyajua (BONYEZA HAPA KUSOMA COMMENTS HIZO.)Nami nimjibu kwa barua-pepe kusisitiza kwamba nilichoandika kilikuwa sahihi,na imani yangu kwamba utetezi wake kwa Lowassa ilikuwa sehemu tu ya utekelezaji wa majukumu yake ya kazi (SOMA BARUA-PEPE HIYO KWA KUBONYEZA HAPA)8 Feb 2008
8.2.08
Evarist Chahali
JK, LOWASSA, RICHMOND
No comments
Mwezi Novemba mwaka 2006,niliandika makala moja iliyotoka katika gazeti la KULIKONI (toleo la tarehe Novemba 3-9, 2006 2006).Katika makala hiyo (BONYEZA HAPA KUISOMA),nilizungumzia kusikitishwa kwangu na habari kwamba ex-PM Edward Lowassa alikuwa akifanya jitihada za kuwanyamazisha wabunge wa CCM kuhusu shinikizo la kujadili mkataba wa Richmond.Pia katika makala hiyo nililaumu staili ya uongozi wa Lowassa ya kuwaumbua hadharani watendaji walio chini yake badala ya kufanya hivyo kimaandishi au ofisini.Nilieleza kwamba japo dhamira ya Lowassa kukosoa utendaji wa subordinates ni njema,njia anazotumia sio mwafaka.Nilihoji kiongozi angejisikiaje iwapo Bosi wake,JK,akitokea kumkosoa hadharani badala ya kufanya hivyo faraghani.Nilipoandika makala hiyo,sikujua kuwa kuna siku,Lowassa atakumbana na fedheha ileile aliyokuwa akiwapatia ma-DC,RAS,Katibu Kata,nk kwa kuwaumbua hadharani (pengine kwa kujitafutia tu umaarufu wa kisiasa).Leo siku hiyo imetimia.Siku chache baada ya makala hiyo kuchapishwa,Mwandishi wa Habari wa Lowassa,aliandika makala kupinga hoja zangu,kabla ya kunitumia barua-pepe ya shutuma na hatimaye aliweka comments kwenye blog hii.Contents za makala,barua-pepe na comments za muungwana huyo zilikuwa na ujumbe unaolingana,ambapo pamoja na mambo mengine alipingana na hoja zangu huku akishutumu kwamba sie wanafunzi tulio nje tukisomeshwa kwa kodi za masikini hatupaswi kukosoa mambo tusiyoyajua (BONYEZA HAPA KUSOMA COMMENTS HIZO.)Nami nimjibu kwa barua-pepe kusisitiza kwamba nilichoandika kilikuwa sahihi,na imani yangu kwamba utetezi wake kwa Lowassa ilikuwa sehemu tu ya utekelezaji wa majukumu yake ya kazi (SOMA BARUA-PEPE HIYO KWA KUBONYEZA HAPA)6 Feb 2008
6.2.08
Evarist Chahali
BOT, BUNGE, CCM, IPC, MCCAIN, RAIA MWEMA, REPUBLICANS, SLAA, UFISADI
No comments
Makala yangu ndani ya toleo la wiki hii la gazeti la Raia Mwema iliandaliwa kabla ya "kimuhemuhe" kilichoanza leo huko Bungeni.Kwa kifupi,makala hiyo inaelezea namna siasa inavyoboa (au ni wanasiasa ndio wanaoboa?) na kutoa mfano wa namna baadhi ya wahafidhina katika chama cha Republicans "wanavyotiana vidole kwenye macho" kufuatia mwenendo mzuri wa harakati za Seneta John McCain kuingia White House kwa tiketi ya chama hicho.Pia makala hiyo inagusia vimbwanga vya siasa za huko nyumbani kwa kuonyesha mshangao wa namna Spika Samuel Sitta "alivyoruka kimanga" kwamba aliwahi kuweka vikwazo dhidi ya harakati za Dr Slaa kufichua ufisadi wa BoT.Pia makala inazungumzia "utoto" wa CCM (licha ya kuwa majuzi ilitimiza miaka 31) pale inapodai kuwa yenyewe ndiyo iliyoibua hoja ya ufisadi.Hivi Chama hicho kimeishiwa busara namna hiyo hadi kusahau kwamba sababu ya mawaziri wake kuzomewa mikoani ilikuwa ni reactions za wananchi dhidi ya jitihada za vigogo hao kuua hoja za wapinzani kuhusu ufisadi!!!?
Lakini kali zaidi ni pale Spika wa Bunge alipotoa maelekezo kwa Naibu wake kwamba "asikurupuke" kuendesha mijadala ya Richmond na BoT/EPA hadi yeye (Spika) ataporejea kutoka ziarani Marekani.Angalau sasa tunaelewa kwanini Spika alitaka kutumia mbinu za kupoteza muda katika mjadala wa Richmond,kwani RIPOTI YA KAMATI TEULE YA BUNGE KUHUSU MKATABA KATI YA SERIKALI NA KAMPUNI HIYO (BONYEZA HAPA KUISOMA)imemu-implicate Spika kwa namna flani (kwa vile Kituo cha Uwekezaji-IPC-kikiwa chini ya uongozi wa Sitta,kiliiruhusu Richmond iwekeze pasipo kuchunguza uwezo halisi au uwepo wa kampuni hiyo).
Pamoja na makala nyingine zilizokwenda shule ndani ya gazeti hilo,bingirika na makala yangu hiyo kwa KUBONYEZA HAPA.
1 Feb 2008
1.2.08
Evarist Chahali
BBC, KENYA, MTANZANIA, NEWSNIGHT
No comments
Makala yangu hii ilitoka katika toleo la jana la gazeti la MtanzaniaMiongoni mwa adha za kumiliki runinga hapa Uingereza ni kuilipia ada ya leseni (TV Licence Fee).Ada hiyo kwa kiasi kikubwa hutumika kuendesha BBC ambalo ni shirika la utangazaji la nchi hii.Wananchi wengi wamekuwa wakilalamika kwamba baadhi ya vipindi vya BBC havina ladha inayoweza kuhalalisha shirika hilo kuendelea kupewa ruzuku inayotokana na ada ya leseni za runinga.Hata hivyo,BBC imeendelea kuwa shirika la habari maarufu na lenye mtandao mkubwa sio tu ndani ya Uingereza bali duniani kwa ujumla.Na miongoni mwa vipindi maarufu vya shirika hilo la habari ni Newsnight,kipindi kinachoonyeshwa siku za wiki kuanzia saa 4.30 usiku.
Kipindi hicho huchambua habari muhimu zilizojitokeza katika siku husika ndani na nje ya nchi hii.Hivi karibuni,Newsnight ilizungumzia machafuko yanayoendelea nchini Kenya.Kwa hakika ilikuwa inatia uchungu kuona namna watu wanavyotaabika nchini humo.Moja kati ya mambo yaliyolinisikitisha zaidi ni mahojiano mafupi kati ya mtangazaji wa BBC aliyeko nchini Kenya na mwanamama mmoja ambaye wakati wa mahojiano hayo alikuwa kamanda wa polisi wa eneo flani (jina la afande huyo na mahala alipokuwa anaongoza vimenitoka kidogo).
Kamanda huyo alianza mahojiano hayo kwa kukanusha madai kwamba jeshi la polisi la Kenya limekuwa likiuwa raia wasio na hatia katika kutekeleza sera ya “piga risasi kuua” (shoot-to-kill policy).Alidai kuwa wanachofanya wanausalama ni kudhibiti machafuko na uhalifu.Mwishoni mwa mahojiano,afande huyo alieleza uchungu alionao kuona nchi yake ikiteketea.Alisema kwamba ameshatembelea sehemu nyingi duniani na kuona watu wa nchi hizo wakiwa na fahari na nchi zao,jambo ambalo lilimwongezea mapenzi kwa nchi yake.Aliwalaumu wanasiasa wa Kenya kwa kuzorotesha jitihada za kuleta amani.
Cha kusikitisha ni kwamba kamanda huyo aliyeonekana kuguswa sana na madhila yanayowakumba Wakenya wenzie aliondolewa kwenye usimamizi wa operesheni za mitaani na kukabidhiwa majukumu ya kiofisi (desk job).Yaani aliadhibiwa kwa kusema ukweli wa moyoni mwake kuhusu namna wanasiasa wanavyoendekeza maslahi yao kuliko ya nchi na wananchi.Naamini mwanamama huyo ni mmoja tu kati ya askari wengi ambao wanalazimika kupiga na hata kuua Wakenya wenzao katika kutekeleza amri “halali” za serikali.
Ilielezwa katika kipindi hicho cha Newsnight kwamba licha ya matokeo ya uchaguzi mkuu wa rais na wabunge mwezi Desemba mwaka jana kuwa chanzo kikuu cha machafuko hayo yasiyoonyesha dalili ya kupungua,msingi wa matatizo ulijengwa miaka kadhaa iliyopita.Kwa mujibu wa uchambuzi wa wajuzi wa siasa za Kenya,kwa muda mrefu kumekuwa na manung’uniko miongoni mwa baadhi ya makabila kuhusu umiliki wa njia za uchumi ambapo inadaiwa Wakikuyu wamekuwa na upendeleo zaidi.
Tofauti za kikabila na kidini ni miongoni mwa vyanzo vikubwa vya machafuko sehemu mbalimbali duniani hususan barani Afrika.Lakini tofauti hizo hustawi vizuri zaidi mahala ambapo kuna manung’uniko kuhusu haki na usawa hasa katika uchumi.Ni rahisi kumshauri fukara aingie mtaani “kujikomboa” kuliko kumshawishi mtu afunge biashara zake akashiriki maandamano.Pia ni vigumu kwa watu wa makabila au dini tofauti wanaoshirikiana katika ajira na utoaji au upokeaji huduma kuanzisha vurugu ambazo kwa vyovyote zitapelekea kuathiri mahusiano yao (kwa mfano, mahusiano kati ya mfanyabiashara na mteja au mwajiri na mwajiriwa).
Tofauti na nchi kama Uingereza ambapo mvuto wa kisiasa miongoni mwa wapiga kura uko chini hasa kwa vijana,wengi wetu tulishuhudia namna kampeni za uchaguzi nchini Kenya zilivyogusa karibu kila sehemu ya maisha ya Wakenya,kama ambavyo chaguzi zetu huko nyumbani zinavyokuwa na mvuto mkubwa.Ni dhahiri kwamba amani ingeshapatikana iwapo nguvu nyingi zilizotumiwa na wanasiasa wa Kenya na vyama vyao kushawishi wapiga kura zingeelekezwa pia kwenye kutafuta mwafaka katika vurugu zinazoendelea.
Ni vigumu kubashiri namna gani vurugu hizo zitadhibitiwa na kumalizwa kwa vile Kibaki na Raila wanaonekana kutokubaliana katika njia sahihi za kuleta amani.Yayumkinika kusema kwamba hakuna uwezekano wa Kibaki na serikali yake kukubali mapungufu yaliyojitokeza kwenye uchaguzi huo kwa vile kwa kufanya hivyo watakuwa wameongeza nguvu kwenye hoja za Raila na wafuasi wake kwamba matokeo ya uchaguzi huo ni feki.
Kwa upande mwingine,Raila anafahamu gharama kubwa ya maisha na mali wanayoipata wafuasi wake kwa kupinga matokeo ya uchaguzi huo,na kukubali kushirikiana na Kibaki pasipo makubaliano ya kutengua ushindi wa rais itakuwa ni sawa na usaliti wa daraja la kwanza.Historia nayo haitoi matumaini ya amani kwa jirani zetu wa Kenya kwani hakuna rais yeyote (hasa barani Afrika) anayeamini alishinda uchaguzi kwa njia halali aliye tayari kukubali uchaguzi urejewe kwa minajili tu ya kuridhisha wapinzani wake au kutuliza machafuko nchini mwake.
Madhara ya muda mrefu ya kinachoendelea nchini Kenya ni kuzaliwa kwa kizazi chenye kinyongo.Ni kipi kinachoweza kufuta kinyongo cha mtoto aliyepoteza wazazi wake katika machafuko hayo?Kibaya zaidi ni kwamba kadri machafuko yanavyoendelea ndivyo kizazi hicho cha kinyongo kinavyozidi kuongezeka.
Miezi michache iliyopita Watanzania walitoa maoni kuhusu wazo la kuunda muungano wa nchi za Afrika Mashariki,na wengi wao walipinga uharakishaji wa muungano huo.Ni kama walifahamu kwamba kelele za kuwa na muungano zilikuwa za kisiasa zaidi kuliko kuzingatia hali halisi ndani ya nchi husika. “Mikoa” ambayo ingeunda “nchi” hiyo (yaani sie na Uganda,na pengine Burundi na Rwanda) imeshindwa kuwa na mchango wa maana wakati “mkoa mwingine” (Kenya) unazidi kuteketea.Sijui ingekuwaje iwapo haya yangekuwa yanatokea ndani ya muungano huo!
Baadhi ya wapinzani wa muungano huo walieleza bayana kwamba japo wanafahamu umuhimu wa ushirikiano,au hata kuungana kisiasa,ukweli unabaki kwamba nchi husika zina matatizo yake lukuki ambayo yanapaswa kushughulikiwa kwanza kabla ya kuyakuza kwa kuunda “nchi” kubwa zaidi iliyojaa vipande vyenye matatizo binafsi.
Jeuri za wanasiasa wa Kenya kutosikiliza vilio vya wananchi wao na kupuuza jitihada mbalimbali zinazofanywa na wasio Wakenya ni onyo muhimu kwa wenye ndoto za ya muungano wa Afrika Mashariki kwamba kama wanashindwa kuweka mbele maslahi ya nchi yao na wananchi wao watajali vipi maslahi ya Watanzania au Waganda.
Kubwa la kujifunza katika sakata hili ni jinsi ilivyo amani iliyojengwa kwa miaka miongo kadhaa inavyoweza kuyeyuka ndani ya kipindi kifupi kabisa.Harakati za kumfukuza mkoloni nchini Kenya zilichukua miaka mingi na kugharimu maisha mengi.Wakenya walikuwa bado wako katika harakati za kupata uhuru wa kweli hadi wakati machafuko yanaanza nchini humo.Kinachoendelea sasa ni sawa na kusigina jitihada na damu za mashujaa waliopigania uhuru wa nchi hiyo.
Kwa Watanzania,wakati tunaendelea kuwaombea jirani zetu amani (yaelekea hakuna la ziada tunaloweza kufanya zaidi ya hilo) ni muhimu kutambua kwamba amani na utulivu tulionao unaweza kudumu milele iwapo tu jitihada za makusudi zitafanyika kuondoa umasikini,kuhakikisha pato la taifa linatumika kwa maslahi ya wote na “haki” kuwa haki ya kweli kwa kila Mtanzania bila kuangalia tabaka.Kelele dhidi ya ufisadi na mafisadi ni sehemu muhimu ya harakati za kuhakikisha amani na utulivu nchini inadumu milele.

30 Jan 2008
Pamoja na mambo mengine,makala yangu katika toleo la wiki hii la gazeti la Raia Mwema inatoa changamoto kwa vyombo vya habari vya Tanzania kutumia ipasavyo teknolojia ya habari kwa kuwezesha habari zao kupatikana mtandaoni.Pia nimegusia kwa kifupi "tangazo" la Balozi Ali Karume kuhusu dhamira yake ya kugombea urais wa Zanzibar mwaka 2010.Vilevile nimetumia sehemu kubwa kuelezea namna ziara ya Rais Bush nchini Tanzania inavyoweza kusaidia mapambano dhidi ya ufisadi,hasa kama "tukimwaminisha" kuwa fedha zinazoibiwa na mafisadi hao zinaweza kuishia mikononi mwa akina Osama bin Laden (well,pengine mafisadi hawana uhusiano na magaidi wa kimataifa lakini wengi tunajua kwamba neno UGAIDI likihusishwa na kitu chochote kile/mtu yeyote yule lazima itamsukuma Bush kufanya kitu flani).Bingirika na makala hiyo na nyinginezo zilizokwenda shule kwenye gazeti mwanana la Raia Mwema kwa KUBONYEZA HAPA29 Jan 2008
29.1.08
Evarist Chahali
FLICKS
No comments
Does a ringtone tell anything about a mobile phone's owner?Well,for more than 2 yrs now I've just stuck by one old song,Toploader's Dancing in the Moonlight .What about you?Here's the song's video (it's the flavour-especially kinanda -organ,accordion or whatever)-that I really like,and not the video actually)
Some other clips...for Tuesday.
Busta Rhymes ft Mariah Carey-I Know What You Want
Pharrell ft Snoop-That Girl
ATL-Calling All Girls
Lil' Flip ft Lea-Sunshine
Some other clips...for Tuesday.
Busta Rhymes ft Mariah Carey-I Know What You Want
Pharrell ft Snoop-That Girl
ATL-Calling All Girls
Lil' Flip ft Lea-Sunshine
24 Jan 2008

Siku chache zilizopita Wamarekani waliadhimisha siku ya Dakta Martin Luther King Jr,mmoja wa wapigania haki za Waamerika Weusi.Historia inamkumbuka Dkt King (aliyezaliwa mwaka 1929 na kuuawa kwa risasi mwaka 1968)kama nguzo muhimu katika kupigania haki za Waamerika Weusi nchini humo.Pengine kilichomfanya wanaharakati huyo akubalike zaidi ni imani yake ya kudai haki kwa njia za amani.
Miaka mitano kabla ya kuuawa,mwaka 1963,Dkt King alitoa hotuba ambayo hadi leo imeendelea kuwa na mvuto mkubwa sio nchini Marekani pekee bali pia sehemu mbalimbali duniani katika mapambano ya kudai usawa.Katika hotuba hiyo iliyopewa jina “I Have a Dream” (“Nina Ndoto”,kwa tafsiri isiyo rasmi),Dkt King alieleza matamanio yake kuona Waamerika Weusi na Weupe wakiishi pamoja kwa amani na usawa.Hotuba hiyo iliyotolewa mbele ya watu zaidi ya laki mbili,inakubalika miongoni mwa wengi kama moja ya hotuba za muhimu kabisa katika historia ya Marekani.Mwaka 1999,hotuba hiyo ilichaguliwa na wasomi kuwa ni hotuba bora kabisa za karne ya 20.
Miongoni mwa nukuu muhimu katika hotuba hiyo ni pamoja na (kwa tafsiri yangu isiyo rasmi) “…nina ndoto kwamba siku moja taifa hili litasimama na kuishi kama inavyotamkwa kwenye imani yake….nina ndoto kwamba siku moja watoto wangu wanne wataishi katika taifa ambalo hawatahukumiwa kutokana na rangi ya ngozi zao bali tabia/utu wao….nina ndoto kwamba siku moja watoto wa waliokuwa watumwa na watoto wa waliokuwa wamiliki watumwa watakaa pamoja katika meza ya undugu…”
Msukumo uliotokana na uongozi wa harakati za Dkt King ulisaidia sana kubadili historia ya Marekani hususan usawa kwa (Wamarekani) Weusi, na kupelekea mabadiliko mbalimbali dhidi ya sheria za kibaguzi.Miongoni mwa sheria hizo ni pamoja na “Civil Rights Act” ya mwaka 1964 iliyoharamisha ubaguzi kwenye sehemu mbalimbali katika jamii.Mwaka uliofuata, “Voting Rights Act” ilipitishwa na kufuta kipengere kilicholazimisha wapiga kura watarajiwa kufanya testi za kupima uwezo wa kusoma na kuandika (wengi wa waathirika wa kipengere hicho walikuwa Wamarekani Weusi ambao walikuwa na maendeleo duni kielimu kutokana na kubaguliwa).
Maadhimisho ya siku ya Dkt King yamekuwa yakitoa changamoto nzuri kwa jamii ya Wamarekani kutafakari mahusiano kati ya Weupe na Weusi.Wengi hujiuliza iwapo ndoto za Dkt King zimetimia kweli,zinaelekea kutimia au hazina dalili ya kutimia kabisa.Ni maswali magumu ambayo yanahitaji uchambuzi wa kina kuyajibu,na pengine hata kwa uchambuzi wa kina bado inaweza kuwa vigumu kupata jawabu moja linalokubalika.Kingine kinacholeta ugumu wa kupata jawabu ni tofauti ya vizazi.Kwa walioishi nyakati za ubaguzi wa rangi na kushuhudia harakati za Dkt King wanaweza kuwa na mtizamo tofauti kuhusu kutimia kwa ndoto za mwanaharakati huyo ukilinganisha na kizazi cha hivi karibuni ambacho kinamwelewa Dkt King kupitia kumbukumbu za historia tu.
Hata hivyo ni rahisi kukubaliana kwamba harakati za Dkt King na wenzie zimesaidia kuleta mabadiliko makubwa ikiwa ni pamoja na hayo ya kisheria niliyotaja awali.Wapo wanaokwenda mbali zaidi na kutoa mifano ya mafanikio ya Waamerika Weusi maarufu kama Jenerali Colin Powell na Condoleeza Rice ambao wameshika nafasi nyeti katika uongozi wa taifa hilo.Lakini mfano mzuri zaidi ni Barack Obama,seneta Mweusi anayewania kuteuliwa kugombea urais wa nchi hiyo kupitia chama cha Democrats.Akiteuliwa kuwa mgombea,ataweka historia ya pekee nchini humo,na akifanikiwa kushinda urais basi hiyo itakuwa zaidi ya kuweka historia (tuite kuandika historia upya).Hata kama atashindwa,mafaniko aliyokwishafikia hadi sasa ni hatua muhimu katika kutimia kwa ndoto za Dkt King.
Afrika nayo imetoa akina Dkt King kadhaa,na kwetu Tanzania tunajivunia Baba wa Taifa marehemu Julius Nyerere ambaye (kama Dkt King) alikuwa na ndoto zake kadhaa ambazo kimsingi zilihusu kuwa jamii yenye usawa.Ndoto za Mwalimu zilivuka mipaka ya Tanzania kuhakikisha kuwa Afrika yote inakuwa huru.Mchango wa Mwalimu katika mapambano ya ukombozi kusini mwa Afrika utaendelea kukumbukwa milele.Na pengine hapo ndipo baadhi yetu tunagundua mabadiliko ya vizazi yanavyochangia kusahaulisha historia.Mara nyingi napokutana na vijana Waafrika wenzangu (wanaoishi hapa Uingereza) kutoka nchi kama Zimbabwe,Zambia,Angola,Msumbiji,Afrika Kusini,Namibia na Uganda,nabaini kwamba wengi wao aidha wamesahau au wanapuuza mchango wetu katika ukombozi wa nchi zao (kwa Uganda ni kumng’oa Nduli Idi Amini).Angalau Wazimbabwe wanaweza kuwa na kisingizio kwamba kutokana na ubabe wa Mugabe,baadhi yao wanaweza kutoona faida ya kumkimbiza mkoloni na kujipatia uhuru.
Lakini pengine si busara sana kuwalaumu wanaopuuza mchango wa Mwalimu na Tanzania kwa ujumla katika ukombozi wa nchi zao kwani inawezekana kabisa wanafuatilia kinachoendelea nchini mwetu na kugundua kwamba baadhi yetu tumetupilia mbali kabisa jitihada za Baba wa Taifa kuhakikisha tunajenga jamii yenye usawa.Kwa vile dunia ni kama kijiji,katika zama hizi za utandawazi,majirani zetu hao watakuwa wanasoma na kusikia habari kuhusu ufisadi nchi mwetu,na pengine kubaki wanajiuliza “hivi hawa si ndio waliokuwa wanapigania usawa barani Afrika?Mbona wenyewe wako sasa wanafanyiana hivi?”.
Mwalimu alifariki huku baadhi ya ndoto zake zikiwa hazijatimia.Wachambuzi wazuri wa siasa wanadai kwamba baadhi ya ndoto hizo zilishindikana hata kabla hajang’atuka (kwa mfano upinzani wake wa awali dhidi ya ushirikiano na mashirika ya fedha ya kimataifa).Lakini nadhani Mwalimu aliumia zaidi kuona Azimio la Arusha likizikwa hai na Azimio “la kimyakimya” la Zanzibar (naliita hivyo kwani sijawahi kuona “document” yoyote rasmi inayoelezea kilichomo kwenye Azimio hilo).
Wakati Dkt King anaweza kufarijika huko aliko iwapo angeweza kufahamu baadhi ya mambo yanayoendelea sasa nchini Marekani (hususan kuhusu Obama) nashindwa kuhisi ni lipi litakalokuwa linampa furaha Mwalimu huko aliko tukiweka pembeni suala la amani na utulivu.Na hata katika hilo (la amani na utulivu) wapo wanaodai kuwa ni ya kufikirika zaidi kwani ni ukweli usiopingika kwamba masikini ni wengi zaidi kuliko matajiri,na yayumkinika kusema kwamba matumbo ya masikini hao hayana amani wala utulivu.
Kadhalika,kuna wanaodai kwamba kigezo cha amani na utulivu kimekuwa kikitumiwa vizuri zaidi na mafisadi wanaoamini kwamba Watanzania ni wapole sana na hawako tayari kuchezea lulu ya amani na utulivu kwa vile tu flani kakwiba mabilioni ya umma.Pengine mafisadi hao wako sahihi kwani tumekuwa tukishuhudia baadhi ya watu wakiua,wakapewa dhamana za chapchap na kuendela na maisha yao kama kawaida huku hatima ya kesi zao ikisubiri isahaulike akilini mwa watu.Wakati hayo yakitokea,magereza yetu yamejaa wamachinga wanaotafuta ridhiki mitaani na wafungwa wengine ambao inawezekana kabisa walijiingiza kwenye wizi wa nyanya au kuku kwa vile tu hawakuwa na njia nyingine ya kujipatia kipato.Uhalifu ni uhalifu,na kila mhalifu anastahili adhabu lakini inatatiza kuona wahalifu wengine wakiendelea kula raha kana kwamba waliyofanya si kinyume cha sheria.
Tofauti kubwa kati ya ndoto ya Dkt King na Mwalimu ni kwamba wakati Wamarekani Weusi wanafanya kila jitihada kuenzi jitihada za Dkt King kwa kuendeleza mapambano dhidi ya ubaguzi na kupigania usawa,sie tuko kwenye mgawanyiko mkubwa kati ya wachache walionacho wasiosubiri kuongezewa bali wanapora, na wengi wasio nacho ambao hata kile kidogo walicho nacho kinaporwa.Hili ndio tishio kubwa,sio tu kwa ndoto za Mwalimu,bali hata kwa hiyo lulu yetu ya amani na utulivu.

24.1.08
Evarist Chahali
LUDACRIS, MAFISADI, MTANZANIA, TEKNOLOJIA
3 comments
Alfajiri hii nimepata barua-pepe kutoka kwa mtu mmoja anayeelekea kuumia moyo kwa namna navyoshutumu ufisadi na mafisadi.Mzembe huyo ametoa shutuma lukuki kuhusu makala zangu magazetini na humu "bloguni" kuhusiana na suala la ufisadi.Kwa kutompa ujiko aliokuwa anatafuta,nimeamua kupuuza barua-pepe hiyo na sikumjibu.Binafsi,nilikuwa natambua bayana kwamba mafisadi wameshabaini kwamba mtandao una nguvu pengine zaidi ya magazeti yetu huko nyumbani,hasa ikizingatiwa kwamba ni machache tu yaliyopo kwenye mtandao.Mapepe aliyeniandikia barua-pepe amejitahidi kadri ya uwezo wake mdogo alionao kuni-discourage kuandika chochote dhidi ya mafisadi,huku akidai kwamba sie tulio ughaibuni tuna tabia ya kujifanya tunajua kila kitu (cha ajabu ni kwamba naye anadai yuko ughaibuni,tena hapahapa Uingereza).
Sitaki kuifanya case yangu kuwa universal lakini naamini kwamba teknolojia ya habari kupitia mtandao imetokea kuwa silaha kubwa dhidi ya wanyonge na wakati huohuo ikiwa mwiba mkali dhidi ya ufisadi na mafisadi.Kuna watakaopambana nasi tunaopigia kelele ufisadi kwa vile wao ni vibaraka wa mafisadi na wengine watasigishana nasi kwa vile wao wenyewe ni mafisadi.Wito wangu kwa wale wote ambao kwa namna moja au nyingine wameamua kusimama kidete kupigania haki na usawa kwa kila Mtanzania,Mwafrika na raia wengine wa dunia wanaonaoporwa stahili zao,ni huu:kila kelele ya fisadi itafsiriwe kama full tank za mafuta ya mtambo wa kukabiliana na maovu kwenye jamii.
Kwa fisadi "wangu" Mapepe,pokea zawadi hii kutoka kwa Ludacris kwenye clip ya Get Back (Caution: explicit lyrics)

23 Jan 2008
Rafiki yangu mmoja amenitumia barua-pepe muda mfupi uliopita baada ya kusoma makala yangu ndani ya toleo la wiki hii la gazeti la Raia Mwema.Hakuwa na pongezi wala malalamiko bali alidai kwamba wakati anasoma makala hiyo alijiskia kama anaongea nami uso kwa uso japo tuko umbali wa maili elfu kadhaa.Ni kweli,napoandika makala huwa najitahidi kadri ya uwezo wangu kuiwasilishalisha kwa kutumia staili ya mazungumzo (conversational style).Lakini sio mazungumzo kama ndani ya semina-elekezi,warsha,kongamano au semina bali yale yanayoweza kuwa yanafanyika mahala ambapo "tunaongea kwa kijinafasi" (comfortably).Tukiachana na hilo,makala yangu ndani ya toleo la wiki hii la gazeti la Raia Mwema inagusia michuano ya soka ya Mataifa ya Afrika huko Ghana,na kuielezea kwamba ni moja ya habari njema chache kutoka bara hilo,hasa kwa vile kwa takriban mwezi sasa habari zinazotawala kutoka huko ni kuhusu vurugu zinazoendelea Kenya zilizotokana na matokeo ya uchaguzi mkuu nchini humo.Kwa kutumia mfano hai,makala hii pia inaelezea ugumu anaoweza kukabiliwa nao Mtanzania pindi akidadisiwa chanzo cha umasikini wa nchi yetu,kabla ya kuwachambua mafisadi wa fedha na wale wa mawazo.Pamoja na habari na makala nyingine zilizokwenda shule katika jarida hilo la Raia Mwema,bingirika na makala hiyo kwa KUBONYEZA HAPA.
Ukimaliza kusoma makala hiyo,unaweza kuangalia clips hizi za versions mbili za Jesus Walks ya Kanye West.Naamini nasi tunahitaji nguvu za kiroho kukomesha ufisadi huko nyumbani.
22 Jan 2008
22.1.08
Evarist Chahali
BEN TV, KISWAHILI, LONDON, SONY ERICSSON, TID
No comments
Usiku huu (kwa saa za hapa Uingereza) msanii wa Bongofleva,T.I.D,alifanya mahojiano mafupi na kituo cha runinga cha BEN cha jijini London,kuhusu ziara ya msanii huyo nchini hapa.Inapendeza kuona msanii kutoka nyumbani akihojiwa,lakini nahisi kulikuwa na tatizo kidogo katika mfumo wa mahojiano hayo ambapo kwa mtizamo wangu,nadhani mtangazaji alitaka interview iwe ya Kiswahili lakini T.I.D alijibu maswali mengi kwa "Lugha ya Mama" (kimombo),japo sina budi kumsifu kwamba aliimudu kwa kiasi chake.Pia sidhani kama mtangazaji huyo atajiskia vibaya iwapo atatokea mtu wa kuhoji kama alijiandaa vya kutosha kufanya mahojiano hayo au ilikuwa ni ghafla.Anyway,kuna clips mbili hapa nilizozirekodi kwa kutumia simu ya zamani kidogo,Sony Ericsson W810i lakini nadhani itakuwa imejitahidi kwenye ubora wa video.Enjoy
22.1.08
Evarist Chahali
BOT, CAC40, DAX, FTSE, GREENSPAN, MERVYN KING, NIKKEI, WORLD MARKETS
1 comment

Wafuatiliaji wa blog hii watakuwa wameshasoma mara kadhaa niki-confess kwamba mie nina "allergy" na masuala ya namba (hisabati).Sasa hii mada fupi nayoandika inahusu uchumi,na kwa "kilaza" wa namba kama mie,ipo kazi kuiwasilisha vema ieleweke.Ntajitahidi hivyohivyo.Jana,masoko mbalimbali ya fedha (au hisa?),kwa kimombo stock markets,yaliyumba sana kiasi cha kuleta hofu miongoni mwa wachumi.Index ya FTSE (Uingereza) ilianguka kwa asilimia 5.48,Paris CAC40 ya Ufaransa ilikuwa asilimia 6.83,Frankfurt DAX ya Wajerumani asilimia 7.16 na huko Japan,index ya Nikkei ilianguka kwa asilimia 4.Masoko ya Marekani yalikuwa yamefungwa kufuatia maadhimisho ya siku ya Dr Martin Luther King,Jr.
Sina idea yoyote kuhusu hizo asilimia,lakini angalau katika gazeti la The Sun la hapa Uingereza nimepata mwangaza kuhusu uzito wa ishu hiyo.Kwa mujibu wa gazeti hilo,jumla ya hisa zenye thamani ya pauni bilioni 77 "zimepotea" (ki-stock market),na limetafsiri "hasara" hiyo into pauni 1,266 kwa kila mkazi wa nchi hii (sawa na shilingi 2,816,261.95 za Kitanzania)
Je akina sie na kijisoko chetu pale Mtaa wa Samora tunapaswa kuhofu kufuatia kuyumba huku kwa masoko haya makubwa duniani?Au tunapaswa kuhofia zaidi kuhusu mabilioni (wengine wanadai ni zaidi ya trilioni) yaliyoibiwa huko BoT kuliko habari hizi zinazohusu FTSE,DAX,CAC,et cetera?Je wewe msomaji unaonaje?
Subscribe to:
Posts (Atom)