12 Sept 2008

Ama kweli wenzetu wako serious na siasa zao.Kama kutokea kwenye kipindi cha televisheni cha mapishi kumemng'oa madarakani aliyekuwa Waziri Mkuu wa Thailand,Samak Sundarajev,sijui ingekuwa ishu kama ya Richmond huyu mwanasiasa angeepuka kitanzi.In a bigger picture,effectiveness ya Mahakama za Katiba ingeweza kuwa nyenzo muhimu sana kwa uwajibikaji wa viongozi wetu na maamuzi/matendo yao.Habari kamili kuhusu mkasa huu BONYEZA HAPA

Nani kasema vibaka na wezi wanaenda likizo mwezi wa toba?Hebu cheki kituko hiki kilichojiri ndani ya msikiti.Kwa mujibu wa gazeti la Dar Leo,JESHI la Polisi (huko nyumbaniTanzania) linamsaka mwanaume mmoja ambaye hakuweza kufahamika jina lake mara moja kwa tuhuma za kumpa Baraka Rwambow (22), futari yenye dawa za kulevya kisha kumpora pikipiki yake katika msikiti wa Tambaza. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Kanda Maalum Dar es Salaam, Jamal Rwambow amesema kuwa tukio hilo limetokea jana saa 11 jioni, msikiti wa Tambaza. 
Amesema kijana huyo alikodiwa Kimara Temboni na mtu anayemfahamu kwa sura ili ampeleke msikiti wa Tambaza kwa ajili ya kuswali swala ya magharibi. Amesema kuwa baada ya kufika msikitini hapo mtu huyo aliingia ndani kuswali na baada ya kutoka alimpa dereva wa pikipiki futari hiyo ambapo alikataa na alimbembeleza akaamua kula. Baada ya kula mtu huyo alianza kulegea na mwishowe alimuomba mteja wake huyo amuendeshe ili waweze kurejea nyumbani ambapo mteja huyo aling'oa pikipiki na kwenda moja kwa moja Salender Club na kumtupa kijana huyo akiwa hajitambui. 

Walinzi waliokuwepo jirani walimuokota mtu huyo na kwenda kutoa taarifa kituo cha polisi.Polisi wanaendelea kumsaka mtu huyo na pikipiki hiyo aina ya Royck.

Ama kweli dunia haijaishiwa vituko.Hebu tumwangalie na huyu nae.Jana dunia iliungana na Wamarekani kuadhimisha mwaka wa saba wa mashambulizi ya kigaidi ya September 11,2001.Licha ya kusababisha majonzi na kubadili mwenendo wa mambo ulimwenguni,tukio hilo lilizaa mashujaa kadhaa:kwa mfano watu waliojitolea mhanga kuokoa maisha ya wenzao na wale walionusurika kufa katika majengo yaliyoshambuliwa.Kumbe kuna "wasanii" walioona nafasi ya kujichukulia ujiko wa kuwa mashujaa wa September 11 hata kama hawakuwepo mahala pa tukio.Mfano ni HUYU SHUJAA FEKI WA 9/11.

11 Sept 2008

Sidhani kama kuna ubishi kwamba Kanye West ana kipaji cha hali ya juu katika muziki,both as a rapper and a producer.Sasa sijui ni yale ya mgema akisifiwa tembo hulitia maji au ni matokeo ya ile ajali ambayo almanusura ichukue uhai wake,lakini something is wrong with Kanye.Hebu angalia HAPA kasheshe aliyoizua leo huko Los Angeles Airport.

Hapa chini kuna kazi mbili za msanii huyo.Ya kwanza ni wimbo wake mwenyewe wa Through The Wire na ya pili ya ni production yake kwa The Game katika wimbo Dreams.




Wakati Waamerika na wapenda amani wengine duniani wanakumbuka mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea siku kama leo mwaka 2001,kibosile wa polisi wa Devon&Cornwal hapa Uingereza,Colin Terry,ameadhimisha siku hiyo kiaina kwa kuvaa sanamu la Osama bin Laden.Kitendo hicho kimezua kimbembe na tayari wapo wanaotaka awajibishwe pengine kwa vile afande huyo pia ni mwandamizikatika eneo lake  kwenye mapambano dhidi ya ugaidi.Habari zaidi iko HAPA


10 Sept 2008

Jana niliongelea kidogo kuhusu The Big Bang Theory,na hofu zilizojitokeza kwamba huenda leo,Jumatano,ingekuwa mwisho wa dunia.Well,experiment hiyo inaendelea huko kwenye underground tunnel lililosambaa mpakani mwa Uswisi na Ufaransa na hakuna dalili kwamba dunia itafikia tamati leo!Hata hivyo,hofu ya Big Bang imepelekea mwisho wa dunia huko India.Well,sio kwa nchi nzima bali kwa binti mmoja ambaye aliamua kujitoa uhai wake baada ya kuwa traumatized na taarifa za vyombo vya habari kuhusu uwezekano wa mwisho wa dunia kutokana na experiment ya Big Bang.Pengine tutasikia mengi pindi experiment hiyo itapomalizika.Habari kamili kuhusu binti wa India ni hii HAPA

Pamoja na kuchukua sabbatical leave ya lazima katika uandishi wa makala katika gazeti la Raia Mwema,blogu hii itaendelea kuwaletea kinachojiri kila wiki katika jarida hilo mahiri huko nyumbani.Miongoni mwa habari zilizochukua uzito wa juu katika toleo la wiki hii ni pamoja na kauli ya Spika wa Bunge la Muungano,Samuel Sitta,kwamba amejiandaa vya kutosha kufuatia taarifa kwamba watuhumiwa wa ufisadi wameingiza sumu huko Bongo kwa lengo la kuwadhuru Sitta na Mbunge wa Kyela,Dr Harrison Mwakyembe.Sidhani kama inahitaji kujumlisha mbili na mbili kupata jawaba as to akina nani watakuwa the usual suspects wa unyama wa aina hii.Zaidi BONYEZA HAPA kusoma habari hiyo na nyingine motomoto.

Kuna hii kitu wanaita The Big Bang Theory inaelekea kuwachanganya watu wengi wakiwamo wanasayansi wenyewe.Kwa vile mie sio mzuri sana kwenye maeneo hayo,BONYEZA HAPA kupata undani zaidi wa hii kitu.

Kwa upande wa siasa za Marekani,kuna wanaomuona Sarah Palin kuwa hana tofauti na Islamic fundamentalists ambao mgombea-mwenza wake,John McCain,amefanya kuwa moja ya ajenda zake kuu za kushinda uchaguzi.Habari nzima iko HAPA

Na burudani kidogo kutoka kwa John Legend ft Andre 3000 katika Green Light.

Matatizo ya kidunia yalinifanya nishindwe ku-update blog hii kwa takriban miezi miwili hivi.Kupoteza mzazi inaweza kuwa tukio la kawaida iwapo litatokea kwa mtu mwingine.Lakini ukweli mchungu ni kwamba once ikitokea kwako ni vigumu mno kuhimili matokeo yake.Inaumiza zaidi pale mmoja wa watu aliyekuwa inspirational katika kufikia malengo yake flani (kwa upande wangu,suala la shule) anapoondoka duniani miezi michache kabla ya wewe kufikia lengo hilo.Lakini kwa sie tunaoamini katika mapenzi ya Mungu na usahihi wa maamuzi yake inalazimu kufika mahala kukubali kuwa yote,hata kama machungu kiasi gani,ni MAPENZI YA BWANA.

Blogu hii itaendelea kuwaletea uchambuzi wa masuala mbalimbali,hususan ya kisiasa.Kwa vile tunaelekea kwenye uchaguzi wa rais huko U.S.A,blogu hii itajitahidi kuleta mkusanyiko wa habari mbalimbali.Pamoja na hayo ni picha mbalimbali kutoka Tanzania zilizopigwa katika kipindi cha takriban miezi mitano niliyokuwa huko.

Karibuni tena

Kwa kuanza,kuna hapa chini ni picha kadhaa kutoka angani.Picha ya kwanza ni Addis Ababa kutoka angani,ya pili ni Dar kutoka angani,ya tatu ni Schiphol Airport,Amsterdam na ya mwisho ni Aberdeen Airport.









18 Jul 2008

The family of the late Hon. Richard Mwakasege (MP) of Mbeya Town would like to inform you:

Hon./Rev./Prof./Mr 7Mrs./Mr./Miss.

...............................................................................

That their beloved son Leonard Richard (Ghetto) intend to wed on october 2008. Being a close relative or friend, we kindly ask you to donate to this event.

Please submit your donation to the one who gave you this card before 30th September 2008.



we thank you in advance.



Familia ya Marehemu Mhe: Richard Mwakasege (MB) wa Mbeya Mjini wanayofuraha kukujulisha/kuwajulisha

Mhe./Mch./Prof./Bw & Bi./Bw./Bi.

...............................................

kuwa kijana wao mpendwa

Leonard Richard (Ghetto) anatarajia kubariki ndoa mwezi wa oktoba 2008. Ukiwa kama ndugu, jamaa au rafiki wa karibu tunaomba mchango hali na mali ili kufanikisha shughuli hii.

tafadhali wasilisha mchango wako kwa aliyekupa kadi hii kabla ya tarehe 30/09/2008.

tunatanguliza shukrani zetu.



wasiliana na

Mhe. Salehe Ramadhani Njaa (Advocate) simu 0784-333375

Shaibu Buzohera 0713-333375

Lwitiko Mwalukasa 0754 520353

Everly Mwakyulu 0716 303808

Leonard Richard (Ghetto) 0754 286157.




7 Jul 2008

Binti aitwaye MAGDALENA THOMAS KATIMAKAMU (alias NJEA) anawatafuta Baba yake THOMAS KATIMAKAMU na Mama yake SELINA NDIMINI,ambao inasemekana wanaishi NAIROBI,nchini KENYA.Magdalena,ambaye kwa sasa anaishi Ifakara, alipoteana na wazazi wake mwaka 1989 walipokuja Tanzania mara ya mwisho.Yeyote anayewfahamu wazazi hao anaombwa kufikisha salamu hizo.Kwa mawasiliano zaidi,waweza kutuma barua-pepe kwa [email protected] au sms/simu kwa +255773957709/+255783957709 au +447814843356.Asanteni

Jamaa yangu mmoja mkazi wa Kwa Jongwe (Zimbabwe) kanitumia fedha hii kama rambirambi rambi yake kwa msiba ulionikumba hivi karibuni.

27 Jun 2008

Katika toleo la wiki hii la jarida la Raia Mwema nazungumzia dalili zakutimia kwa utabiri wa Mwalimu Nyerere kwamba upinzani wa kweli unaweza kutoka ndani ya CCM.Kwa namna mambo yanavyokwenda mramba ndani ya chama hicho nidhahiri kwamba kuna tofauti kubwa za kiimani na kimtazamo miongoni mwa viongozi wake.Ili kutokukunyima uhondo zaidi,bingirika na makala hiyo,pamoja na nyinginezo zilizopanda vidato,kwa KUBONYEZA HAPA

19 Jun 2008

Makala yangu katika toleo la wiki hii la gazeti la Raia Mwema inaanza kwa kuwashutumu watangazaji wa radio na runinga za Bongo ambao wanafanya mzaha kwenye shughuli muhimu.Makala inawalenga watangaza taarifa za habari ambao aidha hawajiandai vya kutosha kabla ya news bulletins kiasi cha kuchapia maneno,especially majina ya watu na sehemu,au wanaokuwa too obsessed na sauti za akina Jacob Tesha,Ahmed Kipozi,Ahmed Jongo,Abubakari Liongo,Charles Hillary,nk to an extent wanaishia kusoma madudu badala ya habari.Kuiga sauti sio uhaini lakini kwa kufanya hivyo isiwe sababu ya kusoma vitu vya ajabu.


Pia makala yangu inazungumzia suala zima la ushirikina hapa nyumbani ambapo nimejaribu kulitazama kwa upande mmoja kama mwanafunzi wa zamani wa sosholojia ya dini (sociology of religion) na kwa upande mwingine kama mwanajamii ninayeelewa nini kinanizunguka,hata kama tunaona aibu kukiongelea.Sio siri kwamba mambo ya ushirikina yameshika hatamu sana katika jamii mbalimbali za Kiafrika,lakini hii ya Fisadi Mzee wa Vijisenti kumwaga ndumba ndani ya Bunge inaonyesha jinsi gani mambo yanakwenda mrama sana katika nchi hii tuliyoahidiwa kuwa maisha bora kwa kila aliyezaliwa hapa yanawezekana.Nisikunyime uhodno,bingirika na makala hiyo pamoja na nyingine zilizokwenda shule ya kutosha KWA KUBONYEZA HAPA

14 Jun 2008

Wapendwa,naomba mniwie radhi kwa kupotea hewani kwa muda mrefu.Nilikuja nyumbani kumuuguza mama mzazi lakini kwa bahati mbaya tarehe 29/05 Bwana aliamua kumchukua na kumrejesha kwake.Makanisani wanatuambia tulitoka kwenye mavumbi na tutarejea kwenye mavumbi.Nawashukuru nyote mlioshiriana nasi kumuombea mama apone na nyote mliotoa salamu za rambiarambi ambazo kwa hakika ndio zinazotuwezesha kuwa na nguvu ya kuingia tena bloguni.
Naomba kuwapatia makala chache ambazo kutokana na matatizo niliyokuwa nayo sikuweza kuzitundika hapa.Katika makala yangu ndani ya gazeti la Raia Mwema la tarehe 28/05 nilizungumzia suala la wagombea binafsi na kutabiri kwamba huo unaweza kuwa ndio kifo cha mafisadi.Makalahiyo ilikwenda kwa kichwa WAGOMBEA BINAFSI:KIFO CHA MAFISADI CHAJA. Katika toleo lililofuatia,yaani la tarehe 04/06,nilizunguzmia kuhusu utendaji kazi wa Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu,Bwana Salva Rweyemamu.Zaidi,soma makala hiyo yenye kichwa KAULI ZA MKURUGENZI IKULU KUHUSU BALLALI MKANGANYIKO MTUPU.Makala ya wiki hii,yaani iliyotoka Jumatano ya tarehe 11/06 inazungumzia Mkutano wa Sullivan uliomalizika huko Arusha hivi karibuni.Katika makala hiyo nimejaribu kuhoji iwapo Mkutano huo umekuwa/utakuwa na faida yoyote kwa Watanzania.Makala hiyo imebeba kichwa kisemacho MKUTANO WA SULLIVAN:WAZAWA WAMENUFAIKA VIPI?

3 Jun 2008

NINASIKITIKA KUWATANGAZIA KIFO CHA MAMA YANGU MZAZI ADELINA MAPANGO KILICHOTOKEA IFAKARA MOROGORO TAREHE 29/05/2008 NA MAZISHI YALIKUWA JANA TAREHE 02/06/2008 KATIKA MAKABURI YA UKOO WA CHAHALI HAPA IFAKARA.NAWASHUKURU NYOTE AMBAO KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE MLIUNGANA NAMI KATIKA KUMUOMBEA MAMA APONE LAKINI BWANA AMEMPENDA ZAIDI NA HATIMAYE KUMREJESHA KWAKE.UKOO WA CHAHALI NA MAPANGO UNAWASHUKURU SANA KWA USHIRIKIANO WENU.BWANA AMETOA BWANA AMETWAA,JINA LA BWANA LIHIMIDIWE MILELE.

13 May 2008

Niliposikia mara ya kwanza nilidhani ni stori tu za mjini.Jana nimesikia tena,na safari hii ni kutoka kwa mwanafunzi aliyehitimu kidato cha sita hivi majuzi.Ishu yenyewe iko hivi:eti wanafunzi wa kidato cha sita waliletewa mashuleni fomu za kuomba udhamini wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu.Hadi hapo hakuna tatizo,Bodi inawajali wanafunzi hai inawaletea fomu shuleni.Mgogoro unaanzia kwenye taratibu za kurejesha fomu hizo ambapo kila mwanafunzi alipaswa kulipia shs 10,000/= ambazo ni non-refundable.Mgogoro zaidi ni ukweli kwamba zoezi zima la kujaza na kurejesha fomu hizo lilifanyika hata kabla wanafunzi hao hawajafahamu matokeo yao.Kwa maana hiyo,mwenye kufaulu na kufanikiwa kupata admission ya chuo anakuwa amenufaika lakini kwa aliyepata maksi zisizomruhusu kuendelea na masomo ndio ameliwa.This is what we call daylight robbery.Kwanini wasingechukua hiyo elfu 10 baada ya matokeo ili wale wasio na sifa wasiliwe fedha zao bure?Deadline ya kurejesha fomu hizo ilikuwa tarehe 30/04 na matokeo ndio yametoka majuzi.Sipendi kuona mikopo ya wanafunzi inageuzwa kuwa kama bahati nasibu flani,or to be more precise,ujambazi wa mchana kweupe.

10 May 2008

Hapa nilipo,mtandao unasumbua sana.Kwahiyo,nawaomba mniruhusu niwape tu LINK HII ya makala yangu katika toleo la wiki hii la gazeti la Raia Mwema.

3 May 2008

Hivi karibuni,eneo la Mlimani (UDSM) liligeuka Baghdad kwa muda kufuatia ghasia kubwa kati ya wanafunzi na vyombo vya dola.Hali sasa ni shwari,na majuzi walifanya uchaguzi wa viongozi wapya wa DARUSO japo inasemekana kwamba turnout ilikuwa ndogo sana.Ni kutokana na ushwari huo ndipo nami nilibahatika kuwatembelea wanazuoni flani hapo,na kufanikiwa kunyaka picha hii inayoonyesha eneo la Ubungo kama sijakosea,japo halionekani vema sana.

Miongoni mwa maeneo ya hapa jijini yanayotuwezesha kuendeleza libeneke la bloggin-japo nyakati nyingine kwa kusuasua-ni cafe moja iliyopo Millennium Tower.Kuna jamaa kanidokeza kuwa yeye huwa mwenyeji sana eneo hili kwa ajili ya kuangalia MIGONGO!Well,inawezekana alikuwa anazungumzia mgongo wa Twiga huyu,jirani na mwanga wa taa,ambaye ni kivutio mwanana!

Sina budi kuwataka radhi wasomaji wapendwa kwa kutoweka chochote hapa kwa zaidi ya wiki sasa.Napenda sana ku-update blog hii lakini wakati mwingine mazingira ya hapa yanakuwa kikwazo.Hata hivyo,nadhani mtaburudika na makala yangu katika gazeti la Raia Mwema toleo la wiki inayoisha leo.Makala hiyo ni reaction dhidi ya wababaishaji flani ambao wanajaribu kuhoji usafi wa akina-sie tulioamua "liwalo na liwe" dhidi ya mafisadi.In fact sio kama wanahoji as such,wanachofanya ni kuwa servants wa mafisadi,nisicho na uhakika ni whether wanafanya hivyo kutokana na njaa zao au mfilisiko wa mawazo.Anyway,makala nzima inapatikana kwa kubonyeza hapa

Jasusi ChatBot

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.